Uchakavu wa CCM na propaganda za Ushindi wa CDM Arumeru East | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchakavu wa CCM na propaganda za Ushindi wa CDM Arumeru East

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WOWOWO, Apr 3, 2012.

 1. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakuu nimekuwa nikifuatilia sababu zinazotolewa juu yakubwagwa kwa CCM huko Arumeru East naziona kama zimejaa propaganda naupotoshaji wa makusudi ambao ni wazi unaonekana umelenga kuuficha ukweli nakujenga mazingira ya hatari huko tuendako.
  Sababu zinazotolewa na watu mbalimbali ukianza na gazetila magamba la Uhuru kwenye Editorial yake, Maggid Mjengwa (Tafsiri yangu gazetila Ufahamu), media mbalimbali na baadhi ya wanazuoni ni pamoja na zifuatazo;

  1. Mbioza kuwania urasi mwaka 2015
  2. Mpasukoulioko ndani ya CCM
  3. Mgombeawa CCM Sioi Simari hakuwa chaguo la Wana Arumeru

  My Take;

  - Sikwamba Wananchi sasa wameichoka CCM na hawaitaki?
  - Si kwambaufisadi, duluma ya ardhi, ukosefu wa maji, ujambazi wa rasilimali za nchi nk. Ndiyochanzo?

  - Tutasemajechanzo ni mpasuko ndani ya CCM wakati pande zote za makada walishiriki kwenyekampeni bila mafanikio? (Rejea uwepo wa Lowassa kwa upande mmoja na akinaSendeka, Mkapa, Nape, Mkama, Wassira, Kichaa Lusinde na wengine lukuki)

  - Kwanini tunakuwa wazito kuamini kuwa Watanzania wanaweza kufika wakati wakasema basina ikawa?
  - Tutasemajeanguko la CCM Kiwira (Anne Kilango) na Kirumba (Samwel Sitta)?

  - Kwanini inakuwa vigumu kukubaliana na ukweli mchungu kuwa CDM imekuwa verystrategic kwenye kampeni zake na ilibeba kweli kaulimbiu zenye kubeba mguso wajamii? (Rejea; M4C, Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu)

  - Lakinitusemeje kuhusu CCM kujikita kwenye kunadi matusi majukwaani badala ya sera?
  - Vipikuhusu dharau za kuwahonga fedha, khanga, kofia, chakula wana Arumeru wakatiwana shida lukuki?

  Nawasilisha
   
Loading...