Uchambuzi Kitabu cha Mwinyi: Sitawasahau Maalim Seif, Mrema na Mtikila katika utawala wangu

Mimi watoto wa mkapa siwajui majina yao

Naomba nitajie majina boss wako wapi baba yao alikuwa kiongozi mkubwa tu Ila wao wanaishi mafichoni

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Mkuu sasa unataka kuwafichua watu watoke mafichoni wakati wao hawapendi maisha ya kujifichua?

Kuna huyo Peter Maro alikuwa Mkurugenzi wa Simu 2000 wakati wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma.

Kuna Nico yuko serikalini, siku hizi yupo wizara moja ni Naibu Katibu Mkuu.Aliteuliwa Unaibu Katibu Mkuu na marehemu Magufuli na juzi kateuliwa tena na Rais Sasha

Kuna Stephan yupo na biashara zake.

Inakuwa si rahisi kuwasikia, walifundwa kwao yani ile mshua anaweka beat kunywa maji mpaka umalize kula kwanza.True story.

Vibweka vyao wanavijua watoto wa Sea View / Upanga.
 
Kayatoa keshafariki, hamna jinsi ya kujitetea, tutatoa hukumu ya upande mmoja tu!
Nani aliekwambia Hapo kamhukumu,hiyo ni historia ya safari yake na hayo mambo yalitokea na wala mpaka Maalim anafariki walikuwa hawana ugomvi na mwingi
 
Dah JK tena? Sasa si bora huyo Malima, JK ndio jambazi nambari moja kwenye hili taifa, Jamaa ametupiga kupita kiasi
JK alipelekwa kurekebisha hali Hazina na alifanya hivyo bila kujali alikuwa muislamu mwenzake. Hilo la ujambazi ndio wewe unaniambia.

Amandla...
 
Mkuu sasa unataka kuwafichua watu watoke mafichoni wakati wao hawapendi maisha ya kujifichua?

Kuna huyo Peter Maro alikuwa Mkurugenzi wa Simu 2000 wakati wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma.

Kuna Nico yuko serikalini, siku hizi yupo wizara ya moja ni Naibu Katibu Mkuu.Aliteuliwa Unaibu Katibu Mkuu na marehemu Magufuli na juzi kateuliwa tena na Rais Sasha

Kuna Stephan yupo na biashara zake.

Inakuwa si rahisi kuwasikia, walifundwa kwao yani ile mshua anaweka beat kunywa maji mpaka umalize kula kwanza.True story.

Vvibweka vyao wanavijua watoto wa Sea View / Upanga.
Shukrani mkuu

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
True fighter wa Watanzania na wa Siasa za Tanzania ni Mtikila pekee,wengine wote Mwinyi,Mkapa,Kikwete,Magufuli ,Malando,Mbatia,Mbowe,Self,Mrema wote wachumia Tumbo.
 
Nimeanza kukosa hamu ya kukisoma hicho kitabu kimajaa mipasho. Mbona hajisemi alivyouza kitalu kwa mtoto wa Mfalme wa saudia? Mbona haongelei deals alizokuwa anajadili akiwa ikulu? Yani deals za wahindi akina Patel? Jamaa walisupply magari zaidi ya 500 na hakuwalipa mchuzi na hela ilikuwa imetengwa alipeleka wapi? Kizee kinafiki sana hiki?
 
Peter ni mwanae kama ni hivyo kwanini kamtenga.
Kamtenga vibaya sana, halafu nimeshangaa sana kwa sababu kuna parties alikuwa anamsifia sana kwamba "Peter is very bright".

Kwenye kitabu kamkata kama kikao cha CCM kinavyokata watangaza nia.

Sasa hilo jambo la familia tu kuitaja kakata watu, huko kwenye ma scandal ndiyo usiseme, kitabu cha Mkapa kilitakiwa kuwa volume lenye nondo zote. Kimekuja kuwa kama dibaji ya kitabu kilichotakiwa.

Ila, kwenye vitabu nafikiri kitabu kitakachoanika mengi kitakuja kuwa kitabu alichoandika Mama Joan Wicken, yule msaidizi wa Nyerere Mama Muingereza.

Aliandika kitabu akasema kisichapishwe mpaka miaka mingi sana baada ya kufariki Nyerere.

Inaelekea atakuwa kaeleza mengi humo ambayo hakutaka wahusika wawe hai bado wakati kinachapishwa.

Yule Mama alikuwa na Nyerere bega kwa bega kuanzia mwanzo kabisa mwaka 1960, kwenye miaka yote ya urais, mpaka Nyerere amestaafu yuko naye yule Mama kwenye South to South Commission.

 
Naona kachagua ya kusema hakugusia haya
Mchele mbovu wa mfanyabiashara maarufu uliosababisha mkemia mkuu na msaidizi wake wauawe kikatili
Kashfa ya Loliondo
Mrema na Twiga kwenye makontena bandarini

 
Tueleze hapa huo ujanjajanja wa Maalim Seif
Yeye ndiye aliiba nyaraka za jumbe kuhusu mpango wake wa serikali tatu lakini baadae akajifanya anataka serikali tatu, kwenye msiba wa jumbe aligoma kumpa miono Shein huku akisahau yeye ndiye alimaliza safari ya kisiasa ya Jumbe
 
Kuna masuala kadhaa alitakiwa ayaweke wazi ili aaminike.
Hivyo katika kupiga kura katika vikao vya CCM kuna kura tafauti kati ya Wapemba na Waunguja.
Wakati jumbe anafukuzwa Maalim Seif alikuwa na madaraka gani Zanzibar hata aweze kuingia ikulu.
 
Yeye ndiye aliiba nyaraka za jumbe kuhusu mpango wake wa serikali tatu lakini baadae akajifanya anataka serikali tatu, kwenye msiba wa jumbe aligoma kumpa miono Shein huku akisahau yeye ndiye alimaliza safari ya kisiasa ya Jumbe

Sasa kesi za Jumbe na Shein zina mahusiano gani? Hizo ni ishu 2 tofauti, SHein ni mwizi wa kura katawala kwa kipitia mkono wa bunduki ulitaka akumbatiane nae kwa lipi?

Na Kuhusu Jumbe acha kuwa na mihemko, fatilia tukio vizuri utafahamu hasa kilichotokea
 
Sasa kesi za Jumbe na Shein zina mahusiano gani? Hizo ni ishu 2 tofauti, SHein ni mwizi wa kura katawala kwa kipitia mkono wa bunduki ulitaka akumbatiane nae kwa lipi?

Na Kuhusu Jumbe acha kuwa na mihemko, fatilia tukio vizuri utafahamu hasa kilichotokea
Acha ujuaji kijana hoja hujibiwa kwa hoja huna hoja kaa kimya
 
Hili wazo la serikali tatu kumbe lilikuwepo siku nyingi, inakuwaje mpaka leo bado halijatekelezwa, huu ukweli iko siku wataukubali tu, kitendo cha Seif kuzikataa serikali tatu halafu baadae akaja kuzikubali tuzeme ndio hadaa ya wapinzani au ni kweli alikuja kujua umuhimu wake baadae!.

Kuhusu hilo la Seif kutaka kugombea Urais akishindana na Idrisa Abdulwakil, naona huo ndio ulikuwa mwanzo wa Seif kuanza kuibiwa kura Zanzibar, Mwinyi anasema Seif alipata kura 80% toka kwa wajumbe wa Pemba na Abdulwakil akapata 80% kwa wajumbe wa Unguja, ila Abdulwakil akamzidi Seif idadi ya kura.

Kwanini hawakuweka mpangilio mzuri wa kuhesabu hizo kura, kama wakiona kuweka percentage ingeleta matatizo basi wangetangaza mshindi kwa idadi ya kura alizopata, kama ni 77/78 ijulikane, kuliko kuweka mpangilio wa asilimia ambao mwishowe ukazua mgogoro, naona wajumbe wa Pemba walikuwa na haki ya kulalamila.

Mwishowe kabisa Mtikila na udini, hapa ningependa Mwinyi aende deep zaidi, kutumia kigezo cha kumteua Profesa Kighoma Malima Waziri wa Elimu pekee sitaki kuamini moja kwa moja kama ndio ilikuwa sababu ya Mtikila kupiga kelele, naamini kuna mengine Mwinyi kayaficha hapa, angekuwepo Mtikila leo angetuelezea upande wake.
Nasubiri Mwinyi aeleze zile dhahabu, almas na fedha za kigeni zilikuwa za nani vinginevyo hivyo vitabu wasome na familia zao bila kusahau mauaji ya Stan Katabalo
 
Amewataja baadhi ya waliokuwa makada wa chama hicho mbali na Marando kuwa ni pamoja na Makongoro Nyerere (sasa amehamia CCM), James Mbatia, Masumbuko Lamwai na Prince Bagenda.

“Kuhama kwa Mrema na kusimama akiwa mgombea urais kupitia chama cha upinzani kulitusumbua sana kwenye CCM,” anaeleza Mwinyi.

Anakumbusha mkutano wa kumtambulisha Mrema uliofanyika Machi 25, 1995 Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

“Uwanja ulijaa watu wakiwamo baadhi ya wana CCM waliorudisha kadi zao za chama na kumjaza Mrema matumaini ya kushinda na kufikia ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania,” ameandika.

1620912162579.png
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom