Uchambuzi wangu na maoni kuhusu serikali na rais John Pombe Magufuli

remosa

Senior Member
Oct 3, 2014
161
141
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
Nawasalimu All great thinkers.. (hii inahusu wale wote wanaosimamia facts na sio imani).
Nimekaa mda mrefu nkifatilia mijadala ya watu mitaani, ofisini, mitandaoni na hata maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi.

Na nimegundua kuwa %85 ha watz hawana uelewa kabisa juu ya sheria, kanuni, na taratibu za nchi na kibaya zaidi hata katiba hawaijui KABISA!

SI hivo Tu Bali pia hata hawajui kwa nini serikali ipo na kwa nini bunge lipo na kwa nini Kuna mahakama... Sana Sana wanaongea Yale waliokariri tu.... Na hii ndo fursa kubwa ambayo wanasiasa wanaitumia kujipatia sifa na pia kujiona wao ndo kila kitu..... Kuna mambo machache nataka niongee kama ifuatavyo;

(1) BUNGE.
Labda nianze na kwa nini bunge.
Hapo zamani before population haijawa kubwa ( zama za mawe mpaka za vyuma) jamii zilikaa either chini ya mti or kwa kiongozi na kuanza kujadili matatizo kadha WA kadha yaliokuw yanawakabili na kupanga mipango (Ni kama bajeti hivi) na kuunda sheria ili ziwaongoze jamii husika.

Na mikutano hii sababu watu walikua wachache hawajazaliana Sana basi wananchi wote walishiriki mijadala.
Baadae baada ya jamii kuongezeka (population growth) ikaonekana kua SI rahisi watu milion moja au 2 wakakaa pamoja na wakasikilizana mbele ya chifu au mtawala wao ambapo hata wakisema wote wachangie mada hawataweza kumaliza.

Basi wakaona waunde bunge (kila watu waliita kwa lugha Yao) basi wanasema haya kila kabila na Kila jamii iteue mjumbe wake na hao wajumbe(wabunge) wawe ndio wanaoenda kujadili katika mikutano yote na kutoa maoni kwa niaba ya jamii iliomtuma.

Basi nae kiongozi akapewa ruksa ya kutafta washauri (kwa Leo mawaziri) ataokua anasaidiana nao.. Basi na ikawa hivo... Na mikutano yote haikuwa na usiri wowote kwani mambo yalihusu jamii husika hivo usiri haukutakiwa...

Haya Leo hii serikali haitaki mijadala ya bunge iwe live.(nasema serikali coz great thinkers yeyote atakua ashasoma mazingira na hiyo ndo sifa kubwa ya great thinker cas huweza kugundua jambo lililojificha kwa kusoma mazingira.... How? Why? Kwa nini ikataze?? Hatujiulizi?

MMOJA akatumwa aseme ooh mda huo WA bunge live watu wanakua makazini.. Who told them that? Na je zile tv maoficn tena ya serikali kazi yake huwa Ni nini?

Na je mbona wasikataze channel zingine kuonekana muda huo? Ni kweli kwamba Ni bunge Tu ndo linalofanya watu wasifanye kazi?
Mbona raisi anafanya ziara na mikutano ambayo sometimes inaoneshwa live who is he? So mda huo watu wanakua wamefumba macho au?

Na hizo kazi Ni kweli znafanyika ofisini Tu? Vipi wale wafanyabiashara ambao wapo kwenye maduka Yao mda huo? Au Ni wafanya kazi Tu WA maofisini ndo ambao wanatakiwa kuwa regarded?? Nina maswali mengi juu ya hili mpaka naugua..

akatumwa tena yule yule mtu aje aseme ooh tunasave bajeti
Sasa mbona watu walipojitolea kughalamia matangazo ya bunge mkakataa? Why? Ni nini hicho ambacho mnajadili huko ambacho mwananch hatakiwi kukijua?

Kama Kuna jipya mnalojadili na sio kwa manufaa ya nchi is Better mfunge bunge coz kazi ya bunge Ni moja Tu!! Kujadili maswala yanayohusu wananchi tena kwa uwazi.

jamani wananchi tuelewe kua bunge lipo kwa ajili ya wananchi.. Na ukiona kiongozi Wako anakuficha jambo ujue Kuna walakin..
USHAURI: Serikali muache kuingilia uhuru WA bunge.. Na kama kweli serikali Ina Nia ya dhati kwa wananchi wake basi bunge live Na isiwe ombi Bali Ni lazima...!!

*BAADHI YA MAONI YA WANANCHI
-Kuna wanaosema ooh tunataka kazi Tu na sio kuona bunge live..
sikieni nyie mliotokwa na akili hiyo kazi Tu mtaijuaje kama hakuna uhuru wa habari? SI tuna migodi? SI tuna misitu? SI na kazi znafanyika mnaziiona? Haya bila bunge lililopita kuoneshwa live mngejuaje kuwa kwenye migodi tunapoteza pesa nyingi?
Nani angejua kuhusu escrow.. Nani angejua Kuna wabunge wana akili fupi kama lusinde? Nani angejua nk......

-Kuna wanaosema ooh wabunge wanataka wauze sura Tu.... Nyie hata sjui niwajibu nn cas nahisi hamtaelewa coz Hamtumii akili kufkili ngoja nikijua mnawaza kutumia nini labda tafanikiwa kuwashauri.

(2)NCHI YA VIWANDA
jamani serikali Ni nani aliewaambia viwanda Ni kama uyoga unaokua hata sehemu chafu?

Nchi ya viwanda ni ndoto na nawaambia hakika kama mwendo Ni huu huu basi hakuna viwanda vitavyojengwa....

Serikali haipo upande wa wafanya biashara wala wa wananchi.... Sjui hata ipo uoande gani coz hakuna mtu yoyote tajiri ambae ataenda kuwekeza mahala ambapo serikali sio rafiki....

Na nyie wananchi mnaobeza wanaosema serikali ya viwanda Ni ndoto jueni kua hivo viwanda anavoongerea magu Ni vya watu binafsi...

Yani Mimi Nina pesa zangu ndo nije kuwekeza.... Nakwambia hakuna mtu ambae atakuja kurisk pesa zake kwa kuanzisha viwanda vikubwa wakati sera ya nchi Tu haijakaa sawa.....

Inabana watu kwenye kodi mno... Kodi Ni kubwa Sana... Sisemi kwamba hawatakiw kulipa kodi no! Kodi sio ombi Ni lazima Bali mimi naongelea kiwango cha kodi... Hata process zetu za uwekezaji jaman Ni mbaya mno.

Mtaendelea kuwafurahia wachina na wahindi Kuja kuwekeza but trust me hakuna watu wezi na wababaishaji kama wachina na wahindi...

Wachina wapo hapa kwa maslahi ya nchi yao and not as you think!! Serikali haina budi kuandaa mazingra mazuri kwanza kwa kurekebisha sheria zote za kodi.... Tuache ubabaishaji jamani....

Raisi nae anaongea mno kuliko vitendo.... Anawapa watu hopes ambazo si rahisi na kuaminisha umma kwamba Ni rahisi.

.Viwanda Ni process jamani hata nchi zwnye viwanda vingi iliwachukua more than 30 yrs kufika walipo....
Na viwanda tusitegemee watu watoke nnchi zao waje wawekeze kwetu jaman... Hebu serikali ifanye kuwawezesha wananchi wawez kuwekeza kwanza....

Serikali iache kukataa ushauri jamani.... I dislike a lot hii mambo ya viongozi wa serikali kutwa kukimbizana na wapinzani kwenye media mala huyu kasema hiki mara huyu kafanya vile mara tetesi mara sijui wadudu gani....

Tuache jamani tukae chini tuone Ni nini kifanyike ili after some years tuwe na viwanda nchini... Sio lazma Magufuli atekeleze Hilo jaman sio rahisi lakini anaweza kuanza sasa kuandaa mazingira kwa kuwekeza katika utalii kwa kuunda miundombnu ya kisasa ya kitalii ili kila mtalii ataekuja avutiwe na kuja kuwekeza hivi viwanda....

*BAADHI YA MAONI YA WANANCHI
-Ooh tumuache raisi cas hajamaliza hata mwaka.... Nasema tena mkome kuleta mambo yenu ya miaka hapa...
Who told u that mpaka mwaka uishe ndo tumkosoe? Nambieni hii miezi alokaa madarakani kafanya nn ambacho kimemgusa mwananchi WA kawaida direct??

Sana Sana mtanambia maneno ya kisiasa Tu mala ooh alisema hivi alisema vile but what we need here is Ni kwa jinsi gani hayo yatafanyika? Hebu tuone basi hata progress ya Yale yaloanza kusemwa na kuahidiwa kitambo.....

USHAURI.
Serikali sasa ikae chini ijitathmini upya... Iteni Sana wanuchumi iteni watu mashughuri kutoka nchi zilizoendelea basi mkae mdiscuss jinsi gani ya kuwapata wawekezaj wa hivyo viwanda...
Haya maswala ya media achieni diamond na wema na zari nyie hamuyawezi....

(3) RAISI MAGUFULI
Nakupenda Sana raisi wangu ILA upendo wangu unapungua siku hadi siku and now umebaki 23% Tu...

Na hii Ni baada ya kugundua kuwa wewe pia ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine ambao sifa Yao kubwa Ni uongo, maneni mengi bila vitendo na kupenda kujitetea na kutafta huruma ya wananchi....

Vyote hivo unavyo.... Kama unavosema hapa kazi Tu kaa ukijua kuwa wewe Ni mfanya kazi wetu... Tumekuajiri na Ni lazima ututumikie sisi maboss zako...

Mwaswala ya kutafuta sympathy Ni unafki mkubwa coz mtu serious na mwenye Nia na msimamo huwa haitaji huruma ya mtu kwa sababu anayofanya wananchi watayaona....

Haya maswala ya kutumbua majipu sjui chunusi sio wakati wake sasa.... Huu Ni mda WA wewe kutafta namna ya kuzba mianya ya wizi WA fedha za umma na kuweka sheria kali kwa wafanyakazi (sio kuwatisha) na kutengeneza mfumo unaotenda kazi bila shuruti...

Unajua watu now sio kwamba wamebadilika bali wanafanya kazi kwa hofu kitu ambacho sio kizuri coz hata kama kuna jambo fulan watu hawataweza kukushauri au kusema wataacha Tu mambo yaharibike ili nawe uisome namba...

Ogopa Sana watu wanapokuwa kimya wasikwambie Ni nini wanawaza coz hautaamini watachokufanyia....

Acha maneno mengi coz uongozi sio kuongea na kutisha watu au kufanya ubabe no!! Uongozi Ni kutumia hekima....
Mtu mwenye hekima hupima upepo.... Hujua wakati na majira sahihi ya kusema jambo... Na nikuambie kitu Rais wangu... Biblia inasena ole wao wanafiki!!

Nadhani maana ya unafki ipo kwenye kamusi ya kiswahili pia... Je hekima halii?? Ufahamu kutoa sauti yake.... Hekima hekima hekima sina mengi ya kuelezea ILA kwa ufikiri ni wapi ambapo hukutumia hekima coz hekima Ni bora kuliko mali na ukiwa na mali ukakosa hekima Ni sawa na kujilisha upepo..

Wapata faida gani? Kwa mimi naona mwenendo WA sasa WA wewe na serikali yako hauna direction maybe direction ipo but I don't see it... Tengenezeni upya njia zenu... Kama mguu Wako ukikukosesha katika kufkkia malengo yako basi huna budi kuukata... Halikadharika jicho PIA...

NIKIPATA MDA WA KUANDIKA TENA TAENDELEZA MAKALA HII... SIJAMALIZA BADO... NINA MENGI MENGI AMBAYO YAMENIKERA
 
Soma warumi.13:1-7 utaelewa.Fanya kazi.zako.za maendeleo.acha siasa..
huwwzi tenganisha maisha yako na siasa labda uhame duniani cas impact ya siasa inakugusa direct... Kama hujawah kulalamika kuhusu miundombinu basi itakua uliwah kulalamika kuhusu kodi, kama sio kodi basi mishahara ,kama sio mshahara basi huduma za hospital, kama sio hyo basi kupanda kwa gharama za maisha.. Kama hujawah kulalamika hayo PIA bado naamini Kuna mahali ulikwazaka.... I'm telling that huwez kujitenga na siasa no matter what!
 
Umeandika kwa uchungu mkubwa sana pamoja na makosa madogo madogo ya kiuandishi. Lakini umeandika ukweli mchungu. Ngoja waje wale watetez wa mfalme uone watakavyoporomosha matusi
Mi huwa nashangaa Sana wale wanaotukana watu mkuu pale wanapojaribu kumkosoa raisi.. Jamani sisi ndo tuliemuajiri na tumempa only 5 years kiasi kwamba asipofanya vizuri basi tunamfukuza kazi kwa kura zetu... Sasa nashangaa badala tuungane kukemea uovu na kumkosoa pale anapokosea sisi tunakalia kumnanga mtoa hoja.... Jaman maendeleo hayaji hivi guys... Wamarekani walisimama wakapinga kwa nguvu zote na kwa umoja haya yalipotaka kutokea kwao lakin Leo hii demokrasia kwao Ni kitu kikubwa na haki inatendeka... We know that hatuwez kuwa na full democracy but we can reduce uonevu.... Utalipwa pesa Leo ya kutukana mtandaoni but impact yake watakuja kuipata vizazi vyako... Kama ambavyo watu ambao wazazi wao hawakusoma zamani vizazi vyao Leo ndo vinavyo hangaishwa na umaskini sababu wazazi walibweteka katika kutafuta... Maamuzi ya Leo ndo matokeo ya kesho...
 
Miezi km mitatu iliyopita mi binafsi nilikuwa naona nchi inakoelekea, kwa sasa nimepotea njia kabisa, cjui km ndo tunarudi nyuma? tunaenda mbele? tumesimama? tunaelekea kushoto au kulia? Ktu gani kinaendelea serikalini? Hivi bungeni wanajadili nn?Hivi katba mpya ilishapatkana? Vipi kuhusu vitambulisho vya Taifa? Ishu ya Lugumi tumefka mwisho? UKAWA watarudi bungeni lin? Naomba kujua aliko Spika wangu wa Bunge? Na akina Tundu Lissu ndo tuseme hadi 2017?Lipumba nae anaenda mara mi narudi tena! Zitto nae hatakiwi kuongea chochote! Gwajima nae kakinukisha! Ofisi zote za serikali zmejaa hofu! Kwani kuna nn? Mtaani hakusomeki! Vipi bei elekezi ya sukari? Jamani ndo tuseme wafanya biashara wamekaidi agizo la serikali?…. Kwa kweli mi naona giza tu, nimesahau Tulikotoka,?Tuko wapi? Na Tunaelekea wapi?
 
China isingefika ilipo kama ingekuwa na kizazi cha vijana kama walio wengi Tanzania.,kila Mara nauliza swali bunge halipo live miezi kibao sasa hivi ni taarifa IPI ya bungeni mliyoikosa??,kwanini watanzania hatutaki kuwa bize kabisa kutwa kulalamika tu??.,bajeti inayojadiliwa imetenga pesa kibao kuwasaidia vijana,Mimi nimeenda juzi wizara ya viwanda na simjui mtu,nikapewa takwimu ila nikaambiwa nisubiri ikipita ndo nipeleke mawazo yangu,ila wengi humu JF mpo bize kukandia serikali na kubishana kuhusu wanasiasa bila kuja muda unawaacha.Hata mkionyeshwa bunge live wabunge wenu ndo hao wanatoka nje kila siku,waliobaki wanajadili utumbo tu.Ukiruhusu kuwa mlalamishi huwezi kupiga hatua.,serikali ni ile ile,miaka mitano itaisha,itarudi tena hii hii maana tume ya uchaguzi ni ile ile,ila wengi humu mtakuwa mmepoteza muda mwingi Kwa kelele nyingi sana.Maendeleo yako yanakutegemea wewe kwanza,siasa zinarudisha nyuma Sanaa.Hasa siasa zetu za ulimwengu wa tatu.Ni ushauri tu.
 
Yani Ni vulugu Tu... Na watz sisi jamani Ni warahic mno kusahau... Na waandishi wetu cjui wakoje... Yani hawaibui mambo kabisa.. Wala hawayafatilii yalipo.... Badala serikali ikae chini iangalie sasa Ni miradi gani ya maendeleo itayowagusa wananchi.. Wao wamekalia mambo ya miaka 20 mbele... Mambo yanayowagusa watu wote mpaka WA hali ya chini ndo hayo we need... Jamani maji, afya, kushughulikia,mfumuko WA bei, uzalishaji na upatikanaji WA vyakula kwa gharama nafuu, usafiri, umeme, nk hayo ndo ya msingi... Ni kweli we need money but zilizopo zikitumika vizuri zinatosha kufanya hayo yote.... Sasa unapobana mzunguko WA fedha unawaumiza wananchi.... Cas kama mtu kipato chake kilikia 50000 aliweza kunnua sukari, nguo, chakula nk ( wauzaju WA sukari, nguo, vyakula nk walioingiza kipato) Leo hii akawa hapati hiyo elf 50 automatically hawa wauzajj WA sukari, vyakula na nguo wataathirika cas huyo haji kununua kwao tena... Na akija basi anannua kidgo tena kwa nadra Sana..... Swala hapa Ni kuhakikisha Kuna vipato vya uhakika kwa wananchi wote
 
Nakupenda Sana raisi wangu ILA upendo wangu unapungua siku hadi siku and now umebaki 23% Tu...

Na hii Ni baada ya kugundua kuwa wewe pia ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine ambao sifa Yao kubwa Ni uongo, maneni mengi bila vitendo na kupenda kujitetea na kutafta huruma ya wananchi....

Vyote hivo unavyo.... Kama unavosema hapa kazi Tu kaa ukijua kuwa wewe Ni mfanya kazi wetu... Tumekuajiri na Ni lazima ututumikie sisi maboss zako...

Mwaswala ya kutafuta sympathy Ni unafki mkubwa coz mtu serious na mwenye Nia na msimamo huwa haitaji huruma ya mtu kwa sababu anayofanya wananchi watayaona....

Haya maswala ya kutumbua majipu sjui chunusi sio wakati wake sasa.... Huu Ni mda WA wewe kutafta namna ya kuzba mianya ya wizi WA fedha za umma na kuweka sheria kali kwa wafanyakazi (sio kuwatisha) na kutengeneza mfumo unaotenda kazi bila shuruti...

Unajua watu now sio kwamba wamebadilika bali wanafanya kazi kwa hofu kitu ambacho sio kizuri coz hata kama kuna jambo fulan watu hawataweza kukushauri au kusema wataacha Tu mambo yaharibike ili nawe uisome namba...

Ogopa Sana watu wanapokuwa kimya wasikwambie Ni nini wanawaza coz hautaamini watachokufanyia....

Acha maneno mengi coz uongozi sio kuongea na kutisha watu au kufanya ubabe no!! Uongozi Ni kutumia hekima....
Mtu mwenye hekima hupima upepo.... Hujua wakati na majira sahihi ya kusema jambo... Na nikuambie kitu Rais wangu... Biblia inasena ole wao wanafiki!!

Nadhani maana ya unafki ipo kwenye kamusi ya kiswahili pia... Je hekima halii?? Ufahamu kutoa sauti yake.... Hekima hekima hekima sina mengi ya kuelezea ILA kwa ufikiri ni wapi ambapo hukutumia hekima coz hekima Ni bora kuliko mali na ukiwa na mali ukakosa hekima Ni sawa na kujilisha upepo..

Wapata faida gani? Kwa mimi naona mwenendo WA sasa WA wewe na serikali yako hauna direction maybe direction ipo but I don't see it... Tengenezeni upya njia zenu... Kama mguu Wako ukikukosesha katika kufkkia malengo yako basi huna budi kuukata... Halikadharika jicho PIA..
 
China isingefika ilipo kama ingekuwa na kizazi cha vijana kama walio wengi Tanzania.,kila Mara nauliza swali bunge halipo live miezi kibao sasa hivi ni taarifa IPI ya bungeni mliyoikosa??,kwanini watanzania hatutaki kuwa bize kabisa kutwa kulalamika tu??.,bajeti inayojadiliwa imetenga pesa kibao kuwasaidia vijana,Mimi nimeenda juzi wizara ya viwanda na simjui mtu,nikapewa takwimu ila nikaambiwa nisubiri ikipita ndo nipeleke mawazo yangu,ila wengi humu JF mpo bize kukandia serikali na kubishana kuhusu wanasiasa bila kuja muda unawaacha.Hata mkionyeshwa bunge live wabunge wenu ndo hao wanatoka nje kila siku,waliobaki wanajadili utumbo tu.Ukiruhusu kuwa mlalamishi huwezi kupiga hatua.,serikali ni ile ile,miaka mitano itaisha,itarudi tena hii hii maana tume ya uchaguzi ni ile ile,ila wengi humu mtakuwa mmepoteza muda mwingi Kwa kelele nyingi sana.Maendeleo yako yanakutegemea wewe kwanza,siasa zinarudisha nyuma Sanaa.Hasa siasa zetu za ulimwengu wa tatu.Ni ushauri tu.
Haya tell us China waliendelea kwa njia zipi? Hivi unajua serikali inamchango mkubwa katika kutengenez Ama kuharibu maisha yako? Au hata kupunguza kasi ya mafanikio yako?? Umeajiliwa au umejiajiri... Kama umeajiliwa nachelea kusema Ni haki yako kuongea hayo mashudu... Lazima uelew kuwa sera za nchi husika na sheria ndizo zinazoeeza kukuganya upate maendeleo ya haraka.. Kama sera Ni mbovu hata ufanyw kazi vipi hautapata maendeleo ya uhakika... Sheria za china hata zingekuja hapa bongo nakwambia tungeendelea Tu tutake tusitake.... Sasa katiba yetu Tu mboooovu sjapata kuona... Hebu chukua ya china afu ufananishe na ya tz alafu tena chukua sheria za china za kila sekta ufananishe na za tz alafu ndo ucompee vijana WA china na WA tz... Then utagundua kua serikali inamchango mkubwa katika kukufanikisha WW katika mafanikio yako.... Kaaa fikiri upya... Tunachotaka sisi Ni serikali tuone inatufanyia nn ili na sisi tuifanyie vitu vikibwa nchi yetu....
 
hatutafikia malengo kama serikali aito jitathimini kwa kina kwa mambo ambayo wanayatenda saizi,siasa imekuwa kubwa kuliko utendaji,viongozi wengi wanafanya kazi na wanatoa maamuzi kw hulka ili tu waonekane wachapakazi
 
Yani watu hawafanyi kazi kwa weledi Bali wanafanya ili waonekane na raisi... Wwngne wanatetea ujinga ilomladi mwisho WA siku wapeww hisani kama walivopewa kina Humphrey pole pole.... Kwa mwendo kasi huu.. Hakika gari lazma lipate ajari cas dereca hasikii wala haelewi na abiria nao wanajipendekeza kwake na kumshangilia na wengne kubeza wale wanaoomba apungze spidi...wanasahau kua njia yetu yenyew Ina mabonde hakuna mfano nakwambia tunakoelekea lazma tutapata ajari.... Na itatuathiri wote bila kujali ulimshangilia dereva au la... Na ajali itakua mbaya kiwahi kutokea katika ajali zote...na kulitengeneza gari tena itatuchukua miaka na ghalama kubwa
 
Back
Top Bottom