Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,849
2,000
Amani iwe nanyi Wadau.

kama wote mnavyojua leo ndo siku ile ambayo watanzania kwa pamoja wameweza kushuhudia hotuba ya kwanza kutoka kwa gwiji la upinzani, ndugu Tundu Antipas Lissu. Hotuba iliyokuwa imejaa utulivu, akili, busara na hekima iliyotukuka.

Kama kawaida CCM walipanga yao, kwanza walipanga vijana wao kushambulia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook na Youtube ili tu kujaribu kuonesha umma na dunia kuwa Lissu hakubaliki ila kiukweli Lissu kwa hotuba ya leo ameonesha kuwa amejiandaa vizuri na amejipanga vizuri kuwa Raisi wa Tanzania mwaka 2020.

Lissu ameweza kuelezea kwa kifupi na kueleweka sana hoja zote zilizotikisa kwenye miaka hii Mitano ambazo sio tu Chadema ila hadi CCM na watanzania kwa ujumla zimewagusa sana.

Hakuna ambae hajui kuwa wafanyabiashara wakubwa na wakati wamenyanyaswa sana kwenye kipindi hiki cha miaka Mitano, kwenye hili Lissu kapiga mulemule, hakuna ambayo hajui kuwa awamu ya tano imeharibu sana kwenye uchumi, kilimo na diplomasia, kwenye haya tena Lissu kapiga mulemule.

Alipomaliza Lissu ni pale alipoelezea kwa jinsi gani suala la kuonea watu na kukiuka katiba limekuwa linaumiza watu na hapa tena Lissu amepiga mulemule.

Mwisho kuonesha jinsi gani amekomaa, pamoja na kupigwa risasi 16 amesema amesamehe na hatolipa kisasa. Hapa Lissu kawa sawa na Mandela aliyewasamehe makabulu na Papa John Paul 2 aliye msamehe kijana aliyempiga risasi. Lissu ameonesha amekomaa sio tu kiuongozi ila hata kihekima na busara.

Hotuba ya leo ya Lissu imegusia mambo mengi ikiwemo kurekebisha mfumo wa sheria na vyombo vya ulinzi na usalama ili vifanye kazi kwa weredi. Lissu kusema kweli kumaliza yote.

Ukweli lazima tuseme , Ingawa vyombo vya Habari vya Tanzania ikiwemo Azam , ITV na vingine vikubwa kuogopa hata kurusha Habari ya Lissu kutangaza nia leo. Ila hotuba yale imesikika na imewasisimua watu wengi nikiwemo mie. CCM wametumia mbinu ya kuvitisha vyombo hivi kwa makusudi ila Naona nguvu ya Lissu ni kubwa sana kuliko hujuma dhidi yake.

Itoshe kusema Lissu amethibitisha kuwa anatosha akiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020

Kura yangu anayo akipitishwa na Chadema.

Ushauri kwa Chadema. Isambazeni video ya leo ya Lissu kwenye mitandao mbalimbali kuanzia Insta, Facebook, Twitter na Whatsup’ watu wengi waione maana mkitegemea vyombo vya Habari vya Tanzania vilivyobanw na Ccm mtapoteza.

Jioni Njema!
 

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,912
2,000
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
83,023
2,000
Hoja dhaifu sana ! maneno huumba , anayoyasema Lissu ndiyo atakayotenda , hivyo ndio ilivyo , Kwa mfano , Dr Magufuli amenukuliwa dunia nzima akiwaambia marafiki zake kabla ya kuwa Rais kwamba , nanukuu , " NIKIWA RAIS MTALIMIA MENO " mwisho wa kunukuu , je kwa sasa watu hawalimii meno ?
 

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,316
2,000
Nashangaa sana watu waliotishwa na kahutuba ka lisu, mtoto halali na hela, mwacheni tu ajitutumue ila ukweli anaujua mwenyewe na habari zake tunazo
 

dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
12,045
2,000
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Vipi aliepo sasa
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
56,864
2,000
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Kuna wakati Tundu Lissu alivyokuwa Marekani, alifanya mahojiano na Mtanzania anayeishi vitongoji vya Washington DC, Mubelwa Bandio.

Mahojiano yalirushwa Facebook live. Lissu akajieleza, ukaja wakati wa maswali na majibu.

Kuna jamaa mmoja akamuuliza, kuna wanasiasa wengi wanakuwa na maneno mazuri sana kabla hawajapata madaraka.Tunaelewa maneno yako, tunaelewa unavyopinga uzandiki na uonevu wa serikali, lakini je, tutajuaje kwamba ukipewa madaraka, na wewe hutatugeuka na kuwa miongoni mwa watawala wanaominya haki?

Lissu akajibu kuhusu mabadiliko ya kikatiba na kuwawezesha wananchi wenyewe kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa bubana viongozi.

Sikiliza kwenye hii video kuanzia 1:21

 

Mr Devil

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
3,745
2,000
Ikulu ina itaji waropokaji au sio..kama yule alie anza kutaja TITI na ujinga ujinga mwingne mbele ya watu wenye akili zao Et
 

Craig

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
993
1,000
Thubutuuu. Lisu anaisaidia tu CCM KUWA USHINDI wake ulikuwa na upinzani mkali. Na hivyo kuonekana kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na kikatiba.

Kama atakuwa Rais wa JMT Mimi nitajiua kwa kula sumu siyo kwa jiwe ninalolijua Mimi.
 

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,696
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom