Uchochezi wa Mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Status
Not open for further replies.

Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,801
2,000
Nimesoma maandiko ya ndugu yangu Mohamed Said aliyoyaweka katika kitabu chake akiitacho Historia ya Uhuru upande wa Pili,
Katika maandishi yake ameonyesha wazi kulazimisha dunia iamini kuwa waislamu wamedhulumiwa katika historia ya Uhuru wa nchi hii,
Katika matakwa yake Mohamed Said anataka historia ya Uhuru ingetazama itikadi za kidini kwanza kabla ya kusimamia maudhui halisi ambayo ni Uhuru,

Nikubaliane nae kuwa historia ya nchi yetu inamapungufu na inahitaji masahihisho, lakini kwa hili la Mohamed si masahihisho bali ni upotoshaji mkubwa, Uchochezi na ni Uhaini kwa nchi. Kwa bahati mbaya bwana Mohamed Said histori anayoisimamia ameiakisi kuanzia miaka ya 1950+ tu,

Hajajishughulisha kuutazama utawala wa Kiingereza wala kuutazama upya utawala wa Kijerumani ambao ndio uliosimika misingi ya utawala na mifumo mingi ambayo leo tunaitumia! Mjerumani mfumo wake wa utawala kwa ASILI ni wa kikristu na kwa Tanganyika walisimama hivyo bila kutetereka! (Yaani mfumo kristu 100%)

Akaja Muingereza na yeye mfumo wa utawala wake wa ASILI ni wakikristu!

Imenilazimu kitabu cha bwana Mohamed Said kiitwacho "Maisha na nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968" (Historia ya uhuru iliyofichwa ya upande pili) kukiita ni NGANO za masika.

Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.

Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 – 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.

Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake.

Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake,

Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa.

Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.

Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.

Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya mchikichini Mzizima na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 34 tu, hiyo ni mwaka 1880 hadi 1953

Nje ya kuhudumu katika uislamu, alikuwa ni mvuvi aliyevua pamoja na Ally Ramadhan mwekahazina wa kwanza wa AA,

Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL)

Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele za cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu,

Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake!

Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao.Elimu,

WogaIkumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake.

Mnamo tarehe 7/7/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia!

Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 , Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa Kasisi Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni boss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.

Mpaka hapo ndugu yangu Mohamed Said angalau umepata picha kwa KIFUPI tu ya harakati za uhuru chini ya kanisa.

Nikipata wasaa nitakuletea picha za Mwalimu Nyerere na Edger Aristide Maranta

Kwanini Kasisi huyu wa kikatoliki Edger Aristide Maranta hatajwi popote katika historia ya nchi? Kwanini kanisa katoliki halilalamiki kutokuwepo kwenye kitabu cha kivuko?

Yote hayo nitakushushia taratibu kadiri mnakasha huu unavyoenda.

Sasa nini kilifuata baada ya uhuru?

Nitaeleza kwakifupi tu:

Mwalimu Nyerere baada ya kukabidhiwa mamlaka kamili ya kushika dola na Malkia wa Uingereza alianza mageuzi ya kubadili mfumo huo kristu hasa mwanzoni mwa 1962 na juuhudi zilishika kasi zaidi mwanzoni mwa 1964 baada ya kuunganisha nchi ya Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa kwa Tanzania!

Juhudi hizi zilikwenda taratibu na kwa ufanisi wa hali ya juu kwakupitia hatua kadhaa ambazo ni pamoja na, kutaifisha huduma za kijamii zote zilizokuwa chini ya makanisa, kuanzisha sera ya elimu ya msingi kuwa ni ya LAAZIMA kwa watanzania wote nk, Kumbuka Mjerumani amekaa zaidi ya karne tatu akitumia mfumo kristu kutawala, Muingereza nae akalowea karne kadhaa akitawala kwa mfumo huohuo, Lakini ndani ya miongo miwili tu ya utawala wa Mwalimu Nyerere huku nchi ikitoka kwenye dimbwi la ukoloni aliweza kubadili sura na mfumo huo wa kikoloni na kuwa wawatanzania wote bila kujali dini, kabila rangi au kanda.

Naomba nimfungue macho na akili rasmi Mzee Mohamed Said huyu mpigania Dini kwa mgongo wa Uhuru wa nchi hii.
Nitaeleza kwa kifupi tu yale anayoyalilia Mohamed Said juu ya WAZEE wake.

Ukweli nikuwa kuanzia mwaka 1955 kulianza kuibuka mlengo tofauti kwa baadhi ya washarika wa ukombozi ndani ya TANU,
Hasa hasa mlengo huo ulikuwa ni kuweka itikadi ya DINI mbele, yaani iwe ndio tiketi halisi yakupigania uhuru na sio Utanganyika wao, na baada tu ya kupata uhuru, baadhi ya wazee waliokuwa beba kwa bega na Mwalimu katika harakati za kudai uhuru WALIASI rasmi sera ya Mwalimu nakuanza kuendesha vita ya chini kwa chini yakumpindua Mwalimu chini DINI.

Mwalimu Nyerere kwakutumia falsafa na malengo yake ya tangu akiwa Shule ya Tabora, Chuo kikuu Makerere na pale Scotland akiwa sambamba na wanaukombozi wasomi wenzie waliweza kuanzisha mfumo stahiki wa kufuta UDINI, UKABILA, Rangi, Ukanda na kisha Waliamua kuwafanya Watanganyika kuwa kitu KIMOJA.

Sasa mgogoro ulikuja kwa WAASI, kwakuwa hawakukubaliana na sera za Serikali mpya ya Mwalimu, wakaziidisha vurugu kwakushawishi makundi kadhaa ya kiroho yaenzi uasi huo, hilo lilipelekea serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi yao ambapo mwaka 1962 katika kiwango cha juu cha hekima za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na waambata wake, waliamua kuanzisha sheria ya kumuweka mtu kizuizini.

Sheria hii ilikuwa na mafaa kwa waasi kwani ililinda hadhi zao licha yakuwa waasi waliostahili vifungo vya maisha au kunyongwa kama ilivyokuwa destuli ya viongozi wengi wa dunia ya pili.
Mashehe wengi walitiwa kizuizini na wengine kufukuzwa nchini na makasisi wengi kupewa onyo kali.
Ifahamike kuwa hilo halikuwakumba mashehe tu kwani uasi huo ulikuwa hata kwa makasisi waliotaka itikadi zao ipewe kipaumbele zaidi na serikali ya Mwalimu Nyerere.

Kazi aliyofanya mzee Nyerere ni kubwa na alikumbana na vikwazo vingi sana kutoka kwa wakatoliki, rejea kitabu cha Van Bergen kuna barua nzito ya Mwalimu Nyerere kwenye faharasi ya 15 kwenda kwa makasisi wa kikatoliki akiwatolea karipio kuu kwakukwamisha juhudi zake, katika hii hakuchukua karne kadhaa kuumaliza mfumo uliodumu kwa mvua na mvua.

Japokuwa hakumaliza chembe za mfumo huu lakini kwangu naona ni zaidi ya 98% alimaliza, palipobaki ni mimi, wewe na wale ndio wenye dhamana ya kumalizia.

Uthabiti na tunu aliyoifanya Mzee Nyerere inathibitishwa kwa Hotuba yake ya tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Mzee Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilikuwa thabiti na yenye kuvuta nyoyo za waungwa, Baba wa Taifa Mzee Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wakiwemo Bin Amir ambae Mohamed Said anamlilia, wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Mzee Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisemakuwa "upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake":

Inakera kuona wewe Mohamed unarudisha nyuma juhudi za wanaukombozi wetu na kupandikiza chuki miongoni mwa dini hizi mbili!
Faida unayopata ni ndogo na niyakwako tu kuliko hatari inayolikumba taifa hivi leo!
Sipingi kusahihisha historia ya nchi hasa kama kuna mema yaliyoachwa lakini kupotosha na kuchochea kunatulazimisha tuhoji mamlamla za usalama wa nchi zimelala wapi? Leo mapinduzi matukufu ya Zanzibar, Mohamed Said anataka kutuaminisha kuwa Wanamapinduzi hawa wa Zanzibar waliwadhulumu waislamu wa Zanzibar na kuweka mfumo kristu anaodai upo au mfumo huo upo kwa Tanganyika tu?!

Katika kitabu chake bwana Mohamedi ametoa shutuma nyingi sana kwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo ya eti Mwalimu katika hotuba yake ya kuaga taifa alitamka wazi kuwa hamjui ABDUL SYKES, Inashangaza sana kwani Mohamed Said anajua wazi ameudanganya umma na kudhihaki wanaukombozi wetu.

Ilikujiridhisha ndugu zangu wadau pitieni sehemu ya Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya kuaga taifa tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam,
‘"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

KUVUNJWA KWA TAWA

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA?
Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

WAZEE NA MSIMAMO

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa! Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu. Huko wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

WAINGEREZA WAONGO

Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.

Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana? Nikasema inawezekana. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikwua mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.

Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.

TWAININGI AMEKWISHA

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee."’Mohamed Said kuwa mkweli, waambie ukweli watanzania (waislamu) kuwa umetumia mgongo wa Uislamu na Hayati Abdul Sykes, kwakumkashifu na kumdhihaki Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kuwasafisha wazee wako walioasi serikali mpya ya Mwalimu ambapo ndipo madhila hayo wakayapata.

Juzi nimemuuliza maswali katika mjadala flani hapa, lakini majibu yake yamenifanya nijiridhishe kuwa Mohamed Said ni muhaini na mchochezi mkubwa wa nchi hii, Ameudhihaki Uislamu nchini na duniani kote,

Nilimuuliza hivi:

Naomba unijibu maswali haya kwaufasaha mwanazuoni Mohamed Said:

1) Uliathirika vipi kwa baadhi ya wazee waliopigania uhuru wa nchi hii kutokuwemo kwao katika histori ya nchi hii kama unavyodai?

2) Taifa na waislamu waliathirika vipi kwa baadhi ya wazee unaodai wewe walipigania uhuru wa nchi hii na hawamo katika historia?

3) Ulijuaje kuwa wazee hao walipigania uhuru ilihali hawapo katika historia stahiki ya nchi hii?

4) Unaposema historia ya uhuru wa nchi hii haiwakumbuki ama haiwatambui, ulitaka wakumbukwe katika maandishi ya vitabu au katika nyaraka za serikali za historia ya uhuru wetu?

5) Unatambua kuwa historia ya nchi yoyote ile duniani huwa wapi?

6) Upeo wako umegota kwenye historia ya waislamu wa Tanganyika na Nyerere tu, au historia ya waslamu duniani kote? Kama ndivyo, je matatizo ya waislamu wa Nigeria, Somalia, Sudani, nk Nyerere ndiye kayapeleka?

7) Je ulichokiandika ni historia ya Uhuru wa Tanganyika au ni historia ya baadhi ya Waislamu wa Tanganyika na mapito yao kisiasa?

8) Kwanini unaulazimisha umma kwa maandishi yako uamini kuwa ulichoandika ndio historia sahihi ya Uhuru wa Tanganyika?

9) Je ni kweli Mohamed Said huwajui na huwatambui wale wazee 17 waliosimama kidete kudai uhuru wa nchi yetu? Je wote walikuwa wakrstu?

Naomba majibu ili tujenge hoja mpya yamjadala huu kwa mafaa ya taifa letu!Yericko Nyerere,

1) Nimeathirika kwa kuona wazee wangu hawamo katika historia kwa hiyo hawatakuwamo katika kumbukumbu kama mashujaa wazalendo waliopigana kuung'oa ukoloni Tanganyika.

2) (Hilo la taifa sina haki ya kulijibu watajibu wenyewe wenye mamlaka mimi nitawajibia Waislam). Kizazi kijacho hakitajua ushujaa wa Waislam katika kupinga dhulma kama moja ya mafunzo ya Allah. Pili hawatajua nguvu iliyokuwapo katika Uislam Tanganyika katika karne ya 20 nguvu iliyopelekea kupigana na Wajerumani katika vita vya Maji Maji 1905.

3) Babu yangu Salum Abdallah alikuwa katika African Association na TANU na aliongoza mgomo (general strike) ya 1947 Tabora na 1953 yeye na wenzake walifanya mkutano wa mwisho na wa siri wa TAA kutayarisha mjumbe Germano Pacha kuhudhuria kuasisiwa kwa TANU Dar es Salaam 7 Julai 1954. Juu ya haya alikuwa mmoja wa wafadhili wa chama. 1955 aliasisi Tanganyika Railway African Union (TRAU) akiwa mwenyekiti wa kwanza. 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82. Huu hadi leo umebaki mgomo wa kihistoria hawajaweza wafanyakazi kugoma kwa miezi 3.

4) Nilitegemea Nyerere angeliwaadhimisha katika uhai wake angalau kwa kuwataja au kuwapa heshima zao stahiki lakini akawa anakebehi juhudi za TAA na kufikia kusema kuwa hakumbuki Abdulwahid Sykes alikuwa na nafasi gani katika chama yeye alipoingia TAA Dar es Salaam mwaka 1953. (Nikawa na taarifa nyingine kuwa hakuwa anapenda Waislam wahisishwe na juhudi za kuikomba Tangnayika au yeye binafsi kuhusishwa na Abdu Sykes, Kiyate Mshumi, Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir na wengine wengi.) Kabla ya kustaafu alitoa medali 3, 979 kuwaadhimisha Watanzania walioifanyia makubwa nchi yetu. Hata mmoja katika wale waliopigania uhuru wa Tanganyika alikuwa katika ile orodha.

5) (Sijalielewa swali labda unifafanulie).

6) Najua mengi kiasi changu katika historia ya Uislam duniani lakini kitabu changu ni kuhusu Waislam wa Tanganyika.

7) Nilichoandika ni historia ya uhuru wa Tanganyika na mchango wa Waislam katika vita ile. Jina la kitabu linajieleza.

8) Huwezi kulazimisha watu sina uwezo huo nilichoandika ni historia ya wazee wangu wakati wa kupigania uhuru. Halikadhalika sina uwezo wa kulazimisha vyuo vinialike. Naalikwa kwa kuwa wameona watanufaika na elimu yangu katika somo hilo.

9) Nawatambua wote 17 na najua hadi historia zao. Kuna wengine walistahili wawepo katika ile orodha ya waasisi wa TANU lakini hakuwapo kwa kuwa mkutano usingeweza kuhudhuriwa na kila mtu. Mfano Sheikh Hassan bin Amir, Dk. Michael Lugazia, Ali Migeyo, Hamza Mwapachu na wengine wengi.

Lakini maswali mengine yamsingi yaliulizwa na wadau wengi kama Nguruvi3, Mwanakijiji na moja ya maswali yaliyonivutia ni hapa hapa chini:

By adolay:

Ninakuuliza somalia na nyerere kwasababu waislam wa somalia wanamatatizo makubwa ya kijamii, kisiasa, kieliemu, afya nk

Nani mchawi maana hapa kwetu kwa mujibu wa hadithi zako ni Nyerere. (Tunaongelea matatizo ya waislamu na wanaowahujumu)

Watanzania (Waislam, wakristu pia wa imani zingine na wasio amini) wanamatatizo aghalabu si makubwa kama ya wasomali.

1. Kwanini useme waislam wa Tanzania ni hujuma za nyerere na kwanini wasiwe waislam wa somalia? kunatofauti ya uislam wa somalia na ule wa tanzania?

2. Je katika historia yako ufahamu wako umegota Tanzania kwa hayati JK Nyerere peke yake? kama ndivyo nini ubora na ufahamu wako kujisifu mwanahistoria makini kama sio mbabaishaji?

Tafadhali rejea maswali kutushawishi kwamba wewe ni mkweli na kashifa zako dhidi ya Nyerere ni uwongo na majungu.

Tuanze na Somalia, nataka usome swali uelewe ujibu kama nilivyouliza sio kuniwekea hadithi za maandishi zisizoakisi maudhui ya swali.

1. Nani amewahujumu/aliwahujumu wasomali na uislamu wa somalia mpaka wamefikia hapa walipo je? ni nyerere

2. Ni mfumogani unatumika katika kuitawala somalia kiasi kwamba wamefika hapo walipo ilituutupie lawama

a) Mfumo kristo ndiyo maana wamefika hapo walipo

b) Mfumo islam, mahakama ya kadhi nk

c) hufahamu nakama hufahamu nini mtazamo wako.

Ninakuuliza maswali haya lengo nikutaka kuujuwa ukweli wa pengine Nyerere huyu pia yupo somalia, afghanistan, pakistani, lebanon, syria, libya nk nakwamba machafuko yote yanayoendelea huko ni hujuma za Nyerere na mfumo kristo kama unavyowapotosha watanzania na kuwachochea!

Naomba majibu ya maswali yangu hapo juu kuthibitisha kwamba wewe sio mchochezi na mchonganishi wa waislamu na wakristo kwa kubuni vitu visivokuwepo.

Mohamed Said, baada ya utangulizi huo narejerea maswali yangu ya jana kwa ufafanuzi. Angalizo jibu maswali kama yalivyoulizwa na sio siasa au funika kombe mwanaharamu apite kwa nukuu za maandishi zisizobeba maana wala majibu ya hayo maswali
MAJIBU YA MOHAMED SAID:

By Mohamed Said

Umeingiza mambo mengi sana.
Kuna Zanzibar, elimu ya Waislam, matokeo mabaya ya shule za Kiislam, kuchinja.

Itakuwa tabu kufanya mjadala uliokuwa hauna mwelekeo ulionyooka.

Lakini kwa mukhtasari ukitaka historia ya Zanzibar na maendeleo yake itabidi tuanza kwa kuvamiwa
kwa Zanzibar na jeshi mamluki la Wamakonde kutoka Kipumbwi wakifadhiliwa na utawala wa Nyerere.

Kuanzia hapa tutaingia katika tatizo la Muungano na kwa nini leo Wazanzibari wanadai nchi yao.

Kuhusu elimu ya Waislam itatubidi tuje katika njama za Nyerere kuhujumu chuo kikuu cha Kiislam
kilichokuwa kijengwe Dar es Salaam mwaka 1968 na jinsi alivyotumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS
na kuunda taasisi kibaraka BAKWATA.

Vipi shule za Waislam hazifanyi vyema inabidi tuje katika hujma ya NECTA kwa wanafunzi wa Kiislam na
tuupitie waraka wa marehemu Prof. Malima kuhusu yale aliyoyakuta Wizara ya Elimu mwaka 1987.

Wizara ya Elimu na NECTA vimegeuzwa vigango vya kanisa.

Kubwa zaidi ni kuwa Waislam kwa muda mrefu hatukuruhusiwa kujioganaizi nje ya BAKWATA kibaraka
wa serikali.

Makanisa mnaendelea kwa kupendelewa na serikali iliyojaza watendaji Wakristo sisi tungepewa hayo
mabilioni ya MoU kati ya Makanisa na Serikali tusingekuwa kama hivi.

Yapo mengi sasa chagua tuanze na lipi katika hayo hapu juu niliyokugusia.

Wajerumani waliwaweka Wayahudi katika ghetto kisha wakawa wanawalaumu kwa uchafu.
Kwenye ghetto hakuna maji wala misala sasa watu wafanyeje?

Mnatusimanga kwa hospitali mnazoendesha kwa hela ya kodi ya serikali kodi inayolipwa na raia
wote.

Tunabanwa na mfumokristo kisha mnatulaumu hatuna maendeleoMohamed said

katika pita pita zangu nimekutana na post yako hii ya tare 4 January 2013 #914

Umeongelea kunyanyaswa kwa waislamu katika elimu ni njama ya JK Nyerere - Elimu ya somalia ipo taabani sana na Nyerere hayupo huko

Nakwamba Nyerere alitumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS - lakini ghilba wala uongo wa nyerere haupo Somali na inateketea vibaya

Necta imegeuka vigango vya kanisa - Somalia haina vigango vya makanisa katika taasisi zake hususani elimu lakini ipo taabani

Serikali imejaza wakristo kwa upendeleo na kuwaacha waislam - Somalia serikali takribani yote ni waislam hakuna maendeleo

Wakristo
wanawasimanga kwa hospitali zilizo jengwa kwa kodi ya watanzania- wasomali pia wanatoa na kukusanya kodi hakuna afya bora, elem wala siasa safi!

Waislamu wanabanwa na
mfumo kristo
- Somalia kuna mfumogani unaowabana wasiendelee 

salmar

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
799
500
Mwandishi wa uzi huu udini na kutojua historia ya zanzibar ndio ulokupelekea kuandika pumba zako soma kitabu kinachoitwa uhasidi wa marekani kwa mapinduzi ya zanzibar. Kilichotungwa na giorgio galinoshadjivayansi na abdulrahman babu ndio utajua ukweli wote otherwise u havo no right to question any thng about zanzibar
 
Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,801
2,000
Mwandishi wa uzi huu udini na kutojua historia ya zanzibar ndio ulokupelekea kuandika pumba zako soma kitabu kinachoitwa uhasidi wa marekani kwa mapinduzi ya zanzibar. Kilichotungwa na giorgio galinoshadjivayansi na abdulrahman babu ndio utajua ukweli wote otherwise u havo no right to question any thng about zanzibar

Umeelewa Mada hii na umeshasoma maandiko ya Mohamed Saidi?
 
wimbi la mbele

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
647
195
Guaranteed 250 pages

safi sana JF

Ila nakuonea huruma sana bwana Yeriko, mwenzako Mohammed akiongea anawakilisha vielelezo, je wewe una nini za ku counter argue?

Nyerere na Mkapa wote ni marais ambao walishakiri kuwa kweli hakuna uwiano sawa na waislam hawakupata their equal share sasa wewe una ushahidi gani wa ku counter argue?

Pia kabla hatujaenda mbali unajibuje kuhusuhili:

Attachments

  • MEMO333.jpg
    File size
    109.4 KB
    Views
    26,771

Bwaga ya moyoni

Senior Member
Aug 21, 2012
148
195
Binafsi hua sipendelei hata kidogo tabia yakusema soma kitabu fulani upate ukweli fulani. Hautusaidii hata kidogo. Hakuna msomi hata mmoja duniani aliemaliza vitabu vyote duniani. Vitabu nilivyovisoma mimi kwenye fani yangu ni tofauti na vile ulivyovisoma wewe kwenye fani yako na ni tofauti na alivyovisoma mleta uzi kwenye fani yake na pia alivyovisoma Nadhani kwenye fani yake n.k. so wewe uliyekisoma hicho ambacho mleta uzi hajakisoma, basi tuletee yaliyomo ndani yake ili nasisi tuweze ku-judge who is saying the truth. Tuletee hayo tupate kuelewa kama yaliyomo humo yana-support haya aliyoyasema Mohamedi Saidi na kama kweli huyu jama ni mchochoze kama inavyodaiwa na mleta uzi. Hayo ndio mabishano ya hoja yanavyokwenda. Otherwise, sisi tunalichukulia kuwa na wewe huna hoja ya kuizima hii ya mleta uzi na umeamua kuizima the machiavellian way.

Mwandishi wa uzi huu udini na kutojua historia ya zanzibar ndio ulokupelekea kuandika pumba zako soma kitabu kinachoitwa uhasidi wa marekani kwa mapinduzi ya zanzibar. Kilichotungwa na giorgio galinoshadjivayansi na abdulrahman babu ndio utajua ukweli wote otherwise u havo no right to question any thng about zanzibar
 
Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,801
2,000
Guaranteed 250 pages

safi sana JF

Ila nakuonea huruma sana bwana Yeriko, mwenzako Mohammed akiongea anawakilisha vielelezo, je wewe una nini za ku counter argue?

Nyerere na Mkapa wote ni marais ambao walishakiri kuwa kweli hakuna uwiano sawa na waislam hawakupata their equal share sasa wewe una ushahidi gani wa ku counter argue?

Mkuu,
1) Maswali 9 niliyouliza yanamsingi mpana wa kumleta Mohamed kuyatetea maandshi yake!

2) Unasema Mkapa na Kikwete waliwahi kutoa maelezo yenye kuthibitisha kiile ukiaminicho,

Swali:

A) Walitoa kupitia takwimu zipi?

B) Walitolea wapi?

C) Walisema kama marais au walisema kama wao tu?

NB: Nafadhaika sana kusikia mtu anasema fulani alisema hivi, au alisema vile! Nafarijika sana mtu akija na ushahidi usiiotiliwa shaka kwa hoja yake!
 
wimbi la mbele

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
647
195

Issue hapa inatokana na Dhana ya Serikali kutokuwa na Dini au Serikali ya Kisekula Dhana hiyo ni maarufu Tanzania. Mara nyingi katika masuala yahusuyo dini, viongozi wa serikali husikika wakisema «serikali haina dini, ila wananchi wake wana dini zao ». Hoja ya usekula wa serikali ni ya kihistoria. Ilijengwa kiasi cha miaka miambili iliyopita ikitaka serikali ijiepushe na shughuli za kidini hususan katika masuala ya elimu, mafundisho ya maadili na na ibada.Japokuwa Tanzania imekuwa ikidai kwamba serikali yake ni ya kisekula, hali halisi haioneshi hivyo. Pamoja na madai hayo, serikali ya Tanzania imewahi kuingia katika msuguano na Waislamu na baadhi ya wasiokuwa waislamu pale Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipotaka kuanzisha somo la dini au maadili ya nchi. Kadhia hii ni maarufu kwa jina la "dini mseto". serikali ya kisekula haiwezi ikaja na mipango ya kusomesha dini kwa jina lolote lile liwe la maadili au vyovyote vile.

Mifano mingine inayotia wasiwasi usekula wa serikali ya Tanzania ni hii ifuatayo:

1. Wimbo wa Taifa – unaomba mungu aibariki nchi

2. Dua ya Bungeni – ina muomba mungu

3. Kuapishwa kwa wanaochukua nafasi za uongozi.
Japo wanaoapa huapa kwa dini zao, aneapishasi kiongozi wa dini husika bali wa serikali au wabunge.

Utaratibu huo hauendani na madai kuwa nchi au serikali ya Tanzania haina dini, bali wananchi wake ndiyo wenye dini. Swali ni je, tunapomtaja Mungu katika wimbo wa taifa au katika dua ya bungeni, na kadhalika, tunamkusudia mungu yupi? Mungu wa Waislamu? Wa Wakristo? Wa dini za asili? Je, kuna mungu wa kitaifa? Mungu huyo wa kitaifa ni yupi na ni wa dini gani?Je, katika hali hiyo, ni kweli serikali haina dini? Katika mazingira ya Waislamu kuandamwa na kukandamizwa na mila ya Mfumokristo, mfumo ambao unajidhihirisha zaidi katika vitendo vya kibaguzi vinavyofanyiwa Waislamu na sehemu kubwa ya watendaji serikalini na katika taasisi mbalimbali, kwa nini mwananchi Muislamu asiamini kuwa serikali hii si ya kisekula bali ni ya kidini; na dini yenyewe ni Mfumokristo.

According to TRA / HAZINA....

Mbinu zinazotumiwa na Mfumokristo katika Kujihakikishia Fursa Tanzania

Mfumokristo ni hali ambayo Wakristo wa Tanzania wamehodhi madaraka ya ngazi zote muhimu katika serikali na katika vyombo vya maamuzi, na kuzitumia nafasi hizo kuwaendeleza Wakristo na Ukristo na kuwabagua Waislamu na dini yao.

1. Kuendeleza mfumo wa kibaguzi katika elimu kama ulivyoachwa na wakoloni.
Wakoloni wa kijerumani ndio walioanzisha mfumo wa kuwabagua Waislamu katika elimu baada ya kushinikizwa na makanisa. Ushahidi wa mashinikizo hayo unaweza kupatikana katika rejea zifuatazo: Cameroon and Dodd 1970:56, Kurtz1972:19, Smith 1963:16. Hatimaye kutokana na mashinikizo hayo serikali ilikubali kufaya yafuatayo:-

i. Kuwafukuza kazi Waislamu waliokuwa serikalini na kuwaingiza Wakristo (Tazama Cameroon and Dodd1970: 25, 56, pia Roland 1970:205)

ii. Kuzipa shule za wamisheni msaada wa kifedha kutoka kodi za wananchi huku wakizibagua zile za Waislamu (Tazama Roland: 1970: 205,na Cameroon and Dodd 1970:50)

iii. Kuweka mpango mkakati wa kuwabagua na kuwahujumu Waislamu na Uislamu wao. Tazama Roland 1970:205, Kurtz 1972:29. Cameroon and Dodd 1970:114.

iv. Kujenga hoja kwamba Waislamu kwa asili yao si watu wa kuendelea na kuwa ni wavivu. Tazama E.B Castle 1966:37 ambaye anasema, " Islam hinders progressive attitude to change in society and a community that accepts Islam is less likely to advance in social welfare and education", yaani Uislamu ni kikwazo cha fikra za maendeleo na mabadiliko katika jamii, na kwamba jamii ikiukubali Uislamu haiwezi kamwe kupiga hatua za katika ustawi wa na elimu. Pia Abel Ishumi 1980:208 anasema, "From the beginning Muslims were opposed to western type formal education", Kwamba Waislamu walipinga elimu. Pia Abel Ishumi 1981:43, "Muslims believe highly in fatalism" Kwamba Waislamu wanabweteka na kuamini kwao kuwa mambo yameshakadiriwa.

2. Kuhujumu taasisi za Waislamu na kuweka viongozi mamluki.

Baada ya uhuru Serikali ya Tanzania imekuwa na muelekeo wa kuziandama taasisi zinazoonekana kuwa na mipango madhubuti ya kuwakomboa Waislamu kuondokana na ujinga na umaskini. Rejea Bergan 1981:26 na Sivalon 1992:3 kuhusu kuvunjwa kwa EAMWS na kuanzishwa kwa BAKWATA. Pia soma Anuur na. 13 la Agosti 1992 juu ya taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ya kuitaka Serikali kuifuta EAMWS. Pia tazama Njozi 2000:31. "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania kuhusu kadhia ya kuvamiwa kwa Msikiti wa Mwembechai na hatimaye kuuliwa kwa Waislamu.3. Kuhodhi mfumo wote wa elimu nchini.

Tangu kuondoka kwa Mkoloni Wakristo wamekuwa kama mabaki ya wakoloni na ukoloni. Ukiondoa shule za msingi na sekondari za Kata, huko katika shule za sekondari za Serikali, vyuo vya kati na vyuo vikuu wanafunzi na wafanyakazi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80. Siku hizi katika shule za Kata wanafunzi Waislamu wameanza kuonekana. Katika taasisi za elimu mfano T.I.E, TEA, NECTA, Bodi ya Mikopo, I.A.E na vyuo vyote nchini, uongozi umekuwa ni mali ya Wakristo.Huko mwanzo walidai kwamba hamna Muislamu mwenye elimu ya kutosha kuongoza. Kwa siku za hivi karibuni madai yao kwa wale Waislamu wachache waliofanikiwa kupata elimu ni kuwa hawafai kwa vile wana, "udini".Aidha katika Wizara ya Elimu (MOEVT) tangu Wizara hiyo kuundwa uongozi umekuwa mali ya Wakristo kwa zaidi ya asilimia 90. Nafasi kama ya Kamishina wa Elimu haijawahi hata kuwa na Kaimu Muislamu na wala haitarajiwi chini ya Mfumochristo. Nafasi zawakurugenzi nazo zimemilikiwa na Wakristo. Mfumokristo umejikita barabara.

Uongozi wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu nao umemilikiwa vilivyo. Nafasi za Maafisa elimu Wilaya na Mikoa na wakaguzi wakuu wa elimu wa Kanda kwa zaidi ya asilimia 85 zinaendelea kuwa miliki ya hawa Wakristo.Mfumokristo ni hali ambayo Wakristo wa Tanzania wamehodhi madaraka ya ngazi zote muhimu katika serikali na katika vyombo vya maamuzi, na kuzitumia nafasi hizo kuwaendeleza Wakristo na Ukristo na kuwabagua Waislamu na dini yao.

1. Kuendeleza mfumo wa kibaguzi katika elimu kama ulivyoachwa na wakoloni. Wakoloni wa kijerumani ndio walioanzisha mfumo wa kuwabagua Waislamu katika elimu baada ya kushinikizwa na makanisa. Ushahidi wa mashinikizo hayo unaweza kupatikana katika rejea zifuatazo: Cameroon and Dodd 1970:56, Kurtz1972:19, Smith 1963:16. Hatimaye kutokana na mashinikizo hayo serikali ilikubali kufaya yafuatayo:-

i. Kuwafukuza kazi Waislamu waliokuwa serikalini na kuwaingiza Wakristo (Tazama Cameroon and Dodd1970: 25, 56, pia Roland 1970:205)

ii. Kuzipa shule za wamisheni msaada wa kifedha kutoka kodi za wananchi huku wakizibagua zile za Waislamu (Tazama Roland: 1970: 205,na Cameroon and Dodd 1970:50)

iii. Kuweka mpango mkakati wa kuwabagua na kuwahujumu Waislamu na Uislamu wao. Tazama Roland 1970:205, Kurtz 1972:29. Cameroon and Dodd 1970:114

iv. Kujenga hoja kwamba Waislamu kwa asili yao si watu wa kuendelea na kuwa ni wavivu. Tazama E.B Castle 1966:37 ambaye anasema, " Islam hinders progressive attitude to change in society and a community that accepts Islam is less likely to advance in social welfare and education", Yaani Uislamu ni kikwazo cha fikra za maendeleo na mabadiliko katika jamii, na kwamba jamii ikiukubali Uislamu haiwezi kamwe kupiga hatua za katika ustawi wa na elimu. Pia Abel Ishumi 1980:208 anasema, "From the beginning Muslims were opposed to western type formal education", Kwamba Waislamu walipinga elimu. Pia Abel Ishumi 1981:43, "Muslims believe highly in fatalism" Kwamba Waislamu wanabweteka na kuamini kwao kuwa mambo yameshakadiriwa.

2.
Kuhujumu taasisi za Waislamu na kuweka viongozi mamluki. Baada ya uhuru Serikali ya Tanzania imekuwa na muelekeo wa kuziandama taasisi zinazoonekana kuwa na mipango madhubuti ya kuwakomboa Waislamu kuondokana na ujinga na umaskini. Rejea Bergan 1981:26 na Sivalon 1992:3 kuhusu kuvunjwa kwa EAMWS na kuanzishwa kwa BAKWATA. Pia soma Anuur na. 13 la Agosti 1992 juu ya taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ya kuitaka Serikali kuifuta EAMWS. Pia tazama Njozi 2000:31. "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania kuhusu kadhia ya kuvamiwa kwa Msikiti wa Mwembechai na hatimaye kuuliwa kwa Waislamu.

3.
Kuhodhi mfumo wote wa elimu nchini. Tangu kuondoka kwa Mkoloni Wakristo wamekuwa kama mabaki ya wakoloni na ukoloni. Ukiondoa shule za msingi na sekondari za Kata, huko katika shule za sekondari za Serikali, vyuo vya kati na vyuo vikuu wanafunzi na wafanyakazi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80. Siku hizi katika shule za Kata wanafunzi Waislamu wameanza kuonekana. Katika taasisi za elimu mfano T.I.E, TEA, NECTA, Bodi ya Mikopo, I.A.E na vyuo vyote nchini, uongozi umekuwa ni mali ya Wakristo. Huko mwanzo walidai kwamba hamna Muislamu mwenye elimu ya kutosha kuongoza. Kwa siku za hivi karibuni madai yao kwa wale Waislamu wachache waliofanikiwa kupata elimu ni kuwa hawafai kwa vile wana, "udini". Aidha katika Wizara ya Elimu (MOEVT) tangu Wizara hiyo kuundwa uongozi umekuwa mali ya Wakristo kwa zaidi ya asilimia 90. Nafasi kama ya Kamishina wa Elimu haijawahi hata kuwa na Kaimu Muislamu na wala haitarajiwi chini ya Mfumochristo. Nafasi za wakurugenzi nazo zimemilikiwa na Wakristo. Mfumokristo umejikita barabara. Uongozi wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu nao umemilikiwa vilivyo. Nafasi za Maafisa elimu Wilaya na Mikoa na wakaguzi wakuu wa elimu wa Kanda kwa zaidi ya asilimia 85 zinaendelea kuwa miliki ya hawa Wakristo.

4. Kukataa kutunga sera za kuondoa upendeleo wa Wakristo katika elimu na kuendeleza ulaghai dhidi ya wananchi wasiokuwa Wakristo. Mara baada ya uhuru ilielezwa na viongozi wetu akiwemo Mwl. Nyerere kuwa serikali itachukua hatua kuondoa mpango ulioasisiwa na Wakoloni wa kuwabagua Waislamu. (tazama A. Jumbe 1994:123, Court 1976 na Nyerere in Hansard Desemba 10, 1962). Badala yake hatua zilizochukuliwa hazikulenga kuondoa tatizo la ubaguzi wa kidini katika elimu nchini na kuwaondoa pia katika ajira na madaraka.Mfano wa hatua hizo ni pamoja na:

i. Kufuta ada shule za msingi na sekondari miaka ya 1960/70.

ii.
Kuweka kikomo cha elimu ya msingi kuwa miaka 7 bila kusita.

iii. Kuondoa mitihani ya darasa la 4 na 5. iv. Kuanzishwa kwa mpango wa UPE.

v. Kujenga shule za msingi za bweni kwa watoto wa wafugaji na wavuvi wanaoishi kwa kuhamahama

vi. Kutaifisha shule za binafsi zilizokuwa chini ya mashirika ya dini na watu binafsi. Mpango huu haukuhusisha seminari za Wakristo.

vii.
Kupeleka wanafunzi sekondari kwa kigezo cha KUCHAGULIWA badala ya KUFAULU kulikoendana na kuyafanya matokeo ya mtihani wa darasa la saba kuwa ni siri.

viii.
Kuanzishwa utaratibu wa "quota system" ambapo kila mkoa ulipangiwa idadi ya wanafunzi watakaochaguliwa kwenda sekondari.

ix. Kuweka utaratibu mgumu wa kuanzisha na kuendesha shule binafsi chini ya sheria ya elimu ya mwaka 1978, hivyo watu wote kulazimika kusoma katika shule chache za sekondari za Serikali

x. Kuanzishwa kwa shule maalum za vipaji katika miaka ya tisini mfano: Kibaha, Kilakala, Ilboru, n.k.

xi.
Kutoa upendeleo maalum (Affirmative Action) kwa watoto wa kike kuingia sekondari na vyuo. Aidha kuwepo pia kwa mipango ya kuwasomesha watoto wa kike kutoka familia maskini.

xii. Ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata. Sera hizi zote pamoja na nyinginezo hazikusaidia kuondoa uwiano mbaya au ubaguzi wa elimu kwa Waislamu. Tuangalie mfano michache ifuatayo: Ni ukweli usiopingika kwamba UPE awamu ya kwanza iliyosukumwa na UNESCO na awamu ya pili iliyosukumwa na Malengo ya Milenia (MDGs) na Mpango wa Elimu kwa wote (EFA) zimesaidia kuwahakikishia watoto wengi wa Kiislamu elimu hiyo ya msingi. Lakini sera hii ilikuja katika kipindi ambacho elimu ya msingi haikuwezi tena kumpatia mtu ajira katika sekta rasmi na hata ile ya binafsi.

Ikumbukwe kwamba katika kipindi hicho cha miaka ya 60 hadi 2000 nafasi za masomo ya sekondari ziliendelea kuwa haba. Wakati wote huu watoto wa Kikristo ndiyo walioendelea kufaidika na elimu ya sekondari. Masomo hayo ya sekondari hatimaye yaliwapatia fursa za kuingia vyuo vikuu na hivyo kuwa katika nafasi za kuajiriwa serikalini, kuteuliwa katika vyeo na nyadhifa mbalimbali huku Waislamu waliowaacha shule za msingi wakiambulia ajira za usafi na utarishi.

Naam, Mfumokristo umefanikiwa kuwafanya Wakristo kuwa warithi wa wazungu wakoloni na kuwaacha Waislamu katika hadhi lie ile waliokuwa nayo wakati wa ukoloni. Aidha kutaifishwa kwa shule hakujasaidia Waislamu kupata elimu ya sekondari kama inavyodaiwa kuwa Nyerere alitaifisha shule ili Waislamu wasome.

Kama tulivyoona awali kuwa tangu wakati wa Mjerumani serikali ya kikoloni ilikuwa ikitoa pesa kusaidia ujenzi na uendeshaji wa shule za Wakristo ni dhahiri kuwa shule hizi zilikuwa zimeshalemazwa na pesa za serikali kwa kipindi cha miaka 55, tangu mwaka 1914 hadi mwaka 1969 zilipotaifishwa. Tazama maandiko ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki (TEC) Fr Robinson, D.W 1965:14 kwamba, "The Church is now totally dependent on State aid for the administration of these schools. If this aid were withdrawn the church will be forced to close its schools"

Yaani, Kwa sasa Kanisa limekuwa tegemezi kabisa kwa serikali katika kutoa pesa za kuendesha shule zake na ikiwa serikali itasita kutoa fedha kwa shule hizi basi Kanisa litalazimika kuzifunga. Ni dhahiri basi kwamba hatua aliyochukua Julius Nyerere ilikuwa na malengo makuu ya kuziokoa shule za Kanisa kufungwa kwa sababu ingekuwa jambo la kiroja kwa serikali ya Tanzania kuendelea kutoa pesa za kuendesha shule za Kanisa kwa wakati ule, na pili kuhakikisha kwamba malengo ya shule zile ya kuwasomesha Wakristo yanaendelea kutekelezwa kwa kutumia pesa za umma.

Kimsingi kilichobadilika ni jina la mmiliki tu uongozi na malengo ya shule yalibaki vile vile. Ndiyo maana hakuna mtu yoyote aliyethubutu au atakayethubutu kudai eti kwamba ukienda katika shule zilizotaifishwa mfano, Pugu, Minaki, Tambaza, Zanaki, Jangwani, Kibasila, Ilboru, Weruweru, Tosamaganga, Msalato, Umbwe, Ndanda n.k, utakuta idadi ya kuridhisha ya wanafunzi Waislamu wanaosoma huko. Lakini hata katika shule za sekondari chache mpya ambazo serikali ilijenga au kujengewa mwishoni mwa miaka ya 70, kama vile: Kibiti, Ruvu, Karatu, Bagamoyo n.k , kote walimu, wafanyakazi na wanafunzi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80.

Watoto wachache wa Kiislamu wanaosoma huko huonekana kama wakimbizi wanaosaidiwa katika nchi ya ughaibuni. Kuhusu kuingia sekondari kwa kigezo cha kuchaguliwa na mpango wa quota system, watendaji Wakristo waliojazana katika mfumo wa elimu nchini wamekuwa wakihakikisha kwamba Waislamu hawasomi kutokana mbinu zifuatazo:-

i. Kufanya matokeo ya darasa la saba kuwa ni siri hivyo kuweza kuibadili nafasi walizoshinda Waislamu na kuwapa wengine. Tazama ushahidi mzito uliotolewa na Njozi mwaka 2000; katika kitabu cha Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania uk. wa 62 -70. Hapa vijana wa Kiislamu waliofaulu darasa la saba walinyimwa nafasi kuingia sekondari na wale waliofaulu kidato cha nne walinyimwa kuingia kidato cha tano. Kazi hii ya kuwakwamisha vijana wa Kiislamu ilifanywa vyema na mawakala wa Mfumokristo waliojazana katika mfumo wote wa elimu nchini.

ii. Kuhamisha wanafunzi Wakristo kutoka maeneo yenye ushindani mkubwa kwenda Mikoa iliyokuwa na alama ndogo za kuchaguliwa kama Pwani, Dar, Lindi, Mtwara na Tanga ambayo pia ni maeneo ya Waislamu . Tazama Malekela 1983 in "Access to secondary education in Sub- Sahara Africa"

iii. Huko nyuma kabla ya wanafunzi kupangiwa shule za sekondari namba zao za mtihani ziliambatanishwa na majina ili kujua nani Mkristo apendelewe na nani siyo awachwe iv. Kuhakikisha kwamba viongozi na watendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) wote ni Wakristo. Aidha kwa asilimia kubwa kabisa watungaji wa mitihani na wasahihishaji pia ni dini hiyo hiyo. Tazama kitabu cha Miaka Thelathini ya NECTA, 2004 au www.necta.ca.tz

antoniozagarino

Senior Member
Apr 16, 2012
143
250
DAIMA udini huendekezwa na watu wenye mawazo ya kimaskini, watu hawataki kwenda shule, tazama matokeo ya form 2 shule za kiislam zilivyofeli mawka huu, sasa hawa ndo wakija kukua wanaanza kusema nyerere mchawi kawaonea, hivi mmeona shule za wakatoliki wameshika kumi bora kwa 50% pia mmeona na majina ya watoto hao kumi bora ni ya KIKRISTU. Hii inaakisi kwamba hata form 4, 6 na elimu ya juu, itakuwa hivyohivyo, mtalaumu nyerer weeee na umaskini wa MALI na maazo vitawatafuna mpaka KABURINI
 
sweke 34

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
694
0
Guaranteed 250 pages

safi sana JF

Ila nakuonea huruma sana bwana Yeriko, mwenzako Mohammed akiongea anawakilisha vielelezo, je wewe una nini za ku counter argue?

Nyerere na Mkapa wote ni marais ambao walishakiri kuwa kweli hakuna uwiano sawa na waislam hawakupata their equal share sasa wewe una ushahidi gani wa ku counter argue?

.......

By Mohamed Said

Ndugu yangu mimi nakuomba katika hili mimi unisamehe.

Ila kama kweli una haja ya kupata ukweli nenda kazungumze na wahusika Wizara ya Elimu watakupa taarifa ya kitabu changu.

Oxford wana ujuzi wa miaka mingi katika mambo haya.

Huwa hawachapi na kufanya ''recommendation'' ya kitabu hadi kimepita kwa wataalam wake wake mahiri.

Mkurugenzi Mkuu wa Oxford University Press amewaandikia barua kadhaa.
Ikiwa zipo watakuonyesha.

Hawakuwa wanajibu.
Naomba niishie hapa.
 
Sideeq

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
2,422
0
Nimezungumza kama mtanzania yeyote yule anaekereka na uchochezi wa Mohamed Said,
Sijabeba undugu damu katika hili.
Si kweli! vitendo vyako vipo wazi.
...unatafuta pa kutokea! kwanza ulimdandia mwanasiasa kijana wa chama tawala ili akupe mdahalo, akakushtikia na kukutosa, sasa unaona njia ya kutokea ni kupitia Mohamed Said.

Kama Mohamed Said atakujibu basi itakuwa amekufanyia hisani sana, vizuri kawalete Maaskofu waje hapa na majina yao kamili (kama Mohamed Said anavyojiamini na jina lake kamili) ili waingie mdahalo na Mohamed Said, si wewe Yericko.
 
mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
1,195
DAIMA udini huendekezwa na watu wenye mawazo ya kimaskini, watu hawataki kwenda shule, tazama matokeo ya form 2 shule za kiislam zilivyofeli mawka huu, sasa hawa ndo wakija kukua wanaanza kusema nyerere mchawi kawaonea, hivi mmeona shule za wakatoliki wameshika kumi bora kwa 50% pia mmeona na majina ya watoto hao kumi bora ni ya KIKRISTU. Hii inaakisi kwamba hata form 4, 6 na elimu ya juu, itakuwa hivyohivyo, mtalaumu nyerer weeee na umaskini wa MALI na maazo vitawatafuna mpaka KABURINI

Nadhani hapo juu umedadavuliwa vya kutosha katika sakata la Baraza la Mitihani kwamba limekua kama PAROKIA la Dini fulani, sasa kwa matokeo kama hayo yanayoendelea kutolewa na MOEVT, wewe ukiwa kama MKIRISTO na kwa mfano Baraza hilo lingelikua limesheheni Waislamu kama lilitapika Wakristo sasa; je kwa upande wako wewe ungejenga dhana gani? Na je kwa mfano ungelikua unalilalamikia Baraza hilo (ambalo lingekua limerundikiana Waislamu) kungekua kuna makosa?

Ingelikua upo makini katika kusoma hoja na majibu yanayotolewa usingelithubutu kuweka utumbo kama huu hapa!
 
Hata waziri/naibu wa elimu/wakurugenzi wote baraza la mitihani/necta/watungaji/wasahihishaji mitihani wote wangekuwa ni waislam, bado waislam mngeendelea kulalama kuna mfumo kristo. Mkristo hana sababu ya kulalamikia NECTA ukizingatia mitihani ipo pale karibu mwaka mzima baada ya kusahihishwa...kama umeonewa ni suala la kuappeal tu...
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom