uchambuzi wa kitabu- A Biography of the Continent

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Jina la kitabu
Jina la kitabu A Biography of the Continent.

Mwandishi: John Reader.

Mchambuzi: Nanyaro E.J.

Dibaji.

John Reader ambaye ni mwandishi wa Kitabu hiki ni mtoto wa dereva Tax wa Londoni,ambaye alikuja Afrika mwaka 1955 na kuishi Cape town kwa miaka nane kabla ya kuhamia Nairobi alikoishi kwa miaka kumi.Akiwa Afrika alifanya kazi kama mpigapicha na mwandishi hali iliyomfanya awe na uwezo wa kusafiri maeneo mengi,anasema aliona mazishi ya Tom Mboya na Kwame Nkrumah,alishikana mkono(shake hands) na Mwl Nyerere,Id Amin,Steven Biko,Jomo Kenyata,Ian Smith,Haile Selassie etc.

Anasema ana uelewa mkubwa sana wa mambo ya Kiafrika tofauti na picha waliyo nayo watu wa Magharibi ambao wanaona Afrika kama bara giza(dark continent).

Kitabu hiki kinaeleza ukweli juu ya Afrika ukweli ambao umefichwa kwa miaka mingi.Binadamu wa kwanza aligundulika hapa Afrika kaskazini mwa Tanzania,tena akiwa ameendelea ni ushaidi wa ustaarabu wa mwafrika.

Chapter 1

Building a Continent

Mwandishi anasema kuwa bara la Afrika limeweza kuhimili mabadiliko mbalimbali ya kijamii,kijiografia,kiuchumi, kuliko mabara mengine.Miamba yenye umri wa zaidi ya miaka bil 6 sawa na umri wa Dunia bado ipo Afrika(miamba iliyopo Mwanza,na kule Serengeti National park)Anasema hakuna Bara lingine lenye muundo huu wa maumbile ya Dunia tangu uumbaji hadi sasa kama bara la Afrika.

Mwandishi anasema kuwa uimara wa ardhi na miamba ya Afrika,iliyotokana na miamba hii kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine ndio imesababisha uwepo wa madini mengi anbayo ni faida kubwa kwa uchumi wa Afrika.Anasema Almasi inajitengeneza kwenye hali ya joto la kati ya 1000-1,150 Degrees!

Mwandishi anasema kuwa uchumi mwingi wa nchi nyingi za kiafrika kuanzia wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni ulijengwa kwa misingi ya madini,nchi kama Gabon,Ghana,Mali,Siara

leone,Zaire,Zambia na Zimbabwe na Afrika kusini.Ugunduzi wa Almasi huko Botswana ulifanya uchumi wake kukua kwa kasi hadi miaka ya 1994.Anaendelea kusema mkondo(craton) waKaapvaal pekee una zaidi ya tone 40,000 hadi 1883.

Chapter 2

TRANSITIONS

Mwandishi anasema miaka 3.6 bil iliyopita mabadiliko ya kimfumo na kimuundo yalipelekea hadi mimea kuanza kujitengenezea chakula yenyewe kupita kwa mfumo wa Photosynthesis,ni hapa ndio oksijen ilizaliwa

Kufuatia uwepo wa predators(wanyama wanaokula nyama)Matumizi ya harufu yalianza ili kuwezesha mwindaji na mwindwaji kujihami.Hata hivo ongezeko la wanyama wanaokula nyama lilikuwa

muhimu ili wasiishi muda mrefu na hivo kufa ba kutengeneza rasilimali nyingine ardhini ikiwepo mafuta na uhai wa viumbe wengine.

Mwandishi anasema kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa mabara mengine yamemeguka kutoka bara la Afrika ambalo kwa miaka mingi limebaki bila kutikisika anasema Human evolution has been the primary evidence of supercontinent! anaendelea kusema Africa is the "keystone of the continental drift hypothesis".Kwa miaka 200mil Afrika haijatingishika licha ya uwepo wa matukio makubwa yanayotishia Dunia kama Tsunami etc.

Chapter 3

MISSING LINKS

Uwanda wa misitu ya mvua ambayo imekuwapo kwa miaka 40mil,Sahara region na Misri ya leo inaaminika kuwa chanzo cha primates ambao binadamu ali evolve.Misitu ya kitropical inahifadhi kiwango kikubwa cha viumbe hai Duniani

Kuna jumla ya aina 4500 za mamalia Duniani kote huku Afrika ikiwa na kiwango kikubwa zaidi ya mabara mengine.Hii ni kutokana na bara hili kuwa

Intact na hivyo kuwezesha mabadiliko ya mara kwa mara ya mamalia.

Mwaka 1735 mwanasayansi wa Kisweden(swedish) Carl Von Linne akigundua namna ya kufanya classfication ndio neno HOMO likaanza rasmi kutumika.Neno HOMO liliandikwa kwa kilatin HOMO NOSCE TE IPSUM tafsiri yake MAN KNOW THSELF..

Hii ilikuwa hatua kubwa sana katika maendeleo ya binadamu,hasa kutambua watu kutokana na mahali na

eneo.Anasema kuwa kuna dhana mbili muhimu kuhusu binadamu

1. Kiimani(kidini) wanaaminu katika uumbaji.

2. Kisayansi binadamu ametokana na evolution ya Nyani(chimpazee) aliyebadilika badilika hadi kufikia tulivo leo(evolution hii inaendelea)anasema DNA ya Nyani na Binadamu ina mfanano kwa 99% ila anakiri kuwa 1%inayobaki ina maana kubwa sana

Miaka milion 200 iliyopita,wakati huo Dunia ikiwa moja(Pangae) kwa mujibu wa mwanasayansi Alfred Wegener, Dinosar(Dinosaurs)ndie mnyama aliyekuwa anatawala Dunia na alijaa kila pembe ya Afrika. Mwandishi anasema kuwa katika bonde la Fayum lililopo Misri ya leo kuna ushahidi wa wazi wa maisha ya kale ya. wanyama wa majini(Reptilia) hasa samaki,mamba etc...misitu mingi ilijawa na na popo

Chapter 4

ORIGINS AND CLIMATE

Mwandishi anasema kuwa Mabadiliko ya tabianchi yanaadhiri sehemu kubwa ya mgawanyo wa makazi ya viumbe hai Duniani.Lakini hapa Afrika viashiria vinaonyesha kuwa ushindani wa rasilimali unaadhiri zaidi ya mabadiliko ya tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi ambayo tunayashuhudia leo si kwamba yameanza leo bali yamekuwepo tangu historia ya

kijiojia,ndio yaliyosababisha kupotea kwa Dinosar na ndio yaliyofanya uwepo wa binadamu!kiumbe hai ambaye alishindwa kuwenda sambamba na evolution na adaptation basi kiumbe huyo alitoweka.

Mwandishi anasema kuwa Bara la Afrika lilikuwa limeungana na Ulaya likatengana na baadae miaka mil 16 iliyopita vikaungana tena na ni kipindi ambacho kiliruhusu wanyama ambao walikuwa wanapatikana Ulaya wakahamia upande ambao ni Afrika na ambao ulikuwa ni bora zaidi.Mwandishi anasema

mgawanyo wa pili ulizaa species mbalimbali hata ndani ya bara la Afrika yenyewe.

Anaendelea kusema kuwa Afrika ni chanzo kizuri na cha uhakika cha taarifa mbalimbali za kiutafiti wa viumbe hai na maisha kwa ujumla,kutokana na Uimara wa Bara hili.Afrika ni maabara ya mammalian evolution!

Mwandishi: John Reader.

Mchambuzi: Nanyaro E.J.

Dibaji.

John Reader ambaye ni mwandishi wa Kitabu hiki ni mtoto wa dereva Tax wa Londoni,ambaye alikuja Afrika mwaka 1955 na kuishi Cape town kwa miaka nane kabla ya kuhamia Nairobi alikoishi kwa miaka kumi.Akiwa Afrika alifanya kazi kama mpigapicha na mwandishi hali iliyomfanya awe na uwezo wa kusafiri maeneo mengi,anasema aliona mazishi ya Tom Mboya na Kwame Nkrumah,alishikana mkono(shake hands) na Mwl Nyerere,Id Amin,Steven Biko,Jomo Kenyata,Ian Smith,Haile Selassie etc.

Anasema ana uelewa mkubwa sana wa mambo ya Kiafrika tofauti na picha waliyo nayo watu wa Magharibi ambao wanaona Afrika kama bara giza(dark continent).

Kitabu hiki kinaeleza ukweli juu ya Afrika ukweli ambao umefichwa kwa miaka mingi.Binadamu wa kwanza aligundulika hapa Afrika kaskazini mwa Tanzania,tena akiwa ameendelea ni ushaidi wa ustaarabu wa mwafrika.

Chapter 1

Building a Continent

Mwandishi anasema kuwa bara la Afrika limeweza kuhimili mabadiliko mbalimbali ya kijamii,kijiografia,kiuchumi, kuliko mabara mengine.Miamba yenye umri wa zaidi ya miaka bil 6 sawa na umri wa Dunia bado ipo Afrika(miamba iliyopo Mwanza,na kule Serengeti National park)Anasema hakuna Bara lingine lenye muundo huu wa maumbile ya Dunia tangu uumbaji hadi sasa kama bara la Afrika.

Mwandishi anasema kuwa uimara wa ardhi na miamba ya Afrika,iliyotokana na miamba hii kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine ndio imesababisha uwepo wa madini mengi anbayo ni faida kubwa kwa uchumi wa Afrika.Anasema Almasi inajitengeneza kwenye hali ya joto la kati ya 1000-1,150 Degrees!

Mwandishi anasema kuwa uchumi mwingi wa nchi nyingi za kiafrika kuanzia wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni ulijengwa kwa misingi ya madini,nchi kama Gabon,Ghana,Mali,Siara leone,Zaire,Zambia na Zimbabwe na Afrika kusini.

Ugunduzi wa Almasi huko Botswana ulifanya uchumi wake kukua kwa kasi hadi miaka ya 1994.Anaendelea kusema mkondo(craton) waKaapvaal pekee una zaidi ya tone 40,000 hadi 1883.

Chapter 2

TRANSITIONS

Mwandishi anasema miaka 3.6 bil iliyopita mabadiliko ya kimfumo na kimuundo yalipelekea hadi mimea kuanza kujitengenezea chakula yenyewe kupita kwa mfumo wa Photosynthesis,ni hapa ndio oksijen ilizaliwa

Kufuatia uwepo wa predators(wanyama wanaokula nyama)Matumizi ya harufu yalianza ili kuwezesha mwindaji na mwindwaji kujihami.Hata hivo ongezeko la wanyama wanaokula nyama lilikuwa

muhimu ili wasiishi muda mrefu na hivo kufa ba kutengeneza rasilimali nyingine ardhini ikiwepo mafuta na uhai wa viumbe wengine.

Mwandishi anasema kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa mabara mengine yamemeguka kutoka bara la Afrika ambalo kwa miaka mingi limebaki bila kutikisika anasema Human evolution has been the primary evidence of supercontinent! anaendelea kusema Africa is the "keystone of the continental drift hypothesis".Kwa miaka 200mil Afrika haijatingishika licha ya uwepo wa matukio makubwa yanayotishia Dunia kama Tsunami etc.

Chapter 3

MISSING LINKS

Uwanda wa misitu ya mvua ambayo imekuwapo kwa miaka 40mil,Sahara region na Misri ya leo inaaminika kuwa chanzo cha primates ambao binadamu ali evolve.Misitu ya kitropical inahifadhi kiwango kikubwa cha viumbe hai Duniani

Kuna jumla ya aina 4500 za mamalia Duniani kote huku Afrika ikiwa na kiwango kikubwa zaidi ya mabara mengine.Hii ni kutokana na bara hili kuwa

Intact na hivyo kuwezesha mabadiliko ya mara kwa mara ya mamalia.

Mwaka 1735 mwanasayansi wa Kisweden(swedish) Carl Von Linne akigundua namna ya kufanya classfication ndio neno HOMO likaanza rasmi kutumika.Neno HOMO liliandikwa kwa kilatin HOMO NOSCE TE IPSUM tafsiri yake MAN KNOW THSELF..

Hii ilikuwa hatua kubwa sana katika maendeleo ya binadamu,hasa kutambua watu kutokana na mahali na

eneo.Anasema kuwa kuna dhana mbili muhimu kuhusu binadamu

1. Kiimani(kidini) wanaaminu katika uumbaji.

2. Kisayansi binadamu ametokana na evolution ya Nyani(chimpazee) aliyebadilika badilika hadi kufikia tulivo leo(evolution hii inaendelea)anasema DNA ya Nyani na Binadamu ina mfanano kwa 99% ila anakiri kuwa 1%inayobaki ina maana kubwa sana

Miaka milion 200 iliyopita,wakati huo Dunia ikiwa moja(Pangae) kwa mujibu wa mwanasayansi Alfred Wegener, Dinosar(Dinosaurs)ndie mnyama aliyekuwa anatawala Dunia na alijaa kila pembe ya Afrika. Mwandishi anasema kuwa katika bonde la Fayum lililopo Misri ya leo kuna ushahidi wa wazi wa maisha ya kale ya. wanyama wa majini(Reptilia) hasa samaki,mamba etc...misitu mingi ilijawa na na popo

Chapter 4

ORIGINS AND CLIMATE

Mwandishi anasema kuwa Mabadiliko ya tabianchi yanaadhiri sehemu kubwa ya mgawanyo wa makazi ya viumbe hai Duniani.Lakini hapa Afrika viashiria vinaonyesha kuwa ushindani wa rasilimali unaadhiri zaidi ya mabadiliko ya tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi ambayo tunayashuhudia leo si kwamba yameanza leo bali yamekuwepo tangu historia ya

kijiojia,ndio yaliyosababisha kupotea kwa Dinosar na ndio yaliyofanya uwepo wa binadamu!kiumbe hai ambaye alishindwa kuwenda sambamba na evolution na adaptation basi kiumbe huyo alitoweka.

Mwandishi anasema kuwa Bara la Afrika lilikuwa limeungana na Ulaya likatengana na baadae miaka mil 16 iliyopita vikaungana tena na ni kipindi ambacho kiliruhusu wanyama ambao walikuwa wanapatikana Ulaya wakahamia upande ambao ni Afrika na ambao ulikuwa ni bora zaidi.Mwandishi anasema

mgawanyo wa pili ulizaa species mbalimbali hata ndani ya bara la Afrika yenyewe.

Anaendelea kusema kuwa Afrika ni chanzo kizuri na cha uhakika cha taarifa mbalimbali za kiutafiti wa viumbe hai na maisha kwa ujumla,kutokana na Uimara wa Bara hili.Afrika ni maabara ya mammalian evolution!
 
Kitabu.A biograph of the continent
Mwandishi John Reader
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Sehemu ya 5

THE REAL WORLD
Mwandishi anasema kuwa mabaki ya mifupa ya binadamu wa kale yanayopatikana Afrika yamekuwa msaada mkubwa katika historia na kwa watafiti wa sayansi(African fossil record).Ambayo yanawezakuwa ushahidi wa maendeleo ya binadamu wa kale hadi Binafamu wa leo.Anasema kuna tofauti ya kiumri kati ya eneo ambalo mabaki yanapatikana na mabaki yenyewe.Maeneo mengi(sites) ambako mabaki yamepatikana huwa yana maji
kabla ya kazi ya ugunduzi yaani inawezakuwa mto uliokauka au ziwa.
Nyayo zilizogundulika Laetol huko Oldpai Kaskazini mwa Tanzania zina umri wa 3.7mil,ni wazi kuwa nyayo hizi zilikuwa za AUSTRALOPITHECUS AFARENSIS,kutokana na ushahidi mwingi wa eneo hilo nyayo hizi zinabaki kuwa ushahidi usio na shaka wa uwepo wa binadamu wa kale na maendeleo yake,licha ya upatikanaji wa mabaki maeneo mengine Dunia.Licha ya mabaki haya kusadifu binadamu wa kale lakini pia yanasadifu binadamu wa kisasa

Homo Habilis
@HOMO ERECTUS
homo sapiens
Sisi ni Homo Sapiens binadamu wa leo! Mwandishi anaendelea kiandika kuwa mabaki haya (visukukuu) vinapatikana katika maeneo mbalimbali Afrika kama Kenya,Ethiopia,Libya,Namibia,Tanzania etc na yanatofautiana umri,ila mabaki ya muda nfupi ni miaka 250,000 iliyopita
Mwandishi anasema site nyingi ni matokeo ya tectonic uplift and fracture which created the Great Rift Valley,kilometa 8 Kaskazini mwa Ikweta.Anasema visukukuu(Fossil) zinapatikana katika ngazi za miamba ya sedimentary iliyotenganishwa na layer of volcanic lava.Anasema uwepo wa Bonde la ufa umesababisha uwepo wa Biological barrier kati ya Mashariki na Magharibi.Upande wa magharibi ni vilima na misitu,wakati Mashariki ni kukavu na ni savana.Nyani na binadamu wa kwanza walitenganishwa na mazingira na kila mmoja aliishi kupambana na hali yake na hivo kulazimisha abadilike ili aweze kuhimili Mazingira
yaliyomkabili(Adaptation)Nyani alibaki upande wa Magharibi kwrnye vilima kama misitu ya Kongo na aliitwa PANIDAE wakati binadamu (Homidae) aliishi Mashariki Tanzania,Ethiopia,Kenya etc na ndio site nyingi zinakopatikana

Chapter 6
FOOTSTEPS
Mwandishi anasema volcano iliyotoka vilima vya Lemagurut na Sadiman ndio iliyotengeneza sehemu ya Laetol,eneo muhimu katika maendeleo ya binadamu,Moru Kopjes kaskazini mwa Serengeti kuna michoro kwenye miamba ya aina ya Granite,michoro hiyo ina zaidi ya miaka 1.9ml.
Uwezo wa binadamu kutembea kwa miguu miwili ndio mabadiliko makubwa zaidi kwa binadamu katikaa historia ya
human evolution & adaptation.Swali limebaki ni lini na jinsi gani binadamu wa kale alianza kutembea kwa miguu miwili(bipedalism),(Bado ni mjadala mpana)
Mwandishi anasema kuwa kuna dhana ya mwanasayansi Darwin ambaye anaamini kuwa bipedalism ilianza kabla hata ya kukua kwa ubongo wa binadamu(binadamu wa kale alikuwa na ubongo mdogo sana),ingawa kuna dhana nyingine kuwa ubongo uliongezeka kabla ya sehemu nyingine za mwili.

Chapter 7
THE CUTTING EDGE
Mwandishi anasema kuwa binadamu wa kale alikuwa Bipedal na nomads na sehumu kubwa ya chakula chake kilikuwa matunda,mizizi na misoga ya wanyama na hivo aligundua matumizi ya kutumia mawe makali kukatia nyama. Anaendelea kusema kuwa Lucy aliyepatikana huko Ethiopia alikuwa na urefu wa centimita 122 na Kg 30(sawa na mtoto wa miaka sita wa binadamu wa leo)anasema mikono ya Lucy ilikuwa mirefu karibu kufika chini ya magoti akiwa amesimama wima

Chapter 8
IN THE MINDS EYE.
Mwandishi anasema kuwa mahitaji ya stone-tool yalichangia kasi ya maendeleo ya evolution ya binadamu,hadi kufikia uwezo wa kutengeneza moto kwa kutumia zana za asili,ambazo ziligunduliwa na Homo Sapiens ambaye ndie binadamu wa sasa!
Mwandishi anasema kuwa Homo Habilis(Handy man) ndie binadamu alienza kufanya kazi za mikono yaani
alisha develop uwezo wa kutembea kwa miguu miwili
Homo erectus aliishi baada ya Homo Habilis na tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonyesha kuwa mifupa yake na ubongo vilikuwa bora zaidi ya Homo Habilis.Mabaki ya Homo Erectus yanaonyesha kuwa alikuwa na urefu wa 1.6m(mita moja nukta sita) na mikono yake inafanana na bibadamu wa leo.Ubongo wake(brain size) ilikuwa 900cc
Mwandishi anasema kuwa Homo erectus alikuwa bora zaidi ya Java(homo
neanderthalensis) aliyeishi Ulaya miaka 120,000(laki moja na ishirini)
Kufikia miaka 1.5mil ubongo wa homo erectus uliongezeka hadi kufikia 1000cc wakati ubongo wa binadamu wa leo ni kati ya 1000-2000cc
Mwandishi anasema kuwa wakati Homo Habilis alikuwa hatembei zaidi ya kilometa nne Homo Erectus alikuwa na uwezo wa kutembea zaidi ya kilometa kumi kutafuta materio mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yake na ushahidi wa hili ni umbali ambo visukukuu mbalimbali vilipatikana wakti wa ugunduzi,
Homo erectus ndie aliyeongezeka na kuanza kusambaa maeneo mbaimbali ya bara la Afrika na baadhi ya sehemu ya Asia
Baada ya Homo Erectus kutoweka aka develop Homo Sapiens ambaye ndie binadamu wa sasa ambaye alikuwa Mwembamba na mrefu(Homo Sapiens ndie mimi na wewe)
 
Inavyoonekana mwandishi wa kitabu haamini katika uumbaji, bado anaamini katika Evolution of man.
 
Hapa sio suala la imani ktk uumbaji bali ni ushahidi wa kihistoria. Wewe baki na imani yako waache watafiti watoe ushahidi wa kile walichogundua
 
Inavyoonekana mwandishi wa kitabu haamini katika uumbaji, bado anaamini katika Evolution of man.
nikiwa chumba cha mtihani wa shule nikaulizwa kuhusu binadamu ntajibu kuwa ni yule aliegundulika Oldpai kaskazini mwa Tanzania
Nikiwa ni mtihani wa Dini nitajibu kuwa ni Adam
 
nikiwa chumba cha mtihani wa shule nikaulizwa kuhusu binadamu ntajibu kuwa ni yule aliegundulika Oldpai kaskazini mwa Tanzania
Nikiwa ni mtihani wa Dini nitajibu kuwa ni Adam

Mimi hizo marks ntaziacha nizikose.
 
Kitabu.A Biograph of the Continent

Mwandishi .John Reader

Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 10

OUT OF AFRICA

Mwandishi anasema kuwa binadamu wa leo aliishi Afrika tu kabla ya kuhamia sehemu ngingine za Dunia miaka laki moja iliyopita,anasema wakati huo binadamu alikuwa alikuwa ana uwezo wa cooling system na ubongo mkubwa.

Dhana hii inapewa nguvu na aina ya mabaki yaliyopatikana sehemu nyingine nje ya Afrika ambayo yana umri mdogo zaidi,hakuna mabaki yenye zaidi ya miaka

laki moja n nusu yaliyopatikana nje ya Afrika.

Ukweli Mwandishi anasema kuwa kwa mujibu wa Mitochondria DNA(mitochondria is discrete parts of cell which play a vital role in the enegy production systems of living organisms),kila binadamu wa leo ana chembechembe za DNA za mwanamke wa kiafrika wa vizazi 10,000 vilivyopita.Hata hivyo si justfication pekee bali ile nguvu ya asili ambayo Afrika ndio cradle of mankind,ndio maana wanasayansi wana msemo wao "the African Eve"

Mwandishi anahitimisha kwa kusema kuwa kila binadamu anayeishi leo chanzo chake ni Afrika

Chapter 11

ON HOME GROUND

Mwandishi anasema kuwa bara la Afrika limegawanywa katika sehemu kuu mbili na msitari wa Ikweta,sehemu kubwa ya Afrika ni tropikali hali inayofanya hali ya hewa kuwa nzuri na ambayo ipo stable kulinganisha na mabara mengine.

Mwandishi anaendelea kusema kuwa mahusiano ya ardhi na mimea ya Afrika kwa upande mmoja na wanyama walao mimea kwa upande wa pili yamekuwa mahusiano ya vizazi na vizazi,Mimea ina

uhusiano na walao mimea,mfano ukuaji wake unaruhusu wanyama kula ila sio katika kiwango cha kuadhiri ukuaji wake,mimea ikijua kuwa itafaidika na mbolea hivo kufanya ukuaji kuwa endelevu.Hii ndio sababu ya uwepo wa mimea mingi kuliko wanyama walao mimea,na kuna wanyama wengi walao mimea kuliko walao nyama..ni ili ku balance life cycle

Hata hivo anakiri kuwa udongo unachangia sehemu kubwa katika ubora wa mimea,na hii ndio sababu wanyama wengi walihama kutoka mabara mengine(baada ya uwepo wa mabara) na kurudi kwenye nchi ya asili

Afrika.Anaendelea kusema kuwa wanyama na mimea mingi ina uwezo mkubwa wa kuona nini kitatokea miaka mingi ijayo na huanza adaptation kwa ajili ya kupambana na mazingira yajayo!Huu ndio msingi wa miti mingi kupukutisha majani wakati wa kiangazi ili kupunguza uihitaji wa maji ambao wakati huo huwa hakuna na kuyarejesha tena wakati wa masika.Anatoa mfano mwingine wa mnyama Swala mdogo Dik Dik ambaye ana uwezo wa kukaa miezi mitatu bila kunywa maji na sasa ameongeza hadi minne yaani siku 120 bila kunywa maji,sababu ya swala huyu ni kujiandaa na ukame maana maji yanaendelea kupungua Dunia kutokana na sababu

nyingi lakini pia kwa ajili ya survival yake,Dik dik anajua baada ya miezi mitatu mvua itanyeesha na atakunywa kwenye dimbwi vidogo badala ya kwenda mtoni ambako atakuwa anasubiriwa na wanyam kama Duma,chui,fisi na hata ndege kama Tai,ila hizi dimbwi sio za kudumu bali zinatokea tu baada ya mvua.Katik kipindi cha kutokubywa maji Dik Dik huwa haendi haja kubwa wala ndogo na ikitokea lazima aende inakuwa very concetrated na haja kubwa yake ni vipunje vigumu kama mawe

Chapter 12

WORD OF MOUTH

Mwandishi anasema kuwa ADAPTATIONS ambayo ilisaidia evolution iligusa pia lugha za binadamu wa kale,ndio kusema kuwa LUGHA za mawasiliano ya binadamu zilianzia Afrika.Anasema licha ya kutokuwa documented kwa lugha ndogo ndogo za makabila mengi Afrika lakini ukweli wa wazi kuwa Afrika ndio chimbuko la lugha nyingi Dunia.

Mwandishi anasema kuwa uwezo huu wa binadamu kutoa sauti yenye maana (lugha),ilisababishwa kwa sehemu kubwa

(sio yote)na mabadiliko ya tabia nchi na mazingira,mabadiliko ambayo hufanya binadamu kuwa na ubinafsi,katika ubinafsi huo ndio lugha nyingi zimezaliwa.Hata hivyo anakiri kuwa uwezo huu ndio umechangia maendeleo ya binadamu kukua kwa kasi ya ajabu.

Anasema kuwa Homo Erectus ndie aliyeenza kuwa na sauti ambayo baadae ilikuwa na kuwa lugha.Wakati Homo erectus akikuwa na kujua kutoa sauti(kuongea) viumbe wengine kama spider know how to spin webs

Language is as old as humanity! Mwandishi anatoa mfano wa lugha kongwe zaidi Dunia KHOISAN(hii inazungumzwa na Wadatoga wanaopatikana kule bonde la Yaeda chini Wilaya ya Karatu Arusha Tanzania,na baadhi ya maeneo katika misitu minne ya Congo,hadi leo hii hawa jamaa ni wawindaji na wanapenda sana Bangi)BANTU,Nilotic na Kushi haya ni makundi manne lakini ndani yake kuna lugha zaidi ya 500.Kwa Tanzania pekee kuna kugha zaidi ya 120 katika makabila 120,lakini ukiyachukua yote utapata makundi manne tu yenye uhusiano wa karibu na mabaki yaliyogundulika Oldpai

Chapter 13

ANCENTRAL ECONOMIES

Mwandishi anasema kuwa Hunters & gatherer ndio jamii iliyoasisi uchumi! anasema kutokana na nguvu(energy)inayopatikana kwenye asali ineifanya bidhaa hiyo ASALI kuwa na ushindani mkali tangu enzi na enzi kati ya binadamu na baadhi ya wanyama hasa ndege ambao nao waligundua mikakati ya kuhakikisha kuwa wanafaidika,anasema wakati binadamu akikusanyika kuvuna asali ndege hawa

huwa maeneo ya jirani ili kula mabaki yake(mutual cooperation)

Anasema nyuki wali inspire viumbe wengine na hata binadamu hasa katika mapinduzi ya viwanda yaliyokuwa yanakusudia kuzalisha ziada kwa ajili ya wengine ndio maana tunaSema (as busy as bees)

Mwandishi anasema kuwa wanaume walikuwa wawindaji na wakati mwingine walikuwa wanaenda mawindoni na kurudi Kavu hali iliyofanya wanawake waanze kujishughulisha na uchimbaji wa mizizi na matunda ya ardhini kama viazi

etc ili kukidhi mahitaji ya familia,katika hili wanawake wangetumia muda mrefu zaidi kazini kazini kuliko wanaume,anatoa mfano kuwa wawindaji wanaenda kuwinda na kutumia masaa 30kwa uwindaji wa siku sita,jambo anbalo tafiti zinasema kuwa wanaume walifika huko porini na kupumzika badala ya kufanya kazi!jambo hili lilipelekea binadamu wa kale kuanza kufanya shughuli za kiuchumi ili kukidhi mahitaji yake! Mwandishi anasema kuwa utafiti uliofanywa umegundua kuwa wanaume walikuwa wakiwinda wanaanza kula maini,figo,firigisi,na sehemu zote nzuri hapo hapo kwenye eneo la uwindaji,tabia hii imeendelea hadi leo.

Chapter 14

THE HUMAN POTENTIAL

Mwandishi anasema kuwa uoto wa asili wa kitropical uliopo Afrika una zaidi ya aina 20 za wanyama wakubwa wanaoishi,kuanzia Tembo,Faru etc na mamilion ya wanyama wengine waliotapakaa kutokana na uhitaji wa chakula chao,mfano Twiga lazima aishi sehemu yenye miti miti(Savana).

Mwandishi anaendelea kusema kuwa Wanabaolojia wamegawanya wanyama katika makundi makuu mawili

1.R.Strategies.Anasema kundi hili ni lile la wanyama wenye miili midogo na ambao huzaa mapema na watoto wengi,ila ni wachache ndio huishi,lifespan yao pia ni ndogo

2.K.Strategies,hili kundi huzaa watoto wachache ambao wengi huishi,ni kundi linalozaa wakati mwafaka ili kitoto kiishi(nyumbu na pundamilia wana uwezo wa kusogeza siku ya kuzaa kwa wiki mbili zaidi kusubiria mvua)Binadamu anaaminika kuwa Kundi hili la K,msingi mkuu ni namna binadamu alivofanya evolution na namna alivyo na uwezo wa

kutabiri maisha ya baadae na hivo kufanya maandalizi(kama ambavyo sasa hivi vijana wengi wanazaa watoto wawili hadi watatu ili kuweza kuwapa elimu nzuri na huduma nyingine)

Moto ni moja ya silaha za asili za binadamu dhidi ya wanyama,wanyama wote wanaogopa moto na hilo binadamu alilitambua mapema

Chapter 14

THE HUMAN POTENTIAL

Mwandishi anasema kuwa uoto wa asili wa kitropical uliopo Afrika una zaidi ya aina 20 za wanyama wakubwa wanaoishi,kuanzia Tembo,Faru etc na mamilion ya wanyama wengine waliotapakaa kutokana na uhitaji wa chakula chao,mfano Twiga lazima aishi sehemu yenye miti miti(Savana).

Mwandishi anaendelea kusema kuwa Wanabaolojia wamegawanya wanyama katika makundi makuu mawili

1. R.Strategies.Anasema kundi hili ni lile la wanyama wenye miili midogo na ambao huzaa mapema na watoto wengi,ila ni wachache ndio huishi,lifespan yao pia ni ndogo

2. K.Strategies,hili kundi huzaa watoto wachache ambao wengi huishi,ni kundi linalozaa wakati mwafaka ili kitoto kiishi(nyumbu na pundamili wana uwezo wa kusogeza siku ya kuzaa kwa wiki mbili zaidi kusubiria mvua)Binadamu anaaminika kuwa Kundi hili la K,msingi mkuu ni namna binadamu alivofanya evolution na

namna alivyo na uwezo wa kutabiri maisha ya baadae na hivo kufanya maandalizi(kama ambavyo sasa hivi vijana wengi wanazaa watoto wawili hadi watatu ili kuweza kuwapa elimu nzuri na huduma nyingine)

Moto ni moja ya silaha za asili za binadamu dhidi ya wanyama,wanyama wote wanaogopa moto na hilo binadamu alilitambua mapema

Chapter 15

CLIMATE &CULTURE

Mwandishi anasema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yaliyokuwa recorded ni miaka 18,000 iliyopita.

Mwandishi anasema kuwa mabadiko haya yaliadhiri mimea ba hivo kuleta madhara kwa wanyama walao nyama,jambo ambalo liliadhiri mzunguko wa maisha kwa ujumla.Madhara haya yalimwadhiri pia binadamu wa kale hali iliyomfanya aanze kutafuta mbadala wa

Uwindaji,kurina asali na matunda ya mwituni,ndio akagundua kilimo na kuhifadhi chakula wakati kinapopatikana kwa ajili ya matumizi ya baadae wakati hali itakapokuwa ngumu!(rejea Vihenge au Piramidi za Misri)

Anaendelea kusema kuwa ndio kipindi ambacho binadamu alianza kula samaki(catfish) aliokuwa anawavua kwenye mito midogo midogo

Nanyaro EJ
 
Back
Top Bottom