Uchapaji wa kizamani hivi wakati viongozi wanaelea kwenye bwawa la pesa za walipa kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchapaji wa kizamani hivi wakati viongozi wanaelea kwenye bwawa la pesa za walipa kodi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Candid Scope, Jun 23, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Meneja wa Standard Printers, John Mcharo, (wa pili kulia) akimuonesha pleti ya kuchapishia magazeti Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye,(wa pili kushoto) alipotembelea kiwandani kuona shughuli za uchapishaji wa Magazeti ya Serikali ya Daily News,Sunday News, HABARILEO na HABARILEO Jumapili. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji, Mkumbwa Ally na Msanifu kurasa Mkuu wa Pre Press, Geoffrey Ng'humba

  Serikali inapoteza fedha nyingi katika kwenye anasa za viongozi na watumishi wengine bila kujali taasisi muhimu kama hizi kuziboresha ziwe na vitendea kazi vya kisasa. Magazeti ya serikali na Daily News yanatakiwa yawe na vitendea kazi vya kisasa vya digital badala ya kuwa na plate maker kama hizi ambazo ni za kiwango cha viwanda vidogo na visivyo na matawi mengi yanayotoa nakala za kila siku.

  Nashangaa mtindo huu wa uchapaji kutumia metal plate kwa idadi ya magazeti yanayohitajika nchi nzima tunapoteza fedha nyingi kutengeneza offset metal plates zaidi ya moja kwa kila upande mmoja wa papere sheet. Kama mitambo ya kisasa ya digital ambayo inaweza patikana kwa gharama nafuu ya rais kupunguza safari kama nne tu za kwenda nje unapata mtambo huo na kila asubuhi ya siku hiyo hiyo Mwanza, Mbeya, Arusha, Mtwara na Dodoma wanapata nakala zao.

  Mfumo huu wa uchapaji vifaa vyake mitambo yake bei nafuu lakini vifaa vinavyotumika kila siku ni vingi sana kiasi cha kuumiza kichwa. Kumbuka hapa kwenye pre press department, wanahitaji to develop films kwenye mtambo wake, kisha kuhamishia taswira kwenye hiyo plate wanayoonyesha kwenye picha kwa kutumia mtambo wa plate maker, baada ya hapo hiyo plate inafungwa kwenye offset press kurudufu kurasa. Engrav. printing too big kwa Tanzaania lakini digital ingefaa zaidi.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kikwete akipunguza safari nne kati ya zile alizopanga kwenda nje ya nchi inatosha kununua mtambo wa kisasa, badala ya kuendelea na mfumo huu wa uchapaji wa miaka 50 iliyopita.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Halafu mfumo huu wa uchapaji wa offset kwenye pre press madawa yatumikayo ni hatari sana kwa afya ya binadamu, ingawa ditigal ink ni hatari zaidi lakini haishikwi kwa mkono kama madawa mengine kwenye offset press.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Size ya plate ni kubwa kuliko film na hivyo kingo kubaki na masalia ya tawirai isiyoakisiwa maana awali nilidhani wanatumia negative plate lakini baada ya kuangalia sana inaonekana kama wanatumia positive plates.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nape ni kiongozi wa chama, sasa zile mbio za kuzungukia mikoa zimeishia wapi? Au kwa vile wahudhuriaji walikuwa ni wanafunzi na wale waliogawiwa nguo na hivyo kukosa mvuto sasa anageukia upande wa vyombo vya serikali kuteka wafanyekazi kwa ajili yake?
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Inatakiwa magazeti ya serikali ambayo ndio matoleo makubwa nchini yawe na sub-editorial board za kanda ambazo kuanakuwa na full webpress. Katika vituo huvyo kutakuwa na regular pages amazo hutolwea nchi nzima na insert pages ambazo zina regional end city news. Kwa utaratibu huo mitambo ya kanda ya Ziwa, kaskazini, kati, kusini nyanda za juu na kusini nakala zingetoka muda na wakati huo huo zinapotoka za dar na hivyo kupata nakala muda huo huo nchi nzima walao maeneo yanayofikika kirahisi. Lakini kwa mwendo huu pesa inaliwa na wenye nafasi vyombo hivi vya habari na uboreshaji wake unabaki hadithi za kufikitika tu.
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli mtindo wa kusafirisha magazeti kutoka Dar kwenda mikoa yote kila siku ni wa enzi za mawe za kale!
   
Loading...