benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,032
Katika gazeti la Raia Mwema la leo tarehe 18 Julai 2022, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amechambua uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan akisema yeye anampa asilimia 75 ya utekelezaji.
Kwa ufupi Lipumba amechambua mambo kadhaa katika uongozi wa Rais Samia na kugusia masuala ya Demokrasia, Haki, Usawa na Utawala Bora ambapo amesisitiza kuwa sasa WATANZANIA WANAPUMUA.
Lipumba ameeleza kuwa baada ya Rais Samia kuapishwa, CUF walimshauri kusimamia misingi ya Demokrasia, lakini pia kufuta kesi zote zilizotokana na purukushani za kisiasa lakini pia asimamie mchakato wa kukamilisha upatikanaji wa Katiba mpya pamoja na kufuata kanuni za Afya za kusimamia masuala yahusuyo UVIKO19, masuala anayoeleza kuwa Rais Samia ameyafanyia kazi kw a kiasi kikubwa.
Lipumba amesisitiza kuwa andiko la Rais Samia Siku ya kuadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi limeongeza matumaini ya ujenzi ya demokrasia nchini huku akieleza kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 ulikuwa mbovu kuliko yote ambayo imewahi kufanyika Tanzania/Tanganyika. Lipumba amesema uchaguzi huo uligubwika na ubakwaji mkubwa mno wa demokrasia.
Vipi wewe unaupa asilimia ngapi uchambuzi huu wa Profesa Lipumba?
Na vipi kufikia sasa, wewe unaupa asilimia ngapi uongozi wa Rais Samia Suluhu?