Uchambuzi wa siasa wa Dr Benson Bana wa REDET

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,171
Hivi karibuni Dr Benson Bana ambaye ni muhadhiri wa UD na mkuu wa REDET amekuwa kimbilio la vyombo vya habari pale wanapotaka Uchambuzi wa mambo kwa mtizamo wa kisomi.

Binafsi nimekuwa sipati msisimko na uchambuzi wa msomi huyu. Nimekuwa nikidhani kwamba anafuata mtindo ule ule wa Mukandara, kujikomba kwa wanasiasa ili aonekane (ref. Shairi la Kandoro: Paka akitaka jina hujipitisha kwa watu).

Mfano mzuri ni ule wa mahojiano ya jana baada ya ripoti iliyoitwa ya utafiti unaonyesha umaarufu wa wanasiasa nchini, Kikwete akiongoza.

Prof. Lipumba alionyesha usomi wake kwa ku-challenge ubora wa ripoti hiyo na kutaka idadi ya waliohojiwa na staitistical test zinazothibitisha kwamba kweli ushindi wa Kikwete na wote waliotajwa ktk maoni ni significant. VERY GOOOOOD!

Ajabu ni Dr Benson alipoulizwa. Yeye kwake anasema hiyo inatosha! Eti hata mtaani unaweza kuona huo ushindi. Utadhani siyo muhadhiri! Au hajawahi kufanya utafiti? Au ndo mwisho wa quality ya wahadhiri wetu?
 
Huyu bwana Bana hana tofauti na Makamba. Mitazamo/kauli zake loose zinafanya a'fit' kuwa 'Makamba wa Redet'.
 
Nilimwona jana kwenye luninga. Usimshangae sana. Ajira kamili kwa wasomi wetu hawa sasa ipo kwenye siasa. Nadhani mwaka huu naye ataingia. Alisema REDET nao watatoa matokeo ya utafiti wao April mwaka huu. Wanazo hela nyingi za wafadhili. Lazima wahalalishe matumizi.
 
Niliwahi kutazama wakati anahojiwa na TBC1 na kushangaa sana kuona eti anasema CCM wanajua kusuruhisha migogoro eti ndio ukongwe wa CCM hata mimi huwa napata shida sana kuona au comments zake sijajua huyu jamaa yupo katika mitazamo ipo ila ni aina ya kada maarufu sana
 
Kwani Mkandara anastaafu u-VC apewe huyu. Maana ndiyo style ya UDSM sasa.
 
Kwani Mkandara anastaafu u-VC apewe huyu. Maana ndiyo style ya UDSM sasa.

Mshkaj anataka U proffessor wa heshima (mchafu wa kisiasa) kama mwenyekiti wake wa chama anavyojilambia u Doctor uchwara
 
Back
Top Bottom