UCHOKOZI WA EDO: Nadhani picha ya Komredi Polepole mkutanoni ni ‘photoshop’

magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
6,177
2,000
1550750976915.png

Jana nilivaa miwani, nikavua, nikavaa tena. Sikuamini nilichokiona. Nikamwita kijana mdogo mwenye macho yenye afya
zaidi anisomee maandishi ya chini ya picha ya komredi Polepole. Ilitoka katika ukurasa wa 3 wa gazeti hili toleo la jana.

Picha ilimuonyesha komredi Polepole akiwa katika mkutano wa hadhara pale Karatu akihutubia wananchi katika kivazi maridadi cha chama chake. Mpaka sasa nadhani kuna makosa ya kiuandishi chini ya ile picha. Naamini Namba Moja bado hajaruhusu mikutano ya hadhara.

Namba Moja ameruhusu mikutano ya kisiasa ya wabunge katika maeneo yao.Majuzi tu alikutana na swali korofi la kiongozi mmoja wa dini aliyetaka watu waruhusiwe kufanya siasa zao. Akamjibu kwa ufafanuzi mzuri kwamba mikutano ya siasa ipo kwa ajili ya wabunge katika maeneo yao.

Naamini picha ya Polepole huenda ni ya ‘photoshop’. Tunapozungumza photoshop tunazungumzia ile tabia ya vijana wa kisasa kutengeneza picha na kuziunganisha katika matukio ambayo hayana uhusiano.Siamini kama komredi Polepole anawezakuvunja amri ya Namba Moja kiurahisi.

Wakati huu ambao Namba Moja ametoka kusisitiza haki na kuijenga jamii iliyo sawa siamini kama upande mmoja unaweza kuruhusiwa kufanya mikutano halafu mwingine uzuiwe.

Nategemea komredi Polepole atakuja juu kwa picha yake kutengenezwa akiwa katika mkutano wa siasa kinyume na amri ya Namba Moja au kama ni kweli alikuwa ni yeye katika ule mkutano basi anaweza kumuomba radhi Namba Moja kwa kuvunja amri yake.

Siamini pia kama Polisi wanaweza kumuacha ahutubie wakati imekuwa ikiwakamata wanasiasa wengine hasa wale wa upinzani ambao wamekuwa wakihutubia mikutano ya hadhara.

Hapa ndipo ninapojaribu kujiaminisha kwamba ile picha ya komredi Polepole inaweza kuwa ni photoshop.

Nategemea ataitolea maelezo muda mchache ujao. Siku hizi nchi yetu inaongoza kwa kuwa na watu wa kada mbalimbali wanaopenda kufanya mikutano na waandishi wa habari bila ya sababu za msingi. Nadhani mkutano wa waandishi wa habari na komredi Polepole utakuwa wa msingi sana. Nausubiri kwa hamu.

Chanzo: Mwananchi
 

MO11

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
17,506
2,000
Sheria zipo kwa ajili ya upinzani
kwa watawala kwa kuwa wamezitunga wenyewe hazitumiki
si unajua mbwa ukimjua jina hakupi tabu ukimwita tu atatingisha mkia mambo yanakua safi
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
Chombo kimekua usalama wa ccm siyo usalma wa raia tena.
Wanajiabisha sana.
Ethiopia wapo kwenye mchakato wa kuingia katika demokrasia ya kweli jambo la kwanza ni kuvunja vyombo vyote vya usalama na kuviunda upya kabisa.
Na sisi tanzania yapaswa tufanye hivyo maana tunashuhudia uvccm kuwa TISS
 

mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,220
2,000
Wakitoka hapo kwa vinywa vipanaa wanesema eti hawajakata sisas na ati eti kila mtu afanye siasa kwenye eneo lake.na hata aibu hawana.

wanajua hawakubaliki ndio maana wanazuia wenzao kufanya mikutano ila wao kutwa kusha kiguu na njia,ukiwauliza hapo moja kichwani(polepole)na wenzake wanatangaza dini?.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom