VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Watu waoga na wasiojiamini,hasa katika kujenga na kutetea hoja zao,huwa na hulka ya kufanya au kusema sirini. Au,husema na kufanya pasipo na mtu wa kukosoa. Hupendezwa na kuongea au kufanya peke yao na kushangiliwa peke yao na watu wao. Hizi ndizo sifa kuu za waoga na wasiojiamini.
Waoga huvizia kwenye polisi wengi na kujifanya kusema bila woga. Hadhira inapoguna tu,hushughulikiwa haraka bila baraka. Siasa haipo hivyo. Siasa hutaka mapambano ya maneno,mifano minono na hoja za haja. Waziwazi.
CCM yetu ina zaidi ya robotatu ya Wabunge kwenye Bunge la Tanzania. CCM inaunda serikali iliyopo madarakani sasa. Serikali ya Rais Magufuli. Serikali ya watumbua na watumbuliwa majipu. Lakini,kwenye kuonyeshwa ikipambana kihoja,CCM yetu imejaa woga na kutojiamini. Ina Wabunge wanaoambiwa cha kusema. Ndiyo maana?
CCM ni chama bora,chama kikongwe na kikubwa. Kinaunda serikali imara. Kimeaminiwa tena kuongoza nchi. Kweli kinaogopa midahalo,lakini kisiogope kuoneshwa live pale Bungeni. Wapinzani kwa uchache wao wasitutishe na kutufanya tusijiamini. Tukubali kuoneshwa live ili tutambe hadi wapate wivu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam