Uchambuzi wa movie ya White House Down

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Image may contain: 2 people, people standing and text



..Ni John cale..capitol police officer..baba wa mtoto mmoja wa kike..

..Alimuahidi binti yake kuwa angepata kazi kwenye ikulu ya marekani..kama special agent..mtu anaeangalia maisha ya raisi kwa ukaribu..

...Akaongozana na binti yake..akaenda kufanyiwa interview..

..Na majibu yalipotoka,alishindwa kwenda kumsimulia mwanae..

..Alikuwa hajakidhi vigezo vya kumlinda raisi..ni kweli alipitia mafunzo yote na alipigana baadhi ya vita kama askari wa nchi..

..Lakini kazi aliyoomba ni kubwa kuliko zingine..na shule yake ilipokuwa ni ya kuungaunga na matokeo mabovu..jibu likawa ,moja tu..

...Hana sifa za kuwa special agent wa raisi wa marekani..

..Akakusanya karatasi zake,akamchukua binti yake..wakaungana na watu wengine kwenye kuitalii ikulu...

..Muda ambao John cale ana hasira ya kukosa kazi..ndo muda ambao raisi alikuwa na jambo lake ndani ya ikulu..

...Nchi ilkuwa kwenye taharuki..waandishi wa habari walijawa na wahka wa kuliongelea tukio hilo..alietegemewa kutuliza khofu ni mtu mmoja tu..

..Ndio ni mtu mmoja..nae ni mheshimiwa raisi wa marekani James Sawyer..

..Kuna jambo lililotakiwa kutatuliwa kabla halijawa tatizo,raisi alihutubia taifa na akawaahidi wananchi kuwa waondoe khofu..

..Ni mkataba wa hiari wa kuyaondoa majeshi ya marekani kwenye nchi za middle east...

..Raisi alipiga simu..lakini hakumaliza maongezi..

...Jengo la United States Capitol..likiwa na raisi wa marekani ndani...Lilitenganishwa nusu kwa uzito wa bomu lililolipuka..

..Na ndani ya dakika kumi raisi akiwa anatafutiwa mahali pa usalama..Ikulu ilikuwa ishawekwa lockdown..wa nje wa nje..wa ndani wa ndani..

...Yes..ni magaidi waliokuwa kama watalii..waliihitaji nchi kwa muda waliotaka wao..Target yao ilikuwa ni raisi..

..wakimpata huyo ndo wataiambia serikali ya nje kupitia spika ni nini wanataka...

..Wakamtia raisi nguvuni..na hakuna special agent yoyote aliepona ndani ya ikulu ambae alikuwa anamlinda raisi..

..Walikuwa wamejiandaa kwa vita..missilles zenye kupiga umbali mrefu zilikuwa kwenye mikono yao...

..Wakatangaza vita..na wakaweka kila kitu chao kwenye jengo hilo..yaani ataeenda tofauti na wao..basi wataifanya ikulu majivu na wote waliokuwa ndani...

...Kwenye mateka waliokuwa ndani..na mtoto wa John cale alikuwepo..

..Hapo ndo walipokosea...

...Aliemnyima kazi John cale..akapigiwa simu..Alipopokea akasikia sauti ya kiume ikisema

"mwanangu yupo ndani..na ntamleta pamoja na raisi"..

..What the hell!!.

..Yess..ni kweli john hana vigezo vya kumlinda raisi..lakini ana vigezo vya kumlinda binti yake..

...Mwanaume akaapa kutoondoka ndani ya ikulu mpaka aioneshe serikali kwanini alikuja kuomba kazi ya kumlinda raisi..

..Akavua suti ya interview..akavaa zana za kazi..

..FUNDI AKAINGIA KAZINI...

...Kadri ambavyo magaidi walivyozidi kupungua kimya kimya,ndivyo walianza kuamini kuwa kuna jeshi la siri limeingia mle ndani...

...Walishtuka walipokuja kujua hili..

...Kuwa hawapambani na jeshi..ni mtu mmoja tu..

..Emilly..mtoto wa John cale..akasimama mbele ya magaidi akawaambia kwa ujasiri..

.."Niueni ili babaangu awaue kwa amani..ila mkinitesa..babaangu asijue"...

.."Akijua itakuwa kesi nyingine"..

...Muda ambao mtoto Emilly anawatambia magaidi..ndo muda babaake alikuwa mbele ya muheshimiwa raisi...

..John cale akamwambia raisi wa marekani..ofisi yako imeninyima kazi ya kukulinda...naomba unipe wewe kazi hii kuanzia muda huu..

..Raisi akamuapisha John cale kwenye chemba ya maji machafu ndani ya ikulu...

...Maisha ya kiongozi mkubwa wa marekani yakakabidhiwa kwenye mikono ya special agent combat..

...Alichoona rais mpaka movie inaisha..hakujua kwanini huyu mtu alinyimwa kazi..

..,Ikulu ilipata mwenyewe..John cale akaisimamisha nchi kwa muda..

...Na hata raisi alipofanikiwa kutoka baada ya mchezo kumalizwa kiume na John...muheshimiwa alipanda ndege yake binafsi akisindikizwa na jeshi..

..Akasimama kwenye ngazi za ndege akasema..

.."Nalihutubia taifa muda huu kuwa..siendi popote bila mwanajeshi wangu"..

..Watu waote wakamtazama john cale..

..Wakapiga na saluti,fundi akieelekea kwenye ndege ya raisi..

..Hata yule alomkataa kwenye interview alikuwepo..

...John cale akapata kazi ya ndoto zake bila interview mpya..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom