Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

Ndio hayo tunayasubiria Kwa kweli na bila kusahau 50000000 kila kijiji na barabara nzuri zikiwemo flyover
 
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amefungua pazia la kampeni za chama hicho kwenye Viwanja vya Jangwani katika tukio lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi, huku akieleza mambo 25 atakayoyafanya iwapo Watanzania watamchagua kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Huku akitumia maneno: "Mimi kazi tu", "Tanzania ya Magufuli ni ya viwanda", Dk Magufuli aliyetumia dakika 53 kueleza sera zake, kuanzia saa 11.40 hadi 12.33 jioni alisema Watanzania wanataka kitabu kipya cha mabadiliko na yeye na mgombea mwenza, Samia Suluhu ndiyo wanaoweza kuyaletea.

Mgombea huyo wa urais wa CCM aliahidi kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi, kumaliza tatizo la wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo, kuhakikisha mama lishe hawabughudhiwi, kusimamia haki za wasanii, kulinda Muungano na usalama wa nchi. Aliahidi kutoingilia utendaji kazi wa Bunge na Mahakama, kuheshimu mawazo ya vyama vingine vya siasa, kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama, wafanyabiashara wadogo na wakubwa wote kulipa kodi, kuendeleza kilimo, mifugo, uchimbaji wa madini, majisafi na elimu bora.

Nyingine ni kusimamia nishati ya gesi, ujenzi wa barabara, reli, kuboresha sekta ya utalii, kuimarisha uwekezaji, kuwasaidia walemavu na kusimamia uhuru wa habari.

Mkutano huo ulioanza rasmi saa 9.30 alasiri ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba na Salim Ahmed Salim.

Ahadi alizotoa

Mgombea huyo alitoa ahadi mbalimbali ikiwamo ajira akisema: "Ninataka Watanzania wapate ajira, kazi ya Serikali itakuwa kukusanya kodi tu. Viwanda vinaweza kutengeneza ajira kwa asilimia 40 hasa kwa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini."

Kuhusu ubinafsishaji, alisisitiza: "Kuna viwanda vilibinafsishwa sasa wahusika wasipoviendeleza wajiandae kuvirudisha haraka."

Mbali na kurejesha viwanda vilivyobinafsishwa, alisema akipewa ridhaa hiyo atahakikisha chini ya uongozi wake, anajenga viwanda vingi vipya, akiainisha vile mahsusi kwa shughuli za kilimo, mifugo, kusindika nyama na madini.

Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni kilimo na kwamba atahakikisha sekta hiyo ambayo ndiyo mhimili wa uchumi inaendelezwa.

"Tutaleta vitendea kazi, pembejeo na vifaa vingi vya kisasa na vya kutosha kwa wakulima… kama nilivyosema hapo awali, tutajenga viwanda kwa ajili ya wakulima pia.

Mbunge huyo wa zamani wa Chato alisema pia kipaumbele kingine katika Serikali yake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa mjini wanapata majisafi na salama kwa asilimia 95 na wananchi wa vijijini wanapata maji kwa asilimia 85.

Kuhusu afya alisema: "Tutahakikisha tunakuwa na vituo vya afya, zahanati na hospitali katika maeneo mbalimbali kwa sababu tunaamini maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana kama wananchi hawana afya bora."

Kipaumbele kingine ni mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu akisema watakuwa wanapata mikopo kwa wakati bila kuchelewa na kwamba watajikita pia katika kujenga hosteli kwa wanafunzi wa vyuo.

"Mishahara ya walimu na wafanyakazi wote tutaishughulikia. Hata madereva haki zao za msingi lazima ziangaliwe," alisema huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Mgombea huyo alisema anafahamu kero ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam na kwamba maendeleo ya kweli yatapatikana kama changamoto hiyo itafanyiwa kazi.

"Tutaunganisha mikoa yote kwa barabara zenye viwango vya lami na pia tutajenga barabara za juu saba jijini hapa," alisema Magufuli.

Alisema akipewa ridhaa hiyo itashughulikia suala la reli kwa kujenga reli ya kisasa kwa viwango vya Standard Gauge" na kuboresha bandari na usafiri wa anga.

Kuhusu maliasili, alisema ni kipaumbele katika Serikali yake endapo akipewa ridhaa ya kuongoza nchi huku akieleza kukerwa na ujangili... "Ninapata shida sana ninapoona meno ya tembo yanauzwa Ulaya halafu unaambiwa yanatoka Tanzania… sasa unajiuliza yanapitaje?"

Alisema ili kushughulikia suala hilo atahakikisha watendaji wa sekta hiyo wanaboreshewa masilahi yao ili wachangie mapato ya nchi.

Aliahidi Serikali yake kuwa rafiki wa wawekezaji na kwamba italinda masilahi ya wafanyabiashara.

