Uchambuzi: Kama Urais Ungekuwa Wa Miaka Miwili..

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Niliandika makala mara ile Rais John Pombe Magufuli alipotimiza Mwaka Mmoja akiwa madarakani.

Itakumbukwa, mwaka jana, na kwenye siku yake ya kuzaliwa, Rais wa Awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli aliacha kula keki yake ya kusheherekea siku yake hiyo na kuamua kuwa kazini.

Zikatujia taarifa kubwa mbili katika siku hiyo; utenguzi wa uteuzi wa DCI na ziara ya kushtukiza wizara ya Maliasili na Utalii.

Niliandika, kuwa nataka niwe mkweli kwa nafsi yangu, kuwa hata kama tungekuwa, kama nchi, na utaratibu wa kuwa na Rais wa kipindi cha mwaka mmoja, basi, huyu tuliye naye sasa, John Pombe Magufuli, angekuwa amemaliza muda wake wa mwaka mmoja akiwa ameacha alama nyuma yake. Alama za kudumu muda mrefu.

Nikasema, kuwa ukweli nchi yetu imeanza kubadilika na fikra za watu wake pia zimeanza kubadilika. Maana, ilifika mahali, kuna walioacha kazi kwenye NGO- Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwenda kufanya kazi Serikalini ikiwamo kwenye Halmashauri zetu wakitamka wazi kuwa kwenye NGO kazi ni nyingi, wanarudi Serikalini na kwenye Halmashauri kupumzika na kula posho za safari na nyinginezo.

Nchi haiwezi kusonga mbele ikiwa na watu wenye mitazamo kama hiyo. Ni lazima kuwe na nidhamu ya utendaji kazi na kuheshimu sheria, kanuni na taratibu. Na wenye kukiuka hayo, ni lazima wajue kuna adhabu yenye kuendana na matendo yao maovu. Ndiyo siri kubwa ya nchi za wenzetu zilizoendelea.

Novemba 30, 2015 niliandika kwenye jarida la Raia Mwema, kuwa Magufuli ana uwezo wa kumwona bata na sungura kwa wakati mmoja.

Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana. Hivyo, inahusu uwezo wa kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti.
Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti.

Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.

Captain Thomas Sankara, kiongozi mwanapinduzi aliyeuawa wa Burkina Faso, katika wakati wake, alizungumzia umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya kale.

Sankara aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani. Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.

Sankara alipata kukaririwa akisema: “Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi.

Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali. Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao.” (Hayati, Kapteni Thomas Sankara)

Yumkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni Magufuli's paradigm shift'. Hali ya kuwa na mabadiliko ya msingi.

Nimeona nini kwa Rais Magufuli baada ya miaka miwili?

Kama Urais ungelikuwa wa miaka miwili, basi, Rais tuliye naye, Dr John Pombe Magufuli, angeondoka akiwa ameacha alama chanya za kudumu milele.

Maana, akiingia mwaka wake wa pili, ninachoona ni upepo chanya wa Magufuli wenye kuendelea kuvuma, ndani na nje ya mipaka.

Huo ndio ukweli mwingine ningependa kuusema. Nimepata bahati ya kusafiri sehemu mbali mbali za nchi. Nimekuwa na mazoea ya kuzungumza na waananchi kupata mitazamo yao.
Mahali pengi kabisa, John Magufuli yumo kwenye midomo ya Watanzania wa kawaida walio wengi ikiwamo vijana ma-bayaye wanaoongezeka kwenye miji yetu.

Kwanini?

Naamini, John Magufuli amefaulu kufanya kile watangulizi wake hawakufaulu, ukimwacha Mwalimu. Magufuli sio tu amebeba ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi, Magufuli anaifanyia kazi ajenda hiyo na watu wanaona ikifanyiwa kazi.

Ni kwa kiwango kile ambacho Hayati Sokoine alikuwa anakwenda nacho na akawa kipenzi cha umma.

Nimeandika huko nyuma, kuwa kero nambari moja kwa Watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita ilikuwa Rushwa na Ufisadi, kero nambari mbili ilikuwa Rushwa na Ufisadi, na kero nambari tatu ni Rushwa na Ufisadi. Hivyo, hiyo ndio ilikuwa ajenda kuu.

Huko nyuma upinzani, tofauti na CCM, ndio ulibeba ajenda hiyo, wakaipoteza njiani, sasa upinzani unahangaika kutafuta ilichokuwa nacho.

Ndio maana, tofauti na huko nyuma, maeneo mengi nilimopita, huwezi sasa kuona tofauti za wananchi za kiitikadi, wote wanajadili ajenda moja, ya kupiga vita ufisadi na hali zote zenye kurudisha nyuma maendeleo yao. Wanamuunga mkono Rais John Magufuli. Hao ni Wana CCM na Wana- Chadema.

Jipya jingine ndani ya miaka hii miwili ni kitendo cha Rais Magufuli kuruhusu wananchi kutoa kero zao hadharani kwa kuandika kwenye mabango. Hali hii inaongeza uwajibikaji na kuwatia kiwewe viongozi warasimu na wenye kuwanyanyasa wananchi. Hawa huko nyuma walijificha kwenye risala kwa Rais ambayo ilikuwa na maana ya kumsomea Rais taarifa ya kumfurahisha na wananchi hawakuwa na pa kumsomea Rais risala inayotokana na wao wananchi. Siku hizi inawezekana kupitia mabango.

Wananchi wanamuunga mkono pia Rais Magufuli kwa nia yake ya dhati ya kusimamia rasilimali za taifa hata kuwa tayari kugombana na matajiri wamiliki wa makampuni makubwa ya uchimbaji madini.

Haijawahi kutokea wala kufikiriwa , kuwa, kama nchi, tungeweza kutunisha misuli na kufanikiwa kushinda kwenye meza ya majadiliano, kwenye kudai kipande kikubwa cha keki kwa maana ya kinachopatikana kutokana na uchimbaji wa madini yetu. Vita hivi vya kupigania rasilimali zetu. Vita hivi anavyoviongoza Rais John Magufuli vimemsogeza karibu zaidi kwenye mioyo ya wananchi ambao huko nyuma walianza kukata tamaa.

Kimataifa, Rais John Magufuli ametolewa mfano wa kuwa kiongozi mwenye kusimamia uwajibikaji. Nimepata kuongea na maafisa wawili waandamizi wa Balozi za Kimagharibi walioniambia wazi kuwa Rais Magufuli anafanya vema sana kwenye eneo la uwajibikaji na kukuza uchumi.

Mwingine akafikia kuniambia kuwa, haijawahi kutokea kwa Serikali ya Tanzania kurudisha fedha za misaada ambazo hazikutumika au zimepotea kutokana na ufisadi. Ndani ya miaka hii miwili, kwa mshangao wa afisa yule wa Ubalozi niliyeongea nae, ameniambia kuwa Balozi yao imepokea fedha ambazo Tanzania ilikuwa inadaiwa irudishe.

Nini tafsiri ya jambo hilo?

Kwa mujibu wa afisa yule wa Kibalozi, kubwa kabisa Serikali inayoongozwa na Magufuli sasa inaaminika na wahisani na mabenki yenye kukopesha. Kwamba kuna usimamizi na ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo. Kwamba sasa si rahisi fedha kuliwa na wajanja na kwamba zitafanya yale yenye kuwaletea wananchi maendeleo.

Nini siri kubwa ya hatua hii mpya? Nilimwuliza afisa yule wa Ubalozi;

" Ukiwa na Rais aliye juu na anayesimamia kwa vitendo yale yanayotakiwa kufanyika, basi, huku chini watendaji hubadilika haraka na kufanya kilicho sahihi na hata kuwa na hofu ya kufanya ufisadi." Alianiambia afisa yule wa Ubalozi.

Nini faida na hatari ya mafanikio haya ya Rais Magufuli ?

Kwa nchi, hii ni fursa pekee ya kuungana na kumkabili adui aliye mbele yetu na aliyetufikisha hapa tulipo. Waliotufikisha mahali ambapo akina mama na watoto wetu wakakosa dawa na huduma nyingine.

Wananchi wakakosa mabomba ya maji na mengineyo, huku wachache wakichota fedha za umma kwa rushwa na ufisadi.
Baada ya miaka hii miwili, hatusomi tena habari za ufisadi mkubwa ukifanyika kwenye halmashauri na kwengineko Serikalini.

Hatari ninayoiona mbele yetu ni pale tunapokuwa na Rais mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuongozi ndani ya Chama chake na Serikali. Rais anayekubalika na wananchi wengi.

Kwamba akitumia vema ushawishi huu, na kwa kutanguliza hekima na busara, nchi yetu itakuwa mfano katika bara hili, ikiwamo pia kuimarisha misingi ya kidemokrasia na utawala wa sheria.

Lakini, kama Rais mwenye haya, akaja akaota mapembe, basi, hapo itabaki kuomba majaaliwa ya maanani.

Maggid Mjengwa.
 
Attachments

  • 02.jpg
    02.jpg
    7.7 KB · Views: 21
  • 04.jpg
    04.jpg
    30.4 KB · Views: 29
Naheshimu mawazo yako.Ni haki yako.
Naomba ukumbuke kuwa wengi:
Wameondolewa kazini kinyume cha sheria,taratibu.Wanahangaika bila mfariji!

Masikini waliojinyima kupata " makazi" wamebomolewa kwa kisingizio cha "sheria". Waulize wa Dar,( ambao hawakumpigia kura)! Leo watasimulia kipi?

Watumishi wa umma wana habari yake.Hata wale wa Uhuru sidhani kama aliwafuta "machozi" kikamilifu.

Biashara haziendi.Sote ni mashuhuda na haihitaji msemaji wa Ikulu atengeneze " mkorogo" wa kutengeneza image nzuri.

Deni la nchi linafurika pomoni. Ukuaji wa uchumi na ukuaji wake vina uhusiano?

Siasa sisemi,kwani kuitwa " mchochezi" imekuwa rahisi kama kupiga chafya. Ukijizuia utaumia mbavu bure.

Mfano upo wapi wa kumfanya awe wa pekee? Siyo siri mie namwona upande wa pili wa shilingi.
 
Ndugu zangu,

Niliandika makala mara ile Rais John Pombe Magufuli alipotimiza Mwaka Mmoja akiwa madarakani.

Itakumbukwa, mwaka jana, na kwenye siku yake ya kuzaliwa, Rais wa Awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli aliacha kula keki yake ya kusheherekea siku yake hiyo na kuamua kuwa kazini.

Zikatujia taarifa kubwa mbili katika siku hiyo; utenguzi wa uteuzi wa DCI na ziara ya kushtukiza wizara ya Maliasili na Utalii.

Niliandika, kuwa nataka niwe mkweli kwa nafsi yangu, kuwa hata kama tungekuwa, kama nchi, na utaratibu wa kuwa na Rais wa kipindi cha mwaka mmoja, basi, huyu tuliye naye sasa, John Pombe Magufuli, angekuwa amemaliza muda wake wa mwaka mmoja akiwa ameacha alama nyuma yake. Alama za kudumu muda mrefu.

Nikasema, kuwa ukweli nchi yetu imeanza kubadilika na fikra za watu wake pia zimeanza kubadilika. Maana, ilifika mahali, kuna walioacha kazi kwenye NGO- Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwenda kufanya kazi Serikalini ikiwamo kwenye Halmashauri zetu wakitamka wazi kuwa kwenye NGO kazi ni nyingi, wanarudi Serikalini na kwenye Halmashauri kupumzika na kula posho za safari na nyinginezo.

Nchi haiwezi kusonga mbele ikiwa na watu wenye mitazamo kama hiyo. Ni lazima kuwe na nidhamu ya utendaji kazi na kuheshimu sheria, kanuni na taratibu. Na wenye kukiuka hayo, ni lazima wajue kuna adhabu yenye kuendana na matendo yao maovu. Ndiyo siri kubwa ya nchi za wenzetu zilizoendelea.

Novemba 30, 2015 niliandika kwenye jarida la Raia Mwema, kuwa Magufuli ana uwezo wa kumwona bata na sungura kwa wakati mmoja.

Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana. Hivyo, inahusu uwezo wa kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti.
Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti.

Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.

Captain Thomas Sankara, kiongozi mwanapinduzi aliyeuawa wa Burkina Faso, katika wakati wake, alizungumzia umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya kale.

Sankara aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani. Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.

Sankara alipata kukaririwa akisema: “Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi.

Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali. Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao.” (Hayati, Kapteni Thomas Sankara)

Yumkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni Magufuli's paradigm shift'. Hali ya kuwa na mabadiliko ya msingi.

Nimeona nini kwa Rais Magufuli baada ya miaka miwili?

Kama Urais ungelikuwa wa miaka miwili, basi, Rais tuliye naye, Dr John Pombe Magufuli, angeondoka akiwa ameacha alama chanya za kudumu milele.

Maana, akiingia mwaka wake wa pili, ninachoona ni upepo chanya wa Magufuli wenye kuendelea kuvuma, ndani na nje ya mipaka.

Huo ndio ukweli mwingine ningependa kuusema. Nimepata bahati ya kusafiri sehemu mbali mbali za nchi. Nimekuwa na mazoea ya kuzungumza na waananchi kupata mitazamo yao.
Mahali pengi kabisa, John Magufuli yumo kwenye midomo ya Watanzania wa kawaida walio wengi ikiwamo vijana ma-bayaye wanaoongezeka kwenye miji yetu.

Kwanini?

Naamini, John Magufuli amefaulu kufanya kile watangulizi wake hawakufaulu, ukimwacha Mwalimu. Magufuli sio tu amebeba ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi, Magufuli anaifanyia kazi ajenda hiyo na watu wanaona ikifanyiwa kazi.

Ni kwa kiwango kile ambacho Hayati Sokoine alikuwa anakwenda nacho na akawa kipenzi cha umma.

Nimeandika huko nyuma, kuwa kero nambari moja kwa Watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita ilikuwa Rushwa na Ufisadi, kero nambari mbili ilikuwa Rushwa na Ufisadi, na kero nambari tatu ni Rushwa na Ufisadi. Hivyo, hiyo ndio ilikuwa ajenda kuu.

Huko nyuma upinzani, tofauti na CCM, ndio ulibeba ajenda hiyo, wakaipoteza njiani, sasa upinzani unahangaika kutafuta ilichokuwa nacho.

Ndio maana, tofauti na huko nyuma, maeneo mengi nilimopita, huwezi sasa kuona tofauti za wananchi za kiitikadi, wote wanajadili ajenda moja, ya kupiga vita ufisadi na hali zote zenye kurudisha nyuma maendeleo yao. Wanamuunga mkono Rais John Magufuli. Hao ni Wana CCM na Wana- Chadema.

Jipya jingine ndani ya miaka hii miwili ni kitendo cha Rais Magufuli kuruhusu wananchi kutoa kero zao hadharani kwa kuandika kwenye mabango. Hali hii inaongeza uwajibikaji na kuwatia kiwewe viongozi warasimu na wenye kuwanyanyasa wananchi. Hawa huko nyuma walijificha kwenye risala kwa Rais ambayo ilikuwa na maana ya kumsomea Rais taarifa ya kumfurahisha na wananchi hawakuwa na pa kumsomea Rais risala inayotokana na wao wananchi. Siku hizi inawezekana kupitia mabango.

Wananchi wanamuunga mkono pia Rais Magufuli kwa nia yake ya dhati ya kusimamia rasilimali za taifa hata kuwa tayari kugombana na matajiri wamiliki wa makampuni makubwa ya uchimbaji madini.

Haijawahi kutokea wala kufikiriwa , kuwa, kama nchi, tungeweza kutunisha misuli na kufanikiwa kushinda kwenye meza ya majadiliano, kwenye kudai kipande kikubwa cha keki kwa maana ya kinachopatikana kutokana na uchimbaji wa madini yetu. Vita hivi vya kupigania rasilimali zetu. Vita hivi anavyoviongoza Rais John Magufuli vimemsogeza karibu zaidi kwenye mioyo ya wananchi ambao huko nyuma walianza kukata tamaa.

Kimataifa, Rais John Magufuli ametolewa mfano wa kuwa kiongozi mwenye kusimamia uwajibikaji. Nimepata kuongea na maafisa wawili waandamizi wa Balozi za Kimagharibi walioniambia wazi kuwa Rais Magufuli anafanya vema sana kwenye eneo la uwajibikaji na kukuza uchumi.

Mwingine akafikia kuniambia kuwa, haijawahi kutokea kwa Serikali ya Tanzania kurudisha fedha za misaada ambazo hazikutumika au zimepotea kutokana na ufisadi. Ndani ya miaka hii miwili, kwa mshangao wa afisa yule wa Ubalozi niliyeongea nae, ameniambia kuwa Balozi yao imepokea fedha ambazo Tanzania ilikuwa inadaiwa irudishe.

Nini tafsiri ya jambo hilo?

Kwa mujibu wa afisa yule wa Kibalozi, kubwa kabisa Serikali inayoongozwa na Magufuli sasa inaaminika na wahisani na mabenki yenye kukopesha. Kwamba kuna usimamizi na ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo. Kwamba sasa si rahisi fedha kuliwa na wajanja na kwamba zitafanya yale yenye kuwaletea wananchi maendeleo.

Nini siri kubwa ya hatua hii mpya? Nilimwuliza afisa yule wa Ubalozi;

" Ukiwa na Rais aliye juu na anayesimamia kwa vitendo yale yanayotakiwa kufanyika, basi, huku chini watendaji hubadilika haraka na kufanya kilicho sahihi na hata kuwa na hofu ya kufanya ufisadi." Alianiambia afisa yule wa Ubalozi.

Nini faida na hatari ya mafanikio haya ya Rais Magufuli ?

Kwa nchi, hii ni fursa pekee ya kuungana na kumkabili adui aliye mbele yetu na aliyetufikisha hapa tulipo. Waliotufikisha mahali ambapo akina mama na watoto wetu wakakosa dawa na huduma nyingine.

Wananchi wakakosa mabomba ya maji na mengineyo, huku wachache wakichota fedha za umma kwa rushwa na ufisadi.
Baada ya miaka hii miwili, hatusomi tena habari za ufisadi mkubwa ukifanyika kwenye halmashauri na kwengineko Serikalini.

Hatari ninayoiona mbele yetu ni pale tunapokuwa na Rais mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuongozi ndani ya Chama chake na Serikali. Rais anayekubalika na wananchi wengi.

Kwamba akitumia vema ushawishi huu, na kwa kutanguliza hekima na busara, nchi yetu itakuwa mfano katika bara hili, ikiwamo pia kuimarisha misingi ya kidemokrasia na utawala wa sheria.

Lakini, kama Rais mwenye haya, akaja akaota mapembe, basi, hapo itabaki kuomba majaaliwa ya maanani.

Maggid Mjengwa.
Hayo mapambio marefu sana uliyompamba Mkulu peleka Lumumba ambako yatapokelewa kwa nderemo na vifijo na wanalumumba wenzio!
 
Umefikiri kidogo sana, kama ni utafiti basi umeufanyia moyoni mwako, vinginevyo basi wewe ni wale wanaoitwa diaspora, sio mkazi wa.kudumu wa nchi hii. Kama sivyo basi huenda umejiunga kwenye kile kikundi cha jerry muro. Sihitaji kutoa hoja kwa nini sikubaliani na wewe maana naamini hata hiki ulichoandika umekiandika ukiwa chini ya shinikizo la moyo wako ( u-mimi). Hujaangalia maslahi ya wengine yalivyodhulumiwa chini ya utawala huu.mfano nenda kwenye familia zilizovunjiwa nyumba zao (licha ya zuio la mahakama) uwasomee hili andiko lako halafu usikilize sauti za mwitikio wao. Utakimbia.

Anyway, acha tuheshimu Uhuru wako wa kutoa maoni, mtazamo na hisia zako, japo hii nayo imebaki kuwa haki ya wateule tu.

Ingekuwa heri kama huyu kiongozi wetu ndo angekuwa madarakani kipindi nchi inaenda vitani dhidi ya Idd Amini wa Uganda miaka ya 70. Huenda tusingepigana vita ile kabisa kwa sababu nahisi yeye na mwenzake wa Uganda wangekuwa friends.

Ila pia tuache mapenzi ya Mungu yatimizwe. Tunawajibika kuwaheshimu na kuwaombea viongo wetu hata kama tunachukia matendo yao. Kama unataka kuishi vizuri lazima uheshimu viongozi na sheria za nchi.
 
Nimesoma parapraph ya kwanza tu

Hakuna rais ambae hajaaha alama keep this in mind.
 
Ww maggid naomba nikuite mnafiki wa kutupwa, hujawahi kuandika makala yoyote ya kumkosoa rais aliyeko madarakani, na ulichofanya hapa ni muendelezo huohuo wa unafiki wako. Sio vibaya ulichofanya kwa utawala wa awamu hii unapenda kusifiwa kama ulivyofanya. Kwa hiyo nakushauri japo najua ww ni mnafiki lakini shikilia hapohapo utatoka.
 
Ukuu wa wilaya nini??
 
Rubbish!
Hivi kwa nini kuna idiots wengi hivi?
Maggid huwezi kumfananisha Mwalimu na huyu mtu please spare your s
Ufisadi ufisadi ni nani aliyepelekwa mahakamani mpaka sasa acheni kutuona Watanzania hatuna akili au hatuoni. Uandishi wa habari msijifanye mnajua kila kitu. Shame on you yes I dare to say shame on you
Dhuluma ukiukwaji wa haki za binadamu awamu hii imevunja rekodi Leo unaandika kumsifia nani vileeee eti waliomtangulia hawakuthubutu. Ubutu wa mawazo yenu ndio unatufikisha huku.
GIVE US A BREAK pleaseeeeee kha!
 
Umefikiri kidogo sana, kama ni utafiti basi umeufanyia moyoni mwako, vinginevyo basi wewe ni wale wanaoitwa diaspora, sio mkazi wa.kudumu wa nchi hii. Kama sivyo basi huenda umejiunga kwenye kile kikundi cha jerry muro. Sihitaji kutoa hoja kwa nini sikubaliani na wewe maana naamini hata hiki ulichoandika umekiandika ukiwa chini ya shinikizo la moyo wako ( u-mimi). Hujaangalia maslahi ya wengine yalivyodhulumiwa chini ya utawala huu.mfano nenda kwenye familia zilizovunjiwa nyumba zao (licha ya zuio la mahakama) uwasomee hili andiko lako halafu usikilize sauti za mwitikio wao. Utakimbia.

Anyway, acha tuheshimu Uhuru wako wa kutoa maoni, mtazamo na hisia zako, japo hii nayo imebaki kuwa haki ya wateule tu.

Ingekuwa heri kama huyu kiongozi wetu ndo angekuwa madarakani kipindi nchi inaenda vitani dhidi ya Idd Amini wa Uganda miaka ya 70. Huenda tusingepigana vita ile kabisa kwa sababu nahisi yeye na mwenzake wa Uganda wangekuwa friends.

Ila pia tuache mapenzi ya Mungu yatimizwe. Tunawajibika kuwaheshimu na kuwaombea viongo wetu hata kama tunachukia matendo yao. Kama unataka kuishi vizuri lazima uheshimu viongozi na sheria za nchi.
Busara na hekima ni kitu cha kipekee sana, katika unadishi wako ulikuwa na uwezo wa kutamka vinginevyo juu ya uzi wa huyo ndugu ..lakini hakika nimependa busara yako na hekina katika aya tatu za mwisho kwenye maoni yako,umenena vema sana..Subira yavuta heri na kila jambo lina mwisho.
 
Mbona umesifia tu, onyesha basi na mapungufu!! au mwenzetu hali yako ni nzuri?

Mbona sisi tuko hoi tabani au mwenzetu uko nje ya nchi?
 
Ni kweli kuwa Magufuli ameacha alama isiyofutika! Alama ya kuhalalisha mpinzani wake mkubwa anayekosoa mwenendo wake apigwe risasi na vyombo vyake vya dola. Ameacha alama kuwa yeye ni dikteta mkabila mbaguzi asiyependa watu wa kada fulani na hata ingekuwa uwezo wake basi angeamuru wafutike.
 
Ndugu zangu,

Niliandika makala mara ile Rais John Pombe Magufuli alipotimiza Mwaka Mmoja akiwa madarakani.

Itakumbukwa, mwaka jana, na kwenye siku yake ya kuzaliwa, Rais wa Awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli aliacha kula keki yake ya kusheherekea siku yake hiyo na kuamua kuwa kazini.

Zikatujia taarifa kubwa mbili katika siku hiyo; utenguzi wa uteuzi wa DCI na ziara ya kushtukiza wizara ya Maliasili na Utalii.

Niliandika, kuwa nataka niwe mkweli kwa nafsi yangu, kuwa hata kama tungekuwa, kama nchi, na utaratibu wa kuwa na Rais wa kipindi cha mwaka mmoja, basi, huyu tuliye naye sasa, John Pombe Magufuli, angekuwa amemaliza muda wake wa mwaka mmoja akiwa ameacha alama nyuma yake. Alama za kudumu muda mrefu.

Nikasema, kuwa ukweli nchi yetu imeanza kubadilika na fikra za watu wake pia zimeanza kubadilika. Maana, ilifika mahali, kuna walioacha kazi kwenye NGO- Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwenda kufanya kazi Serikalini ikiwamo kwenye Halmashauri zetu wakitamka wazi kuwa kwenye NGO kazi ni nyingi, wanarudi Serikalini na kwenye Halmashauri kupumzika na kula posho za safari na nyinginezo.

Nchi haiwezi kusonga mbele ikiwa na watu wenye mitazamo kama hiyo. Ni lazima kuwe na nidhamu ya utendaji kazi na kuheshimu sheria, kanuni na taratibu. Na wenye kukiuka hayo, ni lazima wajue kuna adhabu yenye kuendana na matendo yao maovu. Ndiyo siri kubwa ya nchi za wenzetu zilizoendelea.

Novemba 30, 2015 niliandika kwenye jarida la Raia Mwema, kuwa Magufuli ana uwezo wa kumwona bata na sungura kwa wakati mmoja.

Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana. Hivyo, inahusu uwezo wa kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti.
Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti.

Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.

Captain Thomas Sankara, kiongozi mwanapinduzi aliyeuawa wa Burkina Faso, katika wakati wake, alizungumzia umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya kale.

Sankara aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani. Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.

Sankara alipata kukaririwa akisema: “Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi.

Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali. Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao.” (Hayati, Kapteni Thomas Sankara)

Yumkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni Magufuli's paradigm shift'. Hali ya kuwa na mabadiliko ya msingi.

Nimeona nini kwa Rais Magufuli baada ya miaka miwili?

Kama Urais ungelikuwa wa miaka miwili, basi, Rais tuliye naye, Dr John Pombe Magufuli, angeondoka akiwa ameacha alama chanya za kudumu milele.

Maana, akiingia mwaka wake wa pili, ninachoona ni upepo chanya wa Magufuli wenye kuendelea kuvuma, ndani na nje ya mipaka.

Huo ndio ukweli mwingine ningependa kuusema. Nimepata bahati ya kusafiri sehemu mbali mbali za nchi. Nimekuwa na mazoea ya kuzungumza na waananchi kupata mitazamo yao.
Mahali pengi kabisa, John Magufuli yumo kwenye midomo ya Watanzania wa kawaida walio wengi ikiwamo vijana ma-bayaye wanaoongezeka kwenye miji yetu.

Kwanini?

Naamini, John Magufuli amefaulu kufanya kile watangulizi wake hawakufaulu, ukimwacha Mwalimu. Magufuli sio tu amebeba ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi, Magufuli anaifanyia kazi ajenda hiyo na watu wanaona ikifanyiwa kazi.

Ni kwa kiwango kile ambacho Hayati Sokoine alikuwa anakwenda nacho na akawa kipenzi cha umma.

Nimeandika huko nyuma, kuwa kero nambari moja kwa Watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita ilikuwa Rushwa na Ufisadi, kero nambari mbili ilikuwa Rushwa na Ufisadi, na kero nambari tatu ni Rushwa na Ufisadi. Hivyo, hiyo ndio ilikuwa ajenda kuu.

Huko nyuma upinzani, tofauti na CCM, ndio ulibeba ajenda hiyo, wakaipoteza njiani, sasa upinzani unahangaika kutafuta ilichokuwa nacho.

Ndio maana, tofauti na huko nyuma, maeneo mengi nilimopita, huwezi sasa kuona tofauti za wananchi za kiitikadi, wote wanajadili ajenda moja, ya kupiga vita ufisadi na hali zote zenye kurudisha nyuma maendeleo yao. Wanamuunga mkono Rais John Magufuli. Hao ni Wana CCM na Wana- Chadema.

Jipya jingine ndani ya miaka hii miwili ni kitendo cha Rais Magufuli kuruhusu wananchi kutoa kero zao hadharani kwa kuandika kwenye mabango. Hali hii inaongeza uwajibikaji na kuwatia kiwewe viongozi warasimu na wenye kuwanyanyasa wananchi. Hawa huko nyuma walijificha kwenye risala kwa Rais ambayo ilikuwa na maana ya kumsomea Rais taarifa ya kumfurahisha na wananchi hawakuwa na pa kumsomea Rais risala inayotokana na wao wananchi. Siku hizi inawezekana kupitia mabango.

Wananchi wanamuunga mkono pia Rais Magufuli kwa nia yake ya dhati ya kusimamia rasilimali za taifa hata kuwa tayari kugombana na matajiri wamiliki wa makampuni makubwa ya uchimbaji madini.

Haijawahi kutokea wala kufikiriwa , kuwa, kama nchi, tungeweza kutunisha misuli na kufanikiwa kushinda kwenye meza ya majadiliano, kwenye kudai kipande kikubwa cha keki kwa maana ya kinachopatikana kutokana na uchimbaji wa madini yetu. Vita hivi vya kupigania rasilimali zetu. Vita hivi anavyoviongoza Rais John Magufuli vimemsogeza karibu zaidi kwenye mioyo ya wananchi ambao huko nyuma walianza kukata tamaa.

Kimataifa, Rais John Magufuli ametolewa mfano wa kuwa kiongozi mwenye kusimamia uwajibikaji. Nimepata kuongea na maafisa wawili waandamizi wa Balozi za Kimagharibi walioniambia wazi kuwa Rais Magufuli anafanya vema sana kwenye eneo la uwajibikaji na kukuza uchumi.

Mwingine akafikia kuniambia kuwa, haijawahi kutokea kwa Serikali ya Tanzania kurudisha fedha za misaada ambazo hazikutumika au zimepotea kutokana na ufisadi. Ndani ya miaka hii miwili, kwa mshangao wa afisa yule wa Ubalozi niliyeongea nae, ameniambia kuwa Balozi yao imepokea fedha ambazo Tanzania ilikuwa inadaiwa irudishe.

Nini tafsiri ya jambo hilo?

Kwa mujibu wa afisa yule wa Kibalozi, kubwa kabisa Serikali inayoongozwa na Magufuli sasa inaaminika na wahisani na mabenki yenye kukopesha. Kwamba kuna usimamizi na ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo. Kwamba sasa si rahisi fedha kuliwa na wajanja na kwamba zitafanya yale yenye kuwaletea wananchi maendeleo.

Nini siri kubwa ya hatua hii mpya? Nilimwuliza afisa yule wa Ubalozi;

" Ukiwa na Rais aliye juu na anayesimamia kwa vitendo yale yanayotakiwa kufanyika, basi, huku chini watendaji hubadilika haraka na kufanya kilicho sahihi na hata kuwa na hofu ya kufanya ufisadi." Alianiambia afisa yule wa Ubalozi.

Nini faida na hatari ya mafanikio haya ya Rais Magufuli ?

Kwa nchi, hii ni fursa pekee ya kuungana na kumkabili adui aliye mbele yetu na aliyetufikisha hapa tulipo. Waliotufikisha mahali ambapo akina mama na watoto wetu wakakosa dawa na huduma nyingine.

Wananchi wakakosa mabomba ya maji na mengineyo, huku wachache wakichota fedha za umma kwa rushwa na ufisadi.
Baada ya miaka hii miwili, hatusomi tena habari za ufisadi mkubwa ukifanyika kwenye halmashauri na kwengineko Serikalini.

Hatari ninayoiona mbele yetu ni pale tunapokuwa na Rais mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuongozi ndani ya Chama chake na Serikali. Rais anayekubalika na wananchi wengi.

Kwamba akitumia vema ushawishi huu, na kwa kutanguliza hekima na busara, nchi yetu itakuwa mfano katika bara hili, ikiwamo pia kuimarisha misingi ya kidemokrasia na utawala wa sheria.

Lakini, kama Rais mwenye haya, akaja akaota mapembe, basi, hapo itabaki kuomba majaaliwa ya maanani.

Maggid Mjengwa.
Waandishi wa habari uchwara mnajitahidi kujikomba ili kufikiriwa ktk teuzi zake. Hakuna mchambuzi makini anayeweza kuchambua upngozi wa pombe akashindwa kugusia ukandamizaji wa demokrasia, haki za binadamu, Uhuru wa kujieleza na ukabila anaoupalilia.

Usinheshindwa pia kugusia wapinzani wake kupotea bila Maelezo, kutekwa na matumizi ya mitutu kujibu hoja.
 
Ukuu wa wilaya nini??

Ndugu yangu Babuu,

Kama ningelikuwa naandika ili niwe DC basi leo ningekuwa nakaribia kustaafu. Mimi hata ningeteuliwa U-DC leo ningemshukuru aliyeniteua na kumwomba ampe nafasi yangu mtu mwingine. Kazi ninazofanya ni zaidi ya wigo wa Mkuu wa Wilaya, na nitapenda niendelee nazo.
Maggid.
 
Mkuu hongera kwa makala ndefu sana, hakika wewe ni mwandishi mkongwe unayesoma alama za nyakati. Umeona kilichowatokea raia mwema, mawio na wengne, umeamua kuwalamba miguu wakubwa ili uendelee kusavaivu.
Hakika hii inaitwa strago fo ekzisteñsi
 
Ndugu yangu Babuu,

Kama ningelikuwa naandika ili niwe DC basi leo ningekuwa nakaribia kustaafu. Mimi hata ningeteuliwa U-DC leo ningemshukuru aliyeniteua na kumwomba ampe nafasi yangu mtu mwingine. Kazi ninazofanya ni zaidi ya wigo wa Mkuu wa Wilaya, na nitapenda niendelee nazo.
Maggid.
sawa ndugu Majid una nafasi nzuri kuliko DC, ktk maandiko yako haya hukuona chochote cha kukosoa kama kuzuia mikutano,kuzuia bunge live,bomoabomoa kinyume na mahakama, viroba vyenye miili ya ndugu zetu lbd serikali haihusiki lkn ina wajibu wa kulinda raia na mali zao,na mambo kama hayo au unajiunga na je murro ktk kupambania mkate,madaraka mazuri acha bwn.
 
Back
Top Bottom