Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Naamini Tundu Lissu si Mwafaka Kugombea Urais 2020 (1)

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Nimetimiza mwaka tangu nimeandika katika jukwa hili. Sababu za kuachana na JF ni za kibafasi ila jukwaa si huru kwa wale wanaofanya maandiko wasiopenda wenyeJF.

Kwa kuanzia tu, wengine tumekuwa wawazi juu ya nini na nani anafaa kusimama na kusimamia Chama chetu pendwa cha CHADEMA. Tulisema na tutaendelea kusema kuwa Mbowe anafanya maamuzi mengi ya kichama kunyume na mahitaji halisi ya chama hata kama wengi hawataki kusema.

Tukumbuke kuwa katika uchaguzi wa 2015 alifanya kosa lililosababisha CCM kupata penaliti Dk za mwisho mwa mchezo na kuishia kukosa kombe. Leo tumeona 90% ya aliowaamini hawapo pamoja na sisi. Siku zote tujue CCM ni chama kubwa na kupambana nayo tunahitaji akili za ziada na si miemko ya kisiasa. Huwezi kaa pekee yako usiku, asubuhi uamue kitu cha kitaifa kwa wanachama wote kama vile unawapelekea watoto wako matunda wanayopenda hata kama hawajakuagiza.

2020 iko mlangoni. Mwanzo tulisema ili tufike salama tunahitaji kudai Katiba Mpya na Tume Mpya ya Uchaguzi. Madai haya hayahitaji maandamano zaidi ya vikao na mahakama.

Wakati tunasema hayo ngojera za haraka zikaja kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii yakiongozwa na kadada kanakoitwa Mange. Tukaambiwa kuna UKUTA, na matamko zaidi ya 20 yakitolewa ma viongozi kuanzia Msingi hata taifa. Wote walisema "TAMKO LA CHAMA". Sisi tukasema, Tamko la chama hawezi toa WEMA au Sumaye au Makongoro.

Matamko yakakauka na wakati wake. Hata leo tukaamini na AZIMIO LA ZANZIBAR. Nani anaamini azimio la ZANZIBAR? Lazima akili zao uchanganye na zako ndio utaelewa.

"STERLING ameua" ndio tunaweza sema. Amechukuwa, ameweka, ameondoka. Hii ina maana sana. Lowassa alikuwa sterling na mwanamfumo aliyepotea ndani ya upinzani. Achilia Lowassa. Maalim Seif anajua vizuri sana ila hana back up ya kutosha Bara. Yupo ZZK anajua siasa, haaminiki pia katika siasa.

Nani kete ya Upinzani 2020. Lissu? Hana uwezo wa kisiasa kama wengine wanavyomchukulia. Wengi wanamuona kwenye TV tu. Uwanjani anahitaji magongo, maneno, waimbaji na wasemaji ili aweze kusimama. Sijui kama mnajua hilo mnaompigia debe ndani ya chama chetu. Ana akili ya kuongoza taifa ila njia za kufika Ikulu kwake haipo wazi kwa udhaifu wake binafsi na chama au viongozi wenzake.

Endelea kufuatilia sehemu ya Pili.......... Upate uhondo.......................

Ufipa.......
 
Hapa hawaji.umewachanganya,wakija tegemea povu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom