Uchambuzi Yakinifu Kuhusu Matokeo ya Urais 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchambuzi Yakinifu Kuhusu Matokeo ya Urais 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by FarLeftist, Nov 4, 2010.

 1. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wadau naomba michango yenu juu ya hili swala,

  Hivi inawezekana vipi kwenye mkoa mmoja ukakuta CHADEMA imeshinda kata 12 kati ya 14 au imenyakua majimbo yote, wakati huo huo kwenye matokeo ya urais CCM ikaongoza wakifatiwa na CUF, Je kuna punguani yupi ambaye anaweza akapiga kura kuchagua Diwani na Mbunge wa CHADEMA alafu urais akachagua CCM?

  Nashindwa kuelewa hata kama ni kuchakachua si inatakiwa akili kidogo itumike?
   
 2. markach

  markach Senior Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tupe data, Je ni jimbo gani hilo?
   
 3. F

  Ferds JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mbona hujiulizi jimbo la Bukoba mjini Kagasheki na madiwani wameshinda wakati urais Dr Slaa kamwaga baba Ridhwaan, Pumbavu uwe mtu wa kufikiri, kumbe wewe ni kada wa chama na sio mabadiliko, udiwani anagombea mwingine, ubunge ni mwingine na urais ni mwingine japo wapo ndani ya chama kimoja. Mnaniudh mnaposhindwa kureason vitu vidogo vidogo,
   
 4. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakuna punguani yoyote anayeweza kuachagua diwani na mbunge wa CHADEMA alafu urais achague CCM ni logic ndogo tu huitaji kuwa kada wa chama chochote umenisoma mdau ktk tume?
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wachakachuaji utawatambua tu.
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  nafikiri unahitaji elimu ya nini nini maana ya mkoa, wilaya, tarafa, jimbo, kata halafu ndio utaweza kuchangia hoja yako vyema. Kwani huwezi kuzungumzia ngazi ya kata katika mkoa kama ulivyofanya na ukaacha kutaja kata husika ipo katika wilaya ipi, jimbo lipi la uchaguzi n.k.

  Nahisi habari zako ni za kusikia, kuhisi au kutunga. Kibaya zaidi umeshindwa kutupatia reference za mkoa upi unazungumzia, kata zipi zimechukuliwa na chadema na zipi ccm na idadi ya kura za kikwete na slaa kwa mujibu wa tume katika kata unayozungumzia.

  Kabla ya uchaguzi wa 2010, wachangiaji hapa walikuwa wakija na data kamili lakini katika kipindi cha uchaguzi na baada kuna watu wanaonekana kuleta hoja bila uthibitisho. Hii ni hatari katika kipindi hiki cha kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, kwani mnaweza kuleta uchochezi na kuhatarisha amani na tutlivu tulionao.

  Tatizo la wengi wetu tulishiriki katika uchaguzi huu kishabiki tu, wakati naomba kura za wagombea wa chadema mtu kwa mtu wapo wengi waliniahidi kuwa watamchagua mnyika na diwani wake lakini kura watampa kikwete, wapo wengine waliniahidi kuwa watamchagua mnyika kama mbunge lakini uraisi watampa kikwete na udiwani walisema hajaamua kwa kuwa dmgombea udiwani wetiu alikuwa mgeni kidogo.

  Hata katika kuhesabu kura matokeo yalionyesha mnyika alikuwa akizidi kura za dr slaa kuthibitisha kuwa hata waliomchagua kikwete katika ubunge walimchagua mnyika. Hapa sisemi kuwa kura za dr slaa hazikuibiwa, ndio maana ni vyema kusubiri kauli ya chadema kama alivyoahidi marando kuwa watataja ni katika vituo vipi, majimbo yapi kura za dr slaa zilizotangazwa na tume ya uchaguzi zintofautiana na zile zilizokwenye fomu za matokeo zilizosainiwa na wasimamizai wa vituo na mawakala.

  This is home for great thinkers
  , leteni vitu vyenye uthibitisho.
   
 7. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni rahisi tu kusema tupe data. Data zipo hata wewe waweza kupata, lakini swali la kujiuliza ni kuwa ukipewa itakusaidia nini na wewe ni nani? Maana yake maeneo mengi matokeo yanayotangazwa kura zinazotangazwa na wasimamizi ni tofauti na kura zilizopatikana.
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hali halisi niliyo ipata kutoka katika baadhi wa watu waliokuwa wakiziingiza izo data ni kuwa ukikuta JK kapata 10,000 Kata A na Dr. Slaa kapata 8,000 kata Hiyo hiyo basi anaye ingiza atakiwa apunguze zaidi za Dr.Slaa mpaka ifike 2,000, Lakini ukija kweny Original Documents Unakuta sio na ndio maana haiingii akilini mwa mwananchi kuwa CHADEMA mahapi pengine wameshida madiwani,ubunge,na Rais cha ajabu JK atapewa kura nyingi zaid hapo sasa sielewi ni kulipotosha Taifa ili REDET waonekane walitabili vyema kiukweli kama JK alikuwa anapata kura nyingi kusinge kuwepo na malalamiko mengi mbona 2005 haya yeye JK hakuamini kupata kura nyingi na akasema hata wapinzani wamempa kura na jambo ni la kweli sasa imani imepungua kwa wananchi sasa anataka kulazimisha wananchi bado wa naimani nae hilo JK hasijaribu kuupotosha Uma wa watanzani akwani wanajua walipiga kura vipi. sasa hili litawagharimu sana NEC na Usalama wa Taifa na Hao Police wanao tutolea taarifa za uongo ati kuna tukio lataka kutokea mumejua aje kama nyie sio mnaopanga na kujua mlifanyalo wananchi hawtolipenda na si kweli

   
 9. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Tusipende kubisha sana tuu ilimladi umebisha,

  Huyu bwana analolisema lipo kabisa kama kweli wewe ni mtu unae fuatilia siasa za TZ kwa umakini na ukaribu hili ulipaswa ulijue tena mapema siku baada ya matoke yametoka kwani wengine tulikuweko kwenye mchakato kabisa na tunajua sasa nawe usipende kuletewa habari tafuta au umetumwa au hauko TZ? na kama uko TZ hili si swala la kupuuzia hata kidogo

   
 10. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hicho ndicho kilichobaki!
   
 11. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hiyo CCM na NEC yao wamefanya kwenye baadhai ya majimbo ili na wao wakifanya kwenye majiombo ambayo CHADEMA imeshinda isionekane ni issue uwe na akili kijana dada
   
 12. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hivi Pumbavu siyo tusi?
  kama ni kisifa tu basi wewe ni Lipumbavu, tathimini inaonyesha matokeo yamechakachuliwa kiasi kwamba hata ninyi wenyewe mmejiibia kwenye baadhi ya majimbo,i guess bukoba is one of them.
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  NEC ni tawi la CCM, kibaya zaidi wanachakachua kwa KASI ZAIDI, ARI ZAIDI bila kutumia akili hata moja.
   
 14. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  u can fool some people for some time and not all the peole all the time.
   
 15. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Dah..hii kali mkuu.
   
 16. J

  Jafar JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Walituambia ukushapiga kura yako nenda nyumbani ukasubiri matokeo (pale ambapo wali-undo hilo wamefanikiwa)
  " ... wao wana pesa, sisi tuna Mungu ... " (Godbless Lema, MB)
   
 17. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha habari ya lecturer fulani mnoko. Wanafunzi waliiba marking scheme yake na hivyo majibu na kudesa kama yalivyo kwenye mtihani lakini kwa vile ni mnoko alitembeza "below" yaani fail karibu darasa zima na kuwashangaa wanafunzi walifundishwa na mwalimu gani asiye na akili uko A level! CCM inachakachua mpaka inajichakachua!
   
 18. F

  Ferds JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi naona wotw mna mtindio wa ubongo, Dr Slaa c wakwanza kuyakataa matokeo ktk chaguzi duniani, ni chaguzi chache sana ambazo watu wamekubali kushindwa yeye si wakwanza. Hivi watu wengine mna mapenzi hata shetani hana eti jitu zima na minywele yake kila panapostahili kuota nywele linasema eti lilidokezwa kuwa ktk kuingiza data , unapokuta Jk 10000, slaa ana 8000, eti za slaa zinapunguzwa hadi 2000, kwanza tayari kashavukwa kura 2000, halafu wampunguzie we mwehu nini? mimi nimewawakisha chadema kwa taarifa yako jimbo la ukonga, tumegalagazwa mbaya hata kura kuhesabu tumehesabu zaidi ya mara moja halafu kuna pimbi anasema tumeibiwa hata jimbo hilo, kwanza najutia kukesha kwangu na kumobilize watu wasilale walinde kura, leo tunaanza kutafuta visingizio, Arusha mjini hata sisi tumeiba, wamasai kibao walikuwa wanakuja hawajui chadema wanauliza iko wapi ile chama ya kijani mwalimu aliyesimamia kwa bias anawaonyesha chadema, sasa huu nao siwizi mbona hamuusemi, tukaechini tutafakari nini cha kufanya tuache visingizio, wote tulienda vitani tukijua slaa anashindwa, Irregulariries ktk election sio chanzo cha kutupeleka mabarabarani, halafu wewe mkereketwa ulioniita lipumbavu, basi wewe ni lipumbavu mara tilioni mbili zaidi yangu, mshenzi kabisa
   
 19. E

  Elifasi Senior Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...absolutely, katika uongo si ukweli unawekwa kidogo ili kunakshi na kudadisha uongo wenyewe? Mbona fikra zetu znapungua kasi ya kufikiri? Yaani kweli unaweza kuamini kabisa kabisa kwamba the fools that have been fooled for sometimes are here to be fooled all the time? Kumbuka: wanaochakachuliwa si Slaa au Mpendazoe, au Maalim Seif.... wao wanajua jinsi ya kula hata baada ya kukosa.

  WANAOCHAKACHULIWA CHOKA MBAYA NI MIMI NA WEWE ambao tuliacha usingizi tukijidai tunachukua haki yetu kikatiba ya kumchagua tunayempenda, kumbe yote yale ni kiini macho! Tutakaa tunashabikia shabikia KULA kwa wenzetu, mpaka watakuja na uani kwetu, wakimaliza, wanaingia vyumbani...na wanavyopenda visasi hawakwachi! (..unajisemea WASHAANZA?)
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  ili kuepuka uchochezi katika kipindi hiki ambacho green guard wa ccm wakiwa wamevaa mavazi ya chadema wanasubiri wanachadema waanze kupinga matokeo wapige watu, wajeruhi watu na hata kuua ili chadema ionekana haifai mbele ya macho ya jamii. Ndio maana kama kweli una uchungu tunataka ututhibitishie source ya huo uchungu uliokupata. Hoja yako kuwa kuwa" maeneo mengi matokeo yanayotangazwa kura zinazotangazwa na wasimamizi ni tofauti na kura zilizopatikana" inaonyesha kuwa hata haufahamu nani anatangaza matokeo ndio maana kwa kuwa suala hii linagusa maisha ya watu ni vyema likazungumzwa na watu wanaojua nini wanaongea
   
Loading...