Uchenjuaji wa dhahabu kwa ajili ya hifadhi BoT kuanza

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1573198225120.png


TANZANIA sasa itaanza kuchenjua na kusafi sha dhahabu kwa ajili ya kuhifadhiwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa lengo la kulinda uchumi wa nchi. Usafishaji wa dhahabu ni moja ya hatua muhimu ambazo serikali ya awamu ya tano imezifanya katika kuboresha sekta ya madini.

Akizungumza katika Jukwaa la Uziduaji lililofanyika jana katika Wiki ya Azaki jijini hapa, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema dhahabu hiyo itawekwa katika vifurushi vya kilogramu moja, kumi na 100. Alisema mtindo huo wa kuweka dhahabu BoT kama akiba husaidia uchumi ukiyumba kuimarisha kwa kuuza akiba hiyo.

Naibu Waziri huyo alisema hata Uingereza ikiwa katika mpango wake wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya ili kuuza dhahabu ambayo kwa sasa imepanda bei katika soko la kimataifa. Nyongo alisema pia katika kusafisha dhahabu serikali inakusudia kujenga mtambo wa kusafirisha jijini Dodoma na baadaye mtambo mwingine mkoani Geita kwa lengo la kusafisha dhahabu hapa nchini.

Alisema pia wizara hiyo ipo mbioni kuanzisha Mfuko wa Wachimbaji Wadogo ili kuhakikisha kwamba wanakuwa na mfuko wao, wakati ikiandaa mikakati ya kuwa na mfumo maalumu kwa ajili ya wachimbaji. Alisema kuanzishwa kwa masoko ya madini 38 nchini, alisema serikali imepata mafanikio makubwa kwa kuongeza uuzaji wa dhahabu katika masoko hayo.

Akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali, Donald Kassongi alisema Jukwaa hilo la Uziduaji 2019, linalenga kuwapa fursa wadau kujadiliana na serikali namna gani sekta za gesi, nishati Tanzania zinaweza kusaidia wananchi kuwapa maendeleo.

Chanzo: Habari Leo
 
Hivi mimi binafsi nikianza kununua dhahabu na kuzitunza inaruhusiwa au ndo nitakuwa mhujumu uchumi?
 
Hongera Rais Magufuli kwa kusimamia raslimali za Nchi

Tunajivunia kuwa na Rais Mzalendo
 
Back
Top Bottom