Basi kwa neema na baraka zake Mungu baba alie juu mbinguni mahali patakatifu ahimidiwe kwa busara na hekima zake kwa uhai aliotujalia na afya na anijalie niandike vyema ili kusudi langu lieleweke, Kuna jambo katika mambo ambayo yapo, jambo ambalo ni dogo katika mengi ambayo kwangu nimeyaona na kuamini katika hayo kuhusu uchawi.
Nitasema kuhusu nguvu ya uchawi na uwezo wa kuloga kwa nafasi niliyoshudia na kugundua kwa miaka yangu hii michache niliopata kuishi toka nijitambue kwa upana, hili jambo ni muhimu na si la mzaha hata kidogo.
Nitaanza na kukili kuwa uchawi upo duniani kote tena hapa bongo upo mwingi sana mbwa kila siku hawachoki kuwabwekea wakipita usiku saa sita, upo kwa karne na karne na utakuwepo sikuzote za maisha yetu kwa kutaka na bila kutaka.
"Mtanisamehe wenzangu kwa kunukuu hiki kifungu "
"Ufunuo 22:15 inasema hivi Huko nje wako mbwa, WACHAWI, na wazinzi, na wajuaji, na hao waabuduo sanamu , na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Baadhi ya mazoea ya kiuchawi ambayo watu hujihusisha sana nayo ni uaguzi na kuwasiliana na pepo kutia ndani unajimu, ubashiri wa kutumia namba, usomaji wa viganja, kuwasiliana na “wafu” na vilevile ulozi. Mazoea hayo yana historia ndefu, kwani mengi kati yake yalianzia Babiloni la kale (Isaya 47:1, 12, 13)
Inasema (12 Endelea basi na uganga wako, tegemea wingi wa uchawi wako. Wewe uliyapania hayo tangu ujana wako ukitumainia kwamba utafanikiwa au kusababisha kitisho kwa watu! 13 Wewe umejichosha bure na washauri wako. Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe! Wao huzigawa mbingu sehemu sehemu, huzichunguza nyota na kubashiri kila mwezi yatakayokupata.) Kutoka Babiloni, mazoea ya uchawi yalienea kote katika ulimwengu wa kale na kutia mizizi katika tamaduni na jamii nyingi.
Nimenukuu ili kuaaminisha uchawi upo kwa wale ambao hawajawahi kutana na kadhia hii mpaka waamini labda wataamini kwa neno la bwana ili nitakolosema waelewe.
Nguvu za gizaa zinatumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamii nyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.
SASA KWA NINI WANA NGUVU NA WANALOGA KWA MAFANIKO MAKUBWA.
Wameingia maagano na wakuu wa nguvu za giza kiasi wameweza kuwaangusha na kuuwa maelfuu ya watu kuna wengine ni watu wa Mungu na wameweza kuwachezewa watakavyo na kuwa acha katika majonzi, magonjwa, shida, mikosi na kubebewa nyota, hata akili wanachukua na kuvuruga kila walionalo wakiendeshwa na tamaa, wivu pamoja na chuki binafsi wao wakiona unaringa, unafaidi una raha n.k
Kwanza wachawi wanaasheria kali sana, hawana utu na wenye kufata sheria za Maagano yao na wanatekeleza vizuri kabisa sheria zao licha ya kua wachache wao hukwama ila wako vizuri.
Nguvu zao zipo kwenye damu, damu wanazomwaga ndio nguvu ya kwanza kuliko chochote kile halafu ndio yanafata mambo mengine ya mitishamba. Wachawi wanatoa sadaka wanauua watu, wanaua wanyama tena mara nyingi au kila mara, ili kufanikisha kazi zao.
Nataka kutoa mfano " Mtu akitaka kuloga au kuaguliwa lazima alete kimoja wapo kama ni mayai,nazi, njiwa, kuku, mbuzi , mtoto wa mtu, mtu baki au zaidi ili kutimiza lengo lake.
Basi sadaka anayotoa huwa ndio njia ya kufanya mambo yake yaende kwa kutumia majini, mashetani au mapepo kwenda kwa adui yake ambae ndo wewe " upo ofisini, sijui mwinjilisti, mwana jamii una maisha yako, upo kwenye gari, upo bafuni, unacheza mpira , umepumzika, au umelala usiku " kinatumwa kitu 'puuu" unacho.
TUJUE KWA NINI UNALOGWA NA KUCHEZEWA AU KUHARIBIWA MAMBO YAKO.
Kwanza kama huna msimamo husali, hulogi kotekote haupo wewe ni chakula cha wenzio. Hili kundi la watu hubebwa sana labdaa kama kwenu kuna mizimu mikali utapona na haya mawindo .
Mwinjilisti, mwana dini, askofu,padre mchungaji , hata kama una cheo gani upande wa dini hii vitaa ni yaa wote muda wote wapo kazini kuangusha waliojiwekea ngome za kiimani kwa sababu ndio wazuri zaidi na ndio wanaharibu kazi zao zaidi, hawa watu wakiangukia kwenye uzinzi,ulevi, uasherati hapo hapo wakinasa wanapigiwa haraka sana na kuharibu huduma, biashara, mafanikio hawa ni dhahabu muda wote wanatafutwa ndio sehemu ya kupandia cheo .
Sasa kama hujajizindika hesabu kulogwa na kuchezewa au kuharibiwa mambo yako muda wowote na ukizidiwa nguvu lazima yatakusibu.
KWA WALE WANAO TAKA KUTOLOGWA KABISA NA KUISHI KWA AMANI FANYA HAYA.
MTUMAINI MUNGU, Mungu ananguvu kuliko chochote kile hakuna kiwezacho akiweka mkono wake.
Toa sadaka na zaka " Et mtu analipwa mshahara wa laki 4, wengine laki 9 , wengine millioni 1 au zaidi anatoa
SADAKA mia mbili , mia tano, shilingi 100, anaomba Mungu amlinde na Mungu kweli anatulinda na choyo zetu, Muda huo huo unaenda bar unakula na kusaza unaacha elfu 50,laki moja, laki mbili halafu unasema utapata .
Wengine wanahonga nyumba , gari , malaki wanawapa malaya halafu nae anataka Mungu amtendendee makubwa zaidi binadamu tunakwama sana.
" Muda huo mtu kaenda kununua jini la millioni 2 akutumie likumalize, muda huo mtu katoa mbuzi ili ufe, muda huo mtu kachinja kuku ufe, muda huo mtu kavunja nazi kuharibu maisha yako.
Je utafua dafu kwa sadaka yako? Ili kuzuia kombora za maadui zetu.
Tujifunze kutoa sadaka ndugu zangu, tufunge tusali, umeenda mnadaani mmeangusha mbuzi si bora mchange mnunue mwingine aende kanisani, nunua vikuku viwili au kimoja peleka kanisani Watu wapo tayari kupeleka kuku kwa mganga lakini sio kanisani.
TUBADILIKE KWA KUTOA SADAKA NA ZAKA ZA MAANA NA KUSALI ILI KUWASHINDA ADUI ZETU HAWATUWEZI TUKIWEKEZA HUO UPANDE ILI KUKABILIANA NAO.
Mwisho siamini katika uganga lakini hivi vitu vipo na wanatibiana na kupona ila vikiwa chini ya nguvu za giza. Kwahiyo kama wanaweza kuloga basi hawezi kunshindwa kutegua wakilogana na Mungu hafungamani na haya mambo, mimi pia sifungamani na haya mambo ya uganga na uchawi.
Nawasilisha.
Mungu azidi kutulinda, Amina