Uchawi na muujiza ni mapacha

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,986
1,282
1464594018904.jpg


1464594029852.jpg


UCHAWI na MUUJIZA ni masuala tata katika jamii, pamoja na utata wake lakini yamekuwa ni masuala ya kawaida kusikika. Ni kawaida kusikia fulani ni mchawi au nimefanyiwa uchawi. Pia ni kawaida kusikia kuwa fulani ana miujiza au nimefanyiwa miujiza. Uchawi ni nini? Muujiza ni nini? Ipi tafauti kati ya uchawi na muujiza?

Kwanza kabisa naomba nikiri mapema kuwa, mambo haya ni ya kiimani zaidi. Kwakuwa ni ya kiimani, na mimi ufafanuzi wangu utategemea rejea za imani zinazokubali uwepo wa uchawi na muujiza, hususani toka kitabu cha qur-an na biblia.

Katika dini zote, hadi zile za kipagani, zina amini kuwa ulimwengu na vilivyomo ndani yake vimeumbwa na MUNGU. Si ukweli hata kidogo kuwa mungu ni mmoja, kwani kuna watu wanasema kuwa mungu ni mmoja.

Kila dini iko na mungu wake, na kila dini inaamini kuwa mungu wake ndiye aliyeumba ulimwengu na vilivyopo ndani ya huo ulimwengu. Kwakuwa kila dini iko na mungu wake, na kwakuwa dini ziko nyingi, iweje sasa mungu awe mmoja?

“Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnacho kiabudu; Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Wala sitaabudu mnacho abudu. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.” Qur-an 109:1-6

“Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi” Waamuzi 2:12-14

Pamoja na mambo mengine aya hizo kutoka katika qur-an na biblia zinatufunza kuwa, kuna miungu mingi na dini ziko nyingi pia. Kila mtu anaona mungu wake yuko sahihi kuliko mungu wa mwenziwe. Jambo la kuzingatia ni hili, kwa kiwango kile ambacho mtu huona mungu wake ni sahihi, basi ni kwa kiwango hicho hicho mungu huyo huonekana na watu wengine si lolote.

Si lengo la andishi hili kuelezea miungu na dini sanjari na uhalali wake, lakini nimelazimika kuelezea kwa kifupi ili nikija kuzungumzia masuala ya nani hasa aliyeumba ulimwengu nisiwachanganye watu.

Nataka watu wajue kuwa MUNGU ndiye aliumba ulimwengu, huyo mungu anaweza kuwa Yesu, Allah[s.w], Yehova, mzimu, mlungu, nk. Hii itategemea katika dini yako mungu wako ni nani, kama ni Yesu, basi Yesu ndiye atakayekuwa kaumba ulimwengu kwa mujibu wa imani yako, na si vinginevyo!

Mungu ameumba ulimwengu, ulimwengu ambao umegawanyika katika mapute mawili. Pute la kwanza linaundwa na maada(matter & dark matter) Pute la pili limeundwa na sheria zinazotawala hizo maada(energy & dark energy).

Ndani ya sheria za kimaumbile kuna proglamu zinazoamrisha[command] maada zifanye yale tunayoyajua na tusiyoyajua. Cha kuzingatia ni kuwa, hizi sheria ni sehemu ya ulimwengu, na zimeumbwa makhususi ili kuzifanya maada zisikiuke matakwa ya MUNGU.

Upande wa maada ndio kuna (matter &dark matter)
Upande wa sheria za kimaumbile ndio kuna (energy & dark energy)

Vyote kwa pamoja ndio vinafanya ulimwengu.

“Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake? Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?” Ayubu 38:32-33

“Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote” qur-an 7:54

Hiyo “amri ” inayotajwa katika aya hizo ndio sheria za kimaumbile(energy &dark energy), yaani nguvu za mvutano na zinginezo ambazo zipo kuyaongoza magimba na nyota mbali mbali zipite katika njia ambazo zimepangiwa na zifanye mambo yaliyoamriwa kuyafanya. Sheria hizo ndizo zinazotawala maada yanayounda ulimwengu.

Hizi sheria za kimaumbile zilianza kuumbwa kabla hata ya ulimwengu kuwako. Ni vigumu sheria hizi kuvurugwa au kushindwa dhidi ya vitimbi vya waja. Mfano, mtu anapochinjwa shingo hata kichwa kitengane na kiwiliwili ni lazima huyo mtu afe, sababu sheria za kimaumbile zinazotawala mwili huamrisha[command] mwili ufe pindi ukipatwa na tukio hilo. La kuzingatia ni kuwa, kila kitu na kila tukio hutawaliwa na sheria za kimaumbile.

Pamoja na ugumu uliopo katika kuzikiuka na kuzishinda sheria za kimaumbile haiondoi ukweli kuwa watu, majini, malaika na mungu mwenyewe wamekuwa wakizikiuka na kuzishinda sheria hizi mara nyingi tangu ziliposimikwa.

Uchawi ni nini? Uchawi ni ile hali ya kukiuka au kuzishinda sheria za kimaumbile pasina kupata kibali au ruhusa kwa mmiliki wa sheria hizo. Mmiliki wa sheria hizo Mungu. Mtu yoyote anayekiuka au kuzishinda sheria hizo katika muktadha huo huitwa MCHAWI.

Mfano mtu akichinjwa katika namna niliyoeleza hapo juu, na bado akiendelea kuwa hai huku kichwa kikilalamika kwa kitendo cha kuchinjwa, basi jua kuwa sheria za kimaumbile zimekiukwa na kushindwa kufanya kazi yake. Tukio hilo litakuwa ni uchawi endapo aliyefanikisha ukiukwaji na ushindwaji wa sheria hizo hakupewa kibali na ruhusa toka kwa Mungu.

Muujiza nini? Muujiza ni ile hali ya kukiuka au kuzishinda sheria za kimaumbile kwa kupata kibali na ruhusa toka kwa mmiliki wa sheria hizo. Tukio nililolitaja hapo juu, la mtu kuchinjwa na kisha kichwa chake kilalamike kwa kufanyiwa hivyo, utakuwa ni muujiza endapo aliyefanikisha ukiukwaji na ushindwaji wa sheria hizo alipata kibali na ruhusa toka kwa Mungu.

“Bwana akanena na Musa na Haruni, akawaambia, Farao atakaponena nanyi, na kuwaambia, Jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka. Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama Bwana alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.” Kutoka 7:10-12

“Wakasema: Ewe Musa! Je! Utatupa wewe, au tutakuwa sisi wa kwanza kutupa? Akasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinapiga mbio. Basi Musa akaingia khofu nafsi yake. Tukasema: Usikhofu! Hakika wewe ndiye utakaye shinda. Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyo viunda. Hakika walivyo unda ni hila za mchawi tu, na mchawi hafanikiwi popote afikapo. Basi wachawi wakaangushwa wanasujudu. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa Harun na Musa! “ Qur-an 20:65-70

Aya za hapo juu toka katika qur-an na biblia zinaelezea kisa cha Firauni na Musa[a.s] kwa ufupi. Watu wa Firauni walitupa fimbo na kamba zao, kisha zikageuka kuwa nyoka. Naye Musa[a.s] akatupa fimbo yake, nayo ikawa nyoka na ikawameza wale nyoka wengine. Kitendo cha fimbo kutoka katika umbile lake na kuwa nyoka ni kitendo kilichosababishwa na ukiukaji wa sheria za kimaumbile. Kitendo hichi alipokifanya Musa[a.s] kiliitwa “MUUJIZA” na kilipofanywa na watu wa Firauni kiliitwa “UCHAWI” ingawa kimsingi tukio ni moja, na si lingine, bali ni fimbo kugeuka kuwa nyoka!

Uchawi na muujiza ni watoto mapacha na wana fanana sana. Kutokana na kufanana huku ndio maana wakati mwingine watu hujikuta “uchawi” wanauita “muujiza” na “muujiza” wanauita “uchawi”, lakini ukweli uko wazi kuwa “uchawi” na “muujiza” ni vitu viwili tafauti pamoja na kufanana kwao. Aya za hapa chini kutoka katika Qur-an zinaonesha jinsi Firauni alivyoshindwa kutafautisha kati ya “uchawi” na “muujiza”. Aliuita muujiza ni uchawi. Yawezekana alishindwa kutafautisha kutokana kibli chake au ndio upeo wake wa kufikiri ulikuwa umefikia kikomo katika suala husika hata asijue ule ulikuwa ni muujiza na si uchawi.

Ama, kwa kuwa dini ya Farao haikuwa ndio ya Mussa, na kwa vyovyote vile Mungu wa Mussa hakuwa ndio Mungu wa Farao, kama ndivyo, ni sawa muujiza wa Mussa uonekane uchawi kwa Farao, na yale ya Farao mwenyewe aone muujiza.

“Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri. Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao. (Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu. Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani?” Qur-an 26:32-35

Yale mambo yote yasiyoyakawaida aliyoyafanya Yesu Kristo huitwa ni “miujiza”, kwani imethibiti mara chungu nzima katika qur-an na biblia kuwa Yesu alizikiuka sheria za kimaumbile. Alikiuka sheria za kimaumbile kwa kufufua wafu, kuponya viziwi, vipofu, wagonjwa na kwa kulisha maelfu ya watu kwa chakula cha kidogo kabisa. Pia alitembea juu ya bahari pasina kuzama, hata ile saumu yake ya siku arobani bila kula hata kidogo ni muujiza pia.

“Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope” Mathayo 14:25-27

"Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu" Qur-an 5:110

"Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku." Qur-an 5:114

"Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto." Mathayo 14:19-21

Nafikiri hadi kufikia hapa tutakuwa tushafahamu maana ya uchawi na muujiza japo kidogo, si hivyo tu tutakuwa tumeshajua jinsi uchawi na muujiza unavyotafautiana na kufanana. Sasa nataka tujue asili ya uchawi na muujiza. Asili ya uchawi na muujiza ni Mungu mwenyewe.

Tanbihi: nikizungumzia asili ya kitu fulani, jua kuwa nazungumzia muumbaji wa kitu hicho. Mungu ndiye aliyeumba “uchawi” na huo “muujiza” Uchawi na muujiza ni viumbe wa Mungu kama vilivyo viumbe vingine, kama tikikataa kuwa uchawi na mujiiza sio viumbe wa mungu, basi tukubali kuwa kuna “kitu” kingine tafauti na “MUNGU” ndio kimeumba uchawi na muujiza, jambo ambalo halikubaliki katika dini zote, yaani, hata zile za kipagani.

“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;” Qur-an 1:2

“Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.” Mithali 16:4

“Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?” Qur-an 31:4

“Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.” Yohana 1:3

Katika aya za hapo juu zote zinadhihirisha kuwa MUNGU ndiye aliyeumba viumbe vyote ikiwemo na uchawi na nduguye muujiza. Mfano katika andiko hilo la Mithali 16:4, Mfalme Suleiman[a.s] anatuambia kila kitu kimefanywa[kimeumbwa] na MUNGU kwa makusudi yake, kwa vyovyote vile hata uchawi kwa siku ya uchawi na muujiza kwa siku ya muujiza. Sitaki nijikite katika sababu zilizopelekea MUNGU kuumba uchawi na muujiza, kwani nachelea kutoka nje ya mada, kwa ufupi naomba mridhike kuwa MUNGU ndiye aliyeviumba vitu hivi kama nilivyothibitisha kwa kutumia misahafu yetu.

Hivi uchawi na muujiza unafanyaje kazi hata uweze kushinda sheria za kimaumbile? Ili tuweze kujua namna uchawi na muujiza unavyofanya kazi, ni lazima tujue Mungu alitumia nini kuumba ulimwengu. Imethibiti katika dini zote, hadi zile za kipagani kuwa MUNGU alitumia “NENO” katika kuumba ulimwengu, yaani aliposema na iwe bahari, basi papo hapo na ikawa bahari. Tunaweza kusema hiyo papo hapo ni sawa na kitendo cha kufumba na kufumbua.

“Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapo taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa” Qur-an 2:117

“Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza” Mwanzo 1:3-4

Muda kwa upande wa MUNGU haupimwi kwa kutegemea vitendo vifanyavyo na jua, mwezi na dunia, bali hupimwa kwa utaratibu ambao MUNGU mwenyewe ndio anaujua. Ndio maana Mungu alianza kuhesabu siku katika uumbaji wake hata kabla ya kuumbwa jua, mwezi na dunia. Muda kwa upande wa kibinadamu hupimwa kwa kwa kutegemea mzunguko wa dunia katika mhimiri wake, kitendo cha dunia kuzunguka jua na mwezi kuzunguka dunia, kwa MUNGU ni tafauti, utafauti huu ndio hufanya siku moja kwa MUNGU kwa binaadamu ni miaka elfu moja. Je. Kufumba na kufumbua kwa MUNGU kwa binaadamu ni sawa na miaka mingapi?

“Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja” 2 Petro 3:8

“ Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.” Zaburi 90:4

Hii ina maanisha nini? Hii ina maanisha kuwa “NENO” lina nguvu na kasi ya ajabu katika utekelezaji wa majukumu yake, jambo ambalo limefanywa kwa siku moja na “NENO” litatugharimu miaka elfu sisi kulifanya, tena kwa vyovyote vile katika kipindi chote cha hiyo miaka elfu moja itatupasa tuache kufanya kila kitu, yaani hata kula, na kisha tujikite katika utafiti. Je, yupo mwenye uwezo kuishi miaka elfu moja kwa kufanya utafiti tu? Kutokana na sababu hii ndio maana nasema ni vigumu kwa mja kuzikiuka sheria za kimaumbile ili hali yuko mwenyewe.

Pamoja na ugumu huo, lakini waja wangali wanazikiuka sheria za kimaumbile kila uchao. Wanazikiuka sheria hizi si kwa kutumia uwezo wa kibinaadamu, bali inawapasa wawe zaidi ya binaadamu wakati wakizikiuka sheria hizi, kinyume chake kamwe binaadamu hawezi. Kwakuwa ulimwengu na sheria za kimaumbile zimeumbwa na MUNGU kwa kutumia “neno” basi binaadamu hulazimika kutumia “neno” wakati akitaka kukiuka sheria za kimaumbile.

“Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika” Mathayo 8:3

Nataka “takasika” hilo neno nililoliwekea funga na fungua semi ndio neno lilotumika kumponya huyo mtu mwenye ukoma. Ili neno lipate kukiuka sheria za kimaumbile ni lazima liwe na pumzi ya MUNGU aliye hai; Hivyo neno hilo “takasika” lilikuwa na pumzi ya mungu wakati ule linatamkwa na Yesu Kristo, na ndio maana likaweza kukiuka sheria za kimaumbile na hatimaye likasababisha muujiza wa kuondoa ukoma katika mwili wa mhitaji. Hata wachawi hutumia “neno” lenye pumzi ya mungu wakati wakifanya mambo yao ya kichawi, sema wao wanatumia neno hilo pasina kupewa kibali au ruhusa na mungu.

Pamoja na kwamba “neno” ndio kila kitu katika shughuli za kimuujiza na kichawi, lakini haindoi ukweli kuwa kuna vitu vingine hutumika pamoja na neno katika kukamilisha mambo ya kichawi na ya kimuujiza. Kikubwa mfanyaji uchawi au muujiza ni lazima ajue anataka kufanya nini, kwa wakati gani, kwa nani na vitu gani vitahitajika katika kukamilisha huo muujiza au uchawi.

Labda niseme kitu kimoja “nyakati” na “idadi" ya vitu, mambo, vitendo au matukio katika shughuli za kichawi na muujiza ni muhimu sana, usipojua matumizi sahihi ya vitu hivyo inawezekana uchawi au muujiza wako usifanikiwe, au usifanyike kama vile ambavyo ulivyotaka.

“Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona”

Kwa vyovyote vile Yesu Kristo aliona kuwa pindi akitumia “neno” tupu pasina tope lililotokana na udongo na mate yake, yule mtu asingepona ukoma aliokuwa nao. Katika andiko hilo halionekani neno lenye pumzi alilolitumia Yesu Kristo, lakini haiondoi ukweli kuwa alitumia neno pia; kwa maana nia ya kutaka uponyaji ujengwa na “neno” ndani ya moyo, na Yesu alikuwa na nia ya kutaka kufanya muujiza. Nia ambayo kimsingi ndio “neno” katika muktadha huu sanjari na tope ndio vilivyowezesha kukamilisha tukio la muujiza.

“Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo. Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku za mazingiwa zitakapotimia; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma yake. Nawe twaa nywele chache katika hizo, na kuzifunga katika upindo wa mavazi yako. Nawe utatwaa tena baadhi ya hizo, na kuzitupa katikati ya moto, na kuziteketeza katika moto huo; kutoka nywele hizo moto utakuja na kuingia katika nyumba yote ya Israeli” Ezekieli 5:1-4

Katika aya za hapo juu Mungu anamwambia nabii Ezekieli afanye mambo hayo ili apate kuuchoma moto nyumba za watenda maovu katika Israeli kwa kutumia muujiza. Katika kutekeleza huo muujiza, Ezekieli aliambiwa afanye yafuatayo, aliambiwa awe na upanga, kisha kwa kutumia huo upanga anyoe nywele na ndevu. Swali la kujiuliza, kwanini Mungu alitaka atumie upanga kunyolea hizo nywele na ndevu badala ya wembe ambao ndio kitu makhususi kwaajili ya kunyolea? Kwa vyovyote vile kama ungetumika wembe huo muujiza usingekuwa kama vile alivyotaka Mungu.

Kisha akaambiwa hizo nywele na ndevu azigawe katika mafungu matatu kisha na azifanye kama alivyoambiwa. Yaani zingine azitupe kwenye maji[sijui kama aliambiwa mtoni au baharini], zingine azipeperushe kwa kutumia upanga, na zingine katika fungu la tatu kidogo azifunge katika upindo wa vazi[hirizi] na zingine azichome moto. Pindi akitekeleza mambo haya basi nyumba za waovu katika Israeli zitashika moto. Kwanini Mungu alitaka nabii Ezekieli afanye yote haya badala ya kutumia neno tu? Hapo ndipo utakapogundua kuwa muujiza wakati fulani hauwezi kutimia kwa kutumia “neno” tu.

Hata uchawi nao hutumia “neno” na baadhi ya vitu vingine, na hii inategemea na huyo mchawi anataka kufanya nini, kwa nyakati gani na kwa nani. Kuna baadhi ya mambo ya kichawi yanafanikiwa pindi yakifanyika mchana kuliko hata usiku, mengine yanataka saa maalumu , mengine yanataka mahali maalum, mengine yanataka mavazi maalum na mengine yanataka matukio maalum, kwa mfano siku ya tukio la kupatwa jua au mwezi kuna baadhi ya mambo ya kichawi yanataka yafanyike siku ya matukio hayo. Aya ya hapo chini inatujilisha ni kwa namna gani baadhi ya vitu hutumika pamoja na “neno” katika kutimiza mambo ya kichawi.

“Useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?” Ezekieli 13:18

Kumbuka kuwa nilisema anayefanya uchawi hufanya hivyo kwa kutumia "neno" lenye pumzi ya Mungu pasina kupewa kibali na Mungu mwenyewe. Yale mambo aliyoyafanya Ezekieli anaweza kuyafanya mtu mwingine na akafanikiwa kutimiza kama alivyofanya Ezekieli. Ni kawaida sana kwa wachawi kutumia nywele, kufunga hirizi, kuchoma mafusho, kutupa vitu baharini au mtoni, kuchinja wa nyama, na mambo kadha wa kadha katika kutekeleza shughuli zao za kichawi.

Kwanini wachawi wanaroga? ipi tiba ya uchawi? Kwanini Yesu alilazimika kumponya kipofu kwa kutumia tope? Kuna uhusiano gani kati ya jini na uchawi? Kuna uhusiano gani kati ya uchawi na biblia? Kuna uhusiano gani kati uchawi qur-an? Kuna uhusiano gani kati ya uchawi na Mungu? Kuna uhusiano gani kati ya majina yetu na uchawi/muujiza?

USIKOSE SEHEMU YA PILI.

ASANTENI NA UNGU AWABARIKI.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Whatspp/call 0622845394
 
Ngoja nitoke humu nasikia harufu ya udi na ubani wachawi sijui waganga wanajadili yao
 
Kuna mambo mawili hayajakaa vizuri
1.Umekuwa ukirudiarudia kwamba uchawi na nduguyake miujiza,hilo neno siokweli bali uchawi aduiyake miujiza, na hawana udugu wowote.
2.Umetoa ushahidi wa kivitendo namna manabii wanatekeleza miujiza,lakini umeshindwa kuelezea namna wachawi wanavyotekeleza mambo,muda,vitu,mahala na kwa ikiwezekana hata kutaja jina la mchawi mwenyewe,kama Mwanamalundi n.k.
 
Maneno meeeeeeeengi....Swali langu ni ....


Je., Ni mungu Wa dini ipi yupo responsible kwenye kuumba binaadamu??
 
hi ndio faida ya jf hujuti wala kupoteza muda ukiwa jf hupotezi muda badili unapata marifa makubwa ya kujitambua na kujiongoza.
nafuraha sana na jf yangu hii kwani imekuwa ikinifunza mambo mengi sana. ubarikiwe mtoa mada tunaku subiri utufunulie mambo zaidi.
 
Uko sahihi.
Kuna miungu mingi.
Waislam wanaabudu Allah.
Wakatoliki wanaabudu UTATU MTAKATIFU.
Walokole wanaabudu Yesu
Wasabato wanaabudu Yesu.
Mashahidi wa Yehova wanaabudu Yehova.
Wahindu wanaabudu Brahma,Vishnu,Siva(Utatu)
Wabudha wanaabudu Buddha.
Wayahudi wa kale waliabudu Yehova.
 
Maneno meeeeeeeengi....Swali langu ni ....


Je., Ni mungu Wa dini ipi yupo responsible kwenye kuumba binaadamu??

Ukisoma Biblia inasema ni Yehova.Zaburi 83:18
Ukisoma Quran inasema ni Allah.
Biblia ilianza kuandikwa mwaka 1513 BCE Yaani miaka 2,000 kabla ya kuran kuandikwa.Quran inanukuu vifungu vingi kutoka katika Biblia kama mada inavyoonyesha.
kwa hiyo Biblia imetangulia Quran.
 
Ukisoma Biblia inasema ni Yehova.Zaburi 83:18
Ukisoma Quran inasema ni Allah.
Biblia ilianza kuandikwa mwaka 1513 BCE Yaani miaka 2,000 kabla ya kuran kuandikwa.Quran inanukuu vifungu vingi kutoka katika Biblia kama mada inavyoonyesha.
kwa hiyo Biblia imetangulia Quran.

Kwahiyo mungu wa wakristo ndio kaumba mwanadamu?

Na miungu wengine ni feki sio?People are christian-centric....

Kuna dini za mungu mmoja na kuna dini za miungu wengi,kuna madhehebu zaidi ya 30,000 ya kikristo,bado millions of other religions na kila dini ina amini mungu wake ni sahihi wa wengine ni hovyo....ya nini tuamini mmoja na kumkubali mwingine?Kuna uwezekano mmoja akawa wa kweli na wengine wakawa feki?Wa kweli ni yupi?Hatutakaa tujue,kwavile umelelewa kwa mfumo wa abrahmic religion point of view utasema ni ukristo au uislam,kumbuka china,india,japan,russia,etc hawatambui huu ujinga wa abrahmic religilions,na it is not their fault...dini zote ni za kufuta period!
 

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom