Uchawi upo hawa waganga wamenithibitishia hilo

Maxmax72

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
530
981
Wakuu kwema ?

Tukiwa tunaumaliza huu mwaka hakika kuna mengi ya Kusikia na kushuhudia,kwa upande wangu nilisikia kuhusu hawa wataalamu wa tiba asili almaarufu waganga,na haya ndo niliyoyaona kwao na kunishangaza kwani niliamami inapoishia sayansi ndo uchawi unaanzia kiaje?fuatana nami!

Kisa cha mganga wa kwanza,ilikuwa mwaka jana nikiwa katika harakati za uvuvi wa samaki ziwa Victoria moja ya kisiwa maarufu sana Kiitwacho Goziba,nilikuwa na mtubwi mmoja almaarufu bugabuga yaani mtubwi usio kuwa na injini bali unatumia kasia kuendeshea na nilikuwa na nyavu za kuvulia samaki aina ya sagara, basi siku moja jamaa zangu walikuwa kama wafanyakazi wangu waliamua kunizunguka kwa kwenda na kuuza nyavu zangu kijanja, na kurudi kwangu wakidai wameibiwa,Ebhana nilichanganyikiwa kabisa ukizingatia ndo ilikuwa ajira yangu hivo ilibidi nifanye kitu ili kujua ukweli ulivyo maana kazi za ziwani hazina uaminifu ujanjajanja wingi sana,ndo nikaelekezwa kwa mganga ili nikajue huo ukweli ilinibidi nisafiri hadi kijiji kimoja hko wilayani sengerema na nikakutana na mtaalamu ambaye yeye alinionyesha sayansi nyingine kabisa tofauti na ile nilisoma chuo kikuu,

kiufupi huyu mzee anakioo ndani unapakwa dawa usoni na sharti usiwe unakula chochote wala kunawa uso hakika nakwambia kioo kinakuwa screen yenye HD na utaona matukio yote unayopenda kuyaona awe mtu aliye marekani utamuona alipo na anachokifanya kwa uapnde Wangu niliona jinsi wavuvi wangu walivyoniletea usanii kwa kuuza nyavu zangu na niliona hadi jamaa mununuzi na nilifanikiwa kumkamata maana niliona alipo na alipo hifadhi nyavu zangu

Mganga wa pili.hili ni tukio la mwaka huu baada ya jamaa yangu bodaboda kucharagwa mapanga na jamaa waliotaka kumpora pikipiki japo kwa bahati nzuri hawakufanikiwa maana raia waliwahi ila jamaa alijeruhiwa vibaya sana na alizimia siku mbili,ebhana katika harakati hizo nikasikaia kwamba mbona kuna mganga sehemu za ngara mwenye uwezo wa kukupa kinga ambayo panga,shoka,jembe,mkuki na vitu vyote venye ncha kali haviwezi kufua dafu ,basi May nikawa nimeenda kumuona huyo mzee ili kiroboto wa aina yoyote asije akanitoboa na panga hata pale akinifumania na mke wake joke,

Ebhana mzee nikamkuta na kawaida ya watu wenye dawa hawana bwebwe na makelele nilikaa kwa kutulia Kama week hatimae Siku ikawadia ambapo niliwekewa Hiyo kinga kwa kuchanjwa huku nikiwa nimeshikilia silaha zote Kama panga,shoka,mkuki,jembe ikiwa na maana hivo vitu niko juu yake baada ya kuchanjwa ikaja zamu ya test asikwambie mtu mi zoezi ngumu hujawahi ona kwani panga nilinolewa vikali ninanyanyuliwa na kukata tumboni na kila sehemu ila ninadunda ajabu as if nothing applied kinachobaki ni maumivu yale ya kupigwa na kitu wala siyo kukatwa asee nilishangaa maana newton,eisten na magwiji wote wa physics wako wazi kitu chenye ncha kali kikikwatwa popote lazima damage itokee hasaa kama mpini wake ukiwa mfupi na nguvu nyingi zitumike lakn kwa huyu mzee wa Ngara Newton na vilaza wenzake warudi shule wakasome.

Mganga wa tatu,ebhana huyu ni noma kwani ni Kama Pilato kwani anakuwekea kitu Kama laana ukitamka kitu kwa mtu lazima kimtokee,akikwambia kesho huamuki omba sana na uandike wosia maana ni lazima uzikwe,ngoja niifupishe maana nitakuchosha wakulwagwa..

Hebu nawe share mganga wako na utalaamu alio nao maana hii dunia hapana chezea waswahili wanasema mchana gogo usiku linakumlikia,jitahidi kumuheshimu kila mtu kwani haijalishi we ni nani watu wamebeba hatma ya maisha yako ukiwakwaza wakaamua kesho uzikwe utakiacha kila kitu hadi na unachojivunia.

Asanteni,cheeers!
 
Mkuu nimecheka sana na simulizi yako waalah!

Una elimu ya chuo kikuu kweli wewe?

Unakuja kijanja kupromote miujiza ya ushirikina wako humu siyo?

Vyovyote iwevyo, ninakubaliana na wewe kuwa mambo hayo yapo ila wenye elimu halisi ya mambo hayo ni wachache, wengi ni waigizaji na matapeli.
 
Kwa nini usiomwombe huyo mganga akufundishe hayo maarifa badala ya kuja kutafuta wateja humu uwaingize chaka?
 
Vipi risasi??
Hii nilisikia ila kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeona siyo vizuri kusimulia hapa maana yupo hadi mama Samia ila pia majambazi sugu yayotafutwa yakiwa hai au yamekufa...so its either side can take it for their own advantage which is not my intention.
 
Usiombe umpate anaekuonesha waliokudhuru wanaokudhuru etc. Sharti Lazima akupime kifua/hasira daah Mungu ni mwema sana kanipa ujasiri hadi mamba anasubiri. The Jaguar, The Mambas, The Duduz, The Simba.
 
Hivi we jamaa una akili kweli? Au njaa ndo inakusumbua umeona wapi katika maandishi yangu nikiuza hizo dawa ? Acha ujinga na stress za maisha.
Njama zako zimejulikana? Mbona una hasira, acha kupanic we ndo una stress za maisha unadhani utaombwa namba za mawasiliano za huyo mganga?
 
Naomba namba za mganga pliz huyo wa sengerema!Muku tayari nimeshachanja kenya wanaita Pufya au Bundugo!
 
Back
Top Bottom