Uchambuzi Wa Habari: Madaktari Waangusha Mbuyu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchambuzi Wa Habari: Madaktari Waangusha Mbuyu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 11, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Ijumaa ya jana, tena asubuhi na mapema, nilisoma kichwa hicho cha habari kwenye gazeti la Mwananchi la mtandaoni . Kinavutia. Kinaacha tafsiri nyingi.

  Habari hiyo ilitokana na mkutano Waziri Mkuu Mizengo Pinda na madaktari waliogoma. Mkutano ambao ulimalizika kwa kupatikana suluhu ya mgogoro, na hivyo basi, madaktari kumaliza mgomo wao.

  Naam, ni heri hekima inayokuja kwa kuchelewa kuliko inayokosekana kabisa. Watanzania tunashukuru kwa Serikali na madaktari kutanguliza hekima na kufikia suluhu ya mgogoro.

  Na hekima kubwa hapa ni kwa Serikali kutambua hekima za madaktari wetu kuwa hekima iliyohitajika ni kwa Serikali kuwasaidia madaktari katika kuuangusha mbuyu; Blandina Nyoni. Katika hilo tunawapongeza kwanza madaktari wetu kwa kuonyesha uzalendo mkubwa wa kuwa tayari kupambana hadi risasi ya mwisho na hatimaye kufanikiwa kuukata mbuyu ambao sasa ndio tunajua, kuwa ulikuwa mzizi wa mgogoro uliosababisha mgomo wa madakati na kuleta madhara makubwa.

  Maana, ni heri kutibiwa na daktari aliyemaliza mgomo na kurudi kazini na moyo mkunjufu kuliko kutibiwa na daktari aliyelazimishwa kwa nguvu kurudi kazini huku akiwa bado na kinyongo.

  Na Waziri Mkuu Pinda aliweka wazi sababu kuu tatu za Serikali kuwasimamisha kazi vigogo wawili wa Wizara ya afya Na Ustawi wa Jamii; Katibu Mkuu, Blandina Nyon na Mganga Mkuu wa Serikali, Dr. Mtasiwa.

  Kwanza; ni kwa tuhuma za kuingiza nchini robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini.

  Pili; tuhuma za kuanzisha kampuni ya kusambaza nguo kwa madaktari.

  Tatu; kuiingiza kinyemela kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbil.

  Na Waziri Mkuu Pinda alisema mwenyewe, kuwa tuhuma hizo ni nzito zinazoidhalilisha Serikali na kamwe haitakuwa busara kuzifumbia macho huku Serikali ikiendelea kudhalilika. Pinda anasema;

  "Nimeamua kuwasimamisha kazi Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali, ili kuweza kupisha uchunguzi , maana hizi tuhuma zinafedhehesha taifa."

  Aliongeza; "Kwa upande wa Waziri na Naibu Waziri wa Afya, nimeshapeleka ushauri kwa Rais kutokana na yeye kuwa mwenye dhamana, siwezi kuliongelea hili hapa ila yule aliyewateua, atafanya maamuzi, najua kitakachofuata mnakijua," alisema Pinda huku madaktari wakilipuka kwa shangwe na kuimba nyimbo ya mshikamano. ( Mwananchi, Februari 10, 2012)

  Na hapa nachukua fursa hii kumpongeza kwa ujasiri wake wa kuyatamka aliyoyatamka, na pia nampa Waziri Mkuu wangu Mizengo Pinda nyongeza ya sababu za wahusika kuchukuliwa hatua kali zaidi.

  - Wahusika wamesababisha madhara makubwa kwa jamii ikiwamo vifo vya wagonjwa vilivyotokana na mgomo ambao wao , kama wangewajibika ipasavyo, walikuwa na uwezo wa kuzuia usitokee.
  -
  Wahusika wamewadhalilisha madaktari wetu na taaluma yao kwa ujumla.

  - Wahusika kwa kuingiza nchini vifaa bandia ( feki) vya kupimia UKIMWI ni uhalifu mkubwa usiohitaji kuundiwa Tume bali kufunguliwa jarada la uchunguzi kwenye ofisi ya Upepelezi yenye kuhisika na uhalifu wa aina hiyo.

  Matumaini yetu kwa siku chache zijazo?
  Waziri mwenye dhamana na Naibu wake nao wakae pembeni maana tumewapa dhamana ya kuisimamia Wizara husika na wameshindwa kulisimamia hili la mgomo wa madaktari na hatimaye kutufikisha hapa tulipo. Wakikaa pembeni, kwa hiyari yao, au kwa kuombwa na Rais aliye na dhamana kuu, basi, watasaidia kurudisha imani yetu wananchi kwa Serikali. Watachangia pia kurudisha heshima ya Serikali na nchi.

  Je, kwenye pori la mibuyu, yote imeangushwa?
  Hapana, mibuyu iko mingi. Madaktari wetu wameangusha mbuyu mmoja tu. Na si kwa ' shoka moja'. Mashoka yalikuwa mengi yakiwamo ya wanaharakati. Na jamii ikipiga sana kelele mibaya huanza kutingishika. Mibuyu haiangushwi bila kelele za wengi. Ni kama paka aliyeopoa kipande cha nyama chunguni. Ukimwandama sana atakitema. Na ikumbukwe, mibuyu porini inaanza kama mipapai.

  Je, tunafanyaje basi kuitambua mibuyu inapokuwa katika hatua kama ya mipapai na hivyo tukaing'olea mbali?

  Katiba, Katiba, Katiba…Ni kwenye Katiba Mpya inayokuja. Katiba iweke kipengelea kinachohakikisha , kuwa pale unapoonekana mbuyu, basi, kazi ya kuuangusha isihitaji mashoka mengi na hata kuchukua roho za watu. Inawezekana.

  Maggid Mjengwa,
  Iringa
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,614
  Trophy Points: 280
  Mbuyu baada ya kuanguka tunauchoma moto!! Maana kuuangusha haitoshi!!
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Hapa namkumbuka Philemon Luhanjo alivyotuachia manyoya na kupewa marupurupu yake yote ya ustaafu
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kufanya operesheni ya kichwa badala ya mguu!!!!
   
 5. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Maggid,

  Ukiwa ujanywa ulanzi unakuwa na busara sana...
   
 6. m

  maggid Verified User

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Rufiji,
  Asante sana, nawe unakaribishwa Iringa kunywa ulanzi!
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Bado mbuyu mkuu, baba mwanaasha. Naye amechangia mgomo wiki mbili watu wanakufa, waziri mkuu kalikoroga baada ya kutishia nyau madaktari, yeye baba Mwanaasha kakaa kimya, nae ni mbuyu, tunaandaa mashoka ya kuukata.
   
 8. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jamani tutenganishe utendaji wa kiserikali na kisiasa.

  Mgogoro umesababishwa na Blandina Nyoni na mshauri wake mkuu Dr Deo Mtasiwa. Waziri ni mtu anayeandikiwa hotuba na taarifa mbalimbali. Jamani tuwe wakweli tusipende tu kukurupuka rumuonee hurunma Dt Haji Mponda na naibu wake Dr Nkya walikuwa wanafanya kazi na KM ambaye yuko corrupt vibaya sana na ambaye ungeshisi kama vile analindwa na mfumo wa usalama wa nchi.

  Ukizisoma tuhuma za Blandina unaona zimejaa ufisadi, ukabila na wizi wa moja kwa moja. Tuhuma hizi ziko muda mrefu lakini Dr Haji Mponda na naibu wake Nkya hawana tuhuma yeyote ya matumizi ya madaraka wala ufisadi. Maamuzi mengi ambayo yamewakwaza madaktari yamefanyika mwaka 2010 na 2011 na Blandina Nyoni aliyekuwapo hapo tangu 2008 na Dr Mtasiwa aliyekuwapo tangu 2006.

  Mtanzania yeyote angeweza kupatwa na situation iliyompata Dr Haji Mponda kwenye utendaji wa Nyoni.

  Naomba turejee hata kwenye utawLa wa Profesa Mwakyusa, mtakumbuka kuwa hata yeye alikuwa anafunikwa na huyu mama. Kwa mtazamo wangu mimi tatizo ni la mfumo wa utendaji wa serikali, kwa hiyo napendekeza tumpe muda Dr Haji Mponda
   
 9. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Kosa la kuingiza vifaa feki vya kupimia UKIMWI ni mauaji ya kimbari kama yale ya Rwanda na Bosnia. Madhara ya matumizi ya vifaa hivyo ni makubwa. Mtu utaambiwa unao UKIMWI kumbe hauna na hivyo unaweza kuathirika ki saikolojia maisha yako yote. Vile vile, unaweza kuambiwa hauna wakati unao na hivyo ukawaambukiza watu wengine. Hii ni kesi kubwa ambayo wahusika wanatakiwa wapelekwa The Hague mara moja kwavile mahakama ya Arusha karibu inasitisha huduma zake!
   
 10. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180


  Umesahau kuwa akili ya kuambiwa lazima uchanganye na yako? Usiamini kila kitu jumla jumla tu, lazima utumie pia busara zako mwenyewe. Kwa hili, Waziri anawajibika pia na hana pa kutokea!
   
 11. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Masalia ya Luhanjo yaanza kupukutishwa!
   
 12. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Majanga haya yataendelea hadi hapo ombwe hili la uongozi litakapoondolewa
   
Loading...