Uchakachuaji wa uchaguzi unavyopikwa

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
29,111
2,000
VITAMBULISHO ZAN ID PEMBA.
Wajumbe wa Kamati Kuu na Umma wa Wazanzibar:

Ni vyema mtambue hali mbaya mno inayoendelea kisiwani Pemba kuhusu UPATIKANAJI WA ZAN ID.

Kuna baadhi ya watendaji waliopewa kazi hiyo, kwa Uzalendo wao na baada ya kuona wamelazimishwa kufanya yatakayowaingiza katika kufanya Dhulma na Uonevu jambo ambalo litawakosesha wengi kukosa haki zao za kikatiba , wametutonya yafuatayo ili HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE , vinginevyo MAELFU YA VITAMBULISHO VILIVYORUNDIKANA KATIKA WILAYA ZOTE ZA PEMBA, vitarudishwa Unguja.

# VITAMBULISHO VYOTE vya ambao hawajapata VIPO Pemba.

# Watendaji wameahidiwa DONGE KUBWA na Mkuu wa Mkoa , Hemed, endapo watajitahidi kuwanyima VITAMBULISHO Wapinzani.

# Masheha wanakuja ofisini na wanapewa marundo ya VITAMBULISHO ili wachague watu wao na hao ndio wanaopewa VITAMBULISHO.

Alitupa mfano wa juzi ofisi ya Wilaya ya Chake, Mkuu wa Wilaya ya Chake, Rashid Hadid alitupa kila mtendaji Sh.30,000/ kama TUNZO ya kazi nzuri tuliyoifanya baada ya zaidi ya watu 150 kuwakosesha na kuwapa watu 17 tu, lakini majina yote yaliyoletwa na masheha (ambayo alituletea Rashid Hadid) tuliambiwa tusiondike mpaka wote wapatiwe VITAMBULISHO vyao ( tuliwapa wote 219), kwa hivyo siku hiyo tulitoa VITAMBULISHO 236 (CCM 219 na Wapinzani 17).

Jamani baadhi yetu tunatekeleza maagizo haya SHINGO UPANDE, hatuna furaha , tunakuombeni jambo hili mliingilie kati haraka, acheni mambo yote mlishughulie hili, vijana wazalendo hao walisisitiza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom