Ucheleweshaji wa mikopo elimu ya juu baadhi ya vyuo.

Boko halal

Senior Member
May 14, 2014
175
124
Naikumbuka kauli ya mh rais kipindi Rais kampeni kuhusu wanafunzi kucheleweshewa mikopo yao na alisisitiza kabisa kuwa akiwa rais mikopo itapatikana kwa urahisi, ni takribani wiki mbili zimepita tangu vyuo vikuu vifunguliwe lakini mpaka sasa pesa toka HESLB haijapelekwa vyuoni huku wanafunzi wakiendelea na masomo wakiwa na njaa.

Mh Waziri wa fedha na waziri wa elimu tunaomba mfuatilie hili suala la pesa za kujikimu kwani wanafunzi wengi wana hali mbaya sana kutokana na kucheleweshewa fedha hizo.
 
Kuna mdogo wangu anasoma Saut Tabora amenipigia simu akiniomba chochote nikajua anathibitisha anataka kunipiga kumbe hawajapata pesa "pesa yenyewe mkopo kwanini umcheleweshee mtu " in Magu's voice
 
hivi vyuo vya mikoani kwa nini mnasumbuliwaa sana sisi wa huku joto city ni raha tuu ..juzi tumetia sahihi kuanzia jumatatu kitu kinasomaaa ..
 
Back
Top Bottom