Uchakachuaji wa Sheria: Katika hili, niko pamoja na Rais na Mwenyekiti wangu! Dr. John Pombe Joseph Magufuli

Katika hili sijifichi nyuma ya pazia wala kujibanza nyuma ya ukuta. Najitokeza na kumpongeza. Niko na Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM bega kwa bega bila kutega au kuzuga. Namuunga mkono usio na kikomo. Namuunga kwa moyo kuliko maneno. Nipo na Rais wangu; nipo na Mwenyekiti wangu wa CCM. Sambamba.

Naungana na Rais na Mwenyekiti wangu kuinyooshea kidole chenye kilele na kelele Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Kuhusu kuchakachua nyaraka zinazowasilishwa Ofisini hapo. Inaletwa hivi, inatoka vile. Hata sisi TLS tulipeleka Kanuni zetu za Uchaguzi wa AG na zikachakachuliwa. Ingawa Rais hakulaani, maneno yake ya jana yanatuunga mkono.

AG anachakachua kilichoandikwa na kuandika chake. Anawaandikia Wabunge na wanachama wa TLS. Anawalisha maneno. Uchakachuaji katika sheria za mafuta na nyinginezo hauna tofauti na uchakachuaji uliofanyika kwenye Kanuni za Uchaguzi za TLS. Kuandika ya kwake kwa malengo yake. Kumbe Ofisi ya AG imekubuhu na kuzoea kuchakachua. Rais ameliona na kulisema.

Rais na Mwenyekiti wangu, uchakachuaji wa sheria na Kanuni haufanyiki kwa bahati mbaya. Kanuni za TLS zilichakachuliwa ili kuwazuia 'wanaharakati na wanasiasa' kugombea ndani ya TLS. Hata Sheria huchakachuliwa ili madili makubwamakubwa yaendelee kumea na kufanikiwa. Ofisi ya AG imulikwe. Ianikwe. Iwajibishwe. Zilizochakachuliwa zibainishwe. Zirekebishwe.

Bunge lipewe taarifa badala ya kujadili na kuamua kuhusu bajeti!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaa!!!!
Ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaaah!!!
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha aaaaah!!!

Du!!! Inafikia mahali inabidi ucheke tu kwa Sanaa za mikanganyiko, mikurupuko, mivurugiko, mivunjiko, mipasuko ...

Hali kadhalika sanaa za miyeyusho, michemsho, mipasho ...

Matokeo yake ndio haya aibu tupuuuuu!!!

Ama kweli kaka Mrisho ulijua kutuingiza chaka!!!! Haya bana!!! ...

Jamani ndio tunae tena, ndie aliechaguliwa, ndie anaetuongoza, ndie dereva wetu, argh!!! wache atuvuruge tu yana mwisho japo mgumu lakini upo!!!
 
Mtazamo wangu u wazi. Si jambo jema kuchakachua suala ambalo limepitishwa kihalali na wahusika na kwa utaratibu wa kisheria.

Kwa taarifa yako hata mkulu ni mchakachuaji wa sheria, ila uchakachuaji wa sheria hii umemnyima kick ndio maana amefunguka. Hata huyo AG aliyechakachua kamkalia kimya lakini anamchora tu kwamba hata yeye ni mfaidika wa uchakachuaji wa sheria, ila kwa kuwa ana madaraka hana wa kumnyooshea kidole.
 
Back
Top Bottom