OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,072
- 103,284
Uwanja wa ndege aliojenga Mobutu umegeuka kuwa uwanja wa popo na panya
Dikteta Mobutu aliamua kujenga Uwanja wa Gbadolite katika Jimbo la Nord-Ubangi, mwendo wa saa 5 na dakika 16 kutoka mji huo hadi kijijini Lisala (umbali wa 332km) alikozaliwa Mobutu mwenyewe, Gbadolite kilikuwa kijiji kidogo ndani ya msitu mnene chenye watu 1,500 tu, ambapo kwa maslahi yake ya kutaka umaarufu, akaubadili kuwa mji mkubwa akijenga hekalu lake kubwa, hoteli ya kitalii ya nyota tano iliyoitwa Motel Nzekele ambayo viongozi maarufu duniani kama Mfalme wa Ubelgiji, Rais wa Ufaransa Francois Mitterrand na Papa John Paul II walipata kulala.
Huku kwetu kunajengwa uwanja wa ndege wa kimataifa. Haijulikani kama uamuzi wa serikali ya Rais Magufuli umelenga maendeleo ama tu unataka kufanya jambo la kukumbukwa kwa kuanzisha ‘majiji’ mapya kama ilivyokuwa kwa Gbadolite (maarufu kama Versailles of the Jungle – yaani ‘Versailles ya Msituni’ wakifananisha na Hekalu la Versailles nchini Ufaransa).
Taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba, uwanja huo utakuwa na eneo la kurukia ndege (runaway) wenye urefu wa meta 3,000 (sawa na kilometa 3) na upana wa meta 45, ukiwa na tofauti ndogo na uwanja wa ndege wa Gbadolite (urefu kilometa 3.2 na upana meta 60) kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliojengwa na Dikteta Mobutu Sese Seko mwaka 1972 ili kuruhusu midege mikubwa ya Concorde kutua na kuruka.
Hoja inakuja je,kuna hitaji lolote la kujenga uwanja huo kwa sasa?
Katika kipindi ambacho uchumi wa taifa bado haujatengemaa, ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa ndege katika mji wa Chato wenye wakazi 17,508 tu (kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012) unaonekana ni uamuzi usiozingatia maslahi mapana ya taifa.
Hoja ya Mh. Sugu jana kwamba baada ya mda wa Magufuli kwisha nani ataenda kutua Chato? Ni hoja ya msingi sana
Nimelinganisha alichokifanya Mabutu miaka hiyo na kinachoendelea hivi sasa Chato ili kuleta picha ya hali itakavyokuwa mbeleni kwa mradi mkubwa kama ule.
Nini maoni yako?