Uchambuzi Wa Habari ; JK, Shivji, Museveni Na Wanahabari Wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchambuzi Wa Habari ; JK, Shivji, Museveni Na Wanahabari Wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Apr 1, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]Ndugu zangu, [/FONT]
  [FONT=&quot]
  Yamepita majuma kadhaa sasa bila kuwasilisha fikra zangu kupitia ’ Neno la Leo’, ’ Uchambuzi wa Habari’ au ’ Tafsiri Yangu’. [/FONT]


  [FONT=&quot]
  Kwa mwanadamu ni vema wakati mwingine kukaa chini; kusoma na kusikia ya wengine huku ukitafakari. [/FONT]


  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot] Katikati ya taarifa ya habari ya televisheni jana usiku nilianza kujiuliza; ” Hivi nchi hii hatuna televisheni nyingine ’ Ya Kitaifa zaidi’?” Mimi nilitarajia, kuwa katika siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi mdogo kule Arumeru tungeletewa habari moto moto kutoka huko, ikiwamo uchambuzi pia. Wapi?[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Niliposikia kuwa ’ Sasa tunawaletea habari za Afrika Mashariki’ nili-tune BBC News![/FONT]


  [FONT=&quot]
  Kwenye taarifa ile ya habari jana usiku nilimsikia Rais Jakaya Kikwete akizungumzia juu ya tasnia ya uandishi wa habari hapa nchini. Kati ya mambo mengine, JK aliweka wazi, kuwa ameambiwa kuwa waandishi wengi hawana ajira ya kudumu. [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwamba wanafanya kazi kwa kupokea posho tu- These journalists can easily become mercenaries- anasema JK. Kwamba waandishi wa aina hii wanaweza kiurahisi kugeuka mamluki.[/FONT]

  [FONT=&quot]
  JK akaonyesha hofu yake ya kufa kwa taaluma hii. Naam, JK yuko sahihi. Na alipokuwa akiyatamka hayo kuna makofi yaliyokuwa yakipigwa, japo si ya ukumbi mzima. Kuna ambao waliguswa na ukweli huo, si tu wanahabari, bali wamiliki wa vyombo vya habari.[/FONT]


  [FONT=&quot]
  Na ukweli huo wa hali ya wanahabari wetu unafahamika. Lakini, kama taifa, tunafanya nini wakati “ Fourth Estate”- mhimili wa nne wa dola unaundwa na vibarua wapokea posho za siku wakati Wabunge wanakamata laki tatu na zaidi kama posho ya siku kukaa bungeni?[/FONT]


  [FONT=&quot]
  Huko nyuma nimepata kuanzisha mjadala wa umuhimu wa kuwepo kwa ruzuku kwa vyombo vya habari ili navyo viweze kupata nguvu ya kuendesha shughuli zao ikiwamo hata uwezo wa kuwasafirisha wanahabari wao kwenye matukio badala ya gharama hizo za usafiri kutegemea ‘ bahasha’ za wanasiasa na wamiliki wa makampuni ya biashara, ambao , masharti yasiyoandikwa ya wao kutoa bahasha zao, ni namna wanahabari hao watakavyoripoti habari za kuwapamba na zitakazowafurahisha watoa bahasha.

  Vinginevyo, kwa mwandishi asiyejua kumpamba mtoa bahasha, na badala yake akamchafua, ana hatari ya kushushwa njiani, hata kama ni katikati ya pori la mbuga ya wanyama ya Mikumi. Maana yake? Akome ubishi! [/FONT]
  [FONT=&quot]Si tuliambiwa shuleni , kuwa ubepari ni unyama, ongeza sasa, na ufisadi pia. [/FONT]

  [FONT=&quot]
  Naam, wanahabari unganeni. Huu si wakati wa kulilia huruma za watawala ikiwamo wanasiasa. Huu ni wakati wa kupambana kudai ruzuku ya Serikali kwa vyombo vya habari. Ni ruzuku, pamoja na mauzo ( kama ni magazeti) na matangazo ndivyo vitakavyowafanya muwe huru. Vinginevyo, mtaendelea kuachana na jukumu la kuutumikia umma wa Tanzania na badala yake mtabaki kuwatumikia wanasiasa, wafanyabiashara na makampuni makubwa.

  Yumkini, kwa mwanahabari kumtumikia kafiri yaweza kuwa na maana ya kuwaangamiza ndugu zake kwa mamilioni. Na kwa maana ya JK, mwanahabari wa aina hii atakuwa amegeuka mamluki- [/FONT]
  mercenary.

  [FONT=&quot]
  Katika kitabu chake, " The Intellectuals At The Hill" ( Wasomi wa Mlimani); Profesa Issa Shivji alipata kuandika yafuatayo juu ya uandishi wa habari; " Uandishi wa habari huenda usifikiriwe kuwa ni taaluma adimu. [/FONT]
  [FONT=&quot]Na pengine usipewe kipaumbele katika kamati za mipango. Lakini bado, mwanahabari, kama mwasilisha wa taarifa, aweza pia akawa mwangamizaji katika jamii ya kidemokrasia. ( Au, waweza wakawa wasaidizi wa tawala za kidikteta kama wawasilishi wa taarifa potofu.) [/FONT]

  [FONT=&quot]
  Lakini katika nchi zetu demokrasia ni suala la kuhubiri zaidi kuliko vitendo wakati wanahabari si kitu chochote zaidi ya kuwa maofisa uhusiano kwa "kigogo" huyu au yule. Ni nadra kwa yeyote yule ( wakiwemo wanahabari wenyewe ) wenye kuchukulia kazi ya uanahabari kwa umakini, achilia mbali kwa uwajibikaji." Prof. Issa Shivji ( The Intellectuals at the hill, Uk 176) (Tafsiri hiyo ni yangu) [/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]
  Na [/FONT]
  [FONT=&quot]kuna wakati Rais Yoweri Museveni alipata kuulizwa; " Mheshimiwa Rais unapoamka asubuhi unafanya nini kabla ya kwenda ofisini? Museveni alijibu;" Mimi huanza siku kwa kufungulia taarifa ya habari ya BBC London!".[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Hata kama ni jibu la kusikitisha, lakini, namwelewa kabisa Yoweri Kaguta Museveni.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  Maggid Mjengwa,
  Iringa
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mjengwa, ni mtazamo sahihi kudai hali bora za ufanyakazi wa waandishi wa habari.
  Lakini ruzuku itawanufaishaje waandishi?

  Na kwa nini wamiliki wa vyombo vya habari wapewe ruzuku ?

  Uzoefu katika nchi nyingine ukoje? Je ni kweli waandishi wote wanakuwa na ajira za kudumu? Au, tunapoongelea ajira za kudumu tuna maana ya hali bora za ufanya kazi? Vyombo vya kimataifa vina correspondents, stringers je, ajira yao ikoje?

  Uzoefu unaonyesha kuwa media house kuwa na permanent staff peke yake bila vibarua ni jambo gumu kutokana na nature ya kazi yenyewe, ambapo unaweza kupata huduma za mwandishi wa chombo kingine

  mahali pengine kwa mkataba maalum kama correspondent lakini kwa malipo mazuri ambayo hayawezi kumfanya awe mamluki.

  Wakati natambua umuhimu wa kuboresha hali za utumishi wa waandishi wetu, ni vema pia tukaangalia hili litawezekanej.
   
 3. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Zaidi ya hayo mkuu Mjengwa, utumishi katika tasnia yetu hiyo unagubikwa sana na matatizo ya vigezo vya elimu. Vijana wengi wa kidato cha nne na sita walioenda kozi fupi ndiyo waandishi wetu. Hawa hawako kwenye nafasi nzuri ya kudai maslahi bora kwa sababu wao wenyewe wanachukulia ofisi kama kijiwe cha kuzuga. Wamiliki wanatumia hawa kama cheap labour tu wakijua udhaifu wao.

  Je, tunadhani kuweka standards za elimu kwenye sheria ijayo kutaweka daraja zuri kwa kada hii kuwa na watu qualified ambao wanaweza kusimama kwa sauti moja kudai maslahi bora?
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hata mtaala wa kozi ya uandishi wa habari umezinduliwa juzijuzi tu
   
Loading...