Uchakachuaji wa malipo hadi kwa waalimu wapya, tutafika?

MANAKE MKARI

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
281
211
Walimu wagoma kupokea fedha zilizochakachuliwa Send to a friend Saturday, 29 January 2011 09:39 0diggsdigg

Rehema Matowo,
Moshi
VUTA nikuvute imetokea baina ya waalimu wapya walioajiriwa mwaka huu,wakiishutumu Halmashauri ya Wilaya Moshi Vijijini kwa kuwakata fedha zao za kujikimu kwa makusudi.

Mvutano huo, ulitokea jana katika ofisi za halmashauri hiyo baada ya walimu waliokusanyika kudai fedha kubaini kiasi walichotakiwa kusaini ni tofauti na muongozo wa serikali juu ya malipo ya stahili zao.

Waalimu hao walidai kuwa kwa mujibu wa muongozo wa serikali, waalimu wenye shahada walipaswa kulipwa Sh45,000 kwa siku moja katika muda wa siku 14,huku wenye stashahada walipaswa kulipaswa kulipwa Sh 35,000 kwa siku moja katika muda wa siku 14.

Walidai walipokwenda kusaini walitakiwa kusaini Sh35,000 kwa siku moja kwa walimu wenye shahada na Sh25,000 kwa walimu wenye stashahada.

Walidai kutokana na hali hiyo, waliamua kugomea malipo hayo. Katika wilaya hiyo, walipangwa walimu 184 kufundisha kwenye shule mbalimbali.

Walidai sasa ni muda wa wiki moja wamekuwa wakisumbuliwa kuhusu malipo yao kwamba wamekuwa wakipewa ahadi za uongo hadi jana walipobaini mapungufu hayo.

"Tumesota hapa kwa muda wa wiki nzima tangu turipoti na kila siku tunaambiwa njoo kwesho bila kuelezwa sababu za msingi,leo tumekuja asubuhi tunaambiwa turudi saa 8:00 mchana na sasa tunakuta fedha zetu ni pungufu, hatukubali tunachotaka ni fedha zetu kwa ukamilifu,"alisema mmoja wa walimu.

Jitihada za kuwasuluisha walimu hao kwa kuwataka wachukue kiasi kilichopo na nyingine wachukue Januari 31, mwaka huu,zilizofanywa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Morisi Makoi ziligonga mwamba baada ya walimu hao kusisitiza kulipwa fedha zao zote.
Ofisa Utumishi wa halmashauri hiyo,Sadick Mrisho alikiri kuwepo kwa matatizo katika malipo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili fedha hizo zilipwe na kuwasihi walimu hao kuchukua zilizopo kwanza.

Naye,Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo,Ester Mbatiani ambaye alitambulishwa kama mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Anna Mhalende aliwataka walimu hao kutambua kuwa mahusiano baina ya halmashauri na wao yataendelea hivyo ni vyema wakachukue fedha zilizopo wakati wakiandaliwa nyingine.


Waalimu hao, waligoma kuchukua nusu ya fedha na kutaka walipwe fedha zote kwa pamoja na ndio waende kwenye vituo vyao vya kazi.


Source:Mwanachi jumamosi.
 
Wamezoea kuchakachua za waalimu wa primary wenye nidhamu ya woga, hapa wamefika...
 
hata walimu wa wilaya ya mufindi nao walikatwa fedha zao wakagoma kupokea kiasi walichoandaliwa
 
Hata halmashauri ya wilaya ya mbozi bado haijawalipa walimu 31/01/2011.Sijui wata lipwa lini?
 
Back
Top Bottom