UCHOKOZI WA EDO : Neno dhaifu linauma kuliko mabilioni yaliyopotea?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
UCHOKOZI WA EDO : Neno dhaifu linauma kuliko mabilioni yaliyopotea?

Kama tungekuwa China, wiki hii yule jamaa yao anayenyonga watu wanaoiba fedha za umma angekuwa na kazi nzito. Kuna mabilioni ya fedha yamepotea. Namba Moja alituhimiza tulipe kodi lakini kuna watu bado wana ujasiri wa kula kodi zake.

Edo+Kumwembe.jpg

BY Edo Kumwembe

Namba Moja ameanzisha miradi ya treni ya umeme, amenunua ndege, anajenga barabara nyingi. Haya mambo yanataka fedha nyingi, lakini watu bado wanaiba kiujanja. Baada ya ripoti ya CAG tulipaswa kuwa bize na hesabu ya noti zilizopotea pamoja na watu waliohusika.

Tungekuwa China kuna watu wengi katika mafaili ya CAG ilibidi wanyongwe. Ajabu iliyoje kwamba pambano linalovutia zaidi kwa sasa ni kati ya mkuu wa mjengo wa Dodoma dhidi ya CAG. Juzi mkuu wa mjengo wa Dodoma aliita waandishi wa habari kusisitiza anavyokerwa na neno dhaifu.

Pambano linavutia kwelikweli. Neno ‘dhaifu’ ni habari ya mjini. Pambano hili linachekesha sana. linanikumbusha udhaifu wetu. Jinsi ambavyo tunavyoweza kuweka kando jambo la msingi tukajadili jambo ambalo halina maana sana.

Hoja ya msingi ilipaswa kuwa namna ambavyo mabilioni yanaendelea kupotea. Wajanja bado wanapiga fedha. Watu ambao wanatuhumiwa kwa namna moja au nyingine watakuwa wanavutika na mpambano huu, wanautumia kama kivuli kujificha.

Vichwa vya habari vya magazeti vilipaswa kuandika habari kama vile ‘uchunguzi wa mabilioni yaliyopotea waanza’. Hata hivyo haiko hivyo. Kwa sasa vichwa vya habari vinasema ‘Spika amvaa CAG’. Kichwa kingine cha habari kinasema ‘CAG ajibu mapigo ya Spika’.

Ndani ya habari haukuti neno ‘mabilioni’. Unakuta neno ‘dhaifu’. Tulioishia darasa la saba tunashindwa kuelewa nani anapaswa kushughulikia kinachoendelea baada ya ripoti kuonyesha upotevu wa mabilioni?

Nchi ambayo watu wake wapo makini wangesahau haraka habari ya neno dhaifu na kutupia macho upotevu wa mabilioni, lakini sisi inaonekana bado tunapenda siasa na siku hizi wanasiasa wanajaribu kuwageuza waandishi kuwa shimo la takataka.

Kitu kidogo tu utasikia waandishi wa habari wameitwa katika mkutano wa waandishi wa habari. Ukichunguza sana hauoni tija katika mkutano mzima zaidi ya mipasho.
 
Tatizo kubwa tumeshalijua kwamba wezi ni lazima wawe na heshima kwa Bunge.
Ukiwa na heshima kwa mihimili hiyo unasamehewa makosa yako.

Inaonekana wizi unafanywa na kundi la marafiki.
Ni mtandao wa marafiki wanaolihujumu Taifa.

Hawajui kuwa ukada,urafiki,kuheshimiana kinafiki na kwa woga ndiko kuliko tufikisha hapa.
 
Mtandao wa majizi Mkuu. Umesambaa kuanzia Ikulu, Serikalini, Bungeni na ndani ya maccm.

Kinara wao hawa majizi yuko Ikulu Kubwa la majizi. Anauthubutu wa kujichotea hazina $465 millions bila idhini ya Bunge kisha kumzuia CAG Assad asikague matumizi hayo ya zaidi ya trillions ya walipa kodi.

Tatizo kubwa tumeshalijua kwamba wezi ni lazima wawe na heshima kwa Bunge.
Ukiwa na heshima kwa mihimili hiyo unasamehewa makosa yako.

Inaonekana wizi unafanywa na kundi la marafiki.
Ni mtandao wa marafiki wanaolihujumu Taifa.

Hawajui kuwa ukada,urafiki,kuheshimiana kinafiki na kwa woga ndiko kuliko tufikisha hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najihisi dhaifu kuifuatilia bunge bora tungelikua kama bushmen ambao hata kamusi hawakuwahi kuiona uongozi unashindwa kutogautisha kati ya neno dhaifu na pesa inayopotea ambaya sasa inafanya maisha ya mtanzania kuwa DHAIFU NA MAGUMU hebu msitutanie af mambo mkayamaliza kimya kimya... mbona raia mnatuita WANYONGE na hatujawahi andamana kuelekea IKULU wala BUNGENI haha mmeona mlivyo DHAIFU #siasa bana duh!! Kama ikipendeza tuedit hadi lile neno dhaifu kwenye bible ●●●●●●
UCHOKOZI WA EDO : Neno dhaifu linauma kuliko mabilioni yaliyopotea?

Kama tungekuwa China, wiki hii yule jamaa yao anayenyonga watu wanaoiba fedha za umma angekuwa na kazi nzito. Kuna mabilioni ya fedha yamepotea. Namba Moja alituhimiza tulipe kodi lakini kuna watu bado wana ujasiri wa kula kodi zake.

Edo+Kumwembe.jpg

BY Edo Kumwembe

Kama tungekuwa China, wiki hii yule jamaa yao anayenyonga watu wanaoiba fedha za umma angekuwa na kazi nzito. Kuna mabilioni ya fedha yamepotea. Namba Moja alituhimiza tulipe kodi lakini kuna watu bado wana ujasiri wa kula kodi zake.

Namba Moja ameanzisha miradi ya treni ya umeme, amenunua ndege, anajenga barabara nyingi. Haya mambo yanataka fedha nyingi, lakini watu bado wanaiba kiujanja. Baada ya ripoti ya CAG tulipaswa kuwa bize na hesabu ya noti zilizopotea pamoja na watu waliohusika.

Tungekuwa China kuna watu wengi katika mafaili ya CAG ilibidi wanyongwe. Ajabu iliyoje kwamba pambano linalovutia zaidi kwa sasa ni kati ya mkuu wa mjengo wa Dodoma dhidi ya CAG. Juzi mkuu wa mjengo wa Dodoma aliita waandishi wa habari kusisitiza anavyokerwa na neno dhaifu.

Pambano linavutia kwelikweli. Neno ‘dhaifu’ ni habari ya mjini. Pambano hili linachekesha sana. linanikumbusha udhaifu wetu. Jinsi ambavyo tunavyoweza kuweka kando jambo la msingi tukajadili jambo ambalo halina maana sana.

Hoja ya msingi ilipaswa kuwa namna ambavyo mabilioni yanaendelea kupotea. Wajanja bado wanapiga fedha. Watu ambao wanatuhumiwa kwa namna moja au nyingine watakuwa wanavutika na mpambano huu, wanautumia kama kivuli kujificha.

Vichwa vya habari vya magazeti vilipaswa kuandika habari kama vile ‘uchunguzi wa mabilioni yaliyopotea waanza’. Hata hivyo haiko hivyo. Kwa sasa vichwa vya habari vinasema ‘Spika amvaa CAG’. Kichwa kingine cha habari kinasema ‘CAG ajibu mapigo ya Spika’.

Ndani ya habari haukuti neno ‘mabilioni’. Unakuta neno ‘dhaifu’. Tulioishia darasa la saba tunashindwa kuelewa nani anapaswa kushughulikia kinachoendelea baada ya ripoti kuonyesha upotevu wa mabilioni?

Nchi ambayo watu wake wapo makini wangesahau haraka habari ya neno dhaifu na kutupia macho upotevu wa mabilioni, lakini sisi inaonekana bado tunapenda siasa na siku hizi wanasiasa wanajaribu kuwageuza waandishi kuwa shimo la takataka.

Kitu kidogo tu utasikia waandishi wa habari wameitwa katika mkutano wa waandishi wa habari. Ukichunguza sana hauoni tija katika mkutano mzima zaidi ya mipasho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahuni hawa wanataka kututoa kwenye mstari wa wizi na ubadhirifu mkubwa wanaoufanya kwenye pesa za walipa kodi. Kuhusu ripoti hadi hii leo wako kimya kabisa si huyu aliyekabadhiwa au mwingine yeyote yule Serikalini, Bungeni au ccm. Kwa miezi mitatu sasa au zaidi wamemshupalia CAG Assad kwa kusema ukweli kuhusu BUNGE kuwa DHAIFU!

Najihisi dhaifu kuifuatilia bunge bora tungelikua kama bushmen ambao hata kamusi hawakuwahi kuiona uongozi unashindwa kutogautisha kati ya neno dhaifu na pesa inayopotea ambaya sasa inafanya maisha ya mtanzania kuwa DHAIFU NA MAGUMU hebu msitutanie af mambo mkayamaliza kimya kimya... mbona raia mnatuita WANYONGE na hatujawahi andamana kuelekea IKULU wala BUNGENI haha mmeona mlivyo DHAIFU #siasa bana duh!! Kama ikipendeza tuedit hadi lile neno dhaifu kwenye bible ●●●●●●

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli unauma sana, hata tulio watetezi wa chama tawala tunakubali kuna udhaifu wa kutisha katika usimamizi wa fedha za walipa kodi, wakubali na kujirekebisha badala ya kutishia na kujifanya wako wasafi kumbe ni wachafu na "WADHAIFU"...
 
Back
Top Bottom