UCHAMBUZI WANGU JUU YA YESU KRISTO

AROON

AROON

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Messages
8,461
Points
2,000
AROON

AROON

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2014
8,461 2,000
Wayahudi ama Wakristo wa zama za mitume hawakuwa na shida ya uungu, na wala debate yao haikuwa katika mchanganuo wa Mungu.

Hoja ya Wayahudi na Wakristo wa kale ilikuwa ni MASIHI/KRISTO MWANA WA MUNGU NI NANI?

Wayahudi walidai hajaja bado
Wakristo walidai ni Yesu

Hapo ndipo kiini cha hoja kati ya Wayahudi na Wakristo, walisuguana kwa hoja kiasi cha kupelekana mahakamani, ilifika mahali Wayahudi walishindwa kwa hoja wakatumia mabavu, vujo na kuua wapinzani wao.

Ebu turejee hoja iliyo muua Yesu mbele ya Senhedrin/bunge au mahakama ya Kiyahudi.

Mshtaki Kayafa:Kuhani ama mkuu wa Senhedrin, akamuuliza Yesu:-Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu?

Mtuhumiwa YESU akajibu: Mimi ndiye.

Hukumu ikapitishwa: Kuhani Mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna haja gani tena ya mashahidi?
Mmesikia kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa.

Baada ya hapo Yesu alitemewa mate na alipigwa makonde na baadae kusulubiwa kisa tu alisema yeye ni KRISTO MWANA WA MUNGU. Rejea Marko 14:61-65

JE WAKRISTO WALIFUNDISHA NINI BAADA YA HAPO?

MITUME: Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za *Yesu kwamba ni Kristo*. Matendo 5:42

PAULO: Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba *Yesu ni Kristo.* Matendo 18:5

APOLO:Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa *Yesu ni Kristo*. Matendo 18:28

JE NI HOJA GANI ILISABABISHA PAULO KUTAKA KUUAWA?

Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba *yeye ni Mwana wa Mungu*. Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa *huyu ndiye Kristo*. Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue.......Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua.. Rejea Matendo 9:20,22,23,23

BIBLIA INASEMA HIVI:-

Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Waefeso 2:20

NA BIBLIA INAONYA HIVI:-

Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. Wagalatia 1:8,9

Kwahiyo inahitajika uangalifu mkubwa sana kuhubiri injili, na kuhubiri injili ni kumhubiri Yesu Kristo mwana wa Mungu.

NA KUNA FAIDA GANI KUHUBIRI HIVYO?

Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba *Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake*.

Nje ya Ufunuo huo, ni kuangukia katika uharibifu wa milele.

Hitimisho.

UKIKIRI KWAMBA YESU NI KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI, NI KUKIRI UWEPO WA MUNGU BABA, MAANA HAKUNA MWANA BILA BABA. Na huo ni udhihirisho wa uwepo halisi wa Baba na Mwana; ebu tuthibitishe hilo.

Katika vitabu vya agano la kale kuna unabii wa kimasihi, hasa katika kitabu cha Zaburi na Isaya. Ebu tuchukue aya fulani katika Zaburi.

110:1 A Psalm of David. The LORD said unto my Lord, Sit thou at my right hand, until I make thine enemies thy footstool. KJV

BWANA NA Bwana imetenganishwa kwa herufi kubwa na ndogo katika tafasiri; na katika matini yaani gombo la asili la Kiebrania, BWANA ni Yahweh na Bwana ni Adonai. Je kwanini wametofautisha hivyo? ni kwasababu hapo kuna Mungu Baba na Mwana ambaye ni masihi, na Yesu anakiri hivyo kwamba yeye ni Bwana yule wa herufi ndogo wakati anaufumbua unabii huo kwa Marabi wa Kiyahudi. Rejea Mathayo 22:41-46. Pia Yesu alikiri sehemu fulani kwamba Baba ni mkuu kuliko yeye. Nafikiri hiyo ni sababu tosha ya kuwatofautisha katika herufi au majina.

Katika vitabu vya mitume pia, Baba na Mwana wametofautishwa kiuhalisi yaani kwamba ni wawili katika umoja ambao hauondoi nafsi zao. Ebu jaribu kupitia mwanzo mwa kila nyaraka za mitume utaona hilo, ebu tuchukue mistari michache.

PAULO: Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. 1 Kor 1:3

PETRO: Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi. 1 Petro 1:3

YOHANA: hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 1 Yohana 1:3

KANUNI YA IMANI YA MITUME JUU YA MUNGU

Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; lakini kwetu sisi *Mungu ni mmoja tu*, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na *Bwana mmoja Yesu Kristo*, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo. IKor 8:5,6.

Anahitimisha hivi katika aya ya 7: *Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote* .Kwahiyo tunaweza bishana sana kama tu huu ujuzi haumo ndani yetu sote, maana huu ni ufunuo wa Mwana ambao tayari kashaufunua ndani ya kanisa lake baada ya Roho kushuka siku ile ya Pentekoste ya KWAMBA YEYE NI MWANA WA MUNGU NA SI KWAMBA YEYE HUYO HUYO NDIYE MUNGU BABA kama waalimu wa leo wanavyofundisha kwa kupotosha kanisa la Kristo.

Mbarikiwe wote katika jina la Yesu. Amen
 
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2018
Messages
493
Points
250
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2018
493 250

Watu wasipojua Propaganda za Wasabato Ambao Duna nzima Hawazidi Million20Watajikutawana weweseka sana Kidini nakuhamahama Wasabatoni mabingwa wa KUPOTOSHA na EXTREMIST wana UDINI SANA na lazima wazibitiwe na mpango wakuwadhibiti Lazima ubadilishwe
 
MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Messages
1,515
Points
2,000
MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2017
1,515 2,000
WAYAHUDI WABAYA SANA HATA WAFUASI WA KRISTO WANAVYOKWENDA KUHIJI KULE ISRAEL NA MASHAKA MASHAKA

*1. Mathayo*
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya Kanisa la Kristo. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

*2. Marko*
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

*3. Luka*
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

*4. Yohana*
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha *"Ufunuo wa Yohana".* Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana, naye ni mtume pekee aliyefariki bila mateso.

*5. Petro*
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Lakini yeye alisulubiwa tofauti na Yesu Kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya *"X"* Petro mwenyewe aliomba asulubiwe kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18).

*6.Yakobo*
Alikuwa Kiongozi wa Kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu Kristo kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe. Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga mawe mpaka akafa.

*7. Yakobo* (mwana wa Zebedayo)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa Kanisa, Yakobo alichinjwa huko Jerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

*8. Batholomayo*
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo.

*9. Andrea*
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la *"X"* miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri saa kama hii".

*10. Tomaso*
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko India.

*11. Yuda (Thadei)*
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

*12. Yuda (Iskariote)*
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

*Kumbuka:*
*13. Thadayo (au Mathia)* ni Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (Msaliti). Huyu alipigwa kwa mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

*14. Paulo*
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka 100 A.D.

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika Agano Jipya, kama vile Waraka wa Paulo Mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

Kumbuka: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, *"Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka."* Mathayo Mtakatifu 10:
 
Ileje

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Messages
4,838
Points
2,000
Ileje

Ileje

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2011
4,838 2,000

Una maana gani kuandika " dhidi ya kanisa la Kristo" au dhidi ya Yesu"
Unajua matumizi ya neno "dhidi"?
 
G

Greatness is within

Member
Joined
Apr 16, 2018
Messages
72
Points
125
G

Greatness is within

Member
Joined Apr 16, 2018
72 125
Wayahudi ama Wakristo wa zama za mitume hawakuwa na shida ya uungu, na wala debate yao haikuwa katika mchanganuo wa Mungu.

Hoja ya Wayahudi na Wakristo wa kale ilikuwa ni MASIHI/KRISTO MWANA WA MUNGU NI NANI?

Wayahudi walidai hajaja bado
Wakristo walidai ni Yesu

Hapo ndipo kiini cha hoja kati ya Wayahudi na Wakristo, walisuguana kwa hoja kiasi cha kupelekana mahakamani, ilifika mahali Wayahudi walishindwa kwa hoja wakatumia mabavu, vujo na kuua wapinzani wao.

Ebu turejee hoja iliyo muua Yesu mbele ya Senhedrin/bunge au mahakama ya Kiyahudi.

Mshtaki Kayafa:Kuhani ama mkuu wa Senhedrin, akamuuliza Yesu:-Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu?

Mtuhumiwa YESU akajibu: Mimi ndiye.

Hukumu ikapitishwa: Kuhani Mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna haja gani tena ya mashahidi?
Mmesikia kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa.

Baada ya hapo Yesu alitemewa mate na alipigwa makonde na baadae kusulubiwa kisa tu alisema yeye ni KRISTO MWANA WA MUNGU. Rejea Marko 14:61-65

JE WAKRISTO WALIFUNDISHA NINI BAADA YA HAPO?

MITUME: Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za *Yesu kwamba ni Kristo*. Matendo 5:42

PAULO: Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba *Yesu ni Kristo.* Matendo 18:5

APOLO:Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa *Yesu ni Kristo*. Matendo 18:28

JE NI HOJA GANI ILISABABISHA PAULO KUTAKA KUUAWA?

Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba *yeye ni Mwana wa Mungu*. Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa *huyu ndiye Kristo*. Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue.......Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua.. Rejea Matendo 9:20,22,23,23

BIBLIA INASEMA HIVI:-

Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Waefeso 2:20

NA BIBLIA INAONYA HIVI:-

Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. Wagalatia 1:8,9

Kwahiyo inahitajika uangalifu mkubwa sana kuhubiri injili, na kuhubiri injili ni kumhubiri Yesu Kristo mwana wa Mungu.

NA KUNA FAIDA GANI KUHUBIRI HIVYO?

Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba *Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake*.

Nje ya Ufunuo huo, ni kuangukia katika uharibifu wa milele.

Hitimisho.

UKIKIRI KWAMBA YESU NI KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI, NI KUKIRI UWEPO WA MUNGU BABA, MAANA HAKUNA MWANA BILA BABA. Na huo ni udhihirisho wa uwepo halisi wa Baba na Mwana; ebu tuthibitishe hilo.

Katika vitabu vya agano la kale kuna unabii wa kimasihi, hasa katika kitabu cha Zaburi na Isaya. Ebu tuchukue aya fulani katika Zaburi.

110:1 A Psalm of David. The LORD said unto my Lord, Sit thou at my right hand, until I make thine enemies thy footstool. KJV

BWANA NA Bwana imetenganishwa kwa herufi kubwa na ndogo katika tafasiri; na katika matini yaani gombo la asili la Kiebrania, BWANA ni Yahweh na Bwana ni Adonai. Je kwanini wametofautisha hivyo? ni kwasababu hapo kuna Mungu Baba na Mwana ambaye ni masihi, na Yesu anakiri hivyo kwamba yeye ni Bwana yule wa herufi ndogo wakati anaufumbua unabii huo kwa Marabi wa Kiyahudi. Rejea Mathayo 22:41-46. Pia Yesu alikiri sehemu fulani kwamba Baba ni mkuu kuliko yeye. Nafikiri hiyo ni sababu tosha ya kuwatofautisha katika herufi au majina.

Katika vitabu vya mitume pia, Baba na Mwana wametofautishwa kiuhalisi yaani kwamba ni wawili katika umoja ambao hauondoi nafsi zao. Ebu jaribu kupitia mwanzo mwa kila nyaraka za mitume utaona hilo, ebu tuchukue mistari michache.

PAULO: Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. 1 Kor 1:3

PETRO: Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi. 1 Petro 1:3

YOHANA: hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 1 Yohana 1:3

KANUNI YA IMANI YA MITUME JUU YA MUNGU

Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; lakini kwetu sisi *Mungu ni mmoja tu*, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na *Bwana mmoja Yesu Kristo*, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo. IKor 8:5,6.

Anahitimisha hivi katika aya ya 7: *Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote* .Kwahiyo tunaweza bishana sana kama tu huu ujuzi haumo ndani yetu sote, maana huu ni ufunuo wa Mwana ambao tayari kashaufunua ndani ya kanisa lake baada ya Roho kushuka siku ile ya Pentekoste ya KWAMBA YEYE NI MWANA WA MUNGU NA SI KWAMBA YEYE HUYO HUYO NDIYE MUNGU BABA kama waalimu wa leo wanavyofundisha kwa kupotosha kanisa la Kristo.

Mbarikiwe wote katika jina la Yesu. Amen
Amen
 
Amani Jr

Amani Jr

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2015
Messages
249
Points
250
Amani Jr

Amani Jr

JF-Expert Member
Joined May 6, 2015
249 250
Aroon! Nani aliyekwambia Yesu Kristo alipokuja duniani aliwakuta hao wanaojiita Wakristo??!! Haya mafundisho ya kupotosha unayatoa wapi?
 
Forum statistics

Threads 1,313,882
Members 504,678
Posts 31,807,180
Top