Uchina kutukabidhi kijiti cha Maendeleo - W.Mpango (CCM)!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kulingana na Waziri wetu wa Fedha Waziri Mpango (CCM), ni kwamba sasa tunajipanga kwenye kila kona ili Uchina waweze kutukabishi kijiti cha maendeleo ya ngazi ya kati ambapo nchi hiyo sasa inajiandaa ktk huko yaani kutoka kwenye uchumi wa kipato kidogo kwenda kwenye uchumi wa kipato cha juu!

Hivyo basi kama ilivyokuwa nchi wa Uchina wakati wanaanza nchi nyingi zenye Viwanda vingi ktk Dunia nzima viliwekeza huko na moja sababu kubwa ni pamoja na nyingine ni low cost za kufanya biashara Uchina ilikinganishwa na nchi zilizoendelea!

Sasa kulingana na Waziri Mpango(CCM) sisi tunajiandaa vizuri kabisa kuweza kupokea hicho kijiti kutoka Uchina, Uwezo tunao, nguvu tunazo, sababu tunazo na NIA TUNAYO kuivusha TanZania!
 
Huwa najiuliza sana kwann ccm wana mahusiano mazuri hivi na nchi ya China. Nakosaga majibu
Sema sasa serikali baadhi ya wachina wasio na nia njema muwamulike maana ma dili mengi haram wachina wanahusika kuanzia ya pembe za ndovu
 
Wakumulikwa wasiwe wachina pekee ila kila mmoja anaevunja sheria. Kwani walioangusha helicopter ya patrol mbugani juzijuzi wakamuua pilot walikuwa ni wachina. Uhalifu hauna kabila ila ni juu ya vyombo vyetu vya usalama kutimiza majukumu wananchi tukiwapa support kubwa.
 
Viongozi wanataka msaada upite mikononi kwao ndo taratibu nzur mzungu siku izi kutokana na anguko la uchumi na wanapenda kutoa msaada ili wapate baraka kwa mungu na wengine wanatoa kwa kafala ili wapate hela kwa shetani so wanaona wanatukanwa kua wanyonyaji uku wanaotunga izo nyimbo za unyonyaji ndo wanaodaka hela so wanaingia wenye kufanya research na kutoa kiasi na kusimamia kabs ikiwezekana na kusimamia project nzima wachina wanatoa mkwanja cash bila maswal mengi wa proposal sema ngapi nikupe we utanipa nn kina masirahi fresh tufanye kaz
 
Kama ni waziri wa fedha anayejua uchumi watanzania tumempata. Sema ni wachache wanaweza kutokuona umuhimu wa watu kama Dk Mpango.
 
Back
Top Bottom