Uchambuzi wa chaguzi za Kalenga 2005 na 2010 na kwanini CCM iwe makini

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
ukiangalia takwimu za uchaguzi mwaka 2005 na mwaka 2010 utaona kuwa ccm walikuwa wakipata upinzani hafifu na kama unaweza kuuita upinzani kabisa kwani mgombea wa ccm mwaka 2005 alikuwa Stephen Galinoma alipata kura 32000.

kihurahisi kabisa na mwaka 2010 william mgimwa alipata 31000 kwahiyo unaweza kuona nguvu ya ccm katika chaguzi hizi mbili. mgombea wa chadema mwaka 2010 bi rehema makonga alipata kura 3300 kuliganisha na mwenzake wa mwaka 2005 Bw.silvester mwitara aliyepata kura 912 kwahiyo unaweza kuona kuwa chadema ilikuwa ni kama haina chake katika kipindi chote hiki. chadema ilikuwa ikipata less than 10% ya kura za ccm ktk vipindi vyote hivi.

lakini kuna kitu kimejificha katika chaguzi zote hizi kwani kuna mtu mmoja mwaka 2005 akigombea kwa chama dhaifu cha jahazi asilia anaitwa Grace Tendega alipata kura za ajabu sana kwani aliweza kujizolea kura 13,500 huku anayemfuata nyuma akiwa na kura 900.

Kwahiyo unaweza kuona kwamba ccm ina kila sababu za kumuofia huyu mama kuliko hata chadema yenyewe kwani ni tishio na hasa ukizingatia mwaka 2005 hakuwa na resources na machinery zozote za kupambana na ccm. fast forward mwaka 2014 anagombea tena huku nyuma yake akiwa na jeshi kubwa la chadema lenye resources za kutosha na uwezo wa kujibu mashambulizi natoa tahadhari kwa ccm kuwa it won't be business as usual kuna haja ya kuchukua tahadhari zote.

Kama kuna mtu anafikiria ccm itaendelea kupata kura inazopata miaka yote nitashukuru kupata uchambuzi wake kwa kutumia namba na si maneno matupu.

chadema.jpg
 
Ccm ndio mama wa demokrasia kalenga, na tanzania. Itashinda ushindi wa radi

Kalenga wameapa kufa na ccm

Subirini kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa mgimwa

Nikusaidie tu bwana utaifa kwanza mtoa mada amesema

"kama kuna mtu anafikiria ccm itaendelea kupata kura inazopata miaka yote nitashukuru kupata uchambuzi wake kwa kutumia namba na si maneno matupu."

Katika hivyo vimistari vyako hapo juu ni kipi kati ha hivyo ni uchambuzi? Je ni vipi kati ya hivyo ni number? Nimekuwa nikikuambia mara kwa mara weka hoja na sio viroja kama hivyo unavyofanya hapo!
 
tena ukichukulia mgombea wa ccm ni raia wa uingereza lazima wajipange la sivyo wataangukia pua aisee!
 
Naona serikali ya CCM ilivyoboresha maisha ya Watanzania...ikiwezekana hata majimbo yaliyoshikiliwa na upinzani waitishe uchaguzi mwingine wayarudishe kwao ili kuendelea kuboresha zaidi maisha ya wananchi!
 
Ccm safari hii watapigwa misa ya kwanza maana timu iliyopo Kalenga si mchezo!
 
utaifakwanza jifunze kutoka kwa profesa muhongo yeye ni bingwa wa takwimu,sasa tupe takwimu mkuu kwa hicho unacho taka kutu aminisha ok
 
Back
Top Bottom