James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Afrika kabla ya kutawaliwa tulikuwa na mila na desturi zetu. Wakati huo hatukuwa na dini kama vile uislam na ukrito lakini tulikuwa na njia zetu wenyewe za kuomba kitu fulani kitokee au kujiepusha na janga.
Haya mafundisho ya dini kubwa za leo yaliletwa na mabeberu. Na unajua baada ya kutuletea hivyo "vitabu vitakatifu" walitufanya nini? Walitufanyia mambo yote yanayokatazwa na hivyo vitabu vyao kama kututesa na kutudhalilisha.
Binafsi nimezaliwa na kukuzwa katika moja ya hizi dini za mabeberu. Hata hivyo sasa hivi nimekua nafuata hiyo dini kama utamaduni tu niliokuwa nao. Kwa maana nyingine ni kama mfumo tu wa jinsi ya kufanya vitu. Kwa mfano, kama mtu akitangulia mbele ya haki basi mwili wake husitiriwa kwa namna fulani. Au mtu akioa, pia kunakuwa na taratibu zake za kuwatambulisha mume na mke kwa ndugu na marafiki.
Kwasababu Watanzania wengi tumekulia kwenye mazingira ya Uislam na Ukrito, kwa maoni yangu hakuna madhara tukiendelea kufuata tamaduni zake. Bado tunaweza kuendelea kufuata tamaduni za Uislam au Ukristo kwenye mambo kama vile maadili, misiba na harusi lakini haina maana tusahau mila zetu.