Uchambuzi wangu wa hotuba ya JK unaleta maswali mengi yasiyojibika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchambuzi wangu wa hotuba ya JK unaleta maswali mengi yasiyojibika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Nov 19, 2011.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  JK anapolinganisha Uchumi wa nchi EAC

  1. Mbona anakwepa kuelezea kwanini Rwanda wanaofanya vizuri?

  2. Anasema sisi ndiyo tunasupply wenzetu na chakula. Iweje basi anayemlisha mwenzake awe na hali mbaya hata kuliko anayelishwa? Au hatuwauzii tunawapa bure?

  3. Anasema ili kupambana na kushuka kwa dhamani ya shilingi tunadhibiti fedha za kigeni kweli hiyo? Mbona tunaona uholela usiyo kifani- Bureau de change hadi vichochoroni huku ndiko kudhibiti fedha za kigeni?hivi hizi bureau zinalenga kujibu hitaji gani la mtanzania wa kawaida zaidi ya kuvuruga suppy -demand ya fedha za kigeni - kichekesho ukitaka kununua $ 500 kulipia masomo nje kupitia benki unaulizwa maswali lukuki, japo nchi hiyohiyo ukitaka $10,000 za kwenda kutanua Kempsiki serengeti unapata bureau ndani ya dakika.

  4. Unasema tunaathiriwa na kupanda kwa kwa mafuta bei ya mafuta? Sawa mbona hutuambii pia tunaathirikaje na kupanda kwa bei ya dhahabu ambayo mauzo ya Tz yanaongezeka kila kukicha? Hivi haya ndiyo yanayofanya shilingi iporomoke au? Hiki kiini macho mbona huwaelezi wazee?

  5. Unazungumzia waziri kukuta sukari yetu supermarket za nchi jirani -ina maana tumeingiza forex nyingi au?

  Kuhusu mchakato wa katiba mpya

  Hukuhitaji kuanza na kuorodhesha katiba za nyuma kwani ukiwa safarini majuu huku wataalamu walikwisha waeleza kwa ufasaha mkubwa watanzania wote (siyo wazee wa CCM tu) kuhusu hilo. Uchambuzi wao ulikuwa mpana hata kufikia kutaja washiriki walivyopatikana na tafsiri ya kilichopatikana, uhalali wake kwa maana ya kisheria na hata legitimacy yake. Waliweza kufafanua kwa nini leo tunachokitaka ni TOFAUTI. Hivi umefuatiliwa mijadala iliyoendeshwa hapa bara na visiwani kuhusu mchakato huu?

  Wewe umeeleza walivyofanya wengine na kutumia hii kuhalalisha na wewe kuiga (hili la kujilinganisha siku zote linakuangusha, unapenda sana- Mzee wa 'Business as Usual -BAU').

  Nakumbuka ukiwahutubia hao wazee uliwahi kusema kuwa Tz ilimshinda hata Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Swali ni je, kwa hiyo na wewe tuendelee kukuacha wakati tunaona wazi unashindwa? Tusitake kurebisha ili aje anayejiamini kuweza na sio anatetea kushindwa kwake kwa kuwasema waliopita?

  ULICHOSAHAU KIKUBWA KABISA NI KUWA SAFARI HII SISI TUNATAKA KATIBA YA WATANZANIA (WANANCHI)

  Ungelielewa hili tu ungejua ili upate hii katiba ya tofauti wewe unatakiwa utofautiane na waliotangulia.

  Au unaamini katika maajabu kuwa utachemsha upate omlet?
   
 2. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Siku hizi hotuba zake zimepoteza hata mvuto!
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  baada ya kuisoma, nimegundua kuwa mkuu wetu analalamika sana tena kwa mambo amabyo yako ndani ya uwezo wake..................... mfano anaposema "mbona marais wengine walifanya na hakukuwa na maneno, kwa nini rais wa sasa akifanya, yanatokea maneno".............. nadhani anapaswa kutambua kuwa yerye ni rais wa wakti "huu" na sio "ule"...................

  nilijikuta nacheka mwenyewe aliposema kuwa "itabidi ajaribu udikteta kidogo ili wale wanaomuita dikteta waione "tofauti"........., siasa hizi bana!! yaani mtu unaweza kuvunjika mbavu bure kwa kucheka...................... tena kauli ya rais, eti akizungumza na "wazee".............. hebu mshaurini siku moja azungumze na vijana .................
   
 4. Kadamfu

  Kadamfu Senior Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijaickiliza hotuba na wala cjutii 'ma decision coz haina msaada wowote kwa watanzania'na hivi wale wazee wa dar au wazee wa magamba?
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kabla ya kuwa dikiteta amtumie SMS Gadafi kupata ushauri
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Akili kichwani,hawezi kuzungumza na vijana,watamchallenge! Hot soup iko hot kweli kweli!
   
 7. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  usiingize kidole kwenye shimo la siaf
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Mkuu naomba na mie niishibishe thread yako kwa niliyoyaona,kwanza niwe bayana J.K ni dikteta,kwanini?

  J.K anaitumia katiba ya sasa ambayo Mwalimu,Baba wa Taifa aliwahi kusema inaruhusu rais kuwa dikteta kukamilisha kilichosemwa,anasema hajavunja sheria yoyote wala katiba katika kupeleka mswada bungeni kwa mara ya pili huku akisahau tayari amevunja katiba yetu ibara ya 8 inayowapa wananchi mamlaka juu ya serikali yao,hiyo ni moja.

  La pili ni matumizi ya sheria pasipo kutizama mazingira ya maamuzi,kimsingi matumizi ya sheria is to find out the legality of the made decision and not whether the decision was rational...sasa hili katika katiba mpya ni kwa masrahi ya nani?anajua kwamba likatiba hili la leo ni libovu na anatumia nafasi hiyo kuwanyonga watu,sie katika hili hatuhitaji sheria zinasemaje sana kwani kwanza sheria mama yenyewe siyo yetu ni mali ya ccm,sasa ya nini iwe kikwazo?
  Wananchi hatuhitaji sheria inasemaje(legality),tunahitaji atizame wananchi tunahitaji nini na kwanini(rationality) potelea mbali sheria inasemaje,narudia tena J.K akitumia katiba ya ccm kuwanyonga watu kutokupata katiba yao kwa kisingizio cha sheria atakuwa anadhihirisha udikteta na anafaa kabisa kuitwa dikteta hapa duniani

  Mkuu nawasilisha.
   
 9. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,063
  Likes Received: 7,529
  Trophy Points: 280
  Kama akili zingekuwa zinapimwa kwa urefu nisingehitaji kamba ndefu, nadhani ukuchu wangu wa kidole cha mwisho ungefaa, na kama zingekuwa zinapimwa kwa uzito basi zingelingana na nusu ya manyoa yaliyo mwilini mwa kifaranga cha kuku.
  Kuhusu udikteta kuwa 'atajaribu ili waone tofauti' anamlenga nani? Sababu sasa hvi ana makundi mengi hasimu yanayoongezeka kila uchao ikiwemo zaidi ya nusu ya wananchi wake,(rejea chaguzi za mwisho na hotuba yake ya jana).
   
 10. Brine

  Brine JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 376
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata gaddafi alijiona siyo dikiteta kwa mtazamo wake.
   
 11. U

  Userne JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hebu JK, Jiweke kwenye nafasi ya vijana ili uwatambue na UJITAMBUE! Ufahamu kuwa kilicho zaliwa ni bora kuliko kilicho zaa! Wazee ni saa11 na nusu bado jua kuzama, hata hilo hutambui?
   
Loading...