Mgombea urais huyo aliahidi kuwa atalinda uhuru wa habari na atafanya kazi na waandishi wa habari siyo tu wakati wa kipindi cha kampeni, bali hata baada.

Katika ahadi zake, Dk Magufuli hakuwaacha wasanii, alisema atahakikisha wanapata hakimiliki na kuhakikisha wao pamoja na wanamichezo wanaanzishiwa mfuko kwa ajili ya kuwasaidia katika mambo mbalimbali.

Baada ya kupitia hotuba hiyo numegundua kasoro nyingi sana kama ifuatavyo
  • Amesema kuwa ataanzisha mahakama maalum ya kushughulikia ufisadi, Je, Tanzania tunashindwa kuwawajibisha mafisadi sababu ya kukosa mahakama au ni mfumo uliopo wa kulindana? Kwani kwa issue kama ya ESCROW watuhumiwa mbona wanajulikana na wengine walikubali kuchota fedha zetu!
  • Kuhusu elimu ya juu, amesema anashangazwa na mfumo uliopo sasa hv mfumo huu si umeanzishwa na kulelewa na CCM? Sasa yeye atatumia nguvu ipo isiyoandikwa kwenye Ilani ya Chama chake!
  • Amesema kuhusu ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali za rufaa, Je, hajui kwamba miundombinu hiyo ipo ingawa haina dawa na watumishi sasa kama marais 4 waliopita hawakumaliza tatizo la afya yeye atatumia mwarobaini gani tatizo liishe Mfano: Atafanya nini kuondoa matumizi yaliyopindukia kwenye serikali mfano: rais analipwa dola 192,000/= kwa mwezi, wabunge tsh 12,000,000/= na wengine wengi sasa Magufuli haya atayashughulikia aweze akiwa CCM?

Kwa ufupi naona mashaka na ahadi 25 alizootoa!
Hizo ahadi nyingi ni hewa
 
Tuache hizo zote za kufikirika zinazohitaji mitaji, tuangalie tu hizi mbili zisizohitaji uwekezaji wala fedha kuzitekeleza...
  1. Aliahidi kuwa atalinda uhuru wa habari na atafanya kazi na waandishi wa habari siyo tu wakati wa kipindi cha kampeni, bali hata baada.
  2. Aliahidi Serikali yake kuwa rafiki wa wawekezaji na kwamba italinda masilahi ya wafanyabiashara.
Halafu kuna watu wanataka apewe zawadi ya awamu nyingine! Safari hii akina Bashite watanunua hadi ndege na meli binafsi na wake zao kutembea kwa helicopta huku wananchi wakiendelea kutekwa, kuteswa na kuuawa. Je Watanzania tumelogwa?
 
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanikiwa kutimiza ahadi zilizoahidiwa kwa wananchi wakati wa kampeni za Urais, mwaka 2015, na wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Novemba 2015.

Rais alihutubia Bunge kwa mujibu wa matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 91, ibara ndogo ya kwanza inayomtaka Rais aliyechaguliwa kufungua rasmi Bunge hilo.

Akihutubia bunge hilo, Rais Magufuli aliwaambia wabunge kuwa wananchi waliwachagua wakiwa na matarajio makubwa na watawapima kwa namna watakavyokidhi kiu na matarajio yao.

“Wananchi wamewapa imani na ridhaa ya kuwawakilisha katika kipindi cha Awamu ya Tano ambapo matarajio yao ni makubwa sana, sote tuliahidi kuwatumikia na kutokana na utumishi wetu kwao tuweze kutatua matatizo yao mbalimbali na kuongoza mabadiliko makubwa ya kiutendaji” alisema Rais Magufuli.

“Mimi na Mhe. Samia, Makamu wa Rais tuliwaahidi wananchi kuwa tutawatumikia na kuhakikisha kuwa katika utumishi wetu tutawajali wananchi wote, lakini zaidi wananchi wa kawaida” alisema Rais Magufuli.

Ni dhahiri uchapakazi wake umeonyesha mabadiliko makubwa ya kiutendaji, tumeshuhudia Rais akifanya mikutano mbali mbali na viongozi kuanzia ngazi ya mawaziri hadi watendaji wa kata Tanzania bara na kuzungumza nao masuala mbalimbali ya kiuongozi ikiwemo wajibu wao kwa wananchi.

Mkutano kati ya Rais na watendaji wa kata ni mwendelezo wa mikutano yake na watendaji wa serikali wakiwemo Wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa wilaya, Makatibu tawala ya wilaya na Makatibu watendaji wa tarafa.

Akizungumza na Makatibu watendaji wa tarada Rais alisema “Ninyi ni wawakilishi wangu ngazi ya kata, tunapozungumza mafanikio ya Serikali, ninyi ndio wasimamizi wa mwanzo wa mafanikio hayo.”

Hatua ya Rais kuwaita Watendaji hao wa tarafa kutoka Tanzania Bara na kuzungumza nao, ni kitendo kinachoonyesha jinsi anavyowajali viongozi wote kuanzia ngazi ya chini hadi juu. Pia ni kitendo kinachoonyesha kuwa uongozi wa chini ukifanya kazi vizuri utawezesha hata uongozi wa juu kutenda kazi kwa ufanisi na yenje tija kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

Katika bunge hilo Rais pia aliahidi kusimamia matumizi ya mali za umma na rasilimali za Taifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali zetu zinatumika kwa matumizi kwa manufaa ya umma na si kwa manufaa ya mtu binafsi. Aidha, kuhakikisha kuwa ugawaji wa rasilimali hizo unafanyika kwa haki.

Katika siku za mwanzo za utawala wake Rais Magufuli alianza kwa kufanya ufuatiliaji wa rasilimali zetu ambapo aliunda kamati maalum ya kuchunguza mchanga na madini yalikuwa yanasafirishwa nje ya nchi. Kamati hiyo ilionyesha upotevu mkubwa wa mapato na rasilimali za nchi ambapo nchi ilikuwa inapoteza kiasi cha bilioni 829.4 hadi trilioni 1.439 kwa kusafirisha mchanga nje ya nchi.

Ili kuhakikisha anazuia upotevu huo, kamati ilitoa mapendekezo kadhaa ambayo Rais aliyakubali. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni usitishwaji wa usafirishaji wa mchanga huo hadi mrabaha stahiki utakapolipwa, na kujengwa kwa vinu vya kuchakata madini yote ili yaweze kufahamika na kutozwa kodi.

Aidha, Rais aliwaagiza Wakuu wa mikoa inayozalisha madini kuanzisha masoko ya madini ili kudhibiti utoroshaji na uuzaji holela wa madini. Hadi sasa baadhi ya masoko yamekwisha anzishwa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Dar es salaam, Mtwara, Manyara, Morogoro, Kagera na Arusha. Kwa upande wa wilaya masoko hayo yamefunguliwa Simanjiro na Chunya.

Ufunguzi wa masoko hayo umeleta neema si kwa Serikali tu bali hata kwa wauzaji wa madini hayo ambao walikuwa wakiyauza kwa kudhulumiwa na wanunuzi wakubwa. Kwa Serikali na nchi kwa ujumla masoko haya yameongeza pato la taifa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la upatikanaji wa madini.

Eneo lingine ambalo Rais aliahidi kulishughulikia ni kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi mabaya ya fedha za umma. Katika kutimiza ahadi yake kwa upande wa kusimamia mapato tumeshuhudia Rais akifanya mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi katika mamlaka ya kukusanya kodi (TRA) na kuzindua kituo kikuu cha Taifa cha kuhifadhi mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia ya elektroniki ambapo makusanyo ya mwezi Septemba 2019 yalikuwa trilioni 1.7 sawa na asilimia 97.20 kiasi ambacho ni hakijawahi kukusanywa na mamlaka hiyo tangu kuanzishwa kwake Julai mosi, 1996.

Ni dhamira ya TRA kukusanya mapato kwa utaratibu rahisi na wa wazi na walipakodi watapata urahisi wa kupata huduma zinazotolewa kwa wakati. Matokeo ya kuongezeka kwa ukubalifu yatadhihirika kwa kuongezeka kwa mapato kwa ajili ya Serikali kutoa huduma za jamii zinasostahiki na kwa ubora. Hii itaifanya jamii ya walipakodi kufurahia manufaa ya kijamii na kiuchumi kutokana na kodi wanazolipa katika kuboresha hali ya maisha.

Kituo hiki ni mashirikiano ya pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), ambacho kimeundwa ili kusaidia kuondoa mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali zote mbili.

Akizindua kituo hicho Rais alizitaka taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali, kampuni na benki kujisajili katika kituo hicho ili kuweza kukusanya kodi kwa ufanisi. ‘Kituo hicho ni muhimu sana kwa ustawi wa maendeleo ya nchi ili kulinda usalama wa taifa, taasisi za serikali na makampuni binafsi yanayoendesha shughuli zake nchini na kukuza sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo’ alisema Rais.

Katika kuhakikisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inakuwa kinara wa utawala bora, Rais aliahidi kupambana na rushwa na ufisadi. Awali akihutubia bunge la kwanza, Rais aliwaambia wabunge kuwa mojawapo ya maeneo yaliyolalamikiwa na wananchi wakati wa kipindi cha kampeni ni rushwa ambapo sehemu nyingi wananchi walisema kuwa rushwa ni mojawapo ya kero kubwa wanazokumbana nazo.

Baadhi ya mafanikio ya mapambano ya vita dhidi ya rushwa ni pamoja na kuanzishwa kwa ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Hadi ngazi za wilaya.

Pia Serikali hii inajipambanua kwa uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa umma, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu rushwa na madhara yake.

Katika mkutano wa 32 wa wakuu wa nchi za Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mwaka 2017, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alisema kuwa Tanzania ilitajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika ufuatiliaji na utekelezaji wa mapambano dhidi ya rushwa.

Taasisi ya Transparency International imesifu juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuitaja Tanzania kuwa ni nchi ya pili kwa kupunguza rushwa na kufanikiwa kuifanyia kazi mianya mingi ya rushwa.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam aliyekuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, CP. Diwani Athuman alisema kuwa utafiti uliofanywa na taasisi za kimataifa za Transparency International na Afro Barometer inayoitwa Global Corruption Barometer Africa 2019, alisema kuwa Tanzania ni ya kwanza kati ya nchi 35 za Afrika katika kipengele cha juhudi za serikali katika kupambana na rushwa kwa mwaka 2019.

Aliongeza kusema kuwa Tanzania imefanya vizuri katika maeneo mawili ambayo ni utendaji mzuri wa Serikali na kukuza imani kwa wananchi dhidi ya Serikali yao na jitihada za kupambana na rushwa.

Kuhusu kero ya migogoro ya ardhi, Serikali ya Awamu ya Tano imefuta mapori tengefu 12 yenye ukubwa wa ekeri 707,659.94 ambayo yamepoteza sifa na kuyagawa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za makazi, kilimo na ufugaji, na misitu 7 yenye ukubwa wa ekari 46,715 kurudi kwa wananchi.

Hatua hii ilifuatiwa na kubaini uwepo wa vijiji 975 vyenye migogoro, ambapo iliamuliwa kuwa vijiji 920 vibaki ndani ya hifadhi na mipaka irejerewe upya na kupatiwa vibali vya ardhi vya kijiji. Pia serikali iliridhia kumega misitu 14 kwa ajili ya kilimo na mifugo na kufuta mashamba 16 yasiyoendelezwa ili yapangiwe matumizi ya kilimo na mifugo.

Ahadi nyingine ambazo Rais amezitimiza ni katika sekta ya afya na elimu ambapo katika elimu aliahidi elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne. Kutokana na utekelezaji wa ahadi hiyo, kumekuwa na mwamko mkubwa wa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza shule ya msingi ambao idadi yao imefikia 1,670,919 mwaka 2019 kutoka 896,584 mwaka 2016. Kwa upande wa shule za sekondari idadi ya wanafunzi walioandikishwa kwa mwaka 2019 ni 710,436 kutoka wanafunzi 238,365 walioandikishwa mwaka 2016 wakati sera ya elimu bure ilipoanza kutekelezwa nchini.

Katika sekta ya elimu pia tumeshuhudia maboresho mbalimbali ambapo vifaa vya kufundishia na kujifunzia vimeongezwa, michango isiyo ya lazima imeondolewa, kuongezewa madawati na kujengwa kwa nyumba za walimu.

Aidha, katika eneo la afya, dhamira ya Rais kujenga uchumi wa kisasa na suala la kupambana na umaskini amelipa msukumo wenye tija ili kuwa na wananchi wenye afya bora. Tumeshuhudia uboreshaji wa sekta hii ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya, kuzipatia vifaa bora na vya kisasa hospitali, vituo vya afya na zahanati. Lengo likiwa ni kuwaondolea usumbufu wananchi na kutolazimika kupeleka watu kutibiwa nje ya nchi.

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Awamu ya Tano, Kwa tumeshuhudia mafanikio mengi katika sekta mbalimbali kama vile sekta za afya, elimu, miundombinu, nishati na madini, ikiwa ni kutimiza ahadi ambazo ziliahidiwa na Rais wakati anaingia madarakani. Maendeleo yote haya yamewagusa wananchi kwa kiasi kikubwa kwa sababu yameweza kutatua kero nyingi ambazo wananchi walikuwa nazo.
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania

Endelea kuchapa kazi

Wale wasaliti wa nchi pumzi imekata
 
Yaani kwa miaka yote hiyo minne kumekuwa na mafanikio tu! Hakuna changamoto? Kama ni hivyo basi hiyo serikali itakuwa inaongozwa na malaika.
 
Nimeona pendekezo la mtu mmoja kuwa Magufuli aachwe akae madarakani kwa miaka 30 hivi. Mie nadhani hata miaka 30 ni pendekezo dogo. Tufanye hivi: AACHWE AFIE PALE! Hii nadhani inapendeza zaidi kwa "waimba kwaya" na "waabudu sanamu" wa awamu ya tano. Kwa Kizinza, "aachwe afiepo!"
 
Back
Top Bottom