Uchambuzi Kitabu cha Mwinyi: Sitawasahau Maalim Seif, Mrema na Mtikila katika utawala wangu

Tatizo kubwa la uandishi wa vitabu vya wana siasa ni ku edit sana content ili ipendeze kwa Serikali iliopo madarakani, uongo ni mwingi......na ukweli una achwa makusudi, sidhani kama Mwinyi kagusia lile jamba la kushauliwa kumfunga Nyerere, baada ya Nyerere kujutia kumpa madaraka ya uraisi.
Vitabu vya wanasiasa wa Tanzania ni aibu tupu.
 
Tatizo kubwa la uandishi wa vitabu vya wana siasa ni ku edit sana content ili ipendeze kwa Serikali iliopo madarakani, uongo ni mwingi......na ukweli una achwa makusudi, sidhani kama Mwinyi kagusia lile jamba la kushauliwa kumfunga Nyerere, baada ya Nyerere kujutia kumpa madaraka ya uraisi.
Asante sana. Mimi wala sijihangaishi kusoma.
 
Nilitegemea vitabu kama hivyo vibebe mambo ya ndani yaliyotokea kwenye uongozi wao ambayo hatuyajui kabisa lakini naona mengi ni yale yaliyokuwa wazi. Kusema Mrema na Mtikila walimsumbua hilo lilijulikana na siyo jipya.
Mfano mzuri wa hilo unalolisema ni kitabu cha Mkapa.

Mkapa kawa serikalini tangu miaka ya sitini.

Tena kawa mhariri wa magazeti ya serikali kwa miaka mingi, kaona mengi.

Wakati Kambona anafarakana na Nyerere, Mkapa ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumwambia Nyerere kuwa Kambona anakusema vibaya, kwa kuwa Mkapa alikuwa na waandishi wanaomfuatilia Kambona.

Nyerere hakutaka kumuamini Mkapa, kwa sababu alimpenda sana Kambona.

Mpaka mwishoni Nyerere akajiridhisha.

Lakini, ukitaka kusoma habari hizi, itabidi usome vitabu vya waandishi wa nje kama Paul Bjerk , Thomas Moloney au William Edgett Smith.

Kitabu cha Mkapa hakikuandika ugomvi wa Nyerere na Kambona licha ya Mkapa kujua mengi sana firsthand kuhusu hili.

In fact, hata kwenye mambo yasiyo ya kisiasa Mkapa kashindwa kuwa muwazi.

Katika kutaja watoto wa familia yake, kamtenga Peter, hakumtaja kabisa!
 
Aliyekisoma, je, kaandika kuhusu tuhuma za mama Sitti kuwa muuza madawa, na yale madawa yaliyokamatwa airport na Mrema!?
Ile incident iliyopeleke Mrema kuhongwa nafasi ya Naibu Raisi.
Je, anazungumziaje Mwalimu Nyerere kusema ikulu siyo jumba la biashara??

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kwahiyo hapa tuseme ni Mwinyi ndio alikuwa mdini au Kigoma Malima? naona hapa unamaanisha Mwinyi alilaumiwa na Mtikila kwa udini kwasababu ya matendo ya Kigoma Malima akiwa waziri wa elimu.

Kuhusu tuhuma za Mtikila kuwa mbaguzi wa rangi nakubaliana nawe, kipindi fulani alifanya neno "gabachori" ukawa msemo maarufu sana.
Ukweli ni kuwa " the buck stops with the President". Badala ya kuona kama anaonewa, alitakiwa kufanyia kazi malalamiko ya wakina Mtikila. Ni kama vile Mkapa alipokabidhi Chuo cha Serikali ili kiwe cha waislamu ili kupunguza pengo lililopo kielimu kati ya wamisheni na waislamu. Au Nyerere alipomkemea Iddi Amin alipowatimua raia wa Uganda wenye asili ya kihindi.

In fwakt, baada ya malalamiko alimpandisha cheo Kighoma Malima na kumfanya Waziri wa Fedha.

Amandla...
 
Maalim Seif alishalielezea mara kadhaa kuhusu suala la Jumbe, Yeye hakua akipinga serekali 3 ila walichofanya ni kujiokoa kutoka kwa Jumbe ambae alikua na mipango ya kujipa nguvu za kumfanya kuwa Dictator mwenye mamlaka kamili.
 
Mwinyi ni kama anavutia upande wake aonekane mtakatifu, Malina alijenga sehemu ya kusalia wizara ya fedha je sio udini, alishindwa kukusanya kodi hadi nchi wahisani wakagoma hadi atolewe wizara ya fedha kama haitoshi wakawaambia wafunge akaunti zake za nje kitendo kilichopelekea apate ugonjwa wa moyo na kufariki.
Maalim Aeif ndiye aliyeiba nyaraka za Jumbe na kumpelekea Mw. Nyerere kuonyesha mpango wq Jumbe kudai serikali tatu lakini baadae aligeuka na kujifanya anataka serikali tatu kwa wasiomjua Seif alikuwa mtu mjanjamjanja
 
Naona vitabu imekuwa dili sasa... mbaya zaidi vimekuwa kama vya kufanana fulani hivi


Andy Chande
Reginald Mengi
Benjamin Mkapa
Alli Mwinyi
...nk
 
Back
Top Bottom