Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Membe ana athari ndogo Uchaguzi wa 2020, Lowassa ni zaidi yake

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Nimepata kumsikiliza Bernard Membe. Hotuba yake, manuwio na matatajio yake. Lakini pia nimepata kumsikiliza Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharif na Kiongozi Zitto Kabwe.

Kuna ujumbe wa aina tatu. Mosi; Membe anasemwa/anasema yuko tofauti na Edward Lowasa, hivyo asifananishwe naye. Pili; Membe anatajwa/anajiweka katika kiwango cha umaarufu mkubwa na kwamba ana kundi kubwa la wafuasi na tatu, pamoja na neno ‘muungano wa upinzani kusikika’, Membe amejihakikishia ni Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sasa tujadili. Mosi; nini tofauti ya Lowasa na Membe? Pamoja na jitihada nyingi za kuonesha utofauti, ni ngumu kuiona kwa ukubwa wake. Wote Membe na Lowasa wanaziingia Siasa za Upinzani kipindi cha uchaguzi mkuu na baada ya jitihada zoote za kujaribu ndani kuusaka urais kupitia chama chao CCM kukwama. Upinzani ni kimbilio baada ya maji kufika shingoni. Wametoka CCM baada ya kukutwa na matatizo.

Mmoja kafukuzwa uanachama, mwingine alijiondoa. Wote wanaondoka kwa hasira za kukataliwa/kukatwa ndani ya CCM na si hiari yao. Aidha, wote wanaondoka kwa ahadi zilezile, kuja upinzani kuleta mabadiliko. Wanasema wana kundi kubwa nyuma kutoka CCM. Kubwa kuliko yote, wote wanaingia upinzani kuutaka urais na si kuujenga upinzani. Kinachowaleta ni urais si upinzani.

Lakini ni kweli kuna tofauti kubwa baina yao, hata hivyo tofauti ukizipima kwenye mizania Lowasa alikuwa mtaji zaidi kuliko Membe. Hapa tuingie kwenye hoja ya pili ya wingi wa wafuasi. Lowasa aliposema ana kundi nyuma lilionekana, lilisimama naye, halikujificha. Kwa Membe kipindi chote cha kutajwa kuutaka urais alitajwa na majina ya akina Adbulahman Kinana, Yusuph Makamba, Nape Nnauye na January Makamba.

Wote hawa hawaoneshi dalili kuwa wako naye. Wako na CCM yao. Membe anaonekana yeye na mke wake tu, ukiacha tukio la kijijini kwake Rondo ambapo baadhi ya wananchi walirejesha kadi za CCM. Lowasa alikuwa na mtandao mpana ndani ya CCM, alijijenga kwa muda mrefu pia nje ya CCM. Imani yake kwa watanzania ilivuka ufuasi wa vyama. Kwa Membe hili la kuwa na wafuasi pengine tulitarajie baadaye lakini itoshe kusema wafuasi ambao hawajioneshi wazi na hawasikiki kukusemea kwa kujiamini si wa kuwekea imani.

Pengine nguvu ya Membe ipo katika ujenzi wa hoja na uelewa wa mambo. Ukimsikiliza anaonekana kuwa na uelewa mpana wa mambo ya ndani na ya kimataifa. Ana siha na afya njema kiasi cha kuweza kuhimili mikikimikiki ya majukwaani tofauti la Lowasa.

Hata hivyo hili pekee halitoshi kama huna mtandao na ufuasi mkubwa miongoni mwa wapiga kura. Membe wa kuutaka urais ndani ya mtandao wa CCM ni tofauti na anayeutaka ndani ya ACT-Wazalendo. Akiwa ndani ya CCM anaogelea katika mtandao ulio hai na wa uhakika. Akiwa ACT-Wazalendo atatambaa kupitia iliyokuwa nguvu ya CUF (Ambayo sasa ni ACT), kwa hiyo mtandao wake binafsi unapaswa kuwa mkubwa zaidi ili walau ndoto yake ya urais ifikirike. Katika hotuba yake kaishia kutaja maeneo yaleyale ya Mtwara na Lindi kwamba ndiko ana wafuasi.

Vipi Dar es Salaam? Arusha? Mwanza? Mbeya? Dodoma? Hili linarejea palepale, Je ana nguvu ya kushawishi high profile figures kuachana na CCM kuja kumuunga mkono? Amejenga himaya yake kisiasa kiasi cha kuaminisha kushinda kiti cha urais? Hili ndilo pekee litamfanya awe turufu na si vinginevyo. Lowasa alikuwa busy kuzunguka kila kona ya nchi kujijenga. Aliunda vikundi kibao vya ‘Friends of Lowasa’ ambavyo vilikuwa vimezagaa kila kona ya nchi. Alishiriki karibu kila tukio kubwa la imani kubwa za kiroho nchini.

Itoshe kusema Lowasa alikuwa ameuivisha umma wa watanzania na uliiva naye tofauti na Membe ambaye baada ya 2015 alijichimbia Kijijini na Rondo na kupotea kabisa kwenye majukwaa ya kisiasa na kiimani achilia mbali matukio makubwa yenye kukutanisha makundi ya watu.

Katika kuhitimisha hoja ya mwisho ya kuutaka urais. Maalim Seif kasikika anampa uhakika Membe kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia ACT, na kwa maana hiyo awe mgombea wa urais wa chama hicho. Hii ina maana hakuna kinachoitwa muungano wa upinzani.

Hata hivyo katika Hotuba yake, Membe anaonekana kuuhitaji muungano wa upinzani ingawa anaonekana kuamini kwamba yeye pekee ndiye turufu pekee ya Urais na si vinginevyo. Huu ndiyo udhaifu mkubwa wa Bernard Membe. Kuutaka zaidi urais na si kuimarisha kambi ya upinzani dhidi ya CCM.

Kajipiga upofu kabisa wa kuona kwamba katika kambi ya upinzani wapo wanasiasa aliowakuta ambao pia wanapigiwa chapuo na wana nafasi kubwa tu ya ufuasi. Kwamba Membe anasisitiza yuko tayari kuongoza majadiliano na vyama vingine vya upinzani ili kujenga umoja, lakini sharti ni yeye awe mgombea. Mbaya zaidi kashajiandalia na vipaumbele vyake vya kutekeleza akiwa Rais.

HITIMISHO: Kwa ujumla nguvu ya Membe itategemea ufuasi alioujenga ndani ya CCM na kama utamfuata. Hata hivyo ukimya na kusikika yeye peke yake bila utetezi mpana ndani ya Chama chake cha zamani unaashilia kwamba yu ‘yatima’. Ni nguvu yake ndani ya CCM ndiyo itamjenga nje ya CCM.

Hadi sasa hili halionekani. Kinachotia mashaka zaidi ni yeye mwenyewe amesikika akisema ana watu sita (6) wenye nguvu ndani ya CCM wanaomuunga mkono, ila wanaogopa kujitokeza kwamba watafukuzwa. Hii inaashilia kwamba Membe anaingia upinzani akiwa hana mizizi ya kuitikisa CCM. Nguvu yake kubwa anategemea kujijenga kupitia mitandao iliyojengwa na upinzani bila yeye kuongeza thamani. Dalili kubwa ni kwamba ataathiri kidogo mchakato wa uchaguzi wa 2020.
 
mbona umekariri kuwa wamekatwa? aliekatwa ni mamvi, membe hata kwenye mchakato hajapitia, huoni hapo kuna tofauti?

kingine unasema hana wafuasi, subiri kura za maoni zipite
 
Mkuu ulitaka Membe afanye Siasa za Upinzani huku polisi wakiwa tayari kumkamata ..maana Siasa za Upinzani zilipigwa stop
 
Kwa maoni yangu LOWASA ALIKUA SERIOUS NA URAIS ILA BWN MEMBE NAONA ANAJIPOZA MACHUNGU TU ILA AKIFIKISHA KURA HATA LAKI TATU BASI AWEKWE KWENYE HOSTORIA YA TAIFA
 
Hata Hasisimui kabisa huyu mzee,ataaibika Sana Bora hata angejituliza zake alime korosho.
 
Huyo Lowasa alifanya nini wakati alishindwa kama wengine walivyoshindwa, Membe hana tatizo ila asigombee urais
 
Watz mtazidi kuwa masikini tu Sasa wewe
Hakuna kitu Cha maana kwenye habari yako, majungu tu. Huu muda umeupoteza

Membe agombee au asigombee, wenye akili tunajadili ajenda muhimu za kitaifa
 
Tofauti ya lowasa na membe Ni moja tu, membe Ni mwongeaji ila lowasa alikuwa bubu.Mfanano wao wote Ni walewale tu , wamekuja kwa lengo lilelile tu...
 
Kama ni game wanacheza hawa jamaa toka CCM kila tukielekea kwenye uchaguzi mkuu this time wamefeli, walitakiwa wabuni mbinu mpya, lakini sio kurudia mbinu ile ile ya 2015.

Kwangu mgombea Urais upinzani 2020 ni Lissu.
 
Uchambuzi mzuri lakini ndugu yangu jua kuwa sasa wananchi tumechoka mno. Membe hata akileta wabunge kumi tu na akapigiwa kura elfu moja tu ambazo zingeenda kwa Magu kwetu sisi bado ni furaha tu. Kwanza Membe anafikisha ujumbe kwa Magu kuwa demokrasia inatakiwa kuwepo haijalishi inafurahiwa na watu wangapi!
 
Uchambuzi mzuri lakini ndugu yangu jua kuwa sasa wananchi tumechoka mno. Membe hata akileta wabunge kumi tu na akapigiwa kura elfu moja tu ambazo zingeenda kwa Magu kwetu sisi bado ni furaha tu. Kwanza Membe anafikisha ujumbe kwa Magu kuwa demokrasia inatakiwa kuwepo haijalishi inafurahiwa na watu wangapi!

Hao wabunge 10 atawaleta kutokea wapi? Unamwona kweli akikitikisa CCM na kukisaidia ACT Wazalendo kuvuna wanachama?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom