X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,344
- 14,119
leo ningependa niwe mrithi wa mshana jr kwa muda. na nitazungumzia uchawi maarufu wa TALASIMU.
TALASIMU.
Ni karatasi linaloandikwa maandishi au herufu zenye mafumbo maalum, mara nyingi herufi zinazotumiwa katika kuiumba talasimu huwa ni maneno ya kiarabu, na talasimu huwa inatengenezwa kwa kazi maalum kama mapenzi, kuondoa mabalaa, kufanya aliyetengeneza/aliyetengenezewa hiyo talasimu apendwe au akubalike kwenye jamii, vile vile zipo talasimu zenye malengo mabaya haswa ya kutenganisha/kufakaranisha, talasimu zenye kusababisha mikosi na mabalaa ya kimaisha.
ASILI YA UCHAWI WA TALASIMU
chimbuko haswa la talasimu ni kutoka kwa waumini wa kiislam ambao enzi hizo walikuwa wanaandika dua maalum zinazotoka kwenye kitabu kitakatifu cha QUR_AN na walikuwa wanaandika dua hizo kwa minajiri ya kuzisoma mara kwa mara ili wajitibu au watatue matatizo mbali mbali kupitia dua hizo, lakini kutokana na mageuzi ya kimtandao na kimaisha wataalam mbali mbali wakaja na mada zao mbali mbli kuwa inawezekana ukaandika dua ukawa unatembea nayo tuu na ikatosha kukukinga ama kuKUfanyia kile ulichokusudia. na huo ndio ukawa mwazo wa uchawi huu wa TALASIMU
hiyo hapo juu ni picha ya mfano wa talasimu ambayo mtu anaweza kuiandika ama kuandikiwa ili arudishe/amvutie mpenzi ampende. aina hii ya uchawi chimbuko lake haswa ni kutoka nchi za kiarabu na ni uchawi unaoaminiwa sana kwani ni miongoni mwa uchawi wa mwanzoni kabisa.
JINSI TALASIMU INAVYOTENGENEZWA
kama nilivyoelezea hapo juu kuwa kila talasimu ina maana na kazi zake, hivyo kila talasimu ina taratibu za kuiandaa kutokana na kazi inayoenda kuagizwa. zipo talasimu zinazoandikwa kwa wino maalum wa zafarani, na kuna talasimu nyingine zinaandikwa kwa damu za wanyama, damu za ndege hasa kuku ama njiwa, kuna talasimu nyingine zinaandaliwa kwa maji maalum ya baadhi ya matunda pengine ata maji ya muwa muda mwingine yanaweza kutumiwa kutengenezea talasimu.
zipo talasimu zinazoandikwa ama kubebwa kwenye vito vya thamani kama mikufu, pete za dhahabu na pengine ata kwenye saa.
MATUMIZI MBALI MBALI YA TALASIMU
talasimu kama ilivyo kwenye uchawi mwinginewe pia uchawi huu wa talasimu umegawanyika katika kazi nyingi tu, kama ifuatavyo
kujirinda

- kurudisha mpenzi
- kuvuta wateja kwenye biashara
- kumkinga mpenzi asitoke
- kutenganisha watu/kufarakanisha
- kugombanisha jamii au watu
- kufanya mtu au kundi fulani likubalike sana.
- kufanya kundi fulani lisikubalike
hizo ni baadhi ya kazi za talasimu zipo nyingi nzuri na mbaya....na kwa tetesi zilizopo ata ule mchezo wa kutupiana majini ambao upo baadhi ya sehemu hasa Tanga chimbo lake ni kutoka kwenye uchawi huu wa tarasimu.
zifuatazo hapo chini ni aina mbali mbali za talasimu nzuri zenye lengo la kurudisha mahusiano yaliypotea.
talasimu hiyo hapo juu unaweza kuiandika kwenye yai la kuku mweusi, kisha ukalichoma hilo yai baada ya yai kuteketea kabisa utachukua majivu yatakayopatikana kisha utaenda kumtegea unayempenda akifanikiwa tu kuyaruka majivu hayo uwezo wa kumpata utakuwa mkubwa.
talasimu hiyo hapo juu unaweza kuiandika siku ya jumatano. ukiiandika vizuri ukawa unatembea nayo inaweza kukuongezea baraka na mafanikio kwenye kazi zako, hii ni talasimu nzuri sana kwa wafanya biashara.
talasimu hiyo hapo juu uandikwa haswa siku ya jumanne...ukiiweka kwenye biashara ni nzuri sana kwa kuvuta wateja na miongoni mwa talasimu kama hiyo ndio haswa ambazo wafanyabiashara wengi wenye maduka hupewa na dalili moja wapo ya duka lenye kutumia talasimu kuvuta wateja utakuta duka linajaza sana na pengine kuna msululu wa maduka mengine lakini wateja wote hukumbilia kwake kwa kupanga foleni.
kwa leo tuishie hapo....nisameheni nilio wakwaza najua nitakuwa nimeharibu kazi kwa wengine lakini sikuwa na lengo baya...panapo majaaliwa nitakujakuelezea jinsi talasimu mbaya zinavyotengenezwa
USIJARIBU HII NI HATARI NA DHAMBI KUBWA SANA