Uchambuzi wako unaakisi kiwango cha akili na weledi ulionao bahati mbaya kwa makusudi kabisa umeamua kuvitumia vibaya, kwa sababu kwa kukusudia, umeacha mambo ya msingi kabisaWasalaaam wanabodi,
Kampeni za uchaguzi mkuu zinaelekea ukingoni siku mbili zijazo nchi nzima. Tumeona Kila mgombea akijinadi kwa style yake na upekee kulingana na malengo na mikakati thabiti waliyojiwekea...
IDADI YA WANACHAMA
Hawa ni ndio nguzo ya kwanza muhimu ktk kusaka kura WANACHAMA loyal and committed hawayumbishwi hata hoja iwe kali kiasi gani. Hawa sio UNDECIDED VOTERS bali ni kinyume chake hawabadiliki kwa upepo wa nyomi au ubora wa Sera.. kwao chama ni itikadi.
Je Upinzani Wana wangapi
Je CCM Wana wangapi!?
NGOME ZA KISIASA (Political stronghold regions):
NGOME za kisiasa hutengeneza base ya kuanzia mashambulizi..
Kwamba mkoa gani au kanda gani chama fulani kinapendwa na kuwa na ufuasi na ushawishi mkubwa!?
Ukichukia ACT(CUF ya zamani) Ngome yao ni Pemba ambako Wana 100% ya kuchukua majority votes kwa Urais na Wabunge wengi kuliko CCM. Hayo nia maeneo ambayo hakuna TISS, POLISI, NEC au VIFARU vinaweza kubadili matokeo bali wao ndio wanaweza ku manipulate matokeo. Je ngome kama hizo CHADEMA, ACT na CCM wanazo ngapi Kama mtaji wa kuanzia..!?
IDADI YA WBUNGE..
Kikatiba mwenye Wabunge wengi ndio anaunda Serikali, jee Kuna matarajio ya kupata angalau nusu ya Wabunge!?
Ikumbukwe kwamba Wabunge huakisi kiwango cha uungwaji mkono wa Mgombea Uraisi. Uzoefu Unaonyesha maeneo mengi ambako Kuna washindani wenye nguvu ngazi ya Ubunge huleta changamoto upande wa Urais pia. Jiulize Kuna uwezekano wa majimbo mangap mikoani!? Usizungumzie majimbo mawili matatu katika mkoa au kanda... Kwa mfano kule kanda ya ziwa Musoma, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita na Bukoba jumla mikoa 6 majimbo zaidi ya 40 lakini Upinzani hawana hata viti 8 na hakuna matumaini ya kufikisha angalau majimbo 10 mwaka huu.
Ktk Hali hiyo. Moja katibyabSifa Mgombea mwenye uwezo wa kushinda Uraisi ni uwezo wake binafsi kuwabeba Wabunge wa chama chake. Tuna tegemea Wabunge wangapi wanaobebwa na upepo wa Tundu!? Au Wabunge Wangapi Kama kina Heche watambeba Lisu!? Unategemeaje Ushindi wa Urais ktk mazingira haya!??
UPEPO WA MAKUNDI MAALUM,
Hapa namaanisha makundi rika wazee vs vijana, jinsia wanaume vs wanawake, maeneo ya makazi, Mjini vs vijijini, kiwango cha uelewa(ELIMU) wasomi vs watu wa kawaida..
Tupime kujua kundi lipi kwenye uwezo kubadili matokeo dhidi ya mingine na liko upande Gani?
POLITICAL AGENDA
Hapa kwenye agenda bado Kuna ukakasi. Kuna kundi linalazimisha agenda yake ndio ibebe garagumu la uchaguzi na wamefanikiwa kuaminsha watu uchaguzi utaamuliwa na agenda yao bila kujiuliza jinsi wananchi walivyoikubali agenda hiyo!?
Watu tunaaminishwa ati agenda kuu ni UHURU NA HAKI. Tunasahau kwamba CCM chini ya JPM imetoa Uhuru na HAKI kwa raia ya kawaida kuliko kipindi chochote ktk Historia ya Nchi hii. Tuliimba sana kule nyuma juu ya CCM kuwa Kama kambale baba ndevu mtoto ndevu tukimaanisha kuwa hata balozi au mtendaji wa Kijiji anaweza kukunyanyasa na usipate msaada. Leo sio mtendaji tu bali hata Mkuu wa Mkoa au Waziri hawezi kukunyanyasa ukiwa na ujasiri wa kudai haki yako.
Wahanga wakubwa wa UHURU na HAKI ni wanasiasa, wanaharakati na wanahabari, Kwa kuwa Wana access na media wanataka Wananchi tuwapiganie vita vyao huku wakituaminisha eti na sisi ni wahanga watarajiwa..
Jamani kila mmoja ajifunze kupigana vita yake. Leo hii Mimi Raia wa kawaida nahudumiwa vzr zaidi, nasikilizwa vizuri zaidi, napata haki zangu kwa urahisi zaidi, nina Uhuru zaidi mbele viongozi wa ngazi yangu kuliko kipindi chochote ktk Historia ya Nchi hii kwani KAMBALE MWENYE NDEVU amebaki ni JPM pekee, makamu wake na PM Majaliwa, FULL STOP. Kwa hiyo agenda ya UHURU NA HAKI sio hitaji au agenda ya Raia wa kawaida bali Social Media Na Opposition wanatulisha maneno.
Nimalizie kwa kusema kwamba huenda uchaguzi Ukawa na matokeo tofauti sana na mtazamo wa baadhi ya watu kwani wanakimbia towards wrong direction wakiamini eti the commons watawafuata. Wakifika mwisho wa mwendo watashanga watakapogeuka nyuma na kukuta Raia walikimbia opposite direction.
Tujiandae kisaikolojia