"Uchekibobu" unawaponza madaktari nchini Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Uchekibobu" unawaponza madaktari nchini Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Jul 12, 2012.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Gazeti la Mtanzania leo hii limetoa habari hii:

  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD][h=2]Dkt. Chitage azungumzia Dkt. Namala kushitakiwa; Interns kufutiwa leseni; Hali ya Dkt. Ulimboka[/h]12/07/2012


  Siku moja baada ya Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi kufikishwa mahakamani kwa madai ya kuchochea mgomo, Katibu wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Edwin Chitage amesema hali hiyo imewashitua na lolote linaweza kutokea.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dkt. Chitage alisema hali hiyo imeongeza hasira na kushusha morali wa Madaktari, “Kweli hiki kitendo cha Dkt. Mkopi kufikishwa Mahakamani kimetushtua na ukweli kimesababisha kuwepo na fukuto la chini chini. Madaktari wamekatishwa tamaa… lakini kitendo hiki pia kimeshusha morali ya wale ambao walirudi kazini…kwa hiyo wapo Madaktari ambao wapo kazini, kwa maana ya eneo la kazi lakini wanachokifanya hiyo wanajua wao,”alisema Chitage.

  Akizungumzia suala la madaktari wa walioko katika mafunzo (Interns) 390 kufutiwa leseni alisema, kitendo hicho kilitegemewa na hakikuwashitua kwa sababu ni kitu ambacho tayari kilipangwa.

  “Kwetu sisi tulitegemea jambo hilo kwa hiyo hatukushtuka sana…kwetu hiki ni kitu kidogo sana, kwa sasa viongozi wa Interns wanafanya kikao na wanasheria wao wanaangalia jinsi uamuzi huo ulivyotolewa na baadaye tutakutana nao kwa ajili ya kuangalia ni namna gani tutalifanyia katika suala hili,”alisema Dkt. Chitage.

  Akizungumzia hali ya Dkt.Stephen Ulimboka alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na ameanza kutembea na kufanya mazoezi vizuri, “Hivi sasa hali yake imeanza kuimarika. Anaweza kutembea na anafanya mazoezi yake vizuri. Kinachoendelea kumkalisha hospitali ni uangalizi wa karibu wa figo…lakini ingekua si figo angekuwa amesharudi nchini,” alisema.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Source: http://www.wavuti.co

  My take: Hawa madaktari "uchekibobu" ndio unaowaponza. Wanaongea vitu kama viajna wa kijiweni vile!
  1. Chitage ananukuliwa akisema hali ya Rais wa MAT kufikishwa mahakamani imewashtua! Hivi huyu Chitage hajui kuwa Rais wa MAT alipewa amri na mahakama? Ukipewa amri na mahakama una options mbili, aidha kuitekeleza au kuiambia mahakama kuwa hujaridhika na amri hiyo. Huyo Rais wa MAT alifanya chochote kati ya hivyo? Yeye amepewa amri ya mahakama akaifungia sandukuni na kuendelea na shughuli zake za kichekibobu. Sasa kinachowashtua ni nini?

  2. Chitage ananukuliwa akisema swala la interns kufutiwa usajiri halijawashtua kwa sababu walilitegemea! Wakati huohuo anasema viongozi wa interns wanajadiliana na mwanasheria na baada ya majadiliano hayo ndipo Chitage na wenzake waangalie nini cha kufanya. Sasa Chitage kama walishalitegemea hilo, kwanini majadiliano na mwanasheria yanafanyika mpaka baada ya leseni kufutwa? Chitage haoni kuwa anawachelewesha vijana wa internship katika safari yao ya kupata usajiri wa kudumu kwa sababu yeye ana mipango mingine ya maisha! Lakini najiuliza hawa kina Chitage kwanini swala la interns wanawaachia viongozi wa interns? kwa nini wasilisimamie wao kama viongozi wa madaktari? Huu uchekibobu utawaponza vijana wasio na hatia.

  3. Chitage ananukuliwa akisema madaktari wanafanya kazi lakini hawana moyo wa kufanya hiyo kazi. Hivi huyu Chitage ni lini alikuja kuuambia umma kuwa mgomo umeisha? Kwa lugha nyingine ni kwamba mgomo ulioitishwa na kina Chitage umekataliwa na madaktari na Chitage na wenzake wanaona haya kusema ukweli kuwa mpango wao wa kuivuruga nchi umekwama. Labda tumuulize Chitage amejuaje kuwa madaktari hawana ari ya kuwatibu watanzania wenzao. Yeye Chitage kama kagoma, anafuata nini maeneo ya kazi?

  Nawashauri viongozi wa hospitali kuhakikisha machekibobu kama kina Chitage hawaruhusiwi kuingia katika sehemu za kazi. Wao waendelee kugoma na wawaache madaktari wanaotibia watanzania wenzao waendelee na shughuli zao. Wameshawaharibia vijana programs zao za internship sasa wanataka kuharibu na mengine. Hawa wakiachwa wanaweza kuwa radhi kuharibu hata hivyo vifaa vichache chakavu vilivyopo.
   
 2. m

  mwilonga Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo aliyetoa hoja hiyo ndiye chikibobu wa kwanaza na sisi madaktari tunasema wagonjwa njooni mpate huduma hospitalini,wala hatuna kinyongo chochote,niwazalendo,na ni wa pole,ahsanteni sana
   
 3. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  So ingeneous son!

  The tittle,The contents are in East and West.....
  Did you read before copy and paste? Read first na kama huelewi leave it for the brave to it in a right way!
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu anaweza kunisaidia kunihakikishia kama huyu anayekwenda kwa jina la Chitega ni Daktari kamili wa kuusomea katika njia za kawaida kweli,napata mashaka makubwa hasa baada ya kusoma hoja zake alizozitoa,daktari aliyekaa darasani kusoma na kufanya mitihani mbalimbali na kufaulu kiasi cha kupewa leseni ya u'daktari kamili anawezaje kutoa hoja za ki'ushuzi kama hizi....eti kufutwa kwa leseni za ma'interns kulitegemewa...vp kuhusu kushtakiwa kwa Dk Namala kwa kosa la kudharau amri ya Mahakama hakukutegemewa? aisee nimeamini kukaa kimya sometimes kunaweza kulinda hadhi ya mtu kwa kiasi kikubwa sana kuliko kuropoka kwa style hii ya Bwana Chitega.
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Huna hoja...
   
 6. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  You got it wrong dat it!
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ndio uchekibobu wenyewe huo kiongozi. hawa wanaitwa madaktari wa .com

  Just fikiria mtoto yeyote unayemfahamu mwenye maiaka miwili, halafu mfikirie anaumwa homa kali na amepoteza fahamu, halafu anakataliwa kutibiwa kwa sababu daktari hajapewa mkopo wa gari!!! Nimeshangaa sana kuona katika viongozi wa mgomo madaktari wa watoto pia wamo!!!
   
 8. N

  Nambombe Senior Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha kuropoka kama hauna cha kusema,ule mgomo umefanywa na jumuhia ya madaktari ambao kiongozi wake ni dr ulimboka na haukufanywa na chama cha madaktari ambao kiongozi wake ni dr Namala.Hivyo dr Namala hausiki kabisa na
  ule mgomo.Serikali ilienda mahakamani kuzuia mgomo wa chama cha madaktari(MAT) na kweli dr Namala hakuna hata siku moja akuwaambia MAT wagome na MAT hawajagoma,lakini waliogoma ni jumuhia ya madaktari ambacho sio chama na hakina usajili wowote na kwa msingi huo serikali ilpigwa chenga.Hivyo kumpeleka dr Namala mahakamani serikali imechemka na watashindwa.
   
 9. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Red - kama hivyo ndivyo kweli asanteni sana na sie umma tutakuwa nyuma yenu.
   
 10. joramjason

  joramjason JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Sijui kwanini nimeopen this thread inanitia kichefuchefu now. Puuuuuuuuuuuuuuuuuu!
  Madaktari nyie ndo chachu ya mageuzi ya kweli nchi hii now inahitaji watu kama nyie. Naona watu hawajui tofauti ya proffessional na hizo kozi zao za ukifeli PCB or PCM form six unaweza soma yoyote kati ya hizo zilizobaki.
   
 11. oba

  oba JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  You have to learn how to differentiate politics and proffesional, udaktari na profession na usidhani unaweza kuiangusha profession kwa maneno ya kisiasa kama yako.....wait and see ndo utajua the small minds ni zipi na big minds ni zipi
   
 12. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijawahi kuona mchemfu kama weye, KTY huyo daktari wa watoto unayetamani awe ameshiriki mgomo hakuahiriki, mnataka kumbambikizia kesi , au umepewa info nusu nusu, kabla hujakurupuka fanya utafiti.

  Am so ashamed of you!
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Unaweza kujifanya unajuuuuuuuuuuuuuua kumbe unaungua na jua. Ndio watu kama nyinyi. usitetee vitu usivyoelewa, utanunua kesi si yako.
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hakuna mashidano. Kuna kukumbushana, kueleweshana na kuwekana sawa tu. Lengo ni kujenga nchi yetu inayojikongoja katika sekta mbalimbali za maendeleo.
   
 15. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,165
  Likes Received: 1,169
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuathirika na mgomo wa drs.kwa kupoteza ndugu, bado nawaunga mkono ma dr! Selikali haitakwepa lawama katu, kwa jinsi walivoshugulikia tatizo toka mwanzoni inaonesha wasivokuwa na nia ya kumaliza tatizo. Selikali hii yenye viongozi walohamishia hazina kwenda uswiss, wenye matumizi ya anasa, wenye kufanya ubadhirifu wa mabilion na kuadhibiana kawa kubadilshwa vye na nafasi. Wanasiasa ndo wanaotugarim kama taifa, kutokana tabia walizo nazo tutarajie migomo mingine mingi tu, mpaka pale wanasiasa watakapo yaona mambo haya ktk uhalisia wake!
   
 16. k

  kanyabuleza Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu IK aka Marcopolo baada ya juhudi zako za kuwapotosha madaktari wenzako kushindwa sasa umeamua kutumia jukwaa la JF kuwaua madaktari wenzio kwa nini usimwambie Dr Chitange na Dr Namala face to face kwamba ni machekibobu?? kama mwanachama hai wa MAT?? acha izo bana umesahau ulivyosababisha mortality za kufa mtu pale Lugalo mpaka wakakuweka kando you are a just failed physician na sasa unataka kuwatia hila wenzio poor boy!! What a puppet jumuia ya madaktari inakuamini wewe unatumia fursa hiyo kuwavuruga!!
   
 17. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Dokta wawapi huyo bagamoyo au sumbawanga wa kitabu au tunguri
   
 18. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  G.P.A of 3.98 out of 4.0 It is the very warm report of 22-year-old Emmanuel Ohuabunwa who recently made an academic record at the prestigious Johns Hopkins University in the United States of America. Ohuabunwa graduated at the very top of his class with a first class degree in Neurosciences, aggregating a Grade Point Average (GPA) of 3.98 out of a possible 4.0. An indigene of Arochukwu, Abia State, he is the first black person in the history of the institution to achieve such a feat. He was also adjudged by the school as having the highest honours during its graduation last May. Though every top American university was blandishing scholarship at Ohuabunwa, including Texas A&M, Rice, Columbia, Cornell and even Harvard, for him to further his education on their campuses, he settled for the Ivy League, Yale, where he will be studying medicine on full scholarship. awajielei hao acha waumie
   
 19. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Brother....

  You just dont know what you are doing; and its really unfair to yourself and fellow Drs.
   
 20. m

  mangifera Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna imani kuwa taifa limeundwa na mihimili mitatu mikuu yaani BUNGE, MAHAKAMA na EXECUTIVE(BARAZA LA MAWAZIRI) ambalo rais ndo mwenyekiti. Tunadanganywa kuwa mihimili hii ni huru, yaani haiingiliani katika maamuzi na kazi zake. Lakini tunachoshuhudia si kweli. Ni vigumu mtanzania kutofautisha kati ya katibu mkuu wa CCM, jaji wa mahakama, waziri au spika wa bunge. Wote wanafanana kiitikadi kisera na kimtizamo. Na huenda wanakula meza moja.
  Ukiangalia upande wa mahakama ndiyo mbaya kabisa, viongozi wote wa juu kuanzia jaji mkuu huteuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala. Rais huingilia kwa urahisi sana maamuzi ya mahakama kama tulivyoona alivyoingilia mgomo wa madaktari kwa kutoa maamuzi huku akitudanganya kuwa kesi iko mahakamani. Mahakama haijakemea wala kusema lolote. Pia muhimili mwingine wa serikali ambao ni bunge kwa kupitia spika umekuwa ukiilinda sana serikali(executive) pale ambapo amekuwa akiitetea serikali au kuzuia majadiliano yoyote katika hoja ambayo serikali inaelekea kushindwa.
  Hata pale ambapo waziri mkuu aliulizwa swali la msingi la kutakiwa ajiuzulu kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi (mgomo) spika alimlinda kwa kumwambia "hilo usijibu mh. W/K"

  Sasa tunashuhudia serikali kuitumia mahakama kama kichaka chake cha kujificha baada ya kushindwa kutatua matatizo ya afya za wananchi na madaktari kwa kufungua kesi za uongo zisizokuwa na kichwa wala miguu, yaani kosa kafanya kenge, anashtakiwa mjusi eti kwa sababu wote ni damu baridi na wana magamba. Kila ikiambiwa jibuni hoja wanasema kesi ipo mahakamani. Lakini wakitaka kujinufaisha huvunja mwiko wa mahakama bila kuulizwa!!

  Kwa sababu hii mahakama inatumika kama kichaka cha serikali kujifichia na imeshafanya hivyo mara nyingi hata wakati ule wa mgomo ulioitishwa na TUCTA.
   
Loading...