Uchambuzi wa hotuba ya rais ya mwisho wa mwezi wa pili 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchambuzi wa hotuba ya rais ya mwisho wa mwezi wa pili 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Mar 4, 2011.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Naomba sana, bila ushabiki, hasira, tuichambue kwa kina Hotuba ya Raisi ya mwisho wa Mwezi wa pili. Mimi nitaanza halafu wengine kufuatia.
  Kwa ujumla hotuba ilikua ina mapungufu mengi sana, ilitakiwa mwaandaaji wa hotuba ile hafukuzwe kazi mara moja. Hotuba ilitenga kulalamika zaidi kuliko uetekelezaji, Tofauti na hotuba za Mkapa zilizokua zikitaja tatizo na utekelezaji wake na pia utaisha Lini.

  Kuzungumzia chama Fulani

  Mimi kilichonishangaza hotuba inasema HOTUBA YA RAIS YA MWISHO WA MWEZI sasa inapofika wakati wa kuongelea chama, je anaongea kama Rais au kama Mwenyekiti wa SISIMU? Pale alipaswa kuzungumzia usalama wa nchi/taifa na sio maandamano ya chama Fulani, hiyo ni kazi ya Katibu wa chama. Sasa tujiulize je kweli chadema wana lengo la kupindua serikali?
  Unajua uhaini au kuupindua ni vigumu sana, Kupindua serikali ni lazima kuendane na uasi. Hapa Tanzania hamna waasi. Waasi ni kikundi cha watu chenye lengo la moja kwa moja la kuipindua serikali, kikundi hiki kitakua na eneo maalumu, silaha, na siasa kali. Kauli mbiu ya kikundi hicho lazima kiwe serikali iondoke. Kama ilivyofanyiaka Tunisia, Misri na sasa Libya, huu ni uasi au huko DRC
  Ila ukiangalia Chadema hawajafika huko. Kama ulisikiliza juzi mjadala BBC wa Libya, kuna mchambuzi mmoja alifafanua vizuri sana nini maana ya uasi. Akasema Libya kuna uasi kwa sababu kikundi kimejitenga na kina silaha kwa lengo maalumu la kumwaondoa Gadhafi. Lakini Chadema haijafika huko, inachofanya ni kutoa elimu ya uraiya na kuikosoa serikali tu. Kweli ni nani asiyejua maisha sasa ni magumu sana na kupita kiasi? Ndugu zetu wengi hali zao ni mbaya sana, Bei za bidhaa juu, biashara wamefunga kwa sababu umeme hamna kuna watu walikua wanauza maji kwa pampu, nyama, vinywaji, saloon, maziwa, na vingine vingi biashara za aina hii zimekufa kutokana na mgao mkali wa umeme. Pia hamna hata matumaini kwamba siku moja tatizo litaondoka.

  Naomba weka kichwa cha habari kinachohusiana na hotuba ile then ichambue kwa kina. Mfano Rais anaposema siwezi kumaliza matatizo yenu, je wananchi wategemee nini, Je kulalamikia mvua kutonyesha ni sahini wakati kuna maziwa na mito mingi? Chambua kwa kina please
   
 2. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Thread ya kuhusiana na hotuba ya jk ilikuwepo jana lakini mapema ikaondolewa, sasa sijui ni kwa msingi gani! nina wasiwasi na hii haitadumu. .......naona kama hatuko tena salama ndani ya nyumba!!
   
Loading...