Uchambuzi wa hotuba ya Rais Magufuli wakati akimwapisha Waziri wa Katiba na Sheria

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Na, Robert Heriel

Kutokana maombi ya watu wengi wakiwamo viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa, na Watanzania kwa ujumla kuwasiliana nami kwa njia simu, wengine wakinitumia ujumbe kwenye WhatsApp, messenger, au SmS za kawaida, kunitaka nieleze maoni yangu kufuatia hotuba ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli, nami kwa heshima kubwa nichukue nafasi hii kupokea ombi lao. Nami leo hii nichukue nafasi hii kuchambua kile alichokieleza Mhe. Rais ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwenye sehemu kubwa ya hotuba hiyo, na kwa uchache kuikosoa hotuba hiyo.

Ifahamike Uchambuzi huu, ni kwa maslahi mapana ya taifa, huku nikizingatia zaidi uzalendo na kusema ukweli pasi na hofu wala kupendelea.

Uchambuzi wa Hotuba ya Mhe. Rais.

Hotuba ya Mhe Rais inaweza kujadiliwa na watu wengi. Wapo watakaombeza, wapo watakaompongeza, lakini pia wapo watakaozingatia ukweli pasipo kupendelea.

Hotuba ya Mhe Rais imejaribu kueleza mambo kadhaa ambayo mengine yapo dhahiri lakini mengine yakiwa ya siri.

Yafuatayo ni sehemu ya mambo ambayo Mhe. Rais ameweza kuyaeleza katika hotuba yake:

1. Historia ya Magonjwa

Mhe. Rais katika hotuba yake ameweza kueleza kwa kifupi kabisa historia ya magonjwa ikiwamo ugonjwa wa surua, Ukoma, TB, EBOLA, ZIKA miongoni mwa magonjwa mengine. Mhe Rais, ameweza kuelezea historia fupi ya magonjwa hayo na jinsi yalivyokuwa tishio kwa zama hizo lakini licha ya kuwa tishio magonjwa hayo yalipita na kuonekana yakawaida. Pia amewaasa watanzania kuchukua tahadhari. Lengo kuu la kutoa historia ya magonjwa ni kuwatoa hofu baadhi ya Watanzania ili kupunguza athari za kisaikolojia katika afya yao.

Hili naungana naye kwa asilimia mia moja.

2) Sababu za Kukataa Lockdown

Mhe Rais kupitia Hotuba yake ameelezea sababu ya kukataa lockdown nchi nzima au sehemu fulani ya nchi. Moja ya sababu kuu ni suala zima la uchumi. Mhe. Rais anaamini na anataka Watanzania waamini na kuungana naye kuwa kuifungia nchi au sehemu ya nchi kutaumiza uchumi wa taifa. Na hiyo italeta athari kwa nchi kujiendesha mathalani, kulipa wafanyakazi na watumishi wa serikali. Mhe. Rais kupitia hotuba yake amejitetea kwa kutoa mifano dhahiri ya kulipa Waalimu na Wafanyakazi wengine zaidi ya miezi miwili na kuwahakikishia kuendelea kuwalipa licha ya corona kuendelea kuitesa dunia.

Hili naungana naye kwa asilimia mia moja, na kila siku nalihamasisha kila nipatapo nafasi.

3) Hujuma kwenye Sekta ya Afya

Mhe. Rais kupitia hotuba yake ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na baadhi ya Wafanyakazi wa sekta ya Afya hasa katika Maabara kuu ya taifa kuwa huenda kuna hujuma inaendelea. Shutuma za Mhe. Rais katika ofisi hizo ni kutokana na uchunguzi wa kimkakati baada ya kuona matokeo ya shaka katika vipimo vya kupimia Corona.

Mhe. Rais kupitia hoja yake ya uhujumu kwa baadhi ya wataalamu amelenga kuwaambia Watanzania kuwa kuna Wasaliti wa nchi kwa namna ya moja kwa moja au ya kujificha. Hujuma kwa kukusudia au bila kukusudia.

Aidha, hujuma hizo zinalenga vipimo vyenyewe, Au Reagent, pamba, au kuna namna vifaa hivyo vimesetiwa kuwa vitoe majibu kwa mpango maalumu ulioratibiwa, yaani kila wapimwapo watu 20 basi yule wa 21 aonekane anamaambukizi.

Hii inanipa tafsiri kadhaa katika kumuelewa Mhe. Rais, mosi, Mhe Rais anajaribu kuniambia kuwa yeye hawaamini watenda kazi wake. Je ni kosa kwa Kiongozi kutowaamini Watendakazi wake, na hapa ni wahusika wa sekta za Afya? Jibu ni hapana, sio kosa kwake kutokuwaamini. Hasa ukizingatia kanuni ya "Trust no one", ya macheavili.

4) Umuhimu wa Intellejensia imara.

Hotuba ya Mhe Rais imefafanua kwa kina namna gani taifa letu lilivyokuwa na intellejensia imara, na jinsi linavyotakiwa kuwa imara. Kupitia mbinu ya kutuma sampo bandia na kuya-label kwa majina ya watu kisha kugundua kuwa kuna sintofahamu katika matokeo ya vipimo. Kumetoa maana kadhaa, moja wapo ni kuchunguza vipimo vilivyoletwa huenda vimeghushiwa na virusi vya corona, au Wahusika wamenunuliwa.

Intellejensia inasaidia kukusanya taarifa muhimu, kuzichunguza, kuzifanyia kazi, kuzizuia zisitoke ikiwa zitaleta madhara.

Katika Intellejensia Mhe. Rais amejaribu kueleza Watanzania kuwa makini na kila wasemalo mataifa ya nje. Yaani tuache ku-copy na ku- paste kila kitu.

Na hii tutaifanya ikiwa tutakuwa na Intellejensia imara ili kuepusha madhara.

Kupitia Intellejensia Mhe. Rais alilenga kuwaambia Watanzania kuwa kama hatutakuwa na Intelejensia nzuri ni rahisi kuvurugwa na Propaganda za maadui

5) Wazushi na Wapotoshaji

Mhe. Rais, kwenye hotuba yake ameelezea na kukemea wale wote wanaozusha na kupotosha katika janga hili la Corona. Sio kila anayeanguka na kufa kwa Corona, sio kila anayekufa amekufa kwa corona. Uwepo wa Corona hauondoi magonjwa mengine.

Lengo la hoja hii ni kuzuia watu wanaozusha kutengeneza hofu na wasiwasi ndani ya jamii.

6) Viongozi wa Dini Bandia.

Mhe. Rais katika hotuba yake amewaambia watanzania kuwa wakati huu ndio muda muafaka ya kuwatambua viongozi wa dini bandia ambao jambo hili wamekuwa na imani haba. Pia ameonyesha msimamo wake kuwa bado anaamini katika maombi, na anaomba kuungwa mkono katika hilo na Watanzania wengine.

7) Suala la Kupokea Ushauri

Mhe. Rais kupitia Hotuba yake amejibu ile kashfa aliyopewa na baadhi ya wakosoaji wake kuwa "hashauriki". Kupitia maneno yake kuwa ataongea na kushauriwa na Wataalamu wa masuala ya kiafya. Pia katikia kumsifia Katibu, ni dhahiri kuwa kile alichokuwa anakisema hasa kuhusu vipimo vya Sampo bandia inaonekana ni ushauri wa Katibu aliyekuwa akimtaja mara kwa mara huku akimpa sifa.

Hii inatoa maana moja kuwa, Mhe. Rais ni kiongozi anayeshaurika lakini sio kila mtu anaweza kupokea ushauri wake. Hii ni kwa mtu yoyote.

8) Afrika inaweza, ijiamini.

Mhe. Rais pia ameweza kueleza pia suala la Waafrika wakiwemo Watanzani kuwa tuamini kuwa "tunaweza" Mara kwa mara Mhe. Rais amelieleza jambo hili kila apatapo nafasi ya kuhutubia. Amewaomba Watanzania waamini katika tiba zao za asili ikiwamo kujifukiza(hotuba iliyopita aliyokaa na vyombo vya ulinzi na usalama). Pia katika kuthibitisha hilo, amewaambia wananchi kuwa ataagiza Dawa iliyokwisha kutangazwa huko Madagasca.

9) Kukumbusha Tahadhari.

Pia hotuba yake mara kwa mara amekuwa akikumbusha watu kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona.

Baada ya kuona sehemu ya mambo machache aliyoyaeleza Mhe. Rais katika Hotuba yake.

Mapungufu machache katika Hotuba ya Magufuli.

1. Sio kila Mpinzani anayekosoa anatumiwa na Mabeberu.

Mhe Rais, hotuba yake mwishoni mwishoni ameeleza kuhusu wapinzani waliotoa tamko la kutohudhuria vikao vya Bunge. na kutoa amri kuwa wasipewe posho, sijajua ipo kisheria au haipo kuwa mbunge asipohudhuria kikao kimoja asipewe posho au ni tamko la Mhe. Rais la kihisia. Lakini pia sio kila mpinzani anayekosoa serikali anatumiwa na Mabeberu.

b) Kuchanganya kisa cha Yona na Daniel

Mhe. Rais katika hotuba yake ameonyesha udhaifu katika kutoa mfano wa kisa cha biblia kwa kukichanganya. Hii inatoa tafsiri mbili, mosi huenda Mhe Rais amesahau Biblia, pili, hajui biblia.

Hii inaweza tumiwa na wapinzani wake kama kete ya kumsimanga mitandaoni au kwenye majukwaa mbalimbali.

Hata hivyo hakuna mwanadamua aliyekamilika kwa kila kitu.

Mwisho: Nimpongeze Mhe. Rais katika Hotuba yake ambayo kwa sehemu kubwa imetoa faraja, imeondoa hofu, imewatia moyo, imeonyesha uwajibikaji na namna serikali inavyojali wananchi wake licha ya changamoto za hapa na pale.

Watu tuendelee kuchukua tahadhari.

Binafsi tangu jana sipo poah kutokana na dalili kadhaa za homa, nimetumia tiba za jadi huku nikiendelea kujihadhari na wale wanaohusiana nami. Kikawaida sio muoga, ninakabiliana na jambo lolote bila kujali ukubwa wake kwa Maana Mungu Taikon ananguvu.

Robert Heriel

Taikon wa Fasihi

Kwa sasa Morogoro, Tanzania.

0693322300 Ipo pia whatsapp

0711345431

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Komaa kusifu na kuabudu utaonwa pengine utaangukiwa na kautezi..

Ogopa sana mtu anaeweka Kajina na Kanamba ka Simu.. Mwigulu Kawarudisha kwa kasi ya Kimbunga
 
..bwana mkubwa hakufuata ushauri wa wataalamu wa jinsi ya kukohoa bila kuwaathiri walio karibu naye.

..vilevile mpambe alitakiwa asimkaribie sana bwana mkubwa ili kuepuka kuambukizana magonjwa ktk kipindi hiki.
 
Hili swala lilikua la KCMC BUGANDO,ST.JOSEPH na Muhimbili ..lakini kwa lililojitokeza la mapapai SUA lazima waingilie kati
 
Ulikuwa ushaandaliwa tayari in advance
Tumbafu kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom