Uchimbaji wa mabwawa ya maji kwa kweli ungeanza mara tu tulipopata uhuru. Lakini hakukuwa na mwenye maono hayo

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,586
1,678
Kwanza nimpongeze Waziri Bashe kwa kuona umuhimu mkubwa wa hili. Waziri Bashe ni mmoja katika Mawaziri wachache wenye maono kwenye serikali yetu na naomba asichafuliwe aendelee, kwani Tanzania kila afanyaye vizuri atatafutiwa mkwara.

Uchimbaji wa mabwawa ya maji kwa kweli ungeanza mara tu tulipopata uhuru. Lakini hakukuwa na mwenye maono hayo. Au tuseme, ungeendelea baada ya kupata uhuru, maana Wakoloni walichimba mabwawa kadhaa lakini yakaachwa yaharibike.

Mojawapo ni bwawa la Mabatani pale Muheza, Mkoa wa Tanga. Kwa hakika hadi mwisho wa miaka ya 80, bwawa hili lilikuwa chanzo cha maji ambapo hakukuwa hata na siku moja ukakuta Muheza haina maji.

Pia lilikuwa chanzo cha samaki, mandhari mazuri na ndege ziwa. Ila misingi mibovu ya bwawa kutokana na ukosefu wa ukarabati, ilipozolewa na maji bada ya mvua kuu miaka ya 80, basi bwawa limetoweka hadi leo.

Waziri Bashe namtarajia alitie bwawa hilo katika mahesabu yake, kama si bajeti hii ijayo. Lina manufaa mengi hata kwa watu waishio upstream, kilomita hamsini kutoka Muheza.
 
Back
Top Bottom