Uchawi: Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya 'mwanga' toka Dar mpaka Morogoro

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Gazeti la DarLeo linaandika habari hii ya maisha ya msichana Odillia Mikka (15) ambaye alikuwa ni hausigeli jijini Dar nyumbani kwa mzee Naftali Chacha (60) na kudaiwa kuanza kuwawangia.

Baada ya msichana huyo kusafirishwa kutoka Dar es Salaam kurejea kwao Morogoro, taarifa zinasema baada ya kufika kijijini kwao Yangeyange, alikuta umati wa watu ukimpokea kwa shangwe.

Akizungumza leo asubuhi, kijana Makambi Naftali Chacha, ambaye ni mtoto wa mzee Naftali, alikokuwa akifanya kazi hausigeli huyo, amedai kuwa mara baada ya kufika mkoani Morogoro walikwenda Serikali ya Mtaa kwa ajili ya makabidhiano na ndugu zake.

Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa kijiji cha Yangeyange ulisikitishwa na tukio hilo na walipomhoji kwa kina binti huyo alieleza mambo aliyokuwa akifanya. Wakati umati wa watu umefurika katika ofisi hizo kushuhudia tukio hilo, uongozi wa mtaa huo ulidai kuwa umedhalilishwa na vitendo vya binti huyo alivyofanya akiwa Dar es Salaam. Uongozi huo uliamua kuwaita wazee wa jadi ili waweze kubaini ukweli wa mambo hayo. Wazee hao walikaa na binti huyo kwa muda wa saa kadhaa wakizungumza naye. Hata hivyo alikiri kufanya vitendo hivyo na kuelezea jinsi alivyokuwa akivifanya. Wazee wa jadi waliamua kumnywesha binti huyo dawa za kienyeji za kumuondoa uchawi huo ambaye kwa wakati wote alionekana ni mwenye kujiamini katika kila alichokuwa akikinena kutoka mdomoni mwake. Baada ya kumnywesha dawa hiyo alitapika vitu mbalimbali ikiwamo hirizi. Baadaye aliwaomba wazee hao kuongozana naye moja kwa moja hadi kwa bibi yake huyo.

Umati mkubwa wa wananchi wenye shauku ya kushuhudia mambo hayo waliongozana na binti huyo mithili ya maandamano pamoja na wazee wa jadi hadi nyumbani kwa bibi yake ili akawaoneshe vitu vya kishirikina wanavyotumia na bibi yake. Walipofika hapo inadaiwa kuwa walitoa vitu vingi kwenye nyumba yao ambapo Odillia katika maelezo yake alidai kuwa wana misukule ya watu wengi iliyohifadhiwa hapo ambayo inawasaidia kwenye kazi zao mbalimbali, kikiwamo kilimo.

Alidai kuwa chakula kikuu cha misukule hiyo ni pumba ambazo alikuwa akiwapikia yeye na bibi yake wakati wanaishi hapo Morogoro na mara nyingine misukule hiyo hujipikia yenyewe akiwamo rafiki yake anayedai alikuwa akiitwa Rehema, mkazi wa Yangeyange, ambaye alimuua.

Wakati hayo yakiendelea kijijini kwa Odillia, familia ya Naftali ilikuwa imemkabidhi Biblia binti yao ambaye alikuwa amesafiri na hausigeli kwa ajili ya maombi zaidi. Huku familia ya mzee Naftali ikiendelea na maombi zaidi jijini Dar es Salaam kumuombea Odillia ambaye alikuwa akiwaambia kuwa amesukumwa kufanya shughuli hiyo kutokana na kupata fedha kutoka kwa waganga wa jadi ambapo misukule hiyo huenda kuiba fedha hizo.

Hata hivyo, wakuu wa mila waliompokea katika kijiji cha Kitete karibu na Mdumila walipomhoji alikiri kufanya hayo na kuwaeleza mazito zaidi akidai kuwa wana misukule minne ndani kijijini hapo na kuna baadhi ya wanakijiji wanashirikiana nao katika kazi hiyo. Kutokana na kauli hiyo, mkuu wa mila alifedheheka hivyo kushindwa kuendelea na operesheni hiyo, ndipo alipoamua kupeleka jambo hilo kwa mkubwa wa jadi wa kijiji hicho kwa hatua zaidi.

Huku Odillia akiondoka, familia ya mzee Naftali waliendelea kufanya maombi zaidi ya kufunga na wakimkabidhi Mungu mtoto wao Miriama ambaye alikuwa ameongozana na msichana huyo kwa ajili ya kumrejesha nyumbani kwao Morogoro. "Tuna imani kuwa maombi yanafanyakazi na Mungu atatenda miujiza na tunaomba Odillia arejee tena kwetu kwa ajili ya kumuombea aondokane na tabia hizo," alisema Makambi Naftali.
 
mmmmmmmh haya bana. nadhani itakua poa zaidi wakiwarejesha hao misukule uhalisia wao ili wajirudie kwao,hasa kale katoto alikosema walikachukua tangu kana miaka 2 na sasa kanayo 6.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom