Uchambuzi wa sera ya kujitolea katika sekta ya afya

GenuineMan

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
5,249
11,597
Utangulizi.
Serikali kupitia wizara ya afya imezindua sera ya kujitolea katika sekta ya afya. Utaratibu huu utawahusu wahitimu wa ngazi mbalimbali (astashahada, stashada, shahada nk) na fani mbalimbali za afya kama vile madaktari, wauguzi, wafamasia, wataalamu wa maabara n.k. Watakaopata nafasi ya kujitolea ni wale waliokidhi vigezo vyote vya kuajiriwa ikiwemo, kuhitimu mafunzo husika na kuwa na leseni ya fani husika.

Yaliyomo Katika Sera:
Sera hii inatambua uhitaji mkubwa wa watumishi wa afya katika nchi yetu, kati ya wafanyakazi 209,603 wanaohitajika, walioko kazini ni 99,684(48%). Hivyo taifa lina upungufu wa watumishi wa afya zaidi ya 109, 919 (52%). Maana yake walioko kazini wanalazimika kufanya kazi mara mbili zaidi ya uwezo wa kawaida wa binadamu.

Sera hii inatambua kua, tangu 2014 kumekua na ongezeko la wahitimu wa fani za afya katika ngazi mbalimbali. Hii inatokana na dhamira ya serikali ya wakati huo kuwekeza zaidi (kwa kushirikiana na sekta binafsi) katika uzalishaji wa wataalamu wa afya ili kuziba pengo la uhaba wa watumishi wa afya.

Sera hii inatambua kua, mbali na utaratibu na dhamira ya serikali ya awali ya kuajiri watumishi wa afya kila mwaka, serikali ya awamu ya tano na ya sita, kwa kipindi cha miaka sita imeajiri jumla ya watumishi 11,830 tuu ambapo katika mwaka 2015/2016 na 2018/2019 haikuajiri mtumishi hata mmoja kwa kigezo cha ukaguzi wa watumishi hewa na wasiokidhi vigezo. Hii ni tofauti na serikali ya awali ambayo ilikua ikiajiri kila mwaka na kwa mwaka 2013/2014 pekee, iliajiri watumishi 10, 014.

Sera hii inatambua uwepo wa watumishi wa afya waliohitimu miaka mbalimbali ambao hawana ajira rasmi na kwa sababu ya ukali wa maisha wamelazimika kujitolea katika vituo na hospitali mbalimbali nchini. Kila hospitali au kituo wamekua na utaratibu tofauti wa kuwalipa posho wataalamu hao wanaojitolea.

Sera hii inaweka utaratibu wa mikataba ya kujitolea kua kwa kipindi cha mwaka mmoja mpaka miaka mitatu. Lakini haitoi hakikisho la kuajiriwa kwa anayejitolea baada ya kipindi cha mkataba kuisha.

Sera hii inahalalisha vituo na hospitali kuchukua wataalamu wa kujitolea mpaka asilimia 20 (au zaidi kwa kibali cha wizara) ya wafanyakazi wa kituo au hospitali husika.

Sera hii inatoa mapendekezo ya namna hospitali au kituo kinavyoweza kupata pesa za kuwalipa posho wanaojitolea. Hivyo malipo yataendelea kuwa ni jukumu la kituo au hospitali na sio serikali moja kwa moja.

Sera hii inatambua uwepo wa kamati ya kitaifa ya kujitolea "National health volunteer steering committee" kamati hii inaongozwa na katibu mkuu afya na wajumbe wengine ni makatibu au viongozi waandamizi wa wizara pamoja na taasisi za afya kama vile, OR-TAMISEMI, OR-Utumishi wa umma na utawala bora, wawakilishi kutoka vyama vya kitaaluma vya afya, mwakilishi vituo/hospitali binasi na tasisi za afya za kidini. Katika wote, hakuna ambaye anajitolea, (mwakilishi kutoka kundi la wanaojitolea) wote ni waajiriwa wa juu wenye kulipwa mishahara mikubwa.

Sera hii inategemewa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, ili kufanikisha hilo, serikali itatumia jumla ya Tshs. 1,762, 750,000/= kwa ajili ya vikao vya kamati, uchapaji wa nyaraka na ziara za ufuatiliaji wa utekelezaji wa sera hiii. Watalipana kwenye vikao na ziara ili kupanga namna mtaalamu wa afya atakavyofanya kazi kwa kujitolea.

Malengo ya serikali kutengeneza sera hii:
Kulingana na sera hii, serikali ilikuja na sera hi kwa malengo yafuatayo:
1)Kurasimisha ( kuhalalisha) kujitolea kwa wataalamu wa afya ili kuziba pengo la uhaba wa wataalamu hao.

2) Kuwapa nafasi wahitimu wa fani za afya kuendelea kupata uzoefu kwa kipindi ambacho bado hawajapata ajira rasmi.

3) Kuweka ulinganifu wa posho kwa wataalamu wanaojitolea maeneo tofautitofauti.

4) Kuwezesha serikali kutimiza wajibu wa kutoa huduma za afya kwa gharama nafuu.

Mtazamo wangu juu ya sera hii:
Ikumbukwe, kwa mujibu wa sera hii, atakayepata nafasi ya kujitolea ni yule aliyekidhi vigezo vyote vya kuajiriwa, na utatumika utaratibu uleule kama wakati wa kuajiri. Na atakayekua anajitolea atawajibika kufanya kazi kwa kipimo linganifu na mwajiriwa aliye sawa nae.

Ni ukweli kua kumekuwepo na wataalamu wengi wa afya ambao wanajitolea katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya, na wamekua wakipewa posho kidogo au posho inayotokana na kazi za ziada wanazozifanya huku kazi msingi wakiifanya bure. Huu ni mfumo wa kinyonyaji na kutokuthamini wataalamu wetu wa afya ambao ni wachache. Serikali ilikua na jukumu la kuingilia kati kwa kutoa ajira na pia kutoa utaratibu wa kulazimisha vituo au hospitali binafsi kuwalipa stahiki sahihi na sio kuhalalisha unyonyaji huu.

Tukumbuke kua, serikali inawajibika moja kwa moja kuhakikisha inalinda katiba ya nchi yetu, ikiwa ni kuhakikisha haki zote zilizomo kwenye katiba yetu zinalindwa. Katiba yetu article 11, subsection 1 inaeleza hivi "The state authority shall make appropriate provisions for the realization of a person's work, ....... . Shall make provisions to ensure that every person earns his livelihood". Pia inatambua haki ya kila mtu kufanya kazi na kupata kipato kinachoendana na kazi yake, article 22 sub section 1. Article 23 subsection 1 inaeleza hivi "Every person, without discrimination of any kind, is entitled to remuneration commensurate with his work, and all persons working according to their ability shall be remunerated according to the measure and qualification of the work".

Kukubali tuu kufanya kazi hospitalini ni kujitolea, hivyo kulipwa nusu ya mshahara stahiki (ambao pia ni mdogo mno) kama posho ni mateso mengine makubwa zaidi. Pia mtaalamu huyu atakua hana uhakika wa kutibiwa yeye pamoja na wanaomtegemea pale atakapougua kwani atakua hayupo kwenye utaratibu wa uhakika wa bima ya afya, Pia hatapata stahiki zingine za mwajiriwa ikiwemo uhakika wa kazi, fursa ya kupata mkopo pamoja na hifadhi ya jamii.

Mtaalamu wa fani yeyote ya afya, ni mtu aliyejitoa mhanga kwani mazingira ya kazi ni magumu na hatarishi, hivyo afya yake inakua rehani muda wote. Hivyo kwa mazingira yeyote, mtaalamu wa afya anapaswa kulindwa kwa wivu mkubwa na jamii yote ikiwa ni pamoja na kulipwa maslahi mazuri zaidi ili aweze kutoa huduma kwa moyo wote.

Watumishi wa Afya kwa kipindi hiki cha janga la Corona wameathirika sana kiafya na kisaikolojia. Serikali za nchi nyingi duniani, wametumia njia mbalimbali kukabliliana na halli hiyo ikiwemo kuongeza posho, kupunguza kodi kwa watumishi wa afya na kutoa ajira mpya. Tanzania hakuna jitihada zenye mashiko zilizofanywa na serikali kusaidia watumishi wa afya, badala yake inakuja na mpango wa kujitolea badala mpango wa kuajiri.

Matokeo yanayotarajiwa:
Utekelezaji wa sera hii unatarajiwa kuja na matokeo yafuatayo:
1) Utaziba ombwe la uhitaji wa watumishi wa afya katika vituo vya afya na hospitali na hivyo msukumo wa serikali kuajiri utakua haupo. Jamii itapumbazwa kua vituo vina watumishi wa afya wa kutosha. Serikali itakua ikitumia utaratibu huu kama mbadala wa kuajiri.

2)Itaua kabisa uwezekano wa nafasi za ajira katika sekta binafsi, kwani nao pia ni wadau katika utekelezaji wa sera hii, na kwa sababu wanategemea kupata faida, basi watafurahia fursa hii ya kupata cheap labour iliyohalalishwa.

3) itapunguza ubora wa huduma (quality of seevice) zitakazotolewa na wanaojitolea. Hii ni kwa sababu kiasili kazi za afya ni ngumu na zenye changamoto zinazohitaji mtu kudhamiria (dhamira njema) katika utekelezaji wake na mara nyingi ni ngumu kupima/kukagua (audit) kama huduma iliyotolewa ni bora au laa. Hivyo, mkaguzi wa huduma za afya huwa ni mtoaji mwenyewe. Vijana hawa kwa sababu ya kutopewa stahiki zao zinazoendana na elimu zao, wanaweza kutoa huduma ambazo ni chini ya kiwango.

Hitimisho:
Watanzania wana haki ya kuhakikishiwa mifumo bora ya afya nchini ili kuwa na uhakika wa afya zao pale watakapougua au kuhitaji huduma za afya. Hii ni pamoja na kuwa na watumishi wa afya wa kutosha wanaolipwa vizuri, mazingira rafiki na miundo mbinu bora katika maeneo ya kutolea huduma za afya pamoja na unafuu katika gharama za matibabu.

Rai yangu kwa wataalamu wote wa afya walioko makazini, wahitimu wote wa afya, vyama vya kitaaluma vya afya, vyombo vya habari, wadau mbalimbali na watanzania wote kwa ujumla tutumie muda huu kupasa sauti na kuitaka serikali kuajiri watumishi wa afya wa kutosha na sio utaratibu huu wa kujitolea. Hii ndio namna pekee tutakayojihakikishia usalama wa afya zetu. Kama serikali isipoajiri leo, je itaajiri lini!??.

Wenu.
I.E.K
Afisa uuguzi II.
20/9/2021.
View attachment 1946941
 
Nchi ngumu sana hiii
 
Kiongozi Naomba kuuliza ,
1. Utaratibu huu utaanza kutumika kuanzia lini
2. Jukumu la kuwateua , watumishi watakaokua wanajitolea litakuwa la hospitali/kituo ama serikali, Na Kwa utaratibu upi
3. Kuna watumishi wanafanya kazi Kwa kujitolea Kwenye sekta za afya kama wataalmu wa it, wahasibu, wagavi.
Je nao watahusishwa?

Naomba unisaidie Kwa hayo tuu Kiongozi
 
Back
Top Bottom