Uchambuzi Wa Habari: Dr Mwakyembe Naye Amwaga Sumu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchambuzi Wa Habari: Dr Mwakyembe Naye Amwaga Sumu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 19, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Kwenye vyombo vya habari kumekuwa na taarifa zinazochanganya juu ya kinachomsibu Dk. Mwakyembe.

  Na kama utangulizi ufuatao nitauzungumza kama hotuba fupi mbele ya watu wanaojiandaa kwa mlo wa kusheherekea harusi, basi, nina imani, zaidi ya nusu ya wageni waalikwa watainuka kwenye meza zao na kukiacha chakula.

  Maana nitaanza kwa kusema;

  Mabibi na Mabwana,

  Wakati tukijiandaa kwa mlo ulio mbele yenu ningependa kuwaeleza mafupi juu ya sumu na jinsi sumu inavyoweza kuingia kwenye mwili wako na hatimaye kukudhuru. Na bila shaka wote mnajua kuwa sumu inaua.

  Ni hivi; unaweza kuwekewa sumu. Usipoiona na ukaiacha, basi, utakuwa umepona. Ndio, kama kuna sumu imewekwa usiichukue. Kwa mantiki hiyo hiyo, jiadhari, unaweza ukashikishwa sumu. Kuwa makini na wanaokupa mikono ya heri, mingine ni mikono ya kifo. Yumkini anayekupa mkono amevaa glovu yenye sumu.

  Ndugu yangu, unaweza pia ukagusishwa sumu. Kuwa makini na unayecheza nae muziki baada ya mlo huu. Kumbatio la muziki tulivu laweza kugeuka kuwa ni kumbatio la kifo.

  Sumu inaweza pia kukuingia mwilini kwa kulishwa. Uwe makini na anayekulisha kipande cha keki ya harusi. Na kama waweza kulishwa sumu hivyo hivyo waweza ' kujilisha' mwenyewe sumu. Chunga sana na anayekupa kipande cha nyama choma. Ukakipokea na hatimaye kukitia mdomoni.

  Kama ilivyo kwa kulishwa na kujilisha sumu. Yawezekana pia sumu ikaingia mwilini mwako kwa kunyweshwa au kujinywisha. Chunga sana na unayekaa karibu naye. Jichunge mwenyewe pia. Ukinywa vodka nyingi ni sawa na ' kujinywisha' mwenyewe sumu.

  Sumu yaweza pia kukuingia mwilini kwa kumwagiwa. Kaa mbali sana na atakayefungua champeini isije kilichomo kikawa ni sumu. Na wengine hamfahamu, kuwa sumu yaweza pia kukuingia kwa kupuliziwa. Sahani yako ya chakula yaweza kuwa imepuliziwa sumu…


  Ndugu zangu,

  kuna njia nyingi sana za sumu kuingia mwilini mwako. Nisiwachoshe, tuendelee na mlo wetu wa harusi!

  Naam. Habari kubwa katika siku mbili hizi ni kadhia ya Dr. Mwakyembe na madai ya sumu kuingizwa mwilini mwake na wabaya wake. Na kama mlivyoona hapo juu, bado haijawa wazi kama Mwakyembe kalishwa, kawekewa, kanyweshwa au kagusishwa sumu.
  Jitihada za Jeshi la Polisi juzi kutaka kutuambia WaTanzania ukweli juu ya kadhia hii zinaonekana kugonga mwamba kwa kupingwa vikali na Mwakyembe mwenyewe. Tumesoma kwenye magazeti ya leo.


  Nani anaongopa?

  Bila shaka, habari hii imekuwa ikiwavutia wengi kwa vile kiu ya jamii ni kutaka kujua ukweli mzima. Jamii inataka kujua; nani anasema kweli na nani anaongopa. Vita inayopiganwa sasa imebaki kuwa ni vita ya maneno kwenye vyombo vya habari.

  Kila upande unadai una ushahidi na unachosema lakini ushahidi huo hauwekwi hadharani ukaonekana. Wanahabari nao wameonekana kusukumwa zaidi na upepo wa vita na kuandika yale ambayo wanadhani yatauza magazeti. Kimsingi media inaweza ikamaliza vita hii kwa kuwauliza wahusika maswali sahihi na magumu yatakayotokana na maelezo wanayotoa wahusika

  Mfano, DCI Manumba anasema; " Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu , tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe."- ( Mwananchi, Jumamosi, Februari 18, 2012)

  Naam, kama DCI Manumba anadai wamethibitishiwa na Wizara ya Afya iliyofanya mawasiliano na hospitali anayotibiwa Dr . Mwayembe nchini India kwamba Dr Mwakyembe hakukutwa na sumu mwilini ni kwanini wanahabari wasifike Wizara ya Afya kuthibitishiwa juu ya kile ambacho Manumba anadai kuthibitishiwa. Maana, haiyumkini kuthibitishiwa huku kukawa ni kwa mdomo tu.

  Na Dk. Mwakyembe anaposema; " Ripoti inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow ( ndani ya ute wa mifupa) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua." ( Mwananchi, Februari 19, 2012.)

  Kwa wanahabari kazi hapa ingekuwa kumbana Mwakyembe awasaidie kupata maelezo ya ziada kutoka kwa mabingwa hao wa India ili iwasaidie ku-establish, bila mashaka, juu ya dhana ya sumu katika kinachomsibu Mwakyembe.

  Vinginevyo, taarifa ya jana ya Dr Mwakyembe inatoa tafsiri pia ya mtu aliyejeruhiwa na aliyeamua 'kumwaga sumu' hadharani. Taarifa ile ya Mwakyembe imeonyesha jinsi watendaji wetu wakuu Serikalini na hata kwenye chama tawala wasivyoaminiana.

  Tumeona jinsi Mwakyembe alivyorusha makombora makali dhidi ya jeshi la polisi na kutoa tuhuma nzito ya jinsi jeshi hilo linavyotenda hujuma . Kwa mtu wa kawaida atajiuliza; kama Mwakyembe Waziri na kada wa CCM analia kuchezewa faulo, je, hali itakuwaje kwa mtu wa kawaida na kama ni mwanachama wa chama cha upinzani?

  Swali lingine; kama baadhi ya mawaziri wa JK kwenye baraza moja wanaonyesha hadharani kuwa hawaaminiani wanamsaidiaje Rais wa nchi? Na je, Mwakyembe au Sitta wakihamishimiwa wizara ya Mambo ya Ndani watafanyaje kazi na akina Manumba na Said Mwema? Na kuna wengi wanaomtarajia JK kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri kwa vile hawaridhishwi na utendaji wa Baraza lililopo.

  Na haya yote tunayoyashuhudia ni ' maradhi ya taifa' ya tangu uhuru kwa vile tumekuwa na Katiba yenye mapungufu makubwa na kwa sasa isiyokidhi mahitaji ya wakati uliopo. Tunamshukuru Rais wa nchi kwa kuonyesha dhamira ya kutuanzishia mchakato utakaopelekea kupata Katiba Mpya kwa Taifa la Kisasa.

  Katiba ya sasa inaruhusu ' ubaguzi wa kisiasa'. Inawatenga Watanzania wengine katika ushiriki wa uongozi na ujenzi wa nchi. Na dhambi ya ubaguzi ndio inayotutafuna sasa hadi tukafikia hata viongozi watendaji wa juu ndani ya chama tawala kukosa kuaminiana.
  Ndio, Watanzania walio wengi ' hawajalishwa sumu', isipokuwa, kwa miaka mingi Watanzania wamekuwa ' wakibwigizwa ugoro' uliowafanya wasinzie kama watu waliopigwa sindano ya ganzi.

  Wengi sasa , na hususan vijana, wanakataa mchana wa jua kali kubwigizwa ugoro na walio kwenye mamlaka. Wamebumbuluka. Wameanza kusoma katikati ya mistari. Ndio, wameamka na wana kiu ya kuiona Tanzania mpya na inayostawi.


  Maggid Mjengwa,
  Dar es Salaam.
  Jumapili, Februari 19, 2012
   
 2. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Uchambuzi mzuri,ntarudi baadae kuchangia hoja
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  JK alikwisha sema "uhasama uliomo CCM watu hawaachi kinywaji kwenye glass wanapokwenda kujisaidia..." Mwakwembe nadhani hakuwa makini zaidi, maana inawezekana hata glass aliyotumia ilipakwa sumu kabla, inaletwa ikiwa kavu kumbe kitu kilikwisha pakwa ndani ikimsubiri! Kwa vile imekwishatokea, atuambie watanzania alichoficha ili kulinda heshima ya walio mmaliza!
   
 4. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kaka Mjengwa! Nimesoma kwa makini kwa kweli sina la kuongeza ila ukweli mtupu kuwa sasa sumu imemwagwa hadharani mwenye macho na aone! Mwenye masikio na asikie na mwenye akili na achambue!....... Tutasikia mengi mwaka huu!.....
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  naita huu ni mwaka dume!
   
 6. data

  data JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,793
  Likes Received: 6,573
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo..!!??
   
 7. ha ha ha

  ha ha ha JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 641
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naunga mkono hoja.
   
 8. K

  Karata JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ahsante sana Mkuu Mjengwa kwa uchambuzi yakinifu usioegemea upande wowote. Lets wait and seen brother!
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenikumbusha hiyo kauli ya uhasama na kutoachiana glass.
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Tunataka umoja na mshikamano ndani ya CCM-M.R.Kawawa
  Hii kwa sasa ni ndoto
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  PHP:
  Kwa wanahabari kazi hapa ingekuwa  kumbana Mwakyembe  awasaidie  kupata maelezo ya ziada kutoka kwa  mabingwa hao wa India ili iwasaidie  ku-establishbila mashakajuu ya  dhana ya sumu katika kinachomsibu  Mwakyembe.
   
  Kuna ishu inatajwa juu ya kuchakachua ripoti ya uchunguzi ya madaktari wa Apollo juu ya ugonjwa wa Mwakyembe...Hii kitu mimi naona kuwa haiwezekani!
  Kwani kule India hakuna nakala ya kweli(orijino?)
   
 12. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  JK should immediately dismiss either Mwakyembe or Manumba or both for the sake of preventing public trust in the bureaucracy from melting even further as it is already in a very bad shape. Meanwahile, the government should seek help from the Israel intelligence to investigate into Mwakembe's matter since our security system is too incompetent to handle it perfectly.
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Duh tangu sakata la Dr Mwakyembe lianze nimekuwa mwoga kuliko kunguru jana nilikuwa Arusha City Park napata kinywaji ghafla nakajisikia haja ndogo nikaenda msalani niliporejea nikamuita mhudumu nikamwagiza aniletee kinywaji kingine na glass nyingine kinywaji cha zamani nikakimwaga na glass nikaitosa mazima alah wacha mchezo na maisha bwana Tanzania si salama tena nchi imeharibika.
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kazi na Dawa:
  Aisee saa ngapi ulikuwa pale?
  Kama mida saa 2 usiku mlikuwa jirani ya meza yetu!
  Shida yako NGONGO UCHOYO tu!
   
 15. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  kwa kauli hiyo ambayo nimei-highlight hapo.. it shows kwamba bado wataalam hawajajua tatizo na wanaendelea kulifanyia kazi ili kujua.. na kama ni hivyo.. manumba hakuwa na sababu ya kuita waandishi wa habari na kutoa taarifa aliyotoa.. hili ni tatizo la kuwa na viongozi wanaofanya kazi kimazoea zaidi..
   
 16. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  a job true true
   
 17. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Saa 2 usiku nilikuwa nawatazama watani zangu Arsenal wanavyosulubiwa ha ha ha.

   
 18. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mwakyembe ipo very clear, wataalamu wanaendelea kutafiti sababu na hakuna confirmation kwamba kapewa sumu! Acheni chuki zisizo na maana,
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2012
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Maggid,

  Tanzania tunajenga taifa la wapiga majungu; wananchi tunafurahia na kuishi kwenye majungum labda kwasababu hatuna kazi nyingi za kufanya.

  Ukitaka majungu yastawi basi toa taarifa nusu nusu. Kweli hili ukiangalia kila angle unaona jinsi vyombo vya dola kama polisi vinavyotoa habari nususu; jinsi mheshimiwa Mwakyembe anavyotoa habari nusu nusu kuhusu kuumwa kwake. Magazeti nayo yamelala na waandishi wa habari wametumbukia kwenye tope hilo hilo la majungu. Hawawezi kufikiri nje ya box na kuamua kutafuta ukweli kwa faida ya wananchi wote. Badala yake wanavumisha majungu hayo ili yawafikie wananchi wengi zaidi na mduara wa majungu uendelee kupanuka.

  Hapa ndipo nchi ilipofikia, no wonder hatusogei mbele. Dawa pekee ya majungu ni ukweli mtupu. Kuna kitabu kinaitwa TRUTH HEALS, huyo mwandishi mwanamama anasema katika jambo lolote baya, ukitaka kuliponya, hatua ya kwanza ni kukumbatia ukweli. Sio ukweli nusu au robo tatu, au asilimia 99. Ni ukweli kwa asilimia 100.

  Kuna misemo mingine mbalimbali ambayo inahusiana na umuhimu wa kusema ukweli unapokuwa kwenye matatizo. kwa mfano if you're in a hole stop digging; maana yake toa ukweli wote ili kujiokoa. Bahati mbaya viongozi wetu na vyombo vyetu vya dola vinazidi kuchimbia matatizo kwa kushindwa kukumbatia ukweli.

  Huu mduara wa majungu na ushabiki wetu sisi wananchi hautatufikisha popote. Imefika wakati serikali iunde tume huru ya madaktari na vyombo vya sheria wakiwemo wawakilishi wa mheshimiwa Mwakyembe na kuchunguza hili jambo na kuuweka ukweli wote wazi. Wananchi tunataka ukweli, tunataka kujua kama kuna watu wabaya wanalisha wenzao sumu, pia tunataka kujua kama kuna watu wanapiga kelele za sumu wakati hakuna sumu. Ni ukweli tu utaweza kupunguza mduara wa majungu ambao sasa unazidi kuwa mkubwa.

  Ikifika mahali wananchi wanaamini zaidi majungu ya mitaani kuliko statements za viongozi, jua taifa liko njia panda. Tunahitaji Mwarobaini ili uturudishe kwenye ukweli.
   
 20. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #20
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hili sakata sijui litaishia wapi ... lakini kwa nini mwakyembe mwenyewe asianike kila kitu wazi kikaeleweka? why this dangerous cat and mouse game?
   
Loading...