Uchambuzi: Abramovich the billionaire from nowhere

Inawezekana Abramovich is a Russian spy, na alitengenezwa hivyo for a "secret mission", British government washamkosa kosa mara nyingi kumtimua, but still yupo under "surveillance". And it's true Putin anamtumia kwenye "mission" nyingi za serikali yake, the time will tell.
Inasemekana hata biashara anazoendesha nje ya nchi ni uwekezaj wa serikal
 
Inawezekana Abramovich is a Russian spy, na alitengenezwa hivyo for a "secret mission", British government washamkosa kosa mara nyingi kumtimua, but still yupo under "surveillance". And it's true Putin anamtumia kwenye "mission" nyingi za serikali yake, the time will tell.
British Government wamtimue kutoka wapi
 
Tena kwa asilimia 100,japo hana shule.Ni story ya kusisimua sana.Na alikataa madaraka yoyote ya kisiasa akataka apewe umiliki wa kampuni za uchimbaji gesi za Russia.

Yeye alitaka ufalme wa kiuchumi na si kisiasa.

Ni mtu ambaye Putin anamheshimu kuliko.Ni stori ndefu sana jinsi alovyoanza hadi kuwa na urafiki na binti wa rais wa Russia ili aweze kupata access ya kuweza kuwa karib na rais.Na mpaka akawa mshauri wa karibu anayeaminika wa Boris Yelstin,mshauri asiyetajwa popote.

Ni moja ya watu walioinjinia Borris Yelstin kujiuzulu na kabla ya hapo alishampendekeza Putin kuwa PM.Na utajiri wake ni wa jasho na damu.

Elewa tu si mtu wa mchezo mchezo.

Kwahiyo mkuu siku ukipata kuonana na Magu usimwombe UDC au cheo bali mwombe akuwezeshe hata uweze kumiliki kitalu cha Tanzanite au gesi upate ufalme wa pesa.
Walianzisha umoja unaoitwa "The family " ambapo mtoto wa Boris na yeye Abramovich na Boris mwenyewe ndo wali run Urusi ya wakati huo ..kuwepo kwa Putin leo ni mchango mkubwa sana wa Roman Abramovich..huyu jamaa ni mtu na nusu ..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana Abramovich is a Russian spy, na alitengenezwa hivyo for a "secret mission", British government washamkosa kosa mara nyingi kumtimua, but still yupo under "surveillance". And it's true Putin anamtumia kwenye "mission" nyingi za serikali yake, the time will tell.
Uingereza walishamshindwa chanzo cha ugomvi na serikali kama ile ni Kwamba jamaa aliingiza chaka moja ya kampuni kubwa ya uingereza na kuweza kuimiliki kisheria kabisa kitu ambacho waingereza waliona kama jamaa kawazidi akili ivyo wakaanza kumfanyia figisu lakini bado aliwapiga tena bao na kufanikiwa kununua timu ya Chelsea kwa ela ya mboga..
Huyu jamaa ni mfano wa kuigwa ni faita balaa

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE
Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER THREE
HITTING THE JACKPOT

Mwandishi anasema kuwa moja ya sifa kubwa ya Abramovich ni uwezo wake wa kutambua mtu sahihi kwa wakati sahihi na kufanya nae urafiki.Jamaa alikuwa zaidi ya mwanasaikolojia,ukichanganya na upole wake na utaalamu wa kupangilia maneno kulimfanya aaminike zaidi
Unaambiwa jamaa anajua jinsi ya kupangilia maneno yenye hoja na mvuto wa hali ya juu!
Baada ya kuchukua biashara ya mafuta na kufanikiwa sasa ilikuwa muda wa kuzama zaidi ndani ya mfumo wa utawala wa Urusi.Katika jitihada hizi alikutana na kijana Aven aliyekuwa mtaalam,ambaye alimfanya Abramovich kutoka kuwa milinionea mfanyabiashara wa mafuta na kumfanya kuwa bilionea na gwiji wa biashara na viwanda,Mtu mwingine muhimu ni Olgarch Boris Berezovsky (huyu walikuja kusalitiana vibaya)
Unaambiwa Abramovich ni mtu wa mahesabu makali kila hatua anayopiga ni hatua ya uhakika,hana papara wala upesi...anaweka shabaha kwanza ndipo anaachia mshale au risasi!
Sasa Boris alimshawishi Abramovich waingie ubia,wakati huo Boris alikua na miaka 40± na Abramovich alikuwa na miaka 20±lakini Boris aliona umuhimu wa Abramovich akaona amfanye awe mshirika wake.Hali ya Uchumi iliendelea kuwa mbaya kufikia serikali kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wake pamoja na pensheni! Boris ambaye alikuwa networker mzuri akatumia fursa vizuri,alikuwa tayari ni Olgarch mwenye biashara ya kuuza magari,akatumia washauri wa Rais Yelsin akawapa mchongo.....mchongo wenyewe ilikuwa wamshauri Rais akubali kukopa kwa kuweka dhamana ya hisa ya mashirika ya umma! Kwa hiyo serikali idhaminishe mashirika yake kisha zile hisa zake ndio ziwe dhamana kwa mtu au kampuni itakayokubali kutoa mkopo wa fedha ili serikali ipate ela ya kuwalipa watumishi,wazo hili lilikubaliwa na serikali na mashirila ya umma yakawa yanawekwa dhamana ambako yeye Boris na Abramovich ndio walitoa fedha kupitia makampuni yao tofauto tofauti waliyounda! Kwa mfumo huu walijikuta wananunua kampuni na mashirika ya umma kwa bei sawa na bure......mfano kampuno ya mafuta ya Sibneft ilinunuliwa kwa njia ya kukopesha serikali jumla ya dola milion 300 mwaka 1997 na mwaka 2003 dhamani yake ilikuwa dola bilioni 75
Yaani ni kama wale jamaa wanaokopesha fedha za riba kubwa alafu unaweka gari pamoja na kadi yake Orijino...kisha unasaini mkataba kuwa ikifika ile tarehe kama hujalipa badi mkopeshaji anakuwa na haki zote na
Anguko la ujamaa lilitajirisha wachache huku.likiwaacha warusi 150mil wakiwa katika umaskini na mali zao kuuzwa kwa bei ya kutupwa mithili ya yale yalifanyika Tanzania wakati wa serikali ya awamu ya tatu



Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE
Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER FOUR
AN ORPHAN JOINS 'THE FAMILY'

Yelstin aliongoza Urusi kuanzia 1991-1999 katika kipindi chote hiki sio bunge,wala baraza la mawaziri wala vyombo vya ulinzi na usalama vilivokuwa na nguvu...kulikuwa na watu wachache miongoni mwa Olgarch walioitwa the family hawa ndio walikuwa wanaongoza nchi,miongoni mwao ni yule Bwana Boris mshirika wa Abramovich.Hawa ndio walipanga na kuratibu kampeni za mwaka 1996 za kumrejesha mtu wao Yelstin madarakani kwa gharama yoyote!
Rais Yelsin alikuwa na binti yake aliyeitwa Tanya ambaye alikuwa anaongoza moja ya idara nyeti pale ikulu,huyu ndio alikuwa roho ya Rais na mtu anayeaminika zaidi,ili ufanikishe mambo ilikuwa lazima kupitia kwa Tanya!huyu binti alikuwa mshauri wa Rais(baba yake)na Rais Yelsin hakuwa na hofu hasa baada ya kujulishwa kuwa hata huko Ufaransa Rais Chirac amemteua binti yake Claude kuwa mshauri wake! Olgarch Boris alipanga mpango wa kuwakutanisha hawa mabinti yaani Tanya na Claude ili Tanya ajifunze mambo ya magharibi aachane na ushamba kutoka kwenye ujamaa!Ziara ya Paris ilizaa matunda,na aliporejea Tanya alikuwa mtu wa kisasa aliyebadilisha mwonekano wa Rais na ikulu kwa ujumla!
Kwa msaada wa the family na Olgarch wengine Yelsin alishinda awamu ya pili kwa zaidi ya asilimia 50%!ni hawa Olgarch ndio walitumia kila aina ya mbinu na kutoa mchango wa fedha pamoja na kupanga watu wao kwenye kila nafasi
The family waliingia ikulu,na kufanya babeque na vinywaji kila siku,walitumbua raha..kwenye hivi vikao vya mara kwa mara Abramovich alijikuta karibu sana na Tanya na familia nzima ya Rais Yelsin,miongoni mwa the family yeye Abramovich ndie aliaminika zaidi,akawa mtu wa karibu na mshauri wa karibu na anayeaminika na Rais! Abramovich aliendelea kujisimika zaidi kibiashara na kisiasa!
Ilifika pahali the family ikawa ndio Abramovich na Abramovich ndio the family!
May be an image of 1 person and standing










Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE
Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTERSIX
PLAYINGPOLITICS

Mwandishi anasema kuwa mwaka 1999 Putin aliteuliwa na Rais Yelisn kuwa wazir mkuu wa Urusi kwa msaada wa Abramovich,na ndie pia aliyesimamia uundwaji wa Serikal mpya chini ya waziri mkuu Putin.Mara kadhaa amejitahidi kukataa kuwa anahusika na siasa ila ushahidi wa uwepo wake Kremli upo wazi sana!wakati huu alitumia muda mwingi Kremli na aliingia bila appointment!
Wakati huo Urusi iliomba kampuni fulani ya political Consultants ya USA iwasaidie kujua nani alifaa kuwa mbadala wa Rais Yelsin,baada ya utafiti walishauriwa wateue mtu mwenye nguvu(Warusi wanapenda sifa sana) miongoni mwa majina pendekezwa Putin hakuwepo,walikuwa watu kama Yuri Lukhoz meya wa Moscow na wengine wengi.Jinsi ambavo Abramovich alichanga karata zake kwa weledi mkubwa hado kumfanya Putin kuwa si tu Rais bali miongoni wa Marais wenye maguvu duniani imebaki kuwa siro yake tu!
Huyu meya Yuri alikuwa na nguvu na mwaminifu kwa Rais Yelsin lakini alikuwa mwiba kwa watu wa karibu na Yelsin akiwepo Abramovich na Boris,hivo ilibidi waingie kazini kupambana kwa nguvu zote hadi kufanikiwa kumweka Putin ili wawe salama wao binafsi na biashara zao.
Baada ya Ushindi wa Putin mambo yalibadilika kwa Oligarch wengi,siku moja Putin akiwa Rais aliwaita wote,walikuwa zaidi ya Olgarch 30,Rais Putin akawaambia kuwa anawashukuru sana kwa msaada wao, lakimi wajue kuwa sasa yeye ni Rais,kama mtu angetaka kuendelea kufaidi afanye mambo kadhaa
Mosi.Asitumie rushwa na maofisa mawaziri wasiokuwa waaminifu kujipatia mali ya umma
Pili.Asiingilie serikali,wala kuikosoa bila staha
Tatu.Alipe kodi stahiki
Kushindwa kufanya hivo mali zitataifishwa na wao kuozea jela kwa kesi ambazo hazina dhamana.Olrgarch waligawanyika baada ya kikao,wengi waliona wamesalitiwa,wengine waliona waanzishe uasi,almradi kila kundi lilikuwa na mtazamo wake,Abramovich yeye aliamua kufuata maelekezo mapya ya utawala mpya
Baada ya kikao ilitokea kitu cha ajabu Meli kubwa ya kivita ambayo ilikuwa fahari ya Warusi,ikiwa na wanamaji zaidi ya mia moja,ilizama baharini,wakati inazama Rais Putin alikuwa likizo,waziri wake wa mambo ya ulinzi alimpigia simu na kumjulisha kuwa chombo kimepoteza mawasiliano ila wanahangaika kutafuta tena,na akamwambia Putin kuwa sio ishu kubwa hivo yeye Rais aendelee na likizo(Alimficha na haijulikani kwa nini),baada ya siku mbili Rais Clinton alimpigia Rais Putin na kumpa pole na kumtaka wakubali kupata msaada wa kijeshi.Wakati huo.wanamaji wote zaidi ya mia walishazama maji na chombo,ilibidi Putin akatishe likizo na baada ya wiki moja alienda kuonana na ndugu wa wafiwa,ambao walikuwa na hasira Kali kutokana na ukimya wa serikali,Putin aliwaambia watalipwa mshahara kwa miaka kumi kwa kila aliyepoteza mpendwa wake,kwa Mara ya kwanza Rais was Urusi alivumilia maneno mabaya kutoka kwa waombelezaji kwa zaidi ya SAA sita.Kuzama kwa meli kuligeuka skendo kwa Serikali mpya ya Putin,Dunia mzima ililaani jinsi ambavo serikali.ilichelewa Kuchukua hatua,vyombo vya Urusi vilivomilikiwa na Olgarch Boris pia viliandika kuikosoa Serikali,Putin hakuwa na uwezo wa.kuhimili kukosolewa akiwa na Hasira Kali alimpigia Oligarch Boris simu na kumtaka aende ikulu,alipofika tu Oligarch alikutana na katibu mkuu viongozi ambaye alimpa maelekezo ya Rais,kuwa Rais anavitaka vyombo vyako vya habari viwe vyake,unapewa wiki moja tu...Boris alihakikisha anaonana na Rais na kwa mstuko mkubwa Rais Putin alimwambia kuwa anavitaka vyombo kwa namba yoyote ile,Boris hakuwa ma ujanja zaidi ya kuviuza kwa bei ya hasara kwa mshirika wake Abramovich kisha yeye Boris akakimbilia London ambako alipata haki ya mkimbizi wa kisiasa.Huku nyuma alifunguliwa mashtaka ya kila sina....na huko London alifuatiliwa na KGB(FSB) auwawe...hivi ndivo Putin alijikuta anakuwa.mtu mwenye nguvu zaidi Urusi...na hivi ndivo Mwanafunzi alivomzidi mwalimu wake.Leo Abramovich ni mtu wa pili mwenye nguvu zaidi Urusi baada ya Putin
 
Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE
Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER SEVEN
A FROZEN KINGDOM

Mwandishi anasema kuwa Abramovich aligombea kuwa gavana wa jimbo la Chukotka,hili lilikuwa jimbo la jamii ya watu duni,watu maskini.Ila lilikuwa na rasilimali za kutosha.Jimbo hilo lipo eneo la Siberia kama kilometa 60 kutoka Alaska.Baada ya ushindi kila mtu alishangazwa tajiri mkubwa kwenda kugombea jimbo tena la umaskinini...kwa Abramovich kuna kitu alikiona ambacho wengi hawakuweza kukiona!
Kuna binadamu ambao huzaliwa na akili zao za ziada,wenye uwezo wa kusoma nyakati na majira basi Abramovich ni miongoni mwao.Hakuogopa umbali wa kilometa 6000 kutoka Moscow hadi Chuktoka,unaambiwa wakati Moscow ni usiku Chuktoka kulikuwa na usiku,kulikuwa na tofauti ya masaa tisa,lakini Abramovich hakujali hilo! Hakufahamiana na yeyote wakati anagombea lakini alisonga mbele!
Akiwa gavana alijitahidi kuongea na marafiki zake waliokuwa na makampuni kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta muhimu kama afya,elimu na benki,kwa mara ya kwanza raia wengi wakawa na akaunti na kupewa ATM(kwa nchi iliyotoka kwenye ukomunisti kumiliki akaunti ya benk ili bonge la ujiko)!kwa ujumla maendeleo ya watu na vitu yalienda kwa kasi mno! Abramovich alizidi kujichimbia mtandao wa nguvu.Mtandao wa barabara hospital na kwa mara ya kwanza ilijengwa supermarket kubwa pamoja na ukumbi wa sinema,hii ilikuwa mwaka 2003(Wewe Mwafrika unayeamini kuwa Ulaya/Uzunguni hakuna washamba ukome kuanzia leo,Ulaya washamba kibao tu,walikuwa wanaenda kushangaa supermarket)
Mwandishi anasema Abramovich alikuwa analenga hazina kubwa ya mafuta ghafi yaliyokuwa kwenye jimbo hilo la Chukotka!lakini pia alitumia nafasi hiyo kutengeneza mtandao na nchi jirani ikiwepo Canada,na Usa (jimbo la Alaska ni 60km tu kutoka Chuktoka) lengo kuu ikiwa ni kupata wateja wapya wa bidhaa za makampuni yake kutoka nje ya Urusi.Sasa mambo yalimwendea Abramovich vizuri sana na akatumia mwanya huu kukwepa kodi kupitia kampuni yake ya mafuta ya Sibneft ambako,aliuza mafuta kwa jimbo la Chuktoka kwa bei nafuu,kisha alitumia kampuni aliyoisajilia Chuktoka kusafirisha hayo mafuta nje ya Urusi,kampuni yake ya Sibnef ilionekana kutotengeneza faida kubwa hivo kiwango chake cha kodi kikashuka hadi 7% wakati ilipaswa kulipa 24% ya faida yake!
Kwa kuwa yeye Abramovich ndio alikuwa gavana aliweza kufanya jimbo hili kuwa kama sehemu ya kampuni yake, na akalitumia vizuri kukwepa kukodi! Baadae hakugonbea tena kutokana na Duma(bunge la Urusi) kubadili sheria na kufuta uhuru wa majimbo katika kujipangia maswala la kodi! Majimbo yakabaki na mambo ya maendeleo tu,serikali kubwa ikawa na jukumu lote la sera za fedha na kodi!



Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE
Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER EIGHT
A PEOPLE SET APART

Mwandishi anasema kuwa Jewish(Waisrael) ni kama asilimia mbili tu ya Warusi..yaani Warusi wenye asili ya Israel ni asilimia mbili tu,ambao ndio Olgarch wengi zaid ya 80% ya Olgarch wote,tena hawa Olgarch wenye asili ya Israel ndio wale the family,akiwepo Abramovich,, Khodorkovsky, Berezovsky, Gusinsky na Fredman na wengineo! Msingi wa mafanikio yao ni utaratibu wao wa kujaribu,hawaogopi ku "risk" Jew wana msemo wao kuwa....
Licha ya kuwa Jew Abramovich hakuwa anafuata mafundisho na makatazo ya dini yake,alimiliki kiwanda kikubwa huko Siberia (kwenye lile jimbo la Chuktoka) cha kutengeneza mazao ya nyama ya nguruwe ikiwepo bacon,ham etc ambacho kwa mwaka kilizalisha zaidi ya tani laki nne za mazao hayo na kuyauza soko la ndani na nje 'In the land of the blind, the one-eyed man is king
Jews walihamia Urusi ya kale kuanzia karne ya 15 na walikuwa wanapingwa na tawala mbalimbali hadi utawala wa Lenin ndio uliwapa ahueni ikiwa ni pamoja na haki ya kupata elimu,walitumia fursa hii kwa weledi mkubwa,ambako walijiendeleza katika nyanja mbalimbali ikiwepo udaktari,wanasayansi kiasi cha kufanya kuwa bidhaa muhimu,maana walihitajika kila sekta.Walitoka kuwa jamii ya kishamba isiyokuwa na maana hadi kuwa jamii ya wasomi na watalaam wenye kuhitajika kila nyanja.Leo wametapakaa kutoka Mashariki ya Dunia hadi Magharibi,kutoka Kusini hadi Kaskazini



Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE
Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter Nine
Selling up

Mwandishi anasema kuwa Olgarch wengi walipata utajiri wao kwa muda usiozidi miaka kumi,hakuna popote unaweza kupata Utajiri uwe mult bilionea kwenye kipindi kifupi hivo,ni wazi lazima ucheze faulo nyingi,ikiwepo kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu,sasa hawa jamaa walipambana kuhakikisha wanaweka watu wao madarakani,mwishoni mwa 1999 walimfanyia fitina waziri mkuu aliyeitwa Sergei Stephanies akafutwa kazi,kutokana na huyu Sergei kutoaminika kama atalinda masilahi yao,na Bwana Yelsin,baada ya kufukuzwa ndio Bwana Putin aliteuliwa kuwa Waziri mkuu,kabla ya kupata Urais.
Rais Putin alikuwa anajua nguvu ya Olgarchs hivo aliamua kuwapunguza kwa kutumia kanuni ya Divide and rule..alipopata Urais tu alianzisha kitengo cha kufuatilia makosa ya uhalifu,ambako alimteua Bwana Sergei kuwa mkuu wa kitengo,maana yake alikuwa na uwezo wa kumwita yeyote kumhoji juu ya utajiri wao,wengi waliitwa wakiwepo wale waliomfanyia fitina aondolewe,isipokuwa Abramovich tu ambaye kwa muda wote alijua jinsi ya kuchanga karata zake kwa umakini mkubwa!
Unaambiwa jamaa alikuwa na marafiki wale wale kwa muda mrefu sana,kuanzia wakati anauza midoli,hii ilimfanya watu wengi wasijue mambo yake kwa undani!
Sasa alijua kuna siku ataanza kuchimbwa chimbwa hivo aliamua kuuza share zake kwenye kampuni alizonunua serikalini awali,lakini alikuwa anauza kwenye kampuni ingine ambayo yeye ana hisa nyingi,mfano anauza hisa kwenye kampuni Y ambayo inatangazwa kufilisika,kampuni H inanunua hisa zote za Abramovich kutoka Y lakini ni yeye ndio mmiliki wa wa kampuni H.Ilipokuja kuchunguzwa kampuni Y ilikutwa imeshafilisika,chelsea ni miongoni mwa matendo yake ya utakatishaji wa fedha..yaani fedha inapatikana kwa njia haramu,kisha inanunua kampuni halali ambayo inafanya biashara halali inayotambulika na kila mamlaka!
May be an image of Caracal Caracaladventures
 
Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE

Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ


Utangulizi

Mwandishi anasema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 1999 hakuna gazeti lolote lililokuwa na hata picha tu ya Abramovich.Ila hadi wakati huo tayari Abramovich alikuwa tajiri na bilionea wa kutupwa,akiwa miongoni nwa Olgarch kijana zaidi
Pale nchini Urusi ilitokea kundi dogo lililokuwa na maguvu na lililindwa na watawala na hili kundi/genge liliitwa Olgarch hawa ndio waligawana utajiri wa USSR wakati ikianguka,waligawana kama vile mbwa mwitu wanavogawana mnyama akiwa hai,kila mmoja anakata sehemu yake.

Kwa wafuatiliaji wengi wanamfahamu Abramovich kama tajiri na mmiliki wa kilabu ya mpira ya Chelsea

Baada ya tetesi kuanza kusambaa vyombo vya habari vilianza kufuatilia kumjua huyu Abramovich ni nani.....ilibidi chombo kimoja kitangaze dau kubwa la pesa kwa mtu atakayeweza kupata picha ya Abramovich
Mwandishi anasema Abramovich ni miongoni mwa vijana walioweza kutajirika kupitia biashara mbalimbali anbazo msingi wake ni anguko la utawala wa USSR,ambao waliokuwa karibu na watawala waligawana mali ya umma(Kama hapa Tanzania wakati wa ugenishaji mashirika ya umma).Hata hivo Abramovich anaelezwa kama mtu mpole,mwenye aibu,asiyependa makuu,na asiyependa kuonekana hadharani sana,wala sio Olgarch wa kuvaa nguvu za gharama kama wengine,ni mtu ambaye huonekana akitazama mechi ya timu yake ya chelsea aliyoinunua 2003 akiwa hata hajanyoa vizuri kama matajiri wengine!mara nyingi huwa na mkewe na watoto wake watano,aliojaliwa kwenye miaka 13 ya ndoa(spidi ya 5G)!
Mkewe Irina pia anapendelea zaidi kukaa na familia kuliko mitoko isiyokuwa na ulazima.Kwa ujumla ni familia inayopendana na kujali watoto wao,hupendelea kutumia muda mwingi na watoto kama sehemu muhimu ya malezi bora!

Mwandishi anasema ili kumwelewa Abramovich na ukwasi wake wote kuanzia kampuni yake kubwa ya mafuta ya Sibneft unapaswa kumwangalia kama mwanasiasa zaidi kuliko mfanyabiashara! Au tumwite mfanya-biashara-siasa,hii ni kwa kuwa kwa kipindi hicho mfanyabiashara ambaye hakuwa na ulinzi wa Kremlin(Ikulu ya Urusi) au alifilisiwa au alifungwa au vyote kwa pamoja,hivo kutajirika ukiwa Urusi kulitegemeana na uhusiano wako na watawala hasa Kremlin na sio jitihada zako binafsi...vinginevyo unanyanganywa mali zako,unafungwa jela.....mfano wa waliofilisiwa ni rafiki yake Abramovich aliyeitwa Boris Berezovsky au gwiji lenye vyombo vingi vya habari Olgarch Vladimir Gusinsky walilazimishwa kukimbia nchi na Bwana Putin kwa kuwa tu wakienda kinyume cha Kremlin

Abramovich ana kanuni yake muhimu kuwa Rais ndio anamiliki jela na sheria hivo alikuwa mtu makini ambaye alihakikisha kuwa hakosani na watawala ili asiharibu mambo yake,badala yake akawa mshirika wa karibu na mwandani wa watawala kuanzia Boris Yelstin na Rais wa Sasa Putin
Abramovich ni mwandani wa Putin na ndio aliohakikisha Putin anashinda mara ya kwanza 1999 na ameendelea kuwa mtu anayeaminika zaidi na Putin...wakati ambako Putin alitaka kutisha au kukodisha magenge ya kushughulikia wapinzani wake,jukumu hilo lilifanywa na Abramovich ndie anayeaminika zaidi kufanya misheni hatari kulinda ukwasi wao
Unaambiwa Abramovich ana akili nyingi sana,ana uwezo mkubwa wa kujaribu,uwezo mkubwa wa kuona mbali,anaweza kutazama hatua kumi mbele hata kama hatua ya kwanza hadi ya saba zina changamoto,lakini bado atasonga mbele kwa matumaini makubwa! Sio mtu wa kukata tamaa...tutaona huku mbele kuanzia kuzaliwa kwake hadi leo,ili kujua kwa undani kabisa kuwa huyu Abramovich ni kiumbe wa aina gani?



Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE

Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER ONE

BAPTIZED INTO GREATNES

Mwandishi anasema Abramovich alizaliwa mwaka 1966 na mama yake mzazi alifariki mwaka mmoja yaani wakati Abramovich akifikisha mwaka tayari mama yake mzazi alikuwa marehemu.Chanzo cha kifo cha mama yake ni jaribio lake la kutoa mimba kienyeji kufuatia kupata ujauzito kabla mtoto Abramovich hajafikisha hata miezi mitano.Baada ya kifo cha mama yake baba ambaye alikuwa mwajiriwa wa moja ya makapuni ya ujenzi,alimpeleka Abramovich kwa Bibi yake...ndio kusema Abramovich amelelewa na bibi yake.Hata hivo baba yake alikuja kufa baada ya kuumia mguu akiwa kazini,mguu ulivunjika na kusababisha mauti,wakati huo Abramovich alikuwa na miaka miwili na nusu,hivo Abramovich ni yatima tangu akiwa na miaka miwilo ndio kusema hata hawajui wazazi wake!

Abramovich alikuja kulelewa na baba yake mkubwa Leib (Abraham)na Ludmila(kaka wa baba yake mzazi)hii ilikuwa bahati kuwa alikuwa mtoto wa kiume pekee,huyu baba yake mkubwa alikuwa na watoto wa kike wawili,wakubwa kwa Abramovich.Waliishi kwenye apartment chini ya sheria kali za kikomunist,alianza shule akiwa na miaka sita,na inasemwa kuwa alikuwa mtoto makini sana darasani,alipenda mijadala ya kujenga!na alikuwa mdadisi anayependa kujifunza kila kitu!

Baba yake mzazi(alikuwa Mrusi mwenye asili ya Israel
Mwandishi anasema kuwa kuna somo kubwa la kujifunza kuhusu Abramovich mosi alikuwa sio mrusi kwa asili,pili alikuwa yatima na tatu alikulia kwenye mji ambao ulikuwa na baridi kali,kiasi cha kufanya wakazi wake kuwa walevi kupindukia ili kupasha mwili,lakini katika changamoto zote hizo yeye hakuwa hata kunywa Vodka.....na akapenya kuwa miongoni mwa watu hatari zaidi Urusi

Mwaka 1974 Abramovich alihamia Moscow kuishi na bibi yake,kwenye chumba kimoja kufuatia uhaba wa nyumba nchini Urusi enzi za ukomunisti..Akiwa Moscow aliendelea na shule ya msingi kwenye shule 232(Urusi ya Kikomunisti shule zilikuwa zinajulikana kwa namba)akiwa shuleni alikuwa mwanafunzi bora kabisa shuleni,kiasi cha kupendwa na wanafunzi na waalimu wote
Dear Roman Arkadievich,
The pupils and teachers of School 232 thank you for your enormous kindness to us. The good work done by you will always be remembered. When we use the gym we think of you. When we eat in the canteen we think of you. When we use the computer room we think of you ...
The style is reminiscent of the cult of personality promoted under Stalin.In the
Forties and Fifties, newspaper articles lauding the building of a new stadium, for
example, would say, 'Sportsmen are thinking of Comrade Stalin with gratitude'.
In general, he would be paraded as the best friend of everyone from children to
border guards. And so it is with Abramovich within the walls of School No. 232.
There are even plans to create a school museum dedicated to the achievements
of distinguished old boys. It seems likely that Abramovich will find that a
section of the museum has been devoted entirely to him.

Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE

Mwandishi.DominicMidgley and ChrisHutchins
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER TWO

THE MAKING OF THE MAN

Mwandishi anasema hadi mwaka 1983 wakati Abramovich anaanza maisha bado Urusi ilikuwa ya kijamaa,na biashara binafsi ilikuwa kinyume cha sheria! Ilikuwa jinai kuuza kwa faida nchini Urusi! Lakini hali ya mabadiliko Duniani ilikuwa inaenda kwa kasi sana
Wakati huo Warusi wenye asili ya Kiisrael walikuwa asilimia mbilo tu,wengi wakiwa waumini wa madhehebu ya Ki Orthodox na walichukuliwa kama watu wa dini tu wasiokuwa na maana yoyote kwenye jamii! Abramovich alikuwa miongoni mwao ba fursa ya kusoma vyuo vya serikali ilikuwa ndogo sana,hii ilimfanya Abramovich kutafuta chuo kijijini kwao katika mji mdogo wa Ukhuta ambako alisoma Ukhta Industrial Institute,hata hivo miaka miwili baadae aliacha masomo yake chuoni hapo akajiunga na jeshi la kujenga Taifa(Red Army) enzi hizo huko Urusi hakuna mzazi aliyepeleka mtoto wake Jeshini bali walihonga kwa maofisa wa jeshi ili mtoto asiingie jeshini,kwa upande wa Abramovich wazazi wake hawakuwa na fedha za kuhonga hivo akalazimika kujiunga jeshini ambako huitwa salagy(samaki mdogo) na wale wakubwa
Enzi hizo jeshi la Urusi halikuwa na nidhamu kutokana na uhaba wa fedha,hivo walipofika wageni walinyanyaswa na kuporwa hela au chochote cha dhamani na wakubwa!chakula kizuri kililiwa na wakubwa huku Salagy wakilala njaa au kula makombo

Unaambiwa akiwa jeshini Abramovich hakuhangaika na vyeo vya kijeshi badala yake alipambana kutengeneza marafiki na mtandao (network)alikuwa anawapikia wenzake,tena vyakula adimu ikiwepo uyoga ambao alilalizimika kwenda msituni kuuchuma!alikuwa mzuri sana katika kufanya organization ya mambo mbalimbali jeshini,kwa wakubwa na wadogo

Mwaka 1987 Abramovich alirejea kwao kutoka jeshini, na akamchumbia mkewe wa kwanza ambaye alikuwa amemzidi kwa miaka mitatu...yaani mwanamke Olga alikuwa na umri mkubwa kuliko Abramovich! Na alikuwa na mtoto lakini Abramovich alimpenda mama na mtoto wake! Miezi mitatu baadae walioana kwenye sherehe iliyohudhuriwa na watu 15 tu! Hasa ndugu wa karibu! Abramovich alioa akiwa na miaka 21 tu!(wewe hadi leo una miaka 34 hujaoa/hujaolewa unatafuta maisha ambayo hujayapata,huna mke/mume wala maisha)
Baada ya ndoa Abramovich hakurudi kumalizia chuo bali alijiingiza kwenye biashara ya kuchuuza! alichukua bidhaa kutoka Moscow na kwenda kuziuza Ukhuta.Wakati huo ujamaa ulisababisha uhaba wa bidhaa nyingi,ingawa ilikuwa haramu lakini ilikuwa biashara nzuri!alipakia kwenye malori kimagendo na kuzisafirisha miji mbalimbali! Sigara,payfumu,chocolate,na nguo.Hata hivo serikali ilibana zaidi kampuni binafsi na biashara binafsi hasa za bidhaa za kula
Abramovich akalazimika kuanzisha kampuni ya doll(midoli na sanamu)hii kampuni iliitwa Uyut ambayo ilitengeneza na kuuza midoli na sanamu na ikawa inawalipa mara ishirini zaidi ya mshahara wa mtumishi wa umma!.Abramovich aliweka muda mwingi sana kwenye kampuni kiasi cha kukosa muda wa familia na kupelekea kutalakiana miaka miwili tu baada ya ndoa!mke aliona jamaa alipenda kazi kuliko alivompenda yeye na mtoto wake!

Unaambiwa jamaa aliweza kutoka nyumbani alfajiri na kurejea usiku wa manane,yaani maisha yake yalikuwa kazi na kazi ikawa maisha yake

Mwaka 1991 Abramovich alioa tena msichana ambaye alikuwa muhudumu wa moja ya shirika la ndege,na kufanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza Anna.
Kwenye hii miaka inaaminika kuwa tayari jamaa alikuwa na zaidi ya biashara 20,ikiwepo ya maduka ya bidhaa,kuuza tairi na ya kampuni ya ulinzi binafsi(Hii ndio ilikuja kumfanya awe karibu na wadosi,tutaona huko mbele)

Kuna tukio lilitokea Urusi mwaka 1991 Agosti ndio lilibadilisha kabisa maisha ya Abramovich kisiasa na kiuchumi.Mwaka huo kuna jamaa ambao walikuwa hawakubalini na sera za Gorbachev ambao waliamua kuweka shinikizo kubwa la kumwondoa madarakani,ndani ya muda mchache Rais alijiuzulu na kuanguka rasmi kwa USSR(ilishaanguka kabla hapa ilikuwa tangazo rasmi).Baada ya anguko la USSR Yelsin alikuwa Rais wa Urusi mpya,kwenye anguko hilo ambalo uchumi ulikuwa hoi ndiko Abramovich aliona fursa ya biashara ya mafuta,alitumia njia anazojua kupata leseni ya usafirishaji wa mafuta! Enzi hizo wengi wakomunist hawakuona mafuta kama bidhaa muhimu.Kwa Abramovich aliiona kuwa leseni ya kusafirisha (kuingiza na kutoa mafuta) ilikuwa sawa na kukabidhia printa ya kuprint hela unazotaka!
Abramovich akawa tayari ana kibali pekee ya cha kusafirisha mafuta!Urusi ilikuwa nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta Duniani,ikiwa na uwezo wa kuuza kote Duniani!





.
Dah jama
 
Tena kwa asilimia 100,japo hana shule.Ni story ya kusisimua sana.Na alikataa madaraka yoyote ya kisiasa akataka apewe umiliki wa kampuni za uchimbaji gesi za Russia.

Yeye alitaka ufalme wa kiuchumi na si kisiasa.

Ni mtu ambaye Putin anamheshimu kuliko.Ni stori ndefu sana jinsi alovyoanza hadi kuwa na urafiki na binti wa rais wa Russia ili aweze kupata access ya kuweza kuwa karib na rais.Na mpaka akawa mshauri wa karibu anayeaminika wa Boris Yelstin,mshauri asiyetajwa popote.

Ni moja ya watu walioinjinia Borris Yelstin kujiuzulu na kabla ya hapo alishampendekeza Putin kuwa PM.Na utajiri wake ni wa jasho na damu.

Elewa tu si mtu wa mchezo mchezo.

Kwahiyo mkuu siku ukipata kuonana na Magu usimwombe UDC au cheo bali mwombe akuwezeshe hata uweze kumiliki kitalu cha Tanzanite au gesi upate ufalme wa pesa.
kuonana na magu tena??? muogope mungu kaka
 
Abramovich ni Street Genius....kuna vitu tukubali viko kwenye damu tu.

Kuna mzee mmoja darasa la 7 tu hapa bongo anafanya ventures za ajabu ajabu worth multi-billions (hapa bongo wako sana tu wengine wana real estates in city centers, yet very humble)...and u wonder inakuaje someone with soo little education, from a poor family background could end up having soo much money....Dah

Hivi life path ya mwanadamu ina siri gani ?? Walahi sielewagi. Daah
 
Uingereza walishamshindwa chanzo cha ugomvi na serikali kama ile ni Kwamba jamaa aliingiza chaka moja ya kampuni kubwa ya uingereza na kuweza kuimiliki kisheria kabisa kitu ambacho waingereza waliona kama jamaa kawazidi akili ivyo wakaanza kumfanyia figisu lakini bado aliwapiga tena bao na kufanikiwa kununua timu ya Chelsea kwa ela ya mboga..
Huyu jamaa ni mfano wa kuigwa ni faita balaa

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Na juzi Kati walimpiga ban asikanyage uingereza Kama raia wa Russia .

Walisahau jamaa ana asili ya Israel

Sheria za hazina kikwazo kwa raia yeyote wa Israel kuingia uingereza

Jamaa akaenda chukua uraia wa Israel na Sasa anakanyaga uingereza kwa passport ya Israeli
 
Na juzi Kati walimpiga ban asikanyage uingereza Kama raia wa Russia .

Walisahau jamaa ana asili ya Israel

Sheria za hazina kikwazo kwa raia yeyote wa Israel kuingia uingereza

Jamaa akaenda chukua uraia wa Israel na Sasa anakanyaga uingereza kwa passport ya Israeli

Akili za wengine zinapoishia jamaa zake ndio zinapo anza.

Nimekuja note kuwa mfanya biashara mahiri kunaenda samba samba na kuielewa sheria ya nchi husika vizuri how to break the codes effectively....jamaa sishangai akiwa anatumia law firms 10 bora za dunia wanao strategise mishe zake.....huwezi toboa business kama hujui kucheza na sheria.
 
Jina la kitabu.ABRAMOVICH THE BILLIONAIRE FROM NOWHERE

CHAPTER 10

MISTER CHELSKI

Mwandishi anasema kuwa Abramovich alikuwa anapenda mpira wa miguu,na alikuwa mfadhili wa timu kadhaa huko kwao Urusi.Mwanzoni alipenda zaidi ligi ya Italy na Spain na alipenda kumilki klabu kwenye moja ya ligi hizo yaani Serie A au la Liga,akafuatilia ununuzi wa klabu kwenye nchi hizo akashindwa kutokana na sheria tata za raia wa nje kumiliki klabu,wakati huo sheria haikuruhusu umiliki kutoka nje,baada ya kushindwa ndio aligeukia EPL na klabu ya kwanza kutaka kununia ilikuwa MANCHESTER UNITED mwaka 2002.Mwaka huu alitembelea dimba la Old Traford siku ya mechi ambayo Man United ilicheza na Real Madrid,alifurahishwa na mchezo na wakati anatoka rafiki yake ambaye alikuwa mchezaji wa Man united beki kisiki Rio Fernand ndio aliwapa lift kwa gari yake.

Baadae Bwana Abramovich kwa ushawishi wa rafiki zake akapata dili la Chelsea.Wakati huo chelsea ilikuwa ikimilikiwa na Ken Bates taycoon aliyekuwa anakabiliwa na madeni ya kutosha kufuatia uwekezaji mkubwa aliokuwa amefanya eneo ambalo ni uwanja wa Chelsea,wakati huo alikopa paundi 75mil ili ajenge kuanzia maduka,malls,na burudani nyingine lakini kwa bahati mbaya biashara haikwenda vizuri hadi kufkia 2003 hali ilikuwa tete sana hadi kufikia kuweka club sokoni aliweka timu sokoni kwa mbide sana maana alikuwa mtu anayependa sifa na asiyekubali kushindwa! Alikuwa na urafiki na Pin Zahavi ambaye alikuwa miongoni mwa wadau muhimu wa mpira wa miguu Ulaya,huyu alikuwa rafiki wa Bates na alikuwa pia rafiki wa Abramovich(yeye na Abramovich walikuwa Jews)wakati huo Chelsea ilikuwa ina deni la paundi laki na ishirini na sita milion.

Mmiliki wa Chelsea alipokutana na Abramovich kwa msaada wa Zahavi walizungumza kuhusu uwezakano wa kununua na yeye Abramovich alimjulisha kuwa kama wakikukubaliana atalipa cash(taslimu)siku iliyofuata walikutana Stanford Bridge ndani ya dakika ishirini wakamaliza dili,mwanzoni Bates aliuza hisa moja kwa paundi 50 lakini kwa ustadi mkubwa Abramovich alimshawishi akakubali 35p sawa na jumla ya paundi 60mil aidha alichukua deni la paundi mil 80 hivo kufanya jumla ya 140mil paundi.Hivo Chelsea ikawa imeuzwa kwa jumla ya paundi milioni 140(sawa na dhamani ya Harry Maguire pamoja na Wan Bisaka).Hata hivo alichonunua Abramovich ilikuwa sehemu tu ya umiliki wa club kwa kuwa Bates hakumiliki kwa 100%,kulikuwa namakampuni mengine mbalimbalmengine yamesajiliwa kwenye visiwa vinavificha uhalisia,sasa ikawa jukumu LA Abramovich kuhakikisha anawanunua wote.Wakati anainunua Chelsea hakuna mtu anayejulikana ilibid hata waziri wa michezo wa Uingereza aitishe uchunguzi wa uuzaji wa klabu kwa mtu asiyejulikana historia yake

Miezi miwili tangu anunue klabu Abramovich akaanza matumizi ya uwekezaji yaliyouacha ulimwengu mdomo wazi...yaani aliamua kuwafunga mdomo wote,kwanza alinunua wachezaji kwa gharama kubwa

Juan Sebastian Veron kutoka Manchester United kwa £15 million, Claude Makelele kutoka Real Madrid
£14 million,
Damien Duff from Blackburn Rovers for £17 million,
Joe Cole na Glen Johnson from West Ham for £6.6 million Jumla alitumia paundi milioni 110 matumizi haya yalimwongezea imani kwa mashabiki na wanazi wa Chelsea
Abramovicj alikusudia kufanya Chelsea kuwa Global brand ikabidi amlete Peter Kenyon kuwa mkurugenzi kutoka Man United,aliahidi kumlipa Mara mbili ya mshahara wake,inasema Peter Kenyon aligharimu Chelsea hadi paundi million saba kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom