Uchambuzi wa hali ya deni la Taifa, Tanzania na nchi nyingine Duniani

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Anaandika Moses Machali!
Mbunge wa zamani Kasulu Mjini

Nimeona watu mbalimbali kama wakistuka baada ya kusikia kwamba deni ya Taifa limeongezeka kwa Asilimia 17 kutoka Dolla za Kimarekani Bilioni 22 za Juni 2016 hadi Dola Bilioni 26 Juni 2017. Watu wanaenda mbali na kusema kwamba serikali inatupoteza. Watu na hasa wanasiasa wenzangu wanatia hofu wananchi kwamba tutafika mahala pabaya na tusiweze kukopesheka, nk. Ukweli ni kwamba deni la taifa letu ukilinganisha na nchi nyingine bado linahimilika sana tu.

Ifuatayo ni orodha ya MADENI kwa nchi mbalimbali duniani kama wanavyoeleza CIA ktika WORLD FACT BOOK na IMF. Kwa nchi za AFRICA MASHARIKI ( EAC), hali ni kama ifuatavyo yaani kiwango cha asilimia ya deni taifa kwa kila nchi (COUNTRIES PUBLIC NET DEBT AS % OF GDP):
Tanzania 36.6%
Kenya 50.4 %
Uganda 35.4 %
Rwanda 36.6%
Burundi 43.4%
Hiyo ndiyo hali ya deni la taifa kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI kwa mwaka 2016. Kenya na Burundi zinadaiwa zaidi ya Tanzania huku Rwanda ikilingana na Tanzania kiasilimia. Uganda ndiyo yenye tofauti ndogo sana ikilinganishwa na Tanzania ambapo Uganda ina deni la 35.4%.

HALI YA DENI LA TAIFA KATIKA NCHI NYINGINE DUNIANI
Uingereza 92.2%
USA Marekani 73.8%
United Arab Emirates 60.3%
Ureno 126.2%
Ugiriki 181.6%
Italia 132.5%
Eritrea 119.6%
Misri (Egypt) 92.6%
China 20.1%
Ubeligiji 106.7%
Autria 85.8%
Msumbiji 100.3%
Lebanon 132.5%
JAPAN 234.7%
Jamaica 130.1%
South Africa 43.3%
Nigeria 13.2%
Moroco 77.0%
Zambia 57.2%
Nk

HITIMISHO
Nchi kukopa siyo dhambi kama inavyoaminishwa na kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa hapa kwetu ambao huwatia hofu wananchi kwamba nchi imeuzwa. Ukiangalia mifano ya viwango vya madeni ya nchi mbalimbali duniani hapo juu kiasilimia unaona kabisaa TANZANIA hatudaiwi asilimia kubwa sana unapolinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zinadaiwa zaidi ya 100% hadi 234.7%. Sisi bado tuna 36.6% sawasawa na Rwanda hadi ilivyofika mwaka 2016. Tujiulize, maswali kadhaa: kama Marekani yenye Uchumi mkubwa wa zaidi ya DOLA TRILIONI 14 anakopa na kudaiwa deni la asilimia 73.8, je, sisi Tanzania ni nani hadi tuache kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu? Japan anadaiwa kwa asilimia 234.7, je, sisi watanzania ni akina nani? Nchi za Uingereza wanadaiwa kwa asilimia 92.2 ya pato lao la taifa. Sisi ni akina nani. Mtanzania mwenzangu shituka na jihadhari na upotoshwaji unaofanywa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kwa namna yoyote hata kwa kukupotosha ilimradi wakudanganye na kisha uwaunge mkono. Hata wao wakiingia madrakani lazima watakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini. Hakuna mtu au chama kinachoweza kuingia madrakani kisha kikaendesha nchi na serikali bila kukopa;haiwezekani. Jambo la msingi ni kwamba serikali inakopa kwa ajili ya nini? Hapa kwetu tunaona serikali inakopa kwa ajili ya kujenga Barabara, Reli, na Kwa ajili ya sekta za huduma kama afya, maji, Elimu, nk. Hakuna dhambi kukopa tusidanganayane.

09th November, 2017
 
Uchambuzi mzuri, kumbe mbinu ya kuendelea fasta ni kukopa... Ukizichanga sana inachukua muda kuendelea...
Nawatamani sana wachina namna walivyoendelea pasina deni kubwa....

Japan inaishi kwa mkopo ingawa kiuchumi wametuzidi...
 
Tarehe ya leo ni 9/11/2017,kwanini data zitumike za mwaka 2016? Je,tukubaliane na wanaotuaminisha kuwa deni la taifa linakuwa kwa kasi ya ajabu kama hivyo ndivyo ilivyokuwa mwaka 2016? Machali ana kazi ya kufanya tena.
 
Pia atueleze,refunding policies au terms za wenye madeni makubwa zikoje? Unaweza kukopa 100% ya GDP kwa interest rate ya 5% na wingine akakopa akakopa 40% ya GDP kwa interest rate ya 50%. Kwa vyovyote hao wawili hawatalingana katika kuleta maendeleo ya nchi zao.
 
Anaandika Moses Machali!
Mbunge wa zamani Kasulu Mjini

Ifuatayo ni orodha ya MADENI kwa nchi mbalimbali duniani kama wanavyoeleza CIA ktika WORLD FACT BOOK na IMF. Kwa nchi za AFRICA MASHARIKI ( EAC), hali ni kama ifuatavyo yaani kiwango cha asilimia ya deni taifa kwa kila nchi (COUNTRIES PUBLIC NET DEBT AS % OF GDP):
Tanzania 36.6%
Kenya 50.4 %
Uganda 35.4 %
Rwanda 36.6%
Burundi 43.4%
Hiyo ndiyo hali ya deni la taifa kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI kwa mwaka 2016. Kenya na Burundi zinadaiwa zaidi ya Tanzania huku Rwanda ikilingana na Tanzania kiasilimia. Uganda ndiyo yenye tofauti ndogo sana ikilinganishwa na Tanzania ambapo Uganda ina deni la 35.4%.

09th November, 2017

Ni shida sana kwa wachambuzi hawa wapya wa Uchumi, au labda ndio wako kwenye pilika pilika za kutaka waonekane ni watetezi wazuri wa Serikali na faida watakayopata ni kupewa vyeo

Ni ajabu kabisa kwa mtu kuokota data mitandaoni na kuzibandika bila kufanya analysis ya aina yoyote na mwisho anakuja kufanya conclusion za ajabuajabu

Data alizozitoa zinasema ni NET DEBT AS % OF GDP, shida sasa hajatuambia GDP za kila nchi zikoje, lakini mwisho wa siku anakwambia Uganda ndio ina ndogo ikifuatiwa na Tanzania, kisha Kenya ndio ina Deni kubwa sana,

Machali tumekusikia na wamekusikia, sijui kama alimkopy Polepole
 
Ongera kwa thread yenye mantiki. Yaani siku hizi thread moja inajibu threads zaidi ya 20 zinazozungumzia mada hiyo kwa kelele tupu na propaganda.
Serikali inajitahidi kukopa kwa umakini. Rejea Mh Rais alivyokataa mkopo wa China wa SGR kwa sababu ya riba yake. Na kwa mikopo wanayochukua inasimamiwa vyema kwenye miradi inavyoonekana, siyo miradi ya kifisadi kama ilivyowahi kuwa kabla.
 
USA ina madeni lakin na yenyewe kuna nchi inazidai ikiwemo Tanzania. Asilinganishe Tz na USA sisi tunadaiwa tu labda kidogo tunawadai Barrick USD 300
 
Hizo ndivyo analysis za kisomi zinavyopaswa kuwa, siyo kama zile za akina Zitto. Bravo Machali!!! Huko UKAWA ulikokuwa hapakuwa size yako.
 
Kwani nani kasema kukopa ni dhambi? Tunachotaka waache kusingizia kwamba hawalipi haki za wafanyakazi wala kupandisha mshahara wala kutoa 50M walizoahidi kwa vijiji eti kwa sababu miradi wanaiendesha kwa fedha za ndani. Pia watueleze kama wanakopa 10T ndani ya mwaka ambao bajeti ya maendeleo imetekelezwa kwa less than 50 percent, hizo kodi za zaidi ya 1T kila mwezi walikuwa wanazifanyia nini.
 
Anaandika Moses Machali!
Mbunge wa zamani Kasulu Mjini

Nimeona watu mbalimbali kama wakistuka baada ya kusikia kwamba deni ya Taifa limeongezeka kwa Asilimia 17 kutoka Dolla za Kimarekani Bilioni 22 za Juni 2016 hadi Dola Bilioni 26 Juni 2017. Watu wanaenda mbali na kusema kwamba serikali inatupoteza. Watu na hasa wanasiasa wenzangu wanatia hofu wananchi kwamba tutafika mahala pabaya na tusiweze kukopesheka, nk. Ukweli ni kwamba deni la taifa letu ukilinganisha na nchi nyingine bado linahimilika sana tu.

Ifuatayo ni orodha ya MADENI kwa nchi mbalimbali duniani kama wanavyoeleza CIA ktika WORLD FACT BOOK na IMF. Kwa nchi za AFRICA MASHARIKI ( EAC), hali ni kama ifuatavyo yaani kiwango cha asilimia ya deni taifa kwa kila nchi (COUNTRIES PUBLIC NET DEBT AS % OF GDP):
Tanzania 36.6%
Kenya 50.4 %
Uganda 35.4 %
Rwanda 36.6%
Burundi 43.4%
Hiyo ndiyo hali ya deni la taifa kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI kwa mwaka 2016. Kenya na Burundi zinadaiwa zaidi ya Tanzania huku Rwanda ikilingana na Tanzania kiasilimia. Uganda ndiyo yenye tofauti ndogo sana ikilinganishwa na Tanzania ambapo Uganda ina deni la 35.4%.

HALI YA DENI LA TAIFA KATIKA NCHI NYINGINE DUNIANI
Uingereza 92.2%
USA Marekani 73.8%
United Arab Emirates 60.3%
Ureno 126.2%
Ugiriki 181.6%
Italia 132.5%
Eritrea 119.6%
Misri (Egypt) 92.6%
China 20.1%
Ubeligiji 106.7%
Autria 85.8%
Msumbiji 100.3%
Lebanon 132.5%
JAPAN 234.7%
Jamaica 130.1%
South Africa 43.3%
Nigeria 13.2%
Moroco 77.0%
Zambia 57.2%
Nk

HITIMISHO
Nchi kukopa siyo dhambi kama inavyoaminishwa na kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa hapa kwetu ambao huwatia hofu wananchi kwamba nchi imeuzwa. Ukiangalia mifano ya viwango vya madeni ya nchi mbalimbali duniani hapo juu kiasilimia unaona kabisaa TANZANIA hatudaiwi asilimia kubwa sana unapolinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zinadaiwa zaidi ya 100% hadi 234.7%. Sisi bado tuna 36.6% sawasawa na Rwanda hadi ilivyofika mwaka 2016. Tujiulize, maswali kadhaa: kama Marekani yenye Uchumi mkubwa wa zaidi ya DOLA TRILIONI 14 anakopa na kudaiwa deni la asilimia 73.8, je, sisi Tanzania ni nani hadi tuache kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu? Japan anadaiwa kwa asilimia 234.7, je, sisi watanzania ni akina nani? Nchi za Uingereza wanadaiwa kwa asilimia 92.2 ya pato lao la taifa. Sisi ni akina nani. Mtanzania mwenzangu shituka na jihadhari na upotoshwaji unaofanywa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kwa namna yoyote hata kwa kukupotosha ilimradi wakudanganye na kisha uwaunge mkono. Hata wao wakiingia madrakani lazima watakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini. Hakuna mtu au chama kinachoweza kuingia madrakani kisha kikaendesha nchi na serikali bila kukopa;haiwezekani. Jambo la msingi ni kwamba serikali inakopa kwa ajili ya nini? Hapa kwetu tunaona serikali inakopa kwa ajili ya kujenga Barabara, Reli, na Kwa ajili ya sekta za huduma kama afya, maji, Elimu, nk. Hakuna dhambi kukopa tusidanganayane.

09th November, 2017
Mkuu tunaomba sources ya data/taarifa hii ili tujiridishe wenyewe, maana nahisi umefikiri kuwa huenda unaongea na watoto wako
 
Nikikopa nyingi kwa riba ndoooogo kisha nikawakopesha nyie vinchi kamaTanzania kwa riba kubwa nani mjanja? Kwa maana nyingine nakuwa kama Saccos, naenda benki nakopa, kisha nakopesha watu, sasa hata nikionekana nadaiwa kingi lakini si na mie nadai kingi. Na wakirudisha ninaowadai nami nitapunguza au kumaliza deni na hata kuwa na wengine bado nawadai. Je Tanzania tunamdai nani tofauti na Barricks?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom