Ucheleshwaji wa kupata passport, nini kinaendelea Uhamiaji?

Nimekuwa nafuatilia passport tangu mwezi wa saba mwaka huu, kila siku napigwa kalenda. Passport ilitakiwa kuchukuliwa mwezi wa nane lakini mpaka leo bado.

Ukifuatilia unaambiwa nenda makao makuu, kule napo wana majibu ya rejareja kweli, unaambiwa passport yako bado, bila kuambiwa iko hatua gani au hurudi lini.

Nimejiuliza sana utendaji huu wa serikali ya awamu ya tano, naona bado kazi ni kubwa sana mpaka tufike kule tunapotakiwa kwenda.
Pole ndugu.....niliacha rasmi mwezi wa November kufuatilia
Majibu ya mwisho walinipa ni kwamba
1. Wanataka badili mfumo wa passport badala ya kuwa miaka kumi iwe miaka miwili tu ( nadhani aina nyingine ya kupata mapato)
2. Materials za kutengeneza passport hazijaletwa nchini tangu 2015 na muagizaji ni serikali mwenyewe hivyo tusubiri mpaka wakileta wataweza print mpya.
3. Passport nyingi za zamani hazikutolewa kiuhalali so kutucheleweshea sasa kwa sie wa zamani zilizoisha muda na wale wapya ni njia ya kufanya uhakiki na kurekebisha makosa ya nyuma.

Tanzania yetu tuipendayo ndio hii hatuna budi kuivumilia.
Be proud of your country no way out.
" Tanzania, Tanzaniaaaa nakupenda kwa moyo woteeeee, nchi yanguTanzania jina lako ni tamu sana.......
 
Sio umeanza lini, ila ungekuwa hivyo.
Nisamehe sikuwa na maana ya uhalisia ila ni mawazo tu
Lazima system ibadilike kwa kweli
Kila nchi ina utaratibu wake kuna nchi wanakuambia usitupigie wala kutuandikia baada ya kuomba pasi ila usubiri mpaka mda kadhaa na tarehe unapewa ila ikipitawasiliana nasi.
Believe me ikifika siku hiyo lazima upate hata kama ni miaka miwili
Unamaanisha viza?
Passport nchi husika uendayo inakujaje?
 
Nimekuwa nafuatilia passport tangu mwezi wa saba mwaka huu, kila siku napigwa kalenda. Passport ilitakiwa kuchukuliwa mwezi wa nane lakini mpaka leo bado.

Ukifuatilia unaambiwa nenda makao makuu, kule napo wana majibu ya rejareja kweli, unaambiwa passport yako bado, bila kuambiwa iko hatua gani au hurudi lini.

Nimejiuliza sana utendaji huu wa serikali ya awamu ya tano, naona bado kazi ni kubwa sana mpaka tufike kule tunapotakiwa kwenda.
Hiki Ni kilio nchi nzima haswa mikoani walioomba passport za kusafiria kuanzia July 2017 hadi Leo hawajapata.tatizo Ni nini haswa? Na ukiuliza au kufuatilia hupewi majibu ya kutosheleza.ova
 
Hicho kipengele cha barua ya mualiko wangekiwekea option kisiwe ni kikwazo maana kama nakwenda kutalii mwaliko wa nini sasa?
Lazima ualikwe kutalii pia, Hebo!
Hiyo nchi unalotaka kuitalii lazima ielewe kwamba hilo ndio mantiki ya nchi yetu Tanzania... if they want us to visit them, lazima washirikiane nasi na watupatie hizo invitation letters ili tu apply passport huku kwetu....

Sijui nihamie Kenya... ngoja wapitishe rasmi ile tamko ya mkulu wao .. I think ill just go for a few years... nikapunguze stress za kijinga jinga...
 
Hakuna tatizo lolote uhamiaji, kama kweli utafuata sheria na taratibu za upatikanaji wa passport kwa kuambatanisha vitu hv bac hutokaa miezi km wanavosema wengme
Cheti cha kuzaliwa cha muombaji/hati ya kiapo
Cheti cha kizaliwa cha mzazi kati ya mmoja
Barua ya sheha/kata/kijiji ambayo itathibitisha ukaazi wa eneo husika
Picha za passpor size zenye muonekano unaokubalika
Ushahidi wa safari, na hili ndio linakua kikwazo kwa waombaji wengi hawana ushahid mahsusi wa safar kwa mfano: mfanya biashara awe na leseni halali na hai ya biashara, ambae anaenda kwa shughuli za kimasomo awe na barua ya udahili admission letter, mgonjwa awe na barua kutoka kwa doctor/ hosital ambae anatambulika. N.k
Basi hapa sidhani kama utakosa kwa kufuata vigezo km hv
Cheche tu hapo. Masharti kibao kama kwa mganga wa kienyeji. Ukiyafuatilia sana, unaweza kuta tumeyarithi kutoka kwa wakoloni wetu au yaliwekwa wakati dunia ipo kwenye vuguvugu la "NAM". Masomo nje ya nchi kabla ya kupata admission letter, wakati wa kuomba mhusika hutakiwa kujaza nambari yake ya Passport na kuambatisha page ya taarifa. Je hapo inakuwaje?

Ni sheria ya kikoloni kumtaka kila muomba passport kuwa na uthibitisho wa safari. Kama bro unahusika, badilisheni hicho kipengele dunia imebadikika sana sasa hivi.
 
Usishangae hata kidogo ikija sheria kwamba ukisharudi nyumbani baada ya safari yako, urudishe passport yako uhamiaji.... halafu uanze process tena ukitaka kusafiri mara nyingine... kwani mara ya kwanza si walitaka uthibitisho?? sasa inakuwaje watake uthibitisho wa safari yako ONLY ONCE!!??

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo...............................
 
Hafadhali wewe Ni passport .Mimi nimerenew driving license yangu tangu mwezi uliopita mpaka Jana nimeambiwa jiende January kuanzia tarehe 15 Jamani kikadi kill Cha Leseni kinachkkua zaidi ya miezi mitatu.Sasa Passport miezi sita naona kidogo aisee.Mimi naona tunarudi kinyime nyume Sasa.
 
Ushahidi wa safari, na hili ndio linakua kikwazo kwa waombaji wengi hawana ushahid mahsusi wa safar kwa mfano: mfanya biashara awe na leseni halali na hai ya biashara, ambae anaenda kwa shughuli za kimasomo awe na barua ya udahili admission letter, mgonjwa awe na barua kutoka kwa doctor/ hosital ambae anatambulika. N.k
Hivi vipengengele vinaboa sana, mfano mimi nataka nisafiri niende India kutembea, je nitaanza kukata tiketi kabla ya kuwa na passport..

Mfano mwakajana niliona scholarship, Ila Ili uziombe unatakiwa kuwa na passport, sasa ukienda kuomba passport unaambiwa ulete admission letter..
 
Kama unaharaka jitahidi utoe pesa upewe pass kwa two or three weeks.

Mnaosema toka mwezi wa saba mnazungushwa kuna mtu kaenda mwezi wa 11 kapewa mwezi huo huo.
 
Lingekuwa jambo la busara kama idara ya uhamiaji ingetoa tamko kuhusu ucheleshwaji wa hati za kusafiria.
 
Mi nataka niipate hii kitu very soon but naamini kabisa nikifuata protocol nitazungushwa sana so nitamtafuta mdau wa uhamiaji tu nampa ya chai anifanyie makarateee!!!!

Maisha ndivyo yalivyo .
 
Kama unaharaka jitahidi utoe pesa upewe pass kwa two or three weeks.

Mnaosema toka mwezi wa saba mnazungushwa kuna mtu kaenda mwezi wa 11 kapewa mwezi huo huo.
Mwezi? Mkuu jirani yangu alidamkia pale makao makuu asubuhi saa 2 kuomba passport....karudi kitaa kwenye saa 10 mchana akiwa nayo mkononi. Ila hiyo grease iliyotumika usiulize
 
Hivi kupata passport ni lazima uwe unasafiri?

Kwani raia wa kawaida alietimiza vigezo vyote hawezi kufuata taratibu na kupewa passport yake?
Unajua maana ya hati ya kusafiria?

Acheni kuropoka ropoka watanzania.

Uhamiaji hawana shida yoyote.
Shida ni mtu binafsi anataka shortcuts.
Leta document zote ikiwemo barua ya mwaliko inayoonyesha madhumuni ya safari nikupe Passport yako.
 
Me nategemea kufatilia passport yangu mwanzo mwa mwaka huu but kuna baadhi ya vitu vina nicomfuse hususan ushahidi wa safar coz me naenda kusalimia tuu
Utumiwe mwaliko toka huko unakokwenda, so simple Like that.

Kama hakuna barua ya mwaliko usijisumbue bure
 
Back
Top Bottom