Uchambuzi wangu mkubwa juu ununuzi wa madiwani

monjozee

Senior Member
Sep 19, 2016
115
297
TWEN'ZETU ARUSHA KWENYE MADIWANI WANAONUNULIKA BEI CHEE

Jana usiku wa Manani, nilijielekeza kutazama video ambazo zilitajwa kuwa ushahidi wa namna madiwani Chadema wanavyonunuliwa Arusha.

Baada ya kutazama, haya ni maoni yangu.

MOSI: Maelezo yaliyotolewa na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari kuwa vifaa vilivyotumika kurekodi video za mazungumzo ni vya hali ya juu sana ni mbwembwe tu. Vifaa ni vya kawaida na vipo vingi.

Sitaki kuingia kwenye ukawaida wa vifaa vyenyewe. Ila itoshe tu kueleza kuwa vifaa vilivyotumika vinatokana na teknolojia ambayo si ngeni tena katika zama hizi.

PILI: Hakuna ubishi kwamba video ni halisi. Kwa mazungumzo ya kwenye video, ni dhahiri mchezo wa kununua madiwani wa Chadema kisha kutokeza hadharani wakiimba wimbo mmoja kwamba wanahamia CCM kwa kuvutiwa na utendaji wa Rais John Magufuli umethibitika.

TATU: Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti na watu wake waliorekodiwa kisha kuonekana wakimwaga ushawishi kwa diwani wa Chadema ahamie CCM, uelewa wao wa teknolojia ya kurekodi ni mdogo.

Unafanya mazungumzo na mtu ya hatari kiasi hicho. Mazungumzo yenye alama nyingi za kimafia. Halafu hukagui saa yake, kalamu anayotumia, vifungo vya shati au miwani kama amevaa. Unategemea nini? Unajiamini nini? Unamwamini kiasi gani unayezungumza naye?

Wazee wa dili haramu hasa Mafioso wa magenge ya Mafia (Mafia Cartels), kanuni ni kutomwamini mtu (Trust No One). Unaweza kumwamini sana mtu kumbe anakufanyia ushushushu.

Mnyeti na watu wake walizubaa sana. Unamshawishi diwani wa Chadema halafu humtilii shaka kwamba anaweza akawa anakufanyia ushushushu. Video hiyo ni matokeo ya kuzubaa na kujiamini bila kuchukua tahadhari.

Kichekesho: Mbali na video ya ushahidi, pia nimesikiliza mazungumzo ya simu kati ya Mnyeti na diwani wa Chadema aliyekuwa akishawishiwa ahamie CCM. Mnyeti anamuuliza diwani: "Wakati tunazungumza ulinirekodi?"

Yule diwani anakanusha kumrekodi, halafu Mnyeti anasema: "Ahaa, nilidhani ulinirekodi?"

Hayo ndiyo mazungumzo yaliyonichekesha. Ni wazi Mnyeti alipiga simu baada ya kuona video. Na kwa uelewa wa kawaida, unatakiwa ujue tu kuwa diwani aliyekuwa anashawishiwa ahame ndiye aliyerekodi. Maana haonekani.

Kwa kuchukua mandhari ya video kuwa diwani mshawishiwa haonekani pichani, na kwa kutazama uelekeo wa picha, unakuja kubaini kwamba mchukua video alikuwa diwani aliyekuwa anashawishiwa.

Sasa basi, Mnyeti hakupaswa hata kumpigia simu diwani na kumuuliza kama alimrekodi, badala yake alipaswa kulijua hilo mapema. Kitendo cha kumpigia simu kimesababisha arekodiwe tena na kuumbuliwa zaidi.

NNE: Watu wengi wanampongeza Nassari kwamba alifanya kazi kubwa sana kufanikisha uthibitisho kwamba kweli madiwani wa Chadema wananunuliwa.

Pongezi kwa Nassari ni sawa na enzi hizo Idhaa ya Kiswahili BBC, ikiripoti kwa undani habari za machafuko eneo la Maziwa Makuu, umpongeze bosi Tido Mhando aliye ofisini London, akifanya kazi kwa kutoa maagizo na kumsahau Erick David Nampesya anayepishana na milio ya risasi akisaka habari.

Shujaa anayepaswa kupongezwa kwa kufanikisha video ya ushahidi jinsi madiwani wanavyonunuliwa ni diwani aliyethubutu kufanikisha mpango. Diwani alivijika mabomu hasa. Yangeweza kumlipukia.

Ingekuwaje Mnyeti na watu wake wangebaini wanarekodiwa? Siyo siri adhabu ya kwanza yule diwani angelazwa mahabusu. Si unajua matumizi ya kifungo cha saa 48 jela jinsi yalivyo na nguvu siku hizi? Baada ya hapo angekoma.

Nasisitiza; Nassari anastahili kupongezwa kwa uwezeshaji wa mpango, ila shujaa wa kweli ni yule diwani. Huyo ndiye anastahili kulindwa mno. Maana amewaumbua watu wenye mamlaka makubwa sana dhidi yake.

NI USHAHIDI TU

Ndiyo, video iliyopatikana ni ushahidi tu, lakini hata kabla ya video, kwa kila mwenye kutafakari vizuri, angeweza kubaini kuwa Arusha kulikuwa na mchezo.

Kweli madiwani wawe wanahama kwa mkumbo eti hoja ikiwa moja; kuvutiwa na utendaji wa Rais John Magufuli?

Niliandika kwenye Twitter huko nyuma kuwa mkumbo wa madiwani kuhama Arusha ni tamthiliya iliyokosa mtunzi mzuri. Na kama ilikuwa kosa si utunzi, basi muongozaji aliwaharibia.

Watu waache majukumu waliyoomba kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitano kisa kuvutiwa na Rais Magufuli? Kwa nini usimuunge mkono Rais Magufuli kwa kutimiza maono yake kwenye eneo lako.

Unaacha kazi ya wananchi uliyoomba na kupewa kwa hoja moja ya mvuto wa Rais Magufuli. Nilisema siku wabunge wanye mishahara na posho wakihama nitaamini. Siyo madiwani ambao kazi yao ni ya kujitolea zaidi. Haina mshahara wala posho zilizonyooka.

Hivyo, kilichofanikishwa kwenye video hiyo ni uthibitisho tu kwamba kweli madiwani Arusha wananunuliwa, lakini kabla ya video ilikuwa dhahiri kuna mchezo ambao watunzi na waongozaji walikosea jinsi ya kuucheza.

Kama Nassari au Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, wasingefanya kitu kutoa uthibitisho kuwa madiwani wananunuliwa, maana yake wangekuwa wamezubaa.

Biashara ilikuwa dhahiri, lakini haikuwa sawa kupayuka kuwa madiwani wananunuliwa bila ushahidi. Angalau sasa hivi sauti zenye kusema ipo biashara zinasikika na kuheshimika.

Mshangao wangu ni wale ambao kipindi chote ikielezwa madiwani Arusha wananunuliwa, wao walikuwa hawaamini. Jamani, hata siku moja tusithubutu kukubali kutozitumia akili zetu.

NI DHAMBI KUBWA

Ikipita wiki moja kabla Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru), haijawakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani, nitatandika msiba na kulia peke yangu. Nitaililia nchi yangu kama ambavyo nimeshaililia mara nyingi.

Dhambi ya kununua madiwani ni kubwa sana. Ni hasara kubwa kwa nchi. Maisha ya kukomoana kisiasa na kutafuta majaliwa kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 haiwezekani kuyatuleta kwenye matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Kwanza diwani anapojiuzulu maana yake uchaguzi mwingine unaitishwa ili kuziba nafasi yake. Gharama za kuitisha uchaguzi ni za Serikali. Tafakari Arusha madiwani wamejizulu wangapi, halafu fedha za umma zitatumika kuitisha uchaguzi mwingine. Inaumiza sana!

Ndani ya video imebainishwa kuwa madiwani wanalipwa fedha taslimu (mamilioni), wanapewa kazi kwenye ofisi za umma, wengine wanafanyiwa mpango uchaguzi ufanyike ili wagombee na kushinda tena.

Ndani ya video imethibitishwa kuwa kumbe diwani anaweza kuwa anahangaika kutimiza ahadi kwenye kata yake lakini anawekewa ngumu na mamlaka za Serikali Kuu (mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa). Kwamba wenye mamlaka wakiamua, diwani anapewa nguvu ya kuhudumia wapigakura wake.

Binafsi siiti hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Huo nauita unyama wa kisiasa. Wananchi wanatakiwa wahudumiwe lakini kumbe wanabaguliwa kisiasa kwa sababu ya kiongozi waliyemchagua kuwa chama tofauti na walio na mamlaka za juu.

WAJIBU WA RAIS MAGUFULI

Baada ya kuthibitika kuwa madiwani ambao huhama Chadema kwenda CCM hufanya hivyo kwa kununuliwa. Ni wazi sasa yale maneno kuwa wanahama kwa mvuto wa Rais Magufuli ni matumizi mabaya ya jina la Rais na wanamchafua.

Baada ya kubainika kuwa wateule wake wanatumia fedha na kushawishi mamlaka za ajira kwenye ofisi za umma kuajiri madiwani waliohama Chadema bila utaratibu, huku jina la Rais likitumika vibaya kuhalalisha uhamaji huo. Hakika wamemchafua sana Rais Magufuli.

Sasa basi, ni wakati wa Rais Magufuli kujitenga na kashfa hiyo. Rais Magufuli anayo nafasi ya kuuthibitishia umma kwamba wasaidizi wake hawakuwa na kibali chake katika kushawishi madiwani wa Chadema kuhamia CCM.

Kuuthibitishia umma ni kwa Rais Magufuli kumwondoa kazini Mnyeti kisha mamlaka za utumishi wa umma zihusike na wengine wote walionaswa kwenye video hiyo ya ushahidi wa madiwani wa Chadema Arusha.

Rais aoneshe kuumizwa na dhambi iliyotendeka ya uharibifu wa rasilimali za nchi kwa kuiamuru Takukuru kuwashughulikia madiwani wote pamoja wale waliowashawishi.

Naumizwa na Bunge letu. Ingekuwa Bunge lina nguvu na linafanya uamuzi kwa haraka, Spika wa Bunge, Job Ndugai alitakiwa awe ameshaunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza kashfa nzima ya madiwani Arusha.

Marekani, vyombo vya ulinzi na usalama viliposhindwa kufanikisha uchunguzi wa kashfa ya Watergate kati ya mwaka 1972 mpaka 1973, Congress iliingia kati, ikaunda kamati teule iliyotoa ripoti ambayo ilimuondoa madarakani Rais Richard Nixon mwaka 1974. Bunge lisipokuwa na nguvu ni msiba kwa nchi.

Kwa kufunga, nieleze kuwa madiwani wa Arusha wamewadhalilisha mno wapigakura wao. Imeonekana kumbe madiwani wao wananunulika bei chee. Ni wazi kuwa pamoja na vivutio vingi vya utalii vilivyopo Arusha, madiwani wanaoacha kazi na kuhama chama kwa ushawishi wa fedha ni kivutio kingine cha utalii.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Hawa vijana kina Mnyeti waliofanya mambo haya, wachukuliwe hatua kali sana za kinidhamu na kisheria, kwanza wameudanganya Umma na hata mheshimiwa Raisi, na wameidhalilisha hata taasisi ya Urais kwa kitendo chao cha kupika mpango wa kipropaganda dhidi yautendaji wa Raisi. Matendo yao hawa vijana ni ya kukemewa kwa nguvu zote!
 
Umejitahidi kuchambua lakin usitumie nguvu kubwa kuandika maneno ya ushawishi mpaka ukaharibu ujumbe wa habari.
Mfano kichwa cha habari hicho ,kama tangazo la soda,
Pia usipende kujitaja jina kwakua wasiojulikana wanakujua pia na awamu Hii hakuna kuabishana wa kukosoana ukithubutu chumaaa.
 
Huu ni ushahidi wa wazi kabisa kama ule wa mawingu. Najua wahusika hawatachukuliwa hatua. Rai yangu ni tuendelee kuutunza huu ushahidi......wahusika watakuja kuadhibiwa.

Kumbuka Chiluba alimtesa Kaunda.

Mwanawasa akaja kulipa kisasi
 
Tusubiri kama kweli TAKURURU itafanya kazi yake.

Ni juu yake Rais kujisafisha na huu Uchafu maana alisema yeye ni mpigania Rushwa.
 
Jana usiku wa Manani, nilijielekeza kutazama video ambazo zilitajwa kuwa ushahidi wa namna madiwani Chadema wanavyonunuliwa Arusha.

Baada ya kutazama, haya ni maoni yangu.

MOSI: Maelezo yaliyotolewa na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari kuwa vifaa vilivyotumika kurekodi video za mazungumzo ni vya hali ya juu sana ni mbwembwe tu. Vifaa ni vya kawaida na vipo vingi.

Sitaki kuingia kwenye ukawaida wa vifaa vyenyewe. Ila itoshe tu kueleza kuwa vifaa vilivyotumika vinatokana na teknolojia ambayo si ngeni tena katika zama hizi.

PILI: Hakuna ubishi kwamba video ni halisi. Kwa mazungumzo ya kwenye video, ni dhahiri mchezo wa kununua madiwani wa Chadema kisha kutokeza hadharani wakiimba wimbo mmoja kwamba wanahamia CCM kwa kuvutiwa na utendaji wa Rais John Magufuli umethibitika.

TATU: Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti na watu wake waliorekodiwa kisha kuonekana wakimwaga ushawishi kwa diwani wa Chadema ahamie CCM, uelewa wao wa teknolojia ya kurekodi ni mdogo.

Unafanya mazungumzo na mtu ya hatari kiasi hicho. Mazungumzo yenye alama nyingi za kimafia. Halafu hukagui saa yake, kalamu anayotumia, vifungo vya shati au miwani kama amevaa. Unategemea nini? Unajiamini nini? Unamwamini kiasi gani unayezungumza naye?

Wazee wa dili haramu hasa Mafioso wa magenge ya Mafia (Mafia Cartels), kanuni ni kutomwamini mtu (Trust No One). Unaweza kumwamini sana mtu kumbe anakufanyia ushushushu.

Mnyeti na watu wake walizubaa sana. Unamshawishi diwani wa Chadema halafu humtilii shaka kwamba anaweza akawa anakufanyia ushushushu. Video hiyo ni matokeo ya kuzubaa na kujiamini bila kuchukua tahadhari.

Kichekesho: Mbali na video ya ushahidi, pia nimesikiliza mazungumzo ya simu kati ya Mnyeti na diwani wa Chadema aliyekuwa akishawishiwa ahamie CCM. Mnyeti anamuuliza diwani: "Wakati tunazungumza ulinirekodi?"

Yule diwani anakanusha kumrekodi, halafu Mnyeti anasema: "Ahaa, nilidhani ulinirekodi?"

Hayo ndiyo mazungumzo yaliyonichekesha. Ni wazi Mnyeti alipiga simu baada ya kuona video. Na kwa uelewa wa kawaida, unatakiwa ujue tu kuwa diwani aliyekuwa anashawishiwa ahame ndiye aliyerekodi. Maana haonekani.

Kwa kuchukua mandhari ya video kuwa diwani mshawishiwa haonekani pichani, na kwa kutazama uelekeo wa picha, unakuja kubaini kwamba mchukua video alikuwa diwani aliyekuwa anashawishiwa.

Sasa basi, Mnyeti hakupaswa hata kumpigia simu diwani na kumuuliza kama alimrekodi, badala yake alipaswa kulijua hilo mapema. Kitendo cha kumpigia simu kimesababisha arekodiwe tena na kuumbuliwa zaidi.

NNE: Watu wengi wanampongeza Nassari kwamba alifanya kazi kubwa sana kufanikisha uthibitisho kwamba kweli madiwani wa Chadema wananunuliwa.

Pongezi kwa Nassari ni sawa na enzi hizo Idhaa ya Kiswahili BBC, ikiripoti kwa undani habari za machafuko eneo la Maziwa Makuu, umpongeze bosi Tido Mhando aliye ofisini London, akifanya kazi kwa kutoa maagizo na kumsahau Erick David Nampesya anayepishana na milio ya risasi akisaka habari.

Shujaa anayepaswa kupongezwa kwa kufanikisha video ya ushahidi jinsi madiwani wanavyonunuliwa ni diwani aliyethubutu kufanikisha mpango. Diwani alivijika mabomu hasa. Yangeweza kumlipukia.

Ingekuwaje Mnyeti na watu wake wangebaini wanarekodiwa? Siyo siri adhabu ya kwanza yule diwani angelazwa mahabusu. Si unajua matumizi ya kifungo cha saa 48 jela jinsi yalivyo na nguvu siku hizi? Baada ya hapo angekoma.

Nasisitiza; Nassari anastahili kupongezwa kwa uwezeshaji wa mpango, ila shujaa wa kweli ni yule diwani. Huyo ndiye anastahili kulindwa mno. Maana amewaumbua watu wenye mamlaka makubwa sana dhidi yake.

NI USHAHIDI TU

Ndiyo, video iliyopatikana ni ushahidi tu, lakini hata kabla ya video, kwa kila mwenye kutafakari vizuri, angeweza kubaini kuwa Arusha kulikuwa na mchezo.

Kweli madiwani wawe wanahama kwa mkumbo eti hoja ikiwa moja; kuvutiwa na utendaji wa Rais John Magufuli?

Niliandika kwenye Twitter huko nyuma kuwa mkumbo wa madiwani kuhama Arusha ni tamthiliya iliyokosa mtunzi mzuri. Na kama ilikuwa kosa si utunzi, basi muongozaji aliwaharibia.

Watu waache majukumu waliyoomba kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitano kisa kuvutiwa na Rais Magufuli? Kwa nini usimuunge mkono Rais Magufuli kwa kutimiza maono yake kwenye eneo lako.

Unaacha kazi ya wananchi uliyoomba na kupewa kwa hoja moja ya mvuto wa Rais Magufuli. Nilisema siku wabunge wanye mishahara na posho wakihama nitaamini. Siyo madiwani ambao kazi yao ni ya kujitolea zaidi. Haina mshahara wala posho zilizonyooka.

Hivyo, kilichofanikishwa kwenye video hiyo ni uthibitisho tu kwamba kweli madiwani Arusha wananunuliwa, lakini kabla ya video ilikuwa dhahiri kuna mchezo ambao watunzi na waongozaji walikosea jinsi ya kuucheza.

Kama Nassari au Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, wasingefanya kitu kutoa uthibitisho kuwa madiwani wananunuliwa, maana yake wangekuwa wamezubaa.

Biashara ilikuwa dhahiri, lakini haikuwa sawa kupayuka kuwa madiwani wananunuliwa bila ushahidi. Angalau sasa hivi sauti zenye kusema ipo biashara zinasikika na kuheshimika.

Mshangao wangu ni wale ambao kipindi chote ikielezwa madiwani Arusha wananunuliwa, wao walikuwa hawaamini. Jamani, hata siku moja tusithubutu kukubali kutozitumia akili zetu.

NI DHAMBI KUBWA

Ikipita wiki moja kabla Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru), haijawakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani, nitatandika msiba na kulia peke yangu. Nitaililia nchi yangu kama ambavyo nimeshaililia mara nyingi.

Dhambi ya kununua madiwani ni kubwa sana. Ni hasara kubwa kwa nchi. Maisha ya kukomoana kisiasa na kutafuta majaliwa kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 haiwezekani kuyatuleta kwenye matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Kwanza diwani anapojiuzulu maana yake uchaguzi mwingine unaitishwa ili kuziba nafasi yake. Gharama za kuitisha uchaguzi ni za Serikali. Tafakari Arusha madiwani wamejizulu wangapi, halafu fedha za umma zitatumika kuitisha uchaguzi mwingine. Inaumiza sana!

Ndani ya video imebainishwa kuwa madiwani wanalipwa fedha taslimu (mamilioni), wanapewa kazi kwenye ofisi za umma, wengine wanafanyiwa mpango uchaguzi ufanyike ili wagombee na kushinda tena.

Ndani ya video imethibitishwa kuwa kumbe diwani anaweza kuwa anahangaika kutimiza ahadi kwenye kata yake lakini anawekewa ngumu na mamlaka za Serikali Kuu (mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa). Kwamba wenye mamlaka wakiamua, diwani anapewa nguvu ya kuhudumia wapigakura wake.

Binafsi siiti hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Huo nauita unyama wa kisiasa. Wananchi wanatakiwa wahudumiwe lakini kumbe wanabaguliwa kisiasa kwa sababu ya kiongozi waliyemchagua kuwa chama tofauti na walio na mamlaka za juu.

WAJIBU WA RAIS MAGUFULI

Baada ya kuthibitika kuwa madiwani ambao huhama Chadema kwenda CCM hufanya hivyo kwa kununuliwa. Ni wazi sasa yale maneno kuwa wanahama kwa mvuto wa Rais Magufuli ni matumizi mabaya ya jina la Rais na wanamchafua.

Baada ya kubainika kuwa wateule wake wanatumia fedha na kushawishi mamlaka za ajira kwenye ofisi za umma kuajiri madiwani waliohama Chadema bila utaratibu, huku jina la Rais likitumika vibaya kuhalalisha uhamaji huo. Hakika wamemchafua sana Rais Magufuli.

Sasa basi, ni wakati wa Rais Magufuli kujitenga na kashfa hiyo. Rais Magufuli anayo nafasi ya kuuthibitishia umma kwamba wasaidizi wake hawakuwa na kibali chake katika kushawishi madiwani wa Chadema kuhamia CCM.

Kuuthibitishia umma ni kwa Rais Magufuli kumwondoa kazini Mnyeti kisha mamlaka za utumishi wa umma zihusike na wengine wote walionaswa kwenye video hiyo ya ushahidi wa madiwani wa Chadema Arusha.

Rais aoneshe kuumizwa na dhambi iliyotendeka ya uharibifu wa rasilimali za nchi kwa kuiamuru Takukuru kuwashughulikia madiwani wote pamoja wale waliowashawishi.

Naumizwa na Bunge letu. Ingekuwa Bunge lina nguvu na linafanya uamuzi kwa haraka, Spika wa Bunge, Job Ndugai alitakiwa awe ameshaunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza kashfa nzima ya madiwani Arusha.

Marekani, vyombo vya ulinzi na usalama viliposhindwa kufanikisha uchunguzi wa kashfa ya Watergate kati ya mwaka 1972 mpaka 1973, Congress iliingia kati, ikaunda kamati teule iliyotoa ripoti ambayo ilimuondoa madarakani Rais Richard Nixon mwaka 1974. Bunge lisipokuwa na nguvu ni msiba kwa nchi.

Kwa kufunga, nieleze kuwa madiwani wa Arusha wamewadhalilisha mno wapigakura wao. Imeonekana kumbe madiwani wao wananunulika bei chee. Ni wazi kuwa pamoja na vivutio vingi vya utalii vilivyopo Arusha, madiwani wanaoacha kazi na kuhama chama kwa ushawishi wa fedha ni kivutio kingine cha utalii.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Swali msingi, aliyenunuliwa bado ni Chadema au CCM? Mpokea rushwa hana hatia?
 
Back
Top Bottom