Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,671
- 40,912
Kuna ajira mpya ya kisiasa imezuka katika Taifa letu nayo inaitwa uchawa.
Uchawa ni kitendo cha kuwa mfuasi kindaki ndaki wa mtu kwa matendo na kauli zake bila kujali uhalali wa kile kinachofanywa.
Mtu huyo anaweza kuwa Kiongozi mkuu wa nchi au mwanasiasa yeyote mwenye ushawishi.
Kiongozi mwenye dhamana ya kuliongoza Taifa anao wajibu wa kikatiba kulinda maslahi ya watu wake hivyo inategemewa kwamba kila anachokifanya maslahi ya uma yanapewa kipaumbele.
Ila inapotokea kiongozi huyo akakengeuka katika maamuzi yake basi kwa mifumo ya kiutawala tuliyonayo wananchi wana haki ya kumkumbusha wajibu wake.
Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na nafasi za kukosoana na kushauriana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alituasa vijana tuwe na hulka ya kuhoji , kwamba pale tunapoona kuna jambo linafanyika na tunaamini linafanyika sio kwa maslahi yetu ya Taifa basi tunapaswa kuhoji.
Hali sasa ni tofauti kabisa, kizazi cha kuhoji kinapotea na ni kama hakipo kabisa kwani watu wamegeuka wabinafsi na kuangalia maslahi yao binafsi.
Kijana anaona kuliko kuhoji na kukosa fursa kwa kuonekana mtukutu bora akubaliane na kila jambo la nwanasiasa au kiongozi wa kitaifa ili akumbukwe kwa favours mbali mbali wanaita kulamba asali.
Kitendo hiki kina faida za muda mfupi ila hasara kwa muda mrefu wa vizazi vijavyo kwani kunauwezekano wa matendo ya wanasiasa kuwa ya kuliangamiza Taifa.
Kijana au mtu mwingine yeyote anapamua kuwa chawa anashiriki kuliangamiza Taifa lake kwani kiongozi husika hatakuwa na woga wa kufanya jambo lolote kwani anajua hakuna wa kumhoji kwa lolote.
Hivyo basi ni vyema tukaondoa dhana hii ya uchawa kwani inaliangamiza Taifa.