Uchawi ni sayansi kubwa sana; hivi haiwezekani kuboreshwa ikawa wazi na kuleta athari chanya??

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,003
2,000
Wakuu habarini humu,

Kiukweli uchawi ni sayansi kubwa sana tena ina mengi ya kustaajabisha, maajabu yake ni makubwa na yanashangaza.. fikiria kuchoma kisu kwenye kioo ukiwa dodoma na sekunde hiyo hiyo madhara kwa uliyemkusudia yanatokea hata akiwa Mtwara, haya ni maajabu sana, tena hebu fikiria jinsi unavyofunga milango ya nyumba yako lakin wachawi wanapita bila kusumbua hata mende. Kuna matajiri wengi wanatumia hii sayansi na mambo yao yanaenda vizuri

Alafu ni kama kuna faida nyingi tutapata endapo uchawi ukifanya kazi katika upande chanya, sasa kwanini umefichwa?? Uchawi umewekwa siri kwa faida ya nani?? Ikafika mahali nikahisi labda ni propaganda za wazungu ili tusiwazidi kwa upande wa sayansi lakin nikaja kugundua pia hata huko ulaya uchawi upo na still sio wazi pia.

Wanajamvi kwanini mambo ya kichawi yanafichwa na kuwa siri??
 
Heri lee

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
992
2,000
Napenda sana nyuzi kama hizi lakini kwa ujumla nasikia wakuu umu akiwemo mshana Jr wanasema power of meditation ni kila kitu utafanya kila kitu utakacho duniani
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
153,231
2,000
Napenda sana nyuzi kama hizi lakini kwa ujumla nasikia wakuu umu akiwemo mshana Jr wanasema power of meditation ni kila kitu utafanya kila kitu utakacho duniani
Uchawi ni ishu za giza na za Kiroho... Hivi vitu havina ithibati za kisayansi na uchawi mkubwa na wenye nguvu huhusiana kwa sehemu kubwa na kafara za damu.. Na ili utoe kafara inabidi uue
 
Jemedal_bin_chichi

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
497
1,000
Hakuna kitu kisicho kuwa na faida na hasara, na hii ndio tafasir sahihi ya HARAMU itumikayo na waislam kuwa

Kitu chenye faida nyingi na hasara chache hicho ni HALALI

kitu chenye hasara nyingi na faida chache hicho ni HARAMU

Faida za uchawi ktk jamii ni chache na hasara ni nyingi, tukirejea ktk tafasiri ile pale juu bas hichi kitakua HARAMU pia

Labla mleta uzi, kuna mifano unayo, kwamba tunaweza kufanya mambo chanya kwa kutumia uchawi pasina kuingia hasara kubwa zaid ya hayo mambo chanya!?

Kama unamfano huo weka hapa nikuchambulie
 
bahati30

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,626
2,000
Uchawi ni ishu za giza na za Kiroho... Hivi vitu havina ithibati za kisayansi na uchawi mkubwa na wenye nguvu huhusiana kwa sehemu kubwa na kafara za damu.. Na ili utoe kafara inabidi uue
Ndugu mshana naamini kwa weledi ulio nao kwenye haya Mambo unaweza kutubunia mradi mkubwa ambao moja kwa moja unaweza kutusaidia kwenye mkakati wetu wa kujenga uchumi wa viwanda. Wewe pambana suala la rasilimali fedha tutafuta wadau wa maendeleo kwa sababu nao wako njema na naamini hawatatutosa.
 
joely sandu

JF-Expert Member
Nov 24, 2017
1,978
2,000
Uchawi ni ishu za giza na za Kiroho... Hivi vitu havina ithibati za kisayansi na uchawi mkubwa na wenye nguvu huhusiana kwa sehemu kubwa na kafara za damu.. Na ili utoe kafara inabidi uue
Mshana kuna mtu. Uko analalamika kamroga mume wak umeuona huo uzi?
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
153,231
2,000
Ndugu mshana naamini kwa weledi ulio nao kwenye haya Mambo unaweza kutubunia mradi mkubwa ambao moja kwa moja unaweza kutusaidia kwenye mkakati wetu wa kujenga uchumi wa viwanda. Wewe pambana suala la rasilimali fedha tutafuta wadau wa maendeleo kwa sababu nao wako njema na naamini hawatatutosa.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,779
2,000
Uchawi unaendana pia na imani, wewe ukiambiwa upake dawa kisha utembee mjini utupu watu hawataona ila wewe utawaona - utaamini na kukubali kusaula mavazi mchana kweupe?

Au ukiambiwa vua nguo, paka dawa then panda kwenye ungo kisha fumba macho, ukifumbua utakuwa kwenu Mbalizi - je utakubali?

Uchawi ni sayansi ya kiini macho kweli, hivyo maboresho yake ni magumu - uchawi unaendana na traditional belief ambazo msingi wake ni kutokuwa na upeo (elimu). Maeneo ambao watu wapo uncivilized ndiko huko bado mambo haya bado yanapamba moto.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